Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Wanajamvi, hii taarifa ya kuroka ni jana kwa maana ndipo aliripotiwa kuwa ametoroka. Kwa walio mjini ina maana hadi muda huu naandika [1517hrs] bado hakuna taarifa mpya kama amekamatwa au la?
 
Kwa ufupi, kala chochoro. Hakimu aliyelegeza masharti ya dhamana vipi?
Sio kuwa alijua hili?
Hapa anatakiwa bwana Albert Mnali toka Bukoba.
 
Nafikiri ni mchezo kati ya BOT na Mahakama.
Inasemekana wadhamini wawili ni wafanyakazi wa BOT.
Barua za dhamana zilitolewa na BOT kama ni kweli.
Mtuhumiwa amefanya madudu BOT,then BOT wanamdhamini. 'Unethical in every aspect'
Inamaanisha walikubaliana na hakimu namna ya kulicheza movie,ikitiliwa maanani hakimu hawezi kufanywa lolote kisheria hata angetoa maamuzi mabovu namna gani zaidi ya kupoteza ajira. hakuna issue ya reasonable man dhidi ya hakimu.
Hivyo wakaamua kumtoa na kumpa muda wa kutoroka then watoe warrant ya kurejesha mahakamani ili kufuta soo la dhamana kiduchu, then move inaishia kwa mtuhumiwa kuyeyuka kwenye thin air .....

Good thinking kwa timu iliyobuni movie hii, labda itasaidia kuwaamsha watanzania wajue MH.Sitta aliposema kuhusu mahakama alimaanisha nini...
 
Taarifa za uhakika za hivi punde kutoka mahakamani ni kuwa AL hakufika:

Uamuzi ni kama ifuatavyo
1. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 24 ambayo ndiyo ilipangwa awali kwa yeye kufika mahakamani
2. Hati ya kukamatwa wadhamini wake imefutwa. Hivyo watatakiwa tu kuripoti hapa mahakamani siku ya tarehe 24. Iwapo AL hatafika siku hiyo ndipo wanaweza kukamatwa. wameachiwa na wamekwenda makwao.

Habari ndo hiyo
 
Kila mtu anaamini jamaa katoroka, hivi haiwezekani kuwa jamaa kauawa?

Kwa Tanzania lolote linawezekana.
 
Personally siamini kama kauwawa au katoroka. The fact could be kuwa kaamua tu kujichimbia sehemu kwa mapumziko ya muda till that date. Na pia inawezekana akaamua kujificha kuepuka hao wanaoweza kumdhuru kwa kuhofia kuwataja katika kesi.

just a thinking!!
 
Taarifa za uhakika za hivi punde kutoka mahakamani ni kuwa AL hakufika:

Uamuzi ni kama ifuatavyo
1. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 24 ambayo ndiyo ilipangwa awali kwa yeye kufika mahakamani
2. Hati ya kukamatwa wadhamini wake imefutwa. Hivyo watatakiwa tu kuripoti hapa mahakamani siku ya tarehe 24. Iwapo AL hatafika siku hiyo ndipo wanaweza kukamatwa. wameachiwa na wamekwenda makwao.
Habari ndo hiyo

Thanks ffor the updates!

Lakini kwa nini hao wadhamini wameachiwa? hawa wangeendelea kushikiliwa mpaka huyo AL aonekane.....sasa nao kama wameachiwa itakuwaje wakiamua kutembea?
 
Nafikiri ni mchezo kati ya BOT na Mahakama.
Inasemekana wadhamini wawili ni wafanyakazi wa BOT.
Barua za dhamana zilitolewa na BOT kama ni kweli.
Mtuhumiwa amefanya madudu BOT,then BOT wanamdhamini. 'Unethical in every aspect'
Inamaanisha walikubaliana na hakimu namna ya kulicheza movie,ikitiliwa maanani hakimu hawezi kufanywa lolote kisheria hata angetoa maamuzi mabovu namna gani zaidi ya kupoteza ajira. hakuna issue ya reasonable man dhidi ya hakimu.
Hivyo wakaamua kumtoa na kumpa muda wa kutoroka then watoe warrant ya kurejesha mahakamani ili kufuta soo la dhamana kiduchu, then move inaishia kwa mtuhumiwa kuyeyuka kwenye thin air .....

