PreGE2025 Kesi ya Lissu: Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga ashikiliwa uwanja wa Nyerere. Polisi waonekana Kisutu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kumpaisha kimataifa kwa mara ya ngapi tena?
 
Tuko busy kwelikweli.
 
Niko maeneo haya ,kama mnataka tusalimiane ,nipo hapa live bila chenga, lazima muona mwana wa Mungu mh lissu
 
Aibu sana. Nchi inaendeshwa na wacheza vigodoro
 
Picha ya nje madimbwi NI mengi Sana .

Zile fedha za kumpromote janabi zingetumika kukarabati hayo madimbwi
 
Mkuu unakuwa na furaha gani kuandika upumbafu kama huu kwenye kadamnasi?

Kupigwa, kufanywa vilema na kupotezwa kunakokupa wewe ufahari na kujipiga kifua kupongeza unanufaika na nini na uhuni huo unaofanywa na Serikali?

Serikali ina vyombo vya kila aina vya kutenda haki na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wale wote inaoona wanavunja sheria, hilo la kwanza.

La pili, viongozi wote waandamizi kuanzia Rais wanaapa kuilinda Katiba.

Na kuilinda Katiba ni kutawala kwa kufauata sheria, je utekaji na kupoteza watu huko
ni wanafuata sheria?
Kumbe waTz tumegawanyika pakubwa.

Na nchi hii ikiingia kwenye mchafuko kutakuwa na visasi vingi vya umwagaji damu vya kutisha kutokana na chuki zinazojengwa katika jamii kutokana na kauli za watu kama nyie mnaojiona mna haki ya kuchezea maisha ya watu wengine.
 
Kilichonishangaza ni kukukuta jaji mkuu mstaafu wa Kenya naye anazurura kama mwanaharakati wa siasa za nchi ingine. ujaji mkuu kenya ina maana hauna hadhi kiasi kuwa jaji mkuu mstaafu aweza kwenda nchi nyingine kwa mambo ya ndani ya nchi nyingine bila hata kuwa na protocol yeyote ya kualikwa kama VIP na jaji mkuu wa nchi husika na kupokelewa kihadhi.Anawasili nchini kama mkora au kibaka kutoka mitaa ya uswahilini kwenye slums Kibera au gidhurai Kenya? Shame on him
 
Reactions: Tui
Shida ya vyeo vya kupeana kenya kikabila bila kuzingatia sifa.Jaji mkuu mstaafu aliyepewa cheo kihalali sio kikabila hujua vizuri protocol na how to behave

Yeye akisafiri nje kwa shughuli yeyote alitakiwa kuwasiliana na wizara ya mambo ya nchi za nje ya kenya kuwa asafiri Tanzania kisha wizara ya mambo ya nje ya Kenya iwasiliane na Tanzania ili mtu wao apokelewe kama VIP ,apewe hata escort

Shida ya vyeo vya upendeleo Kenya ndiyo hiyo ona sasa majaji wakuu wao wanawasili kinyemela utafikiri wamekimbia kenya kwa kufumaniwa na wake za watu
Ujaji mkuu kenya wameushusha hadhi sana

Mahakama ya kenya iwajadili kwa kweli
They are setting a very bad precedence ya kushusha hadhi za ujaji mkuu mstaafu
 
Siwezi kusoma pumba ndefu hivi
 
Acha uongo
 
ilikuwa sahihi kuwashikilia, hata yule waliyemruhusu wamemhurumia tu. sipendi ccm ila sipendi nchi jirani ijifanye kutusaidia kwenye mapambano, sipendi kenya waingilie siasa za tz. sipendi.
 
ilikuwa sahihi kuwashikilia, hata yule waliyemruhusu wamemhurumia tu. sipendi ccm ila sipendi nchi jirani ijifanye kutusaidia kwenye mapambano, sipendi kenya waingilie siasa za tz. sipendi.
Mkuu wewe si unajulikana?
 
Mkuu wewe si unajulikana?
tupambane tu na ssm ila tusijeamini hata siku moja kwamba kuna mkenya ana mapenzi mema na nchi yetu, kila mtu ana nyumba yake, though nimependa walivyothubutu kuja kwa kuvunja mipaka ya nchi kama tupo federation fulani, ila kuingilia mambo ya ndani hapana, hatuhitaji watupiganie kwa kuja hapa, waongee wakiwa kule kule. wana maslahi gani kwani na sisi? haujiulizi? CJ wawili wa kenya, wameondoka huko, na lazima wameondoka kwa kutaarifua Rais wa nchi yao kwenda nchi nyingine, unajua hao ni waserikali ambao hawatakiwi kuondoka nchini bila ridhaa ya serikali? hivyo ni kama kenya imeingilia siasa za tanzania na nina uhakika hawana mapenzi mema na sisi, wanatamani tuvurugikiwe zaidi ya hapa kwa sababu tumewachapa sana kwenye bandari, sgr na biashara. hakuna kitu wanalala na kuamka wakifikiri kama bandari ya dsm inayowapa competition, kama sgr inayoenda hadi burundi na mwanza na rwanda ili kupunguza matumizi ya landlocked countries kwa mombasa port. hivi mnawajua wakenay au mnawasikia? KWAMBA wanatutakia mema wamekuja kutupigania? mi hapana aisee, tutajipigania wenyewe na serikali imewaheshimu sana walitakiwa wadhalilishwe kabisa kwa sababu siamin kama wana nia njema ya kuja kwenye hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…