Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
sasa tutanufaikaje na huo utaratibu, maana bado serikali itaingia gharama kutunza hizo fisadi,ingawa bado ni wazo zuri.
 
Labda atorokee vijinchi visivyoeleweka.... akienda nchi "zinazofahamika" ambapo tuna makubaliano nazo kurudishiana wahalifu...atarudishwa tu!Labda utoro huu uwe na baraka za wenye mamlaka.

Hawezi kutoroka ki_Kasusura. Huyu ni mtu mwenye akili zaidi. Anajua alichokifanya na anachokifanya.

Nilisema pale tu alipopewa dhamana kuwa sinema ndio inaanza. Sasa hizi ni flashbacks tu.

Naamini huyu jamaa, alifanya kila aliloweza kupewa dhamana akijua kuwa baada ya muda mfupi tangu atoke, atakuwa hayupo tena mahali anapoweza kurudi mahakamani. Kupewa kwake dhamana kunatia hofu.

1. Fikiria jinsi Mawaziri wa zamani walivyohangaika kuomba dhamana na kupewa baada ya kutimiza masharti kikamilifu. Huyu ni nani alieweza kupewa dhamana bila hata kukamilisha masharti? Lazima kuna mkono mkubwa ambao hata wewe huwezi kuushika. Inawezekana kabisa kuwa hata Hakimu hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali kuitoa dhamana tu. Juilize, nguvu hizo ni nguvu gani?

2. Alipotoka tu, alionyesha kuwahi sana kuondoka. Ikiwa na maana kuwa alikuwa anachelewa mahali. Si ajabu alikuwa anawahi ndege hata ya kukodi kumtoa nje ya nchi. Hakuonyesha kuwa na wasiwasi zaidi ya kuonyesha kuwa alikuwa anatakiwa kufuata steps bila kuchelewa. Kama vile alikuwa anaongozwa.

3. Jamaa huyu kutokana na mengi yanayosemwa kuhusiana na maisha yake binafsi, sidhani kama anajali nini kitakachomtokea baadae. Maana hiyo baadae haioni. Anaona ni heri kuishi maisha bora kwa kipindi kilichobaki kuliko kumalizia maisha yake yote mahabusu au gerezani. Amepata opportunity ya kumalizia maisha yake vizuri zaidi. Mahakama imemsaidia kufanikiwa.

4. Maoni yangu: Huyu jamaa akiona hawezi kuishi kwa amani, anaweza kujiua. Ila pia kwa kuwa ana siri kubwa ya watu walioshiriki na kufaidika na pesa hizo, anaweza pia kuuawa ili kulinda maslahi ya watu wanaoofia siri zao kuvuja. Ukweli ni kwamba, kwa cheo chake asingeweza kuiba/kufanya udanganyifu wa fedha zote hizo bila kushirikisha vigogo wakubwa sana serikalini na BoT.

Kamateni Pop-Corn, sinema inaendelea.
 
serikali ya wasanii hufanya mambo ya kisaniii!!
Tatizo hapa siyo serikali ni mahakama.
Je, wajuzi wa masuala ya mahakama,nini hatma ya hakimu aliyempa dhamana?
Kwa uelewa mdogo ni kuwa hakimu hawezi kushitakiwa zaidi ya kuondolewa katika wadhifa wake? wajuzi tunaomba ufafanuzi.
 
Hapa ni patamu zaidi.
1. Hakimu aliruhusu jamaa atoke kwa dhamana ndogo ilihali Mahakama Kuu ilikataa kumpunguzia kiasi cha dhamana. Ni nini hatma ya Hakimu?

2. Aliwasilisha pasi ambayo muda wake umepikwisha. Wazee wa UWT na Uhamiaji mnasemaje kama pasi hiyo imekwisha mtamzuiaje border.

3. Heri LM akamilishe mchakato wa vitambulisho vya uraia ili tuondokane na mambo haya
 
Hawezi kutoroka ki_Kasusura. Huyu ni mtu mwenye akili zaidi. Anajua alichokifanya na anachokifanya.

Nilisema pale tu alipopewa dhamana kuwa sinema ndio inaanza. Sasa hizi ni flashbacks tu.

Naamini huyu jamaa, alifanya kila aliloweza kupewa dhamana akijua kuwa baada ya muda mfupi tangu atoke, atakuwa hayupo tena mahali anapoweza kurudi mahakamani. Kupewa kwake dhamana kunatia hofu.

1. Fikiria jinsi Mawaziri wa zamani walivyohangaika kuomba dhamana na kupewa baada ya kutimiza masharti kikamilifu. Huyu ni nani alieweza kupewa dhamana bila hata kukamilisha masharti? Lazima kuna mkono mkubwa ambao hata wewe huwezi kuushika. Inawezekana kabisa kuwa hata Hakimu hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali kuitoa dhamana tu. Juilize, nguvu hizo ni nguvu gani?

2. Alipotoka tu, alionyesha kuwahi sana kuondoka. Ikiwa na maana kuwa alikuwa anachelewa mahali. Si ajabu alikuwa anawahi ndege hata ya kukodi kumtoa nje ya nchi. Hakuonyesha kuwa na wasiwasi zaidi ya kuonyesha kuwa alikuwa anatakiwa kufuata steps bila kuchelewa. Kama vile alikuwa anaongozwa.

3. Jamaa huyu kutokana na mengi yanayosemwa kuhusiana na maisha yake binafsi, sidhani kama anajali nini kitakachomtokea baadae. Maana hiyo baadae haioni. Anaona ni heri kuishi maisha bora kwa kipindi kilichobaki kuliko kumalizia maisha yake yote mahabusu au gerezani. Amepata opportunity ya kumalizia maisha yake vizuri zaidi. Mahakama imemsaidia kufanikiwa.

4. Maoni yangu: Huyu jamaa akiona hawezi kuishi kwa amani, anaweza kujiua. Ila pia kwa kuwa ana siri kubwa ya watu walioshiriki na kufaidika na pesa hizo, anaweza pia kuuawa ili kulinda maslahi ya watu wanaoofia siri zao kuvuja. Ukweli ni kwamba, kwa cheo chake asingeweza kuiba/kufanya udanganyifu wa fedha zote hizo bila kushirikisha vigogo wakubwa sana serikalini na BoT.

Kamateni Pop-Corn, sinema inaendelea.

Mkuu Recta,

Nimependa sana mchango wako.......Binafsi I was thinking in those lines!

Kwa sababu haka ni kamovie fulani hivi, wananchi wengi tungekuwa na mwamko wa kutosha kuhusu maslahi ya taifa hili, the only solution ilikuwa ni kuandamana kuwashinikiza washika dola kujiuzulu mara moja! Tukisema tumtolea macho hakimu (aliyempa dhamana) inawezekana tukawa tunamwonea wakati nyuma yake kuna WINGU zito la shinikizo kufanya maamuzi hayo.......! Hapa tusipoangalia tutapoteza FOCUS kama tutaishupalia sana mahakama bila kuangalia WHO is really behind this MOVIE.
 
Jamaa atakua yuko na Balali sasa ivi...poleni sana watanzania,bao jingine la kisigino ilo tumeshapigwa
 
Hii ni kweli au macho...?

Currently Active Users Viewing This Thread: 1700 (420 members and 1280 guests)
Mkaa Mweupe, Aljuniortz, asheri, Bazobonankira, bob, Bonnie1974, Bwana, Byabato Kilama, cesc, Chakaza, Damky, don, Godluck, Helly, Heri, Jeni, kidumeso, lingusenguse, Maane, Madaha, Maisha, Mchana, Mfuatiliaji, moelex23, mwalimu, Mzalendohalisi, Mzuzu, Ndahani, Next Level, njilembera, Njimba Nsalilwe, Ochu, Opaque, Pipiro, Recta, sella, tk, Tshala, tzengo, Utamaduni, WomenofSubstanc ...

Watanzania ndio mawazo yetu...
 