Good thinking kwa timu iliyobuni movie hii, labda itasaidia kuwaamsha watanzania wajue MH.Sitta aliposema kuhusu mahakama alimaanisha nini...

kwa taarifa yaho hata hawa wadhamini wa BOT ilikuwa ni usanii maana hawakuwa na barua ya mwajiri mbali na vitambulisho!!!
 
Du nimelitizama na kuwa nalisoma hili sakata la kutoroka kwa Liyumba nimechoka kabisa. Hivi kwa nini hawa wakina serikali (siri-kali) wanatuchezea watanzania kama watoto wadogo? Mimi inaniuma sana na huwa napandwa na hasira sana mtu anaponifanya mtoto mdogo nsiejua kitu. Hapa ni kama walivyosema wenzangu...
1. Liyumba pesa za BOT hakla peke yake. Na si watu wa BOT tu bali hata kabineti ya Serikali kuu inahusika na ulaji huo
2. Ilifahamika wazi kuwa hatakamatwa ama sivyo angetorokea mbali sana kabla hajakamatwa pengine alikwisha hakikishiwa na vigogo waliokula pamoja
3. Kukamatwa kwake kumeleta hofu kwa vigogo walioshiriki katika utafunaji huo hasa ukizingatia watuhumiwa wa EPA walivyowajibishwa so hawa wakaona hatari ya kuumbuliwa kama Liyumba angepandishwa mbele ya haki
4. Wakapanga dili la kumtorosha. Utajuaje au kuamini kama ni dili
- Dhamana iliyomtoa rumande ina utata mkubwa tu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hati za umiliki wa mali zinazohamishika mfano kuku, bata e.t.c. Kisheria haikubalika ila kwake ilikubalika.
- Hakimu alitoa dhamana pamoja na upande wa mashtaka kutoridhia na badala yake akasema atachunguza kama hati zilizotolewa ni halali au batili (lakini mtuhumiwa akiwa nje)- Tunakumbuka jinsi dhamana za yule Somji wa EPA alivyokataliwa kutoka kisa barua moja ya dhamana ilikuwa na walakini?- Kwa Liyumba ni tofauti.
- Thamana haikufikia hata nusu ya kiwango kilichokuwa kinatakiwa alitoa 1.4 asilimia wakati katika kesi ile ya EPA yule Mwakosya alikataliwa kabisa mpaka zipatikane Million zile chache alokuwa ameamriwa

5. Ametolewa kwa dhamana na masharti ya dhamana akasomewa bado ametoroka akijua fika kuwa yuna kesi mahakamani. Hili dili hajalicheza peke yake kuna mkono wenye nguvu kubwa tu ambao umemkingia kifua.

6. Mtajasikia amepelekwa nje kutibiwa afya yake (wakati mtuhumiwa wa kesi ya Zombe, Lema anapelekwa mahakamani pamoja na kuwa na afya mbaya). Akishafika ULAYA Liyumba ataugua sana na katika kuelekea kupata nafuu atakata roho na kisha watanzania wachache viongozi wataalikwa kwa kadi maalumu kwenda kuhudhuria tafrija ya mazishi yake hukohuko ULAYA na mwisho ataungana na "Marehemu" Daudi Balali.

Ah kumbe bado haijafikia huku Movie hii........ ila nimeiforward.
 
Good thinking kwa timu iliyobuni movie hii, labda itasaidia kuwaamsha watanzania wajue MH.Sitta aliposema kuhusu mahakama alimaanisha nini...

- Sawa sawa, tupo pamoja hapa mkuu ndio maana kwa kuogopa haya ya hizi mahakama zetu, serikali ilisema wezi wa EPA warudishe hela serikalini tu now I see, ingawa sio sawa lakini ni bora kuliko haya mazingaombwe.
 
Ili JF iendelee kuwa JF...Inabidi tukafikia pahala tukaanza kuzungumzia right on the money. Issue ni mbili hapa kabla hatujaendelea na blah blah za kutoroka.....

