Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, linatarajiwa kuendelea kusikilizwa leo, Jumatatu, tarehe 10 Agosti 2026, kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Kesi hiyo inasikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Dar es Salaam, na imepangwa kuendelea kusikilizwa mfululizo hadi tarehe 7 Septemba 2026.
Mshtakiwa huyo amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu alipokamatwa na kushtakiwa mwezi Aprili 2025. Hata hivyo, kesi ya msingi ilisimama ili kupisha rufaa iliyowasilishwa na Jamhuri kuhusu kukataliwa kwa ombi la kuongeza ushahidi. Lissu alishinda rufaa hiyo, huku Mahakama ikikubaliana na uamuzi wa kutokubali kuongezwa kwa ushahidi.
Lissu: Nia ya Jamhuri kufungua rufaa ilikuwa kupoteza muda ili niendelee kukaa gerezani
Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na shauri la uhaini, amesema kuwa nia ya Jamhuri kufungua rufaa ilikuwa ni mkakati wa kupoteza muda ili kumfanya aendelee kuwepo gerezani.
Amesema suala hilo alilieleza Februari 24, 2026, akidai kuwa tangu ilipofunguliwa rufaa hiyo, kesi inayoendelea kusikilizwa leo ilisimama bila kuendelea kwa siku 166.
Kwa upande wake, Jamhuri imejibu hoja hiyo ikisema kuwa lengo la kukata rufaa halikuwa kama alivyoeleza mshtakiwa.