Watu mna wasiwasi sana. Liyumba haendi kokote na kizimbani atasimama si masaa mengi yajayo. Kumekuwepo na massive manhunt na vyanzo vya uhakika vinadokeza jamaa atakuwa amedakwa usiku huu kama mtego walioutega utafanikiwa kwani intel yote ilikuwa inaonesha jamaa yupo bado Dar! So.. subirini mahakamani leo... maana wakimkosa leo basi ndiyo watafute shimo kama la Sadam au waende kwenye mapango ya Tora Bora!
 
hayo makubwa. habari nilizonazo ni kuwa alitoa passport iliyokwisha mda so that abaki na mpya atimue zake na hata mali alizotoa tu ilikuwa na thamani ya milion 800 badala ya bilion 50 kama ilivyoamuriwa na mahakama. Nafikiri ni mchezo mchafu ulitendeka.

he may run but he cant hide.
 
UTATATIBU WA KUWEKWA KIZUIZINI URUDISHWE!
THIS will be a big blow to FISADIZ.....!
Huko tulishatoka siku nyingi. Sheria hiyo ni kinyume cha haki za binaadamu. Hata fisadi ni binaadamu ana haki zake. Ndio maana hata adhabu ya kunyongwa ni barbarick. US wana adhabu ya kifo kwa electric chair ama leather dose ili mtu asife kwa mateso na uchungu kama kunyonga kwa kamba.
 
Mi nilishangaa kuona hadi leo hajakimbia mtu,nikaona labda wamesingiziwa ,eti jamani umeshakwapua mabilioni halafu unababaika na kazi za uwaziri ,Chenge mmoja wapo ,unaiibia serikali hii halafu unachemka zako ,na kusubiri mkono mrefu wa serikali.
 
Watu mna wasiwasi sana. Liyumba haendi kokote na kizimbani atasimama si masaa mengi yajayo. Kumekuwepo na massive manhunt na vyanzo vya uhakika vinadokeza jamaa atakuwa amedakwa usiku huu kama mtego walioutega utafanikiwa kwani intel yote ilikuwa inaonesha jamaa yupo bado Dar! So.. subirini mahakamani leo... maana wakimkosa leo basi ndiyo watafute shimo kama la Sadam au waende kwenye mapango ya Tora Bora!

Mkuu MMM,

Kwani wewe huo wasiwasi hukuwa nao kabla ya hizo fununu?

Mkuu wasiwasi ni lazima, think about;

1. Tshs 221 bil?????

2. People behind Tshs 221 bil .......naamini si watu wawili tu ndio waliohusika!

3. What happened to Balali ......linaweza tokea na kwa huyu!

So mkubwa lazima tukumbwe na wasiwasi, coz tunataka tujue mwisho wa hili picha itakuwaje.....then we pick from there!
 
Parapanda italia parapanda, parapanda italia parapanda. Parapanda eh, parapanda italia parapanda. Tutamwona AL mawinguni, akienda kumlaki bwana Yesu!!!!

Kibwagizo hicho jamani. Hivi hizi sinema sijui za Rambo au zile za Angela Mao??? Siku zile ukisikia kijijini kuna sinema ya Rambo na Angela Mao inakuja kuonyeshwa, watoto hawalali!!!Tumefika mwisho wa kudanganywa kama watoto. We need a few heros to raise up and act???!! Machukizo yamefika kwenye koromeo sasa!!! This was a planned saga!!!! Na hakimu alifahamu alichokuwa anafanya!!! For sure hakimu atalindwa!!!!

Naamini Hans Kitine alikuwa right japo wengine kama kawaida wamemponda. I am saying he was right to comment that way!!!.....Hajawahi kuona uongozi wa aina hiii.......hakuna maadili.........kuangalia maslahi binafsi.....

Zile bill Al hakula peke yake. Zina mtandao!!! Je ni akina nani hao??? Sikubaliani kuwa eti ni Balali peke yake na AL walikula bill zote zile??? Who are the other ghost ni this saga?????!!!! Leteni data mnaofahamu???!!!!

Je tufanye privatisation ya Bank of Tanzania???!!!! Ni taasisi ya juu ya serikali ambayo it is a failure!!!??? Hata sasa hivi I doubt if it is clean to serve our country. Au waajiri wafanyakazi wapya nini???? BOT inahitaji reforms ya wafanyakazi kuanzia sweeper hadi ngazi ya juu kabisa. Sina imani na ile Benki ya nchi.

