Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Jmunsh1,

Mkuu ebu nambie wewe ulitaka Kikwete afanye nini na mafisadi?.. sikumbuki kama kuna mtu hata mmoja aliyetaka watu hawa wasifikishwe ktk sheria ila Kikwete afanye kitu tofauti!.. sikumbuki hata kuona maandishi yako wewe mwenyewe ukipnga watu hawa kufikishwa mahakamani..
Sasa tukirudi kwangu mimi issue nzima ya support kuhusiana na Kikwete, ni kukomesha Ufisadi na kitu gani anachotakiwa kufanya kama rais...Amekifanya na ndipo nilipompa support pamoja na kwamba ni sehemu ndogo sana ya zoezi zima.. lakini kulingana na record ya nchi yetu hakuna kionmgozi ambaye amewahi kufanya alofanya Kikwete - Kuwapeleka mawaziri na viongozi wa ngazi za juu ktk sheria...
Sasa upande wa sheria nilitegemea hawa watu wangeoza jela, mali zao kutaififishwa..
Ni katika hatua ya kurudisha utawala bora lazima kuwepo na mwanzo lakini pia ni lazima tuwe makini na zoezi zima tukizingatia watu na mazingira yetu ambayo hujenga hulka au tamaduni..
Bado nitamsifia Kikwete pamoja na kwamba sii kazi yake inapofikia maamuzi ya sheria.. as a fact ndio mapenzi ya raia wengi kuwa na rais anayefuata sheria wakati mimi nataka sana Kikwete awe Dikteta kuweza kukomesha kabisa MAFISADI... why?.. sababu ni ile ile - WATU na MAZINGIRA huwezi kufanikiwa kwa wadanganyia ambao walipuuza kuwa adui yetu mkubwa ni - UJINGA na UMASKINI .

Mkandara tulisema ni usanii toka awali kwani wale samaki wadogo ambao wangewakosti samaki wakubwa zaidi either wamepotea ama kutoweka.

Kina Mramba is NOTHING...Mkapa is SOMETHING...Unaweza kuona wanazunguka mbuyu kwasababu walibanwa sana na ndio maana wanakimbilia uchina...Uchina nao wanawapa kiduchu maana uchina wenyewe walishauwa mafisadi walioiba pesa ambazo hata hazifikii hizo za mafisadi wetu.
Tuliposema ni changa la macho toka awali hatukukusea...Ndio pointi yangu ilipo.
Sasa chini ya serikali ya JK passport iliyokwisha muda imemtowa mtuhumiwa wa mabilioni lupango...Only in TZ....Only under JK....Trully only under JK' law.
 
Nimejaribu kulitafakari hili swala, nikaona kuna mapungufu ya msingi katika utoaji wa habari hii. Sidhani ni sahihi kusema Liyumba ametoroka. Katoroka toka wapi? Liyumba amepewa dhamana na yuko huru kuwa popote ndani ya Dar es Salaam. Ili iripotiwe ametoroka inabidi ithibitishwe kuwa hayupo Dar es Salaam. Nadhani tuvute subira, Liyumba anatakiwa mahakamani tarehe 24. February- hivyo ndivyo alivyoambiwa wakati anaachiwa huru. Kwa hiyo kumripoti ametoroka wakati hakukuwa na makubaliano ya yeye kuja mahakamani au kuwa standby kuitwa na mahakama, si sahihi. Kwa hiyo labda habari hii ingebadilishwa na kuwa Liyumba anatafutwa badala ya Liyumba atoroka.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani hapo kwenye neno "Kutoroka" Hata hivyo si walisema alihitajika mahakamani na hakuonekana? Kwamba anatakiwa mahakamani tarehe 24 feb ni baada ya hakimu ku postpone kesi na kusema kuwa faili liko mahakama kuu.
 
Tarehe aliyotakiwa haijafika, ila wamemuita kwa sababu ambayo haijatajwa.
 
Kwa sheria nyepesi nyepesi kama za TZ

Moja kwa moja haya matatizo ya Balali kufia nchi za mbali,Liyumba kuyumba yumba hadi kuambaa , bila kupindisha maneno ama nini ni matatizo yanayosababishwa na RAIS wa nchi ,Wenda ni laini ama naye ni moja ya matunda ktk fedha hizo. Moja kati ya mawili hayo ni sahihi.
 
