GE2025 Kesi ya Lissu yaahirishwa hadi Novemba 3, 2025, shahidi wa nne wa Jamhuri ‘akwama mkoani’

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu imehairishwa leo, Ijumaa Oktoba 24.2025 hadi Novemba 03.2025

Kesi hiyo imehairishwa kufuatia ombi la Jamhuri lililowasilishwa Mahakamani hapo likieleza kuwa, leo ilitakiwa wamlete shahidi wa Nne (4) aanze kutoa ushahidi wake baada ya yule wa Tatu (3) kukamilisha hapo jana, lakini wameshindwa kuleta shahidi hii leo kutokana na kwamba wameshindwa kumsafirisha kwa wakati na mashahidi wao hitajika nje ya Dar es Salaam (wapo mikoani)

Lissu alionekana kupinga vikali hoja hiyo akidai kwamba hiyo ni janjajanja ya Jamhuri kutaka aendelee kukaa gerezani hadi Uchaguzi Mkuu umalizike hivyo kuiomba Mahakama kuilazimisha Jamhuri kuendelea na kesi leo au Mahakama impatie dhamana aende nyumbani

Katika uamuzi wake, Mahakama kupitia jopo la Mawakili watatu (3) wanaosikiliza kesi hiyo wamesema kesi inayomkabili haina dhamana, na kwamba suala la kuomba hairisho kutokana na changamoto la mashahidi linakubalika kisheria na ikizingatiwa kuwa tangu kesi hiyo ianze hakuna siku ambayo Jamhuri imeshindwa kumleta shahidi

Hivyo kesi hiyo imehairishwa sasa hadi Novemba 03.2025 ambapo shahidi wa Nne (4) wa Jamhuri ataanza kutoa ushahidi wake.

Soma Pia: Kesi ya Lissu kuendelea leo Oktoba 24, shahidi wa nne wa jamhuri asubiriwa kwa hamu
1761297500383.png
 
Kesi ya Lissu ni kama campaign kabisa, yaani baada ya kumaliza kesi anakua kama kashinda Uchaguzi na kamfanya Kizimkazi ushungi kuonekana kama Kinyago kabisa kilichokalia kiti cha Rais
 
baada ya yule king'ang'anizi kuapishwa, ndiyo atolewe.
Mkuu Shemeji Tate Tate Mkuu , ukae ukijua, huyo unayemuita king'ang'anizi, ndie chaguo la Mungu kwa Tanzania, maana ni Mungu pekee ndiye huweka tawala zote za mataifa. Thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

P
 
They know what they are doing. Kiukweli Mama samia ndiyo atabakia kwenye historia kama Rais aliyewahi kuchukiwa na wananchi walio wengi tangu nchi hii ipate Uhuru. Na sababu ziko wazi kabisa;
1. Kuuza uza hovyo raslimali za nchi kwa Waarabu.
2. Kuruhusu kundi la Wahuni kuwa watu wake wa karibu.
3. Kuwaonea wapinzani wa CHADEMA kwa kuwafunga hovyo, kuwazuia bila ya sababu kusafiri nje ya nchi, kuwateka na kuwaua, nk
4. Kuruhusu vitendo vya utekaji na mauaji kutamalaki nchini.
5. Kuiendesha nchi kama mali yake yeye, familia yake na marafiki zake.
6. Kutumia fedha za Tanganyika kujenga miundombinu ya Zanzibar.
7. Kuwabeba ndugu zake Wazanzibari kwenye nafasi nyingi za madaraka na zile nyeti, nchini.
8.
9.
10.
 
Hofu tu hao vilaza mafundi wa viyoyozi wanataka igizo la uchafuzi lipite waje waseme hawana ushahidi wa kutosha na hawana nia ya kuendelea na kesi.
 
Hakuna kazi rahisi kama uhakimu.
Unachotakiwa kua nacho ni simu tu. Mavazi utayakuta kule.
Ukishasikiliza pande zote ahirisha kesi, fungua simu yako yenye full charge then subiri maelekezo kutoka juu.
 
Mkuu Shemeji Tate Tate Mkuu , ukae ukijua, huyo unayemuita king'ang'anizi, ndie chaguo la Mungu kwa Tanzania, maana ni Mungu pekee ndiye huweka tawala zote za mataifa. Thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

P
Tukubali Comrade. Na binadamu wenye nguvu ya kifedha na maarifa; pia huwa wanawaweka watu wao kuongoza kwa maslahi yao binafsi. Na hiki ndicho kitu tunacho kishuhudia nchini.

Hapa sidhani kama Mungu anahusika. Ingekuwa ni Lissu, ningeamini. Ila kwa hizi nguvu kubwa zinazotumika, halafu tunasema ni Mungu! Hata siamini.

Lissu alijaza halaiki kwenye mikutano yake ya hadhara pasipo kutumia wasanii, hakutisha wakuu wa idara kulazimisha watumishi kuhudhuria mikutano yake ya hadhara! Hakuzunguka na wapambe kwenye mabasi nchi nzima! Hakusafirisha watu kwenue malori kutoka maeneo ya pembezoni kuja kujaza mikutano yake! Hakujaza mabango nchi nzima kujitangaza! Hakutoa rushwa kwa wanahabari ili wampambe kwenye vyombo vyao, nk.

Nadhani umenielewa. Natambua fika wewe ni Mwanahabari, mwanasheria, lakini pia ni mchambuzi mahiri wa masuala ya kisiasa nchini. Hii nguvu kubwa ya fedha na vitisho ina malipo yake siku zijazo.
 
Back
Top Bottom