There are so many Liyumbas in that Bank, so many EPA beneficiaries and are still on their chairs, so many fake employees especially those who were behind the back of Balali na Liyumba, so many evils deals inside the bank!!!! I say the taasisi is dead!!!

Cha kushangaza serikali na machinery zake babdo halijaliona hili, na hii ni kwa sababu nchi sasa kila mtu na maslahi binafsi na si kujali maisha ya wengi. Je hapa napo tutampinga Kitine?? The man was right. I admire him for speaking publicly on this.
 
Wengine humu JF mnaonekana kuujadili UHURU wa MAHAKAMA! Yule Mama hakimu pale kafanya kazi yake vizuri tu kumwachia kwa dhamana Liyumba. Anajua Liyumba kagawa kiasi gani kwa akina mama wenzake lile fungu lake?!
 
hivi kulikuwa na uharaka gani wa kumpa dhamana wakati ilikuwa wazi kabisa mbele ya mahakama kwamba hati zile zilizowasilishwa ilikuwa na utata?? ile kauli mi sikuipenda kabisa kwamba huyu mtu aachiwe huku mahakama ikiendelea kujiridhisha na hati zilizotolewa, kwanini wasingejiridhisha kwanza kisha ndio atolewe??? kama sikosei nimesoma kuwa hata hati ya kusafiria aliyoitoa ilikuwa imeisha muda wake,kama ninavyoijua bongo, inawezekana kabisa kwa mtu wa namna yake kuwa alikuwa na hati nyingine ambayo ni valid,ambayo anaweza kuitumia kusafiria, hizi mahakama zetu zinafanya mchezo wa kuigiza hapa. lazima kuna kitu.
 
Ndo kipi hiki? na kama mtu ni m/ke aende kipi? just curious?

Ni figure of speech, it has nothing to do with the toilet madam, sina uhakika kiswahili labda ni nahau mfano amevaa miwani = amelewa. with no intention to humiliate women.
 
Duh!!! Kama ni kweli hii basi mafisadi wote warudishwe rumande haraka sana wakiwamo wale wa EPA na akina Mramba.

U should think b4 u write. wewe ur very small minded. kama ni kutoroka hawo wengine si wangesha toroka..?
again.. think twice b4 u write something as idiotic as this.
 
hapa kwa kweli kinachotuua ni haya mambo ya mtandao yaani kwa kifupi ni CCM, ikifikia point lazima tukubali ukweli, maana hata viongozi wa zamani wa CCM wanalijua hili.

ukiangalia network yote ya mafisadi ni moja na group sio kubwa sana kwa sababu utakuta mtu mmoja amejifisadifisha almost katika kila mwanya wa kuchota fedha.

hii issue labda sisi tunaijadili juu juu tu lakini hatujuhi ni nani alikuwa nyuma ya Liyumba at el, kwa kuepusha usalama wa vigogo ilibidi lazima Liyumba apotee.

hebu angalia kundi la pili la mafisadi ambao hawamo kwenye huu mtandao ambao upo madarakani, mramba na wenzie wamepewa masharti magumu sana hata kutoka nje ya mji lakini fedha walizokwiba azilingani kabisa na ufisadi wa Liyumba, iweje Liyumba apewe masharti Raisi sana pamoja na kuwakilisha vielelezo fake kabisa na vikakubaliwa.

huyo mweshimiwa Khadija tutamjadili bure hapa, lakini hatujuhi alipata msg kutoka kwa nani , labda JK au EL, au RA na wala hatujuhi alitishiwa maisha kwa kiwango gani.

ili tuwe na amani na JK ni lazima atoe kauli ya uhakika na msimamo wake thabiti na sio kutuonyesha kiini macho tu cha kutafutia muhula wa pili wa kuchota fedhwa
 
yaani nyie mnashangaa! this is Tz, bila ufisadi au kuhonga utaishi? 1st of all, is every1 blind? kwanini msiwajie juu watu hao ambao wanoendecha yaho mashtaka n ask them imekuaje huyu mtu katoka kwa kiasi alichotoa navinginevyo. Hamuoni kama kuna some coruptions goin on there? i bet with my life wamehongwa. As i say this is TZ bwana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom