Kesi ya Lissu | Shahidi wa siri (P5): Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha, uchaguzi mkuu hautafanyika

Kesi ya Lissu | Shahidi wa siri (P5): Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha, uchaguzi mkuu hautafanyika

kibaraka muhaini nywele zimeanza kuchange rangi, nuru na weight vimepungua,

hao walokole feki wanafiki wanafanyaje hapo mahakamani? wanaleta drama za kunena kwa lugha hadi mahakamani? :1Head:
We ni *****.
 
Kwa kweli nimeshangaa pia, hivi hata hao wanaokaa kupanga njama za mashahidi fake hawako timamu kichwani??
Kwa ushahidi huu, hata mie sina taaluma ya sheria, ila hapa najua ni uongoo tena wa wazi kabisaa.
Pesa wanazotumia hapo na muda wangeenda kuweka barabara au kujenga madarasa ,Maabara mashuleni.Kuliko hicho wanachofanya..Mimi...shahidi wa Ubungo kibangu😀😀😀Galaxy Sony
 
Pesa wanazotumia hapo na muda wangeenda kuweka barabara au kujenga madarasa ,Maabara mashuleni.Kuliko hicho wanachofanya..Mimi...shahidi wa Ubungo kibangu😀😀😀Galaxy Sony
😂😂😂😂😂😂 hii case ina futuhi kuliko. Lol
 
😂😂😂😂😂😂 hii case ina futuhi kuliko. Lol
Vuta subira kidogo, "futuhi" halisi unaweza kukutana nayo baada ya majaji hao kutoa uamzi wa kipekee sana licha ya hizi futuhi nyembamba tunazozishhudia hivi sasa.

Nchi yetu imekuwa na sifa za kipekee sana miaka hii. Unalofikiri haliwezekani, linafanywa kuwezekana kivyepesi kabisa!
 
Kesi ya kipumbavu Kuwahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru, ya pili ni ile ya kufungiwa chadema mwaka jana kufanya siasa mpaka hukumu ya kesi fake itolewe, zote chini ya Raisi fake la hovyo kutokea tangu uhuru
 
😂😂😂😂😂😂 hii case ina futuhi kuliko. Lol
Wameamua ,watu waseme iwe nongwa.Akili zetu tusamehewe tu..dereva boda boda wapo wengi ni huyo tu kapata ujasiri?Mara muuza chips...
 
Wakichezea hukumu ya Lisu nadhani itakua kama ilivyotokea SA kifo cha Stive Biko 1976 ndio ilikua chavu ya kuwaondoa makaburu madarakani na walifanikiwa baadae..
 
Hizi kesi zinaendeshwa kwa gharama kubwa sana baadae wanaomba China watusaidie kujenga miundo mbinu. Tanzania ni nchi nzuri lakini wahuni wanaturudisha nyuma sana
 
16 February 2026l

EPISODE 22: TUNDU LISSU AMBANA SHAHIDI FUNDI UMEME HADI AMEKIRI POLISI WALIDANGANYA "JAJI ASHANGAA"​

Leo Tarehe 16 February 2026

View: https://m.youtube.com/watch?v=LGvwovxjYWM

KESI YA UHAINI INAYOMKABILI TUNDU LISSU Kesi ya uhaini Na. 19605/2025
kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mh Tundu Antipas Lissu imeendelea Leo mahakama kuu masjala ndogo ya Dar es salaam ambapo shahidi wa 7 ( pw7 ) wa jamhuri anaetambulika kama p7 ametoa ushahidi wake akiwa kwenye kizimba kama shahidi WA Siri na kufanyiwa uchunguzi kama shahidi WA Siri na kufanyiwa kazi ngumu
 
16 February 2026
Mahakama Kuu ya Tanzania
Kivukoni Front
Dar es Salaam

EPISODE 23: TUNDU LISSU AKUTANA NA MUUZAJI WA MATUNDA MWENYE KICHWA KIKUBWA KWA MARA YA KWANZA

KESI YA UHAINI INAYOMKABILI TUNDU LISSU Kesi ya uhaini Na. 19605/2025

View: https://m.youtube.com/watch?v=jBeq1igX_SM
Leo, Februari 16, 2026, tulikuwa na Mashahidi wawili wa Siri, P2 na P8, ambaye ni shahidi wa nane wa Jamhuri na kazi yake ni kuuza matunda, ambapo ametoa ushahidi wake na kuhojiwa na kesi imeahirishwa hadi kesho, Februari 17, 2026, ambapo upande wa Jamhuri ulikosa shahidi mwingine
 
View attachment 3544959
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mwanza, imetoa uamuzi wa kihistoria kwa kuzuia upande wa Jamhuri kutumia mashahidi wa kificho au siri katika kesi zote za jinai, ikitangaza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha katiba ya nchi.

Jopo la Majaji watatu- Jaji Fahamu Mtulya, Jaji K.S Kamana na Jaji W.M Chuma leo limebatilisha Kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) baada ya kubaini kuwa kifungu hicho kinampa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) mamlaka makubwa na ya kipekee ya kuomba ulinzi wa shahidi bila kumpa mshtakiwa haki sawa ya kuhoji, jambo linalokiuka haki ya kusikilizwa kwa pande zote mbili.

Mahakama imetoa muda wa miezi 12 kwa Serikali na AG kufanya marekebisho ya sheria hiyo

Kundi la mawakili 13, likiongozwa na Wakili Mwandamizi Constantine Mutalemwa, liliwakilisha mleta maombi, Wakili Godfrey Mjuni Martin Basasingohe, katika kesi ya kikatiba namba 22482/2025 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na DPP.

Miongoni mwa hoja zilizowasilishwa ni kuwa sheria hiyo inawaficha mashahidi badala ya kuwalinda, hali inayotoa mwanya kwa mtu mmoja kutoa ushahidi mara nyingi kwa kutumia majina tofauti.

16 February 2026
Ufafanuzi mzito watolewa kuhusu maana na mguso wa hukumu hii ya kesi ya kikatiba iliyotolewa uamuzi na Mahakama Kuu, na utaathiri zipi kesi zingine zinazoendelea zenye mashahidi fiche:
Hukumu ya kesi ya mleta maombi Wakili Godfrey Mjuni Martin Basasingohe, katika kesi ya kikatiba namba 22482/2025 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na DPP.

LISSU ASHINDA KESI YA UHAINI?, MASHAHIDI WA SIRI WAZUA KIZAA ZAA, WAKILI MAHINYILA ATEMA CHECHE​


View: https://m.youtube.com/watch?v=j7DlK8Y_CnM
 
Vuta subira kidogo, "futuhi" halisi unaweza kukutana nayo baada ya majaji hao kutoa uamzi wa kipekee sana licha ya hizi futuhi nyembamba tunazozishhudia hivi sasa.

Nchi yetu imekuwa na sifa za kipekee sana miaka hii. Unalofikiri haliwezekani, linafanywa kuwezekana kivyepesi kabisa!
Makubwaaaa! 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom