Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda atorokee vijinchi visivyoeleweka.... akienda nchi "zinazofahamika" ambapo tuna makubaliano nazo kurudishiana wahalifu...atarudishwa tu!Labda utoro huu uwe na baraka za wenye mamlaka.
Tatizo hapa siyo serikali ni mahakama.serikali ya wasanii hufanya mambo ya kisaniii!!
Hawezi kutoroka ki_Kasusura. Huyu ni mtu mwenye akili zaidi. Anajua alichokifanya na anachokifanya.
Nilisema pale tu alipopewa dhamana kuwa sinema ndio inaanza. Sasa hizi ni flashbacks tu.
Naamini huyu jamaa, alifanya kila aliloweza kupewa dhamana akijua kuwa baada ya muda mfupi tangu atoke, atakuwa hayupo tena mahali anapoweza kurudi mahakamani. Kupewa kwake dhamana kunatia hofu.
1. Fikiria jinsi Mawaziri wa zamani walivyohangaika kuomba dhamana na kupewa baada ya kutimiza masharti kikamilifu. Huyu ni nani alieweza kupewa dhamana bila hata kukamilisha masharti? Lazima kuna mkono mkubwa ambao hata wewe huwezi kuushika. Inawezekana kabisa kuwa hata Hakimu hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali kuitoa dhamana tu. Juilize, nguvu hizo ni nguvu gani?
2. Alipotoka tu, alionyesha kuwahi sana kuondoka. Ikiwa na maana kuwa alikuwa anachelewa mahali. Si ajabu alikuwa anawahi ndege hata ya kukodi kumtoa nje ya nchi. Hakuonyesha kuwa na wasiwasi zaidi ya kuonyesha kuwa alikuwa anatakiwa kufuata steps bila kuchelewa. Kama vile alikuwa anaongozwa.
3. Jamaa huyu kutokana na mengi yanayosemwa kuhusiana na maisha yake binafsi, sidhani kama anajali nini kitakachomtokea baadae. Maana hiyo baadae haioni. Anaona ni heri kuishi maisha bora kwa kipindi kilichobaki kuliko kumalizia maisha yake yote mahabusu au gerezani. Amepata opportunity ya kumalizia maisha yake vizuri zaidi. Mahakama imemsaidia kufanikiwa.
4. Maoni yangu: Huyu jamaa akiona hawezi kuishi kwa amani, anaweza kujiua. Ila pia kwa kuwa ana siri kubwa ya watu walioshiriki na kufaidika na pesa hizo, anaweza pia kuuawa ili kulinda maslahi ya watu wanaoofia siri zao kuvuja. Ukweli ni kwamba, kwa cheo chake asingeweza kuiba/kufanya udanganyifu wa fedha zote hizo bila kushirikisha vigogo wakubwa sana serikalini na BoT.
Kamateni Pop-Corn, sinema inaendelea.
Ndo kipi hiki? na kama mtu ni m/ke aende kipi? just curious?wanatupeleka "CHOO CHA KIKE" kwa madai kuwa "ACHA SHERIA IFATE MKONDO WAKE"
Huko tulishatoka siku nyingi. Sheria hiyo ni kinyume cha haki za binaadamu. Hata fisadi ni binaadamu ana haki zake. Ndio maana hata adhabu ya kunyongwa ni barbarick. US wana adhabu ya kifo kwa electric chair ama leather dose ili mtu asife kwa mateso na uchungu kama kunyonga kwa kamba.UTATATIBU WA KUWEKWA KIZUIZINI URUDISHWE!
THIS will be a big blow to FISADIZ.....!
Watu mna wasiwasi sana. Liyumba haendi kokote na kizimbani atasimama si masaa mengi yajayo. Kumekuwepo na massive manhunt na vyanzo vya uhakika vinadokeza jamaa atakuwa amedakwa usiku huu kama mtego walioutega utafanikiwa kwani intel yote ilikuwa inaonesha jamaa yupo bado Dar! So.. subirini mahakamani leo... maana wakimkosa leo basi ndiyo watafute shimo kama la Sadam au waende kwenye mapango ya Tora Bora!
Ndo kipi hiki? na kama mtu ni m/ke aende kipi? just curious?
Duh!!! Kama ni kweli hii basi mafisadi wote warudishwe rumande haraka sana wakiwamo wale wa EPA na akina Mramba.