Tarehe aliyotakiwa haijafika, ila wamemuita kwa sababu ambayo haijatajwa.

Mkuu ndio maana nikasema hapo awali lazima kuna mtu wa UWT aliyekuwa akimfuatilia na baada ya kumpoteza ama kuhisi kumpoteza ndio wakafanya mpango wamwite mahakamani...Kwasababu si hatujui kwanini walimwita mahakamani kabla ya tarehe 24? Ukijumlisha na faili lake kupelekwa mahakama kuu,basi utajuwa kuwa mazingira ya bail yake hayakuwafurahisha wote,sasa na yeye sidhani kama atarudi.
Just my take.
 
Mkuu hili swali la hoja ya Mtikila nilimuuliza waziri wa sheria straight up face to face, akanijibu kwamba waandishi hawasemi ukweli, sheria iko clear kuwa ni bunge tu ndilo linaweza kutengua au kubadili sheria sio mahakama...
Waziri gani huyo alikwambia hicho kitu Mkuu? Tafadhali ndugu.

Nguvu ya mahakama kukagua uhalali wa sheria, judicial review, ipo, na msingi wake umejengwa katika Ibara ya 64 (5) na sehemu ya utaratibu wa batilisho la mahakama umeanishwa katika ibara ya 30 (5) ya Katiba.
 
Mushi kidogo naanza kuwa na shaka juu ya uwezo wako wa kufikiri na kuchambua mambo. Nilikuwa nakuaminia sana lakini sasa unanifanya nifikiri mara mbi mbili. Hivi unaamini kutoka moyoni na kwa akili yako yote kwamba JK na mahakama zilipanga kumtorosha Liumba tangu awali?
 
Huna haja ya kuniaminia wala huna haja ya kuupongeza uwezo wangu wa kufikiri.

Hivi unadhani movie ni live event? Ama we unafikiri mafisadi wakipanga wanapanga kama wewe? We hujui kuna mipango ya kisiasa,na mwenye kutunga movie anajuwa mwisho wake kabla hata hujajuwa title yake, sasa wewe ndio uko theatre.

Kama alivyosema MKJJ kuwa uamuzi ni kuchagua,sasa nani alichaguwa Liyumba atoroke?
Tunapenda laini laini sana,shirikisha ubongo wako la sivyo utapitwa na mjadala,na kama umepitwa na mjadala take your time and read through. Na kama hujaelewa si lazima uchangie saa hiyo hiyo...Nenda kalale kesho unaweza ukaamka umeelewa.
 
Kwa mujibu wa TBC mpaka hivi sasa Liyumba bado hajapatikana.
 
Kama Kweli Liumba ni HIV positive na ni yupo stage za mwisho mwisho wa ugonjwa then inawezekana Hakimu alimpa dhamana kwaajili ya Afya. Kwenye picha zilivyooneshwa wakati wa kutoka mjamaa alikuwa anaonekana si mzima....

i dont know Liumba ila kama story za mitaani ni kweli then jamaa inawezekana ni mgonjwa mahututi then possible hakimu aliconsider dhamana ya kiujinga maana if u work risk analysis ya government kuwa sued for human rights possible ni hakimu alimake wise choice especial ukizingatia probability za hela jamaa alizoiba haita kuwa recovered and life expectation ya Liumba possible ni less than 6 months....

anyway lets all wait and see... this opinion is just based on speculation stories za mitaani
 
Nafikiri ni mchezo kati ya BOT na Mahakama.
Inasemekana wadhamini wawili ni wafanyakazi wa BOT.
Barua za dhamana zilitolewa na BOT kama ni kweli.
Mtuhumiwa amefanya madudu BOT,then BOT wanamdhamini. 'Unethical in every aspect'
Inamaanisha walikubaliana na hakimu namna ya kulicheza movie,ikitiliwa maanani hakimu hawezi kufanywa lolote kisheria hata angetoa maamuzi mabovu namna gani zaidi ya kupoteza ajira. hakuna issue ya reasonable man dhidi ya hakimu.
Hivyo wakaamua kumtoa na kumpa muda wa kutoroka then watoe warrant ya kurejesha mahakamani ili kufuta soo la dhamana kiduchu, then move inaishia kwa mtuhumiwa kuyeyuka kwenye thin air .....

Good thinking kwa timu iliyobuni movie hii, labda itasaidia kuwaamsha watanzania wajue MH.Sitta aliposema kuhusu mahakama alimaanisha nini...

,,,Hiyo si kweli mzee,,ikumbukwe kuwa hata hao wadhamini wake wawili kutoka BoT barua zao zilikua incomplete,kwa kuwa hazikuwa na signature ya mwajiri wao,,,,lakini kwa kua hakimu alisha amua liwalo na liwe,hakuona hilo kosa,,,,,,waaalaah mi nahisi siku hiyo jamaa alimwaga mpunga pande zote mbili,washtaki(prosec) na watu wa mahakama,kwa sababu ukiiiangalia hii kitu in a BIG PICTURE,unaona hata hawa wanaitwa mawakili wa serikali hawakua na nguvu saaaana siku ile,walikua wanajua nini kitafuata,wanakuja kutuzuga sasa hivi ooh tunamtafuta!!!,yaani hii system yoooote KWISHNEY,yaani kila sehemu hakushikiki,,,embu cheki kule kwa ZOMBE,,,yule shahidi muhimu kabisa yu mahututi,inahisiwa askari wa pale weshapenyeza KIMUONZI kwenye msosi wa shahidi MUHIMU kabisa,jamaa anakwisha taratiiiiibu,mwishoni kesi LINAKUFA hili.
 
lisha ashiria kwamba angetoroka kwani aliwasilisha passport feki. Hakimu aliyekiuka mashart ya dhamana itabidi awekwe ndani badala yake.
 
........ni aibu kubwa kwa vyombo vyetu vya usalama......
 
Jmunsh1,

Mkuu ebu nambie wewe ulitaka Kikwete afanye nini na mafisadi?.. sikumbuki kama kuna mtu hata mmoja aliyetaka watu hawa wasifikishwe ktk sheria ila Kikwete afanye kitu tofauti!.. sikumbuki hata kuona maandishi yako wewe mwenyewe ukipnga watu hawa kufikishwa mahakamani..
Sasa tukirudi kwangu mimi issue nzima ya support kuhusiana na Kikwete, ni kukomesha Ufisadi na kitu gani anachotakiwa kufanya kama rais...Amekifanya na ndipo nilipompa support pamoja na kwamba ni sehemu ndogo sana ya zoezi zima.. lakini kulingana na record ya nchi yetu hakuna kionmgozi ambaye amewahi kufanya alofanya Kikwete - Kuwapeleka mawaziri na viongozi wa ngazi za juu ktk sheria...
Sasa upande wa sheria nilitegemea hawa watu wangeoza jela, mali zao kutaififishwa..Ni katika hatua ya kurudisha utawala bora lazima kuwepo na mwanzo lakini pia ni lazima tuwe makini na zoezi zima tukizingatia watu na mazingira yetu ambayo hujenga hulka au tamaduni..Bado nitamsifia Kikwete pamoja na kwamba sii kazi yake inapofikia maamuzi ya sheria.. as a fact ndio mapenzi ya raia wengi kuwa na rais anayefuata sheria wakati mimi nataka sana Kikwete awe Dikteta kuweza kukomesha kabisa MAFISADI... why?.. sababu ni ile ile - WATU na MAZINGIRA - Huwezi kufanikiwa kwa wadanganyika ambao walipuuza kuwa adui yetu mkubwa ni - UJINGA na UMASKINI .

naomba msaada kuweka kumbukumbu zangu sawa. hivi kiula alipopelekwa kwa pilato ilikuwa wakati wa urais wa jk? au hapa kinachozungumziwa ni namba na sio action?
 
kiula litajwa kwenye ile tume ya warioba ya kuchunguza rushwa, akapelekwa kwa pilato wakati wa mkapa, akshinda kesi
 
kwa hiyo jk sio rais wa kwanza katika historia kumpeleka kiongozi wa juu kwa pilato.
 
kuna wakati niliishawahi uliza humu jamvini
"inakuwaje watuhumiwa wa epa wanatakiwa na mahakama
wawasilishe hati zao za kusafiria (passport) wakati serikali
ilikwisha tangaza kwamba ndio iliishazichukua hizo hati?".

leo hii najiuliza tena hivi passport ya liumba haikukamatwa?
kama ilichukuliwa ina maana hao walioichukua hawakuona
hizo kasoro kwamba ilikuwa imekwisha?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom