Kesi ya Lissu imegeuka jukwaa la CHADEMA kuiambia dunia madhila wanayopitia

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Natamani ningekuwa muhenga angalau hata kwa siku moja, ili nionje ladha kidogo ya uwezo wa kuona mbali. Iliwezekanaje miaka tele iliyopita, muhenga mmoja akang'amua kuwa, kumpiga chura teke ni kumuongezea hatua? Leo hiki ndicho kinachoendelea kwenye kesi ya Lissu.

Kwamtazamo wa haraka haraka hii kesi imekuwa ikionekana na wengi kama mkakati mahususi wa kumkomoa mwenyekiti wa CHADEMA, bwana Tundu Lissu. Na kwakweli ukiangalia muda aliokaa gerezani, aina ya gereza pamoja na malalamiko ya ukiukwaji wa haki zake ambao amekuwa akiiambia mahakama mara kwa mara; mkakati huu ulionekana kufanikiwa.

Lakini kwa upande mwingine ni kama Mh. Lissu na wenzake wa CHADEMA waligundua hii kesi ni BLESSING IN DISGUISE. Na kwakweli kama ni kuzichanga karata zao, kwenye hili wamefanikiwa sana. Kwa tathmini ya haraka hii kesi sio tu imeongeza umaarufu wa Lissu na chama chake bali pia imewafanya wananchi wawaone kuwa wanaonewa.

Tazama mwenendo wa kesi toka ulipoanza, maswali ya dodoso ya Mh. Lissu kwa mashahidi wa serikali, hoja zake za utetezi pamoja na ushahidi wa mashahidi wake. Kila siku wanaeleza jinsi wanavyoonewa, wanavyofungwa, wanavyoshitakiwa, wanavyotendewa kwenye vituo vya polisi, watu wao waliotekwa na watu wao waliokufa. Tofauti na ambavyo wakiwa mtaani wanafurushwa kwa mabomu, huko mahakamani wanayaeleza haya wakiwa wanalindwa, na hoja zao zikiwa zinaandikwa, na zitadumu milele kama rekodi ya mahakama.

Kiukweli hii kesi sasa ni kama jukwaa la CHADEMA kujijenga kisiasa. Kama serikali itashindwa hii kesi, basi ni rasmi kwa teke lake itakuwa imemuongezea chura hatua.

Mwisho wa yote pole kwa Mh. Lissu, familia yake na CHADEMA kwa kipindi kigumu wanachopitia.
 
Hiyo kesi serekali haiwezi kushindwa maana hukumu haitokani na ushahidi wa kesi, bali maagizo ya serekali. Na uzuri Lisu kawatega viongozi wa serekali nao wawe mashahidi wake. Lakini hii kesi itadhihirisha kuwa mahakama haziko huru, maana wanachoagiza dhidhi ya serekali huwa hakitekelezwi, na ile hadaa kuwa hakuna aliye juu ya sheria inaenda kudhibitika kuwa ni ulaghai wa mchana kweupe.

Subiri uone vioja vya utetezi wa mahakama baada ya mashahidi wa utetezi upande wa Lisu ambao ni wanachama wa cdm kumaliza kutoa utetezi, kama utaona wale wa serekali hata mmoja ataitwa mahakamani. Jaji alianza jana kusema sio lazima mashahidi wawe wengi, na kesi iishe ndani ya siku 14.
 
Kwamtazamo wa haraka haraka hii kesi imekuwa ikionekana na wengi kama mkakati mahususi wa kumkoa mwenyekiti wa CHADEMA, bwana Tundu Lissu. Na kwakweli ukiangalia muda aliokaa gerezani, aina ya gereza pamoja na malalamiko ya ukiukwaji wa haki zake ambao amekuwa akiiambia mahakama mara kwa mara; mkakati huu ulionekana kufanikiwa.

Lakini kwa upande mwingine ni kama Mh. Lissu na wenzake wa CHADEMA waligundua hii kesi ni BLSSING IN DISGUISE. Na kwakweli kama ni kuzichanga karata zao, kwenye hili wamefanikiwa sana. Kwa tathmini ya haraka hii kesi sio tu imeongeza umaarufu wa Lissu na chama chake bali pia imewafanya wananchi wawaone kuwa wanaonewa.

Tazama mwenendo wa kesi toka ulipoanza, maswali ya dodoso ya Mh. Lissu kwa mashahidi wa serikali, hoja zake za utetezi pamoja na ushahidi wa mashahidi wake. Kila siku wanaeleza jinsi wanavyoonewa, wanavyofungwa, wanavyoshitakiwa, wanavyotendewa kwenye vituo vya polisi, watu wao waliotekwa na watu wao waliokufa. Tofauti na ambavyo wakiwa mtaani wanafurushwa kwa mabomu, huko mahakamani wanayaeleza haya wakiwa wanalindwa, na hoja zao zikiwa zinaandikwa, na zitadumu milele kama rekodi ya mahakama.

Kiukweli hii kesi sasa ni kama jukwaa la CHADEMA kujijenga kisiasa. Kama serikali itashindwa hii kesi, basi ni rasmi kwa teke lake itakuwa imemuongezea chura hatua.

Mwisho wa yote pole kwa Mh. Lissu, familia yake na CHADEMA kwa kipindi kigumu wanachopitia.
Serikali imeyataka wenyewe
 
Hiyo kesi serekali haiwezi kushindwa maana hukumu haitokani na ushahidi wa kesi, bali maagizo ya serekali. Na uzuri Lisu kawatega viongozi wa serekali nao wawe mashahidi wake. Lakini hii kesi itadhihirisha kuwa mahakama haziko huru, maana wanachoagiza dhidhi ya serekali huwa hakitekelezwi, na ile hadaa kuwa hakuna aliye juu ya sheria inaenda kudhibitika kuwa ni ulaghai wa mchana kweupe.

Subiri uone vioja vya utetezi wa mahakama baada ya mashahidi wa utetezi upande wa Lisu ambao ni wanachama wa cdm kumaliza kutoa utetezi, kama utaona wale wa serekali hata mmoja ataitwa mahakamani. Jaji alianza jana kusema sio lazima mashahidi wawe wengi, na kesi iishe ndani ya siku 14.
Mahakama kuu ni court of records, maamuzi yake huwa ni sheria. Sio rahisi sana ikafanya maamuzi ambayo hayana msingi wa kisheria.
 
Aliyeshauri kesi hii iendelee nakiri kusema akili zake zilishikwa na Mungu aone inafaa kuendelea, ingeishia kule ilipotoka dunia isingejua haya yanayoingia kwenye rekodi moja kwa moja dunia ikiona.
Mpaka hapa CHADEMA wameonekana washindi, dunia imejua hichi chama kinapitia kwenye vipindi vingi vya maonevu.
 
Waingereza wanamsemo wao; "Dont make Big decision when you're angry"
Upo uwezekano mkubwa maamuzi haya yalifanywa kwa hasira.
 
Hiyo kesi serekali haiwezi kushindwa maana hukumu haitokani na ushahidi wa kesi, bali maagizo ya serekali. Na uzuri Lisu kawatega viongozi wa serekali nao wawe mashahidi wake. Lakini hii kesi itadhihirisha kuwa mahakama haziko huru, maana wanachoagiza dhidhi ya serekali huwa hakitekelezwi, na ile hadaa kuwa hakuna aliye juu ya sheria inaenda kudhibitika kuwa ni ulaghai wa mchana kweupe.

Subiri uone vioja vya utetezi wa mahakama baada ya mashahidi wa utetezi upande wa Lisu ambao ni wanachama wa cdm kumaliza kutoa utetezi, kama utaona wale wa serekali hata mmoja ataitwa mahakamani. Jaji alianza jana kusema sio lazima mashahidi wawe wengi, na kesi iishe ndani ya siku 14.
Ofcourse wameshaanza kutema bungo..
 
Kweli
Natamani ningekuwa muhenga angalau hata kwa siku moja, ili nionje ladha kidogo ya uwezo wa kuona mbali. Iliwezekanaje miaka tele iliyopita, muhenga mmoja akang'amua kuwa, kumpiga chura teke ni kumuongezea hatua? Leo hiki ndicho kinachoendelea kwenye kesi ya Lissu.

Kwamtazamo wa haraka haraka hii kesi imekuwa ikionekana na wengi kama mkakati mahususi wa kumkomoa mwenyekiti wa CHADEMA, bwana Tundu Lissu. Na kwakweli ukiangalia muda aliokaa gerezani, aina ya gereza pamoja na malalamiko ya ukiukwaji wa haki zake ambao amekuwa akiiambia mahakama mara kwa mara; mkakati huu ulionekana kufanikiwa.

Lakini kwa upande mwingine ni kama Mh. Lissu na wenzake wa CHADEMA waligundua hii kesi ni BLESSING IN DISGUISE. Na kwakweli kama ni kuzichanga karata zao, kwenye hili wamefanikiwa sana. Kwa tathmini ya haraka hii kesi sio tu imeongeza umaarufu wa Lissu na chama chake bali pia imewafanya wananchi wawaone kuwa wanaonewa.

Tazama mwenendo wa kesi toka ulipoanza, maswali ya dodoso ya Mh. Lissu kwa mashahidi wa serikali, hoja zake za utetezi pamoja na ushahidi wa mashahidi wake. Kila siku wanaeleza jinsi wanavyoonewa, wanavyofungwa, wanavyoshitakiwa, wanavyotendewa kwenye vituo vya polisi, watu wao waliotekwa na watu wao waliokufa. Tofauti na ambavyo wakiwa mtaani wanafurushwa kwa mabomu, huko mahakamani wanayaeleza haya wakiwa wanalindwa, na hoja zao zikiwa zinaandikwa, na zitadumu milele kama rekodi ya mahakama.

Kiukweli hii kesi sasa ni kama jukwaa la CHADEMA kujijenga kisiasa. Kama serikali itashindwa hii kesi, basi ni rasmi kwa teke lake itakuwa imemuongezea chura hatua.

Mwisho wa yote pole kwa Mh. Lissu, familia yake na CHADEMA kwa kipindi kigumu wanachopitia.
Kabisa MKUU Maana, maandamano hawataki, Sasa hapa ndo serikali unanianika hata kwa muhimbili mwingine, kweli Mungu hadhihakiwi!
 
Waingereza wanamsemo wao; "Dont make Big decision when you're angry"
Upo uwezekano mkubwa maamuzi haya yalifanywa kwa hasira.

..mimi naamini kwa rasilimali watu na fedha walizonazo Ccm wanaweza kushinda uchaguzi bila kuteka, kutesa, na kuuwa, watu wa upinzani.

..hebu fikiria Mama Abduli alichangiwa BILLION 200 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi, halafu anakuja kulalamika eti kuna watu walihongwa waandamane OCT 29. Does that make sense to you?

..Hivi kweli BILLION 200 sizingeweza kutulizs kila mwenye hasira na OCT 29 ikapita salama? Sitetei matumizi ya rushwa ktk siasa, lakini nadhani kwa maafa yaliyotukuta, kuhonga watu kuna afadhali kuliko kuwauwa.

..Again, mimi sijui mshauri wa Ccm ni nani, na kwanini amewashauri watumie violence ktk siasa zao, na kwanini wamekubaliana na ushauri huo. Inanishangaza sana.
 
Natamani ningekuwa muhenga angalau hata kwa siku moja, ili nionje ladha kidogo ya uwezo wa kuona mbali. Iliwezekanaje miaka tele iliyopita, muhenga mmoja akang'amua kuwa, kumpiga chura teke ni kumuongezea hatua? Leo hiki ndicho kinachoendelea kwenye kesi ya Lissu.

Kwamtazamo wa haraka haraka hii kesi imekuwa ikionekana na wengi kama mkakati mahususi wa kumkomoa mwenyekiti wa CHADEMA, bwana Tundu Lissu. Na kwakweli ukiangalia muda aliokaa gerezani, aina ya gereza pamoja na malalamiko ya ukiukwaji wa haki zake ambao amekuwa akiiambia mahakama mara kwa mara; mkakati huu ulionekana kufanikiwa.

Lakini kwa upande mwingine ni kama Mh. Lissu na wenzake wa CHADEMA waligundua hii kesi ni BLESSING IN DISGUISE. Na kwakweli kama ni kuzichanga karata zao, kwenye hili wamefanikiwa sana. Kwa tathmini ya haraka hii kesi sio tu imeongeza umaarufu wa Lissu na chama chake bali pia imewafanya wananchi wawaone kuwa wanaonewa.

Tazama mwenendo wa kesi toka ulipoanza, maswali ya dodoso ya Mh. Lissu kwa mashahidi wa serikali, hoja zake za utetezi pamoja na ushahidi wa mashahidi wake. Kila siku wanaeleza jinsi wanavyoonewa, wanavyofungwa, wanavyoshitakiwa, wanavyotendewa kwenye vituo vya polisi, watu wao waliotekwa na watu wao waliokufa. Tofauti na ambavyo wakiwa mtaani wanafurushwa kwa mabomu, huko mahakamani wanayaeleza haya wakiwa wanalindwa, na hoja zao zikiwa zinaandikwa, na zitadumu milele kama rekodi ya mahakama.

Kiukweli hii kesi sasa ni kama jukwaa la CHADEMA kujijenga kisiasa. Kama serikali itashindwa hii kesi, basi ni rasmi kwa teke lake itakuwa imemuongezea chura hatua.

Mwisho wa yote pole kwa Mh. Lissu, familia yake na CHADEMA kwa kipindi kigumu wanachopitia.
Hebu tuambie ni jipya gani la siasa za Tz ulikuwa hujawahi kusikia bali umeanza kusikia sasa kupitia kesi ya Lissu
 
Nenda kasome ushahidi wa Heche na Golugwa, harafu njoo utuambie ni lini ulisikia wanayoyasema, wakiyasema kwa details kiasi kile.
Hii kesi imetoa forum ya CHADEMA kusimulia ambayo hawajawahi kuyasimulia kwa undani na ufasaha kama wanavyofanya sasa.
 
Mahakama kuu ni court of records, maamuzi yake huwa ni sheria. Sio rahisi sana ikafanya maamuzi ambayo hayana msingi wa kisheria.
Unazungumzia mahakama zilivyokuwa siku za nyuma, kwa sasa mahakama zimepoteza uwezo huo, ndio maana unaona mahakama ikiagiza chochote kifanywe na serekali haifanyi. Inshort utawala wa sheria nchi hii uliharibiwa sana baada ya Magufuli kuingia madarakani. Itachukua muda mrefu utawala wa sheria kurejea, nasikitika kusema ni hadi umwagikaji mkubwa wa damu ufanyike.

Hizi ni athari za kutawaliwa na chama kimoja kwa muda mrefu, halafu kiwe kinafikia ukingoni kutokana na mabadiliko ya kizazi. Ni lazima kitafanya unyama wote hadi kitoke madarakani. Mojawapo ni kunajisi utawala wa sheria.
 
Back
Top Bottom