1)Ilikuwa vipi mtuhumiwa alikubaliwa kuwasilisha vielelezo vilivyopitwa na muda,nani ana verify hizo document kuhakiki invalidation?(this time passport)

2)Pili, tunazungumzia mambo ya passport na kuunganisha na utorokaji wake lakini mjadala usiende huko kwasababu hauhitaji passport kuweza kutoroka, Unahitaji uzima na pesa,tena passport ni noma zaidi since tayari inajulikana anatafutwa,kwahiyo passport tunaiweka pembeni,hata hivyo tunarudi tena kwenye swali la msingi,kwanini passport iliyokwisha muda ilikubalika dhidi ya mtuhumiwa wa uhujumu uchumi?
Kuna wale wanaosema ilikuwa vipi tulitegemea jambo la tofauti...Na mimi swali langu kwao ni je wanakumbuka jinsi walivyokuwa wakisema hizi kesi hazina usanii? Wakisema JK anafanya kweli?
Hizi mnajuwa Amatus Liyumba angewahusisha vigogo wangapi kwenye kesi hii? Ama mmesahau kuwa kesi ya BOT twin towers ni mojawapo ya mtiririko wa kashfa za ufisadi zilizokuwa connected na kina Balali
 
Na mimi swali langu kwao ni je wanakumbuka jinsi walivyokuwa wakisema hizi kesi hazina usanii? Wakisema JK anafanya kweli?

- Eti JK anahusika vipi na dhamana za watuhumiwa mahakamani? I am reading right au nina-miss something hapa?
 
kwa taarifa yaho hata hawa wadhamini wa BOT ilikuwa ni usanii maana hawakuwa na barua ya mwajiri mbali na vitambulisho!!!

Nasikia walikuwa na barua ambazo hazikuwa na muhuri wala signature. Unajua maana ya hilo? Damn, these people are good. Huwezi kumkamata mtu ambae ametoa udhamini wa namna hiyo. Kwasababu anaweza kuukana mara moja na kuwa batili. Duh, kaaazi kweli kweli.
 
- Eti JK anahusika vipi na dhamana za watuhumiwa mahakamani? I am reading right au nina-miss something hapa?

Sasa kwanini JK alikuwa analaumiwa kama wewe na kina Mkandara mlijuwa nothing will be done and that we shouldn't expect any diferent results? Si mnasema tulikuwa tunategemea nini cha tofauti? Sasa mmejiumbuwa,kwasababu inaelekea maamuzi yote haya ni ya kisiasa,changa la macho....Kama mlijuwa kuwa hakuna kitakachofanyka then kwanini mlimsifia JK kuwa kafanya kweli.

Yani unamjeruhi mtu kwasababu una pesa ya kwenda kumtibu na kwahiyo wakati wa matibabu tumshukuru aliyetujeruhi....Am i the one missing something?
 
- Eti JK anahusika vipi na dhamana za watuhumiwa mahakamani? I am reading right au nina-miss something hapa?

Hapo pia mimi nimechoka kabisa. How do we elevate AL to such a status kwamba dhamana yake mpaka mkulu ahusike????? Bongo kweli kuna mambo!
 
- Hivi hapa mahakama wameingiliwa na bunge nini ndio maana huyu fisadi akaachiwa? Ndio maana yule Jaji Mkuu alipolia kuwa anaonewa na bunge tulisema anyamaze tu maana hana hoja na hajui power aliyonayo kisheria,

- kwa sababu kama hii ndio kazi ya mahakama zake kwa nini asiingiliwe na bunge?
 
Hapo pia mimi nimechoka kabisa. How do we elevate AL to such a status kwamba dhamana yake mpaka mkulu ahusike????? Bongo kweli kuna mambo!

Mkuu, waswahili wanasema ukishangaa ya Musa, Utaona ya Firauni.
 
1. Sasa kwanini JK alikuwa analaumiwa kama wewe na kina Mkandara mlijuwa nothing will be done and that we shouldn't expect any diferent results?

2. Si mnasema tulikuwa tunategemea nini cha tofauti?

3. Sasa mmejiumbuwa,kwasababu inaelekea maamuzi yote haya ni ya kisiasa,changa la macho....

4. Kama mlijuwa kuwa hakuna kitakachofanyka then kwanini mlimsifia JK kuwa kafanya kweli.

5. Yani unamjeruhi mtu kwasababu una pesa ya kwenda kumtibu na kwahiyo wakati wa matibabu tumshukuru aliyetujeruhi....Am i the one missing something?

- Sijakuelewa mkuu unachosema hapa, viongozi wamevunja sheria, wamekamatwa na sheria, wakiwa mikononi mwa sheria mmojawapo amepewa dhamana na sheria, sasa ametoroka,

- Now what this has to do na JK na kuwa au kutokwua serious na vita ya mafisadi, bado I do not get it?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom