Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Inadaiwa jamaa yupo hui kwa kubwia sumu.habari ambazo hazija thibitishwa kwamba baad ya kupewa dhamana aliona mwenendo wa kesi utamletea fedheha na kuamua kuji MKWAWA ILI KUKWEPA FEDHEHA HIYO.TAARIFA HIZO HAZISEMI aina ya sumu aliyobwia na wala hospitali anayougulia ingawa inadaiwa kuwa ANAENDELEA VIZURI.
Duh.ISIJELETA UTATA KAMA ILE YA BOSI WAKE BALALI?

Kwi kwi kwi!!!!!!!!! Nacheka utadahani mazuri. Bongo Bwana!!!!
 
Inadaiwa jamaa yupo hui kwa kubwia sumu.habari ambazo hazija thibitishwa kwamba baad ya kupewa dhamana aliona mwenendo wa kesi utamletea fedheha na kuamua kuji MKWAWA ILI KUKWEPA FEDHEHA HIYO.TAARIFA HIZO HAZISEMI aina ya sumu aliyobwia na wala hospitali anayougulia ingawa inadaiwa kuwa ANAENDELEA VIZURI.
Duh.ISIJELETA UTATA KAMA ILE YA BOSI WAKE BALALI?

Kwi kwi kwi!!!!!!!!! Nacheka utadhani mazuri. Bongo Bwana!!!!
 
2009-02-21 07:37:00
Puzzle over Liyumba whereabouts deepens
THE CITIZEN​

Tanzania People Defence forces servicemen show off their skills after completing their training at Makutupora in Dodoma yesterday
By Rosina John

For the third day running, the authorities failed yesterday to locate a former senior Bank of Tanzania (BoT) official for whom a Dar es Salaam court has issued an arrest warrant.

The revelation was made when Kisutu Resident Magistrate Khadija Msongo called for the case. The Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) prosecutor, Ms Tabu Mzee, told the court that they had no information on the whereabouts of Mr Amatus Liyumba, a former BoT director of personnel and administration. She said they were still looking for him.

Since Wednesday, the court and the PCCB have been trying to trace Mr Liyumba. He couldn't be reached since a day after his release from Keko Remand Prison, where he had been held for nearly three weeks, having failed to meet the bail applications set by the court.

Yesterday, Mr Liyumba�s lawyers urged the court to restrain the prosecutors from pestering their client's family.

Mr Liyumba, who is facing abuse of office charges together with the central bank's former project manager, Mr Dawson Kweka, over the construction of the central bank's Twin Towers building in Dar es Salaam's city centre, was last Tuesday finally granted bail by Magistrate Msongo.

But in an interesting twist, the same magistrate issued an arrest warrant for him only a day after she had granted him bail.

Yesterday , Ms Msongo did not give any explanation as to why she had issued the arrest warrant against Mr Liyumba, whom she had granted bail.

The former bank official was released after his advocates presented to the court a title deed to his Dar es Salaam house valued at Sh882 million. Earlier, he had been required to deposit Sh55 billion or title deeds to property of a similar value.

In another twist in the saga yesterday, Ms Msongo also cancelled the arrest warrants she had issued for two of Mr Liyumba sureties.

On Thursday, PCCB officials had arrested and briefly held in the cells at the law courts the two sureties, who are both BoT employees, Mr Benjamin Nduguru and Mr Otto Agategema. However, they were later set free, but are required to report to the court next Tuesday, when the case comes up for mention.

Yesterday, Mr Liyumba's lawyer, Mr Majura Magafu, who is assisted by four other advocates, asked the court to warn prosecutors to keep off Mr Liyumba's family, saying that the date when he is supposed to appear in court was still far away.

But Magistrate Msongo advised the advocates to raise the matter next Tuesday, when the case comes up for mention.

On their part, the PCCB officials said they would continue looking for Mr Liyumba, as the arrest warrant for him was still valid.

A source told The Citizen that PCCB officials were convinced that Mr Liyumba was in Dar es Salaam.

Following a tip-off on Thursday night, PCCB officials reportedly searched a house at an undisclosed location but did not find him.

Mr Liyumba and Mr Kweka first appeared in the Kisutu Resident magistrate�s Court on January 27.

The prosecution alleges that they abused their powers as public servants by making "sensitive decisions" on the execution of the multibillion project without informing their superiors.

The two men are also accused of inflating the cost of the project, thus causing the Government to suffer a loss of Sh221 billion.

They denied the charges and were remanded after they failed to meet the bail conditions.

Mr Liyumba then appealed to the High Court to ease the bail conditions, but this was turned down last Monday.

On the same day, his lawyers announced that they had collected enough title deeds to post bail for their client and asked that he be brought to court on Tuesday.

On Tuesday, they presented several title deeds, including the one to Mr Liyumba's Sh882 million house.

Apart form Mr Liyumba's own title deed, the prosecution objected to the production of the other documents, including his expired passport.

But Magistrate Msongo released Mr Liyumba on bail despite the prosecution's submission that most of the title deeds had not been verified.

A day later, the magistrate issued an arrest warrant for Mr Liyumba's sureties.
 
"Wakati Takukuru ikifikia maamuzi hayo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kama Takukuru itahitaji msaada wa Wizara hiyo kumtafuta Liyumba iko tayari kutoa msaada huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili Waziri wa Wizara hiyo, Lawrance Masha alisema wakipewa maombi ya kumtafuta Liyumba, watasaidia kumtafuta kwa kuwa wote ni Serikali."

"Juzi nilitoa tamko kuwa hatujaletewa maombi ya kumtafuta, lakini Takukuru wakituletea tutafanya hivyo, kwa kuwa sisi ni Serikali," alisema Masha.

Source: Mwananchi

Wakuu hii mi naona kali. Hivi fugitive anapokata kamba kwenye mkono wa sheria polisi inabidi waandikiwe barua kuombwa wamkamate? i thought ilikua ni automatic duty yao kumkamata.... Nilikua sijui!
 
Na sio kali tu ni KITUKO cha mwaka 2009.

Waziri anajua vzr sheria zetu but ndio kulindana kulivyo tusimlaumu sn. Wizara ya mambo ya ndani na askari wake wanachojua ni kukamata wapinzani bila ya kupewa maagizo na chombo chochote kile, mkubwa akishashiba sembe lake napiga simu pale central polisi "Nataka mukamkamate kiongozi wa chadema/cuf ....., mkutano wao unahatarisha mani" Central wanapiga call kule ukonga then zinamwaga defender , mkutano unavunjwa na viongozi wa upinzani wanakamatwa.

But Mshtakiwa alietoroka baada ya dhamana hakamatwi hadi polisi wapewe taarifa!!!!!

WHY?KWA NINIIIIII!!!!!!!!!!!????
 
"Wakati Takukuru ikifikia maamuzi hayo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kama Takukuru itahitaji msaada wa Wizara hiyo kumtafuta Liyumba iko tayari kutoa msaada huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili Waziri wa Wizara hiyo, Lawrance Masha alisema wakipewa maombi ya kumtafuta Liyumba, watasaidia kumtafuta kwa kuwa wote ni Serikali."

"Juzi nilitoa tamko kuwa hatujaletewa maombi ya kumtafuta, lakini Takukuru wakituletea tutafanya hivyo, kwa kuwa sisi ni Serikali," alisema Masha.

Source: Mwananchi

Wakuu hii mi naona kali. Hivi fugitive anapokata kamba kwenye mkono wa sheria polisi inabidi waandikiwe barua kuombwa wamkamate? i thought ilikua ni automatic duty yao kumkamata.... Nilikua sijui!

Huyu Masha kila akifungua domo lake ni pumba tuu..

Hakimu akitoa amri ya mtuhumiwa kukamatwa, si maana yake Polisi ndio wana wajibu wa kutekeleza amri hiyo...na hao Polisi wako chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani...sasa Masha anasubiri barua kutoka TAKUKURU ya nini??
 
Last edited by a moderator:
TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini(Takukuru) imetangaza kutoa donge nono kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye hadi hivi sasa hajulikani halipo.

Wakati Takukuru ikifikia hatua hiyo, tayari kuna wananchi ambao wametoa taarifa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa wanaweza kutoa taarifa za alipo Liyumba.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani alisema wameamua kutangaza doge nono ambalo hakulitaja ni kiasi gani cha fedha ili wananchi wasaidie kupatikana kwa Liyumba.

Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Dk Edward Hoseah ,anakaribisha watu ambao wanaweza kutoa taarifa au kusaidia alipo Liyumba ili aweze kukamatwa.

"Kuna wananchi tumesikia wako tayari kuisaidia Takukuru, tunawakaribisha na Dk Hoseah anawakaribisha ili waweze kutusaidia na donge nono litatolewa kwa atakayesaidia kukamatwa kwa Liyumba," alisema Kapwani.

Wakati Takukuru ikifikia maamuzi hayo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kama Takukuru itahitaji msaada wa Wizara hiyo kumtafuta Liyumba iko tayari kutoa msaada huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili Waziri wa Wizara hiyo, Lawrance Masha alisema wakipewa maombi ya kumtafuta Liyumba, watasaidia kumtafuta kwa kuwa wote ni Serikali.

"Juzi nilitoa tamko kuwa hatujaletewa maombi ya kumtafuta, lakini Takukuru wakituletea tutafanya hivyo, kwa kuwa sisi ni Serikali," alisema Masha.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifuta dhamana ya Liyumba Februari 19 na kutoa amri ya kuwakamata wadhamini wake ambao walikamatwa siku hiyohiyo na baadaye kuachiwa.

Wadhamini hao ni wafanyakazi wa BoT Benjamin Nduguru (mhasibu wa benki hiyo) na Agaterus Oto (Afisa Usalama wa ndani wa benki hiyo).

Hata hivyo, licha ya mahakama kufuta dhamana kuwakamata wadhamini hao, ilitoa amri ya kumtafuta na kumkamatwa Liyumba,

Liyumba pamoja na aliyekuwa Meneja Miradi wa BoT, Deogratius Kweka wameshitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo na kuisababishia hasara serikali jumla ya Sh221 bilioni.

Liyumba alipewa dhamana na Makimu Mkaazi wa Kisutu, Hadija Msongo kwa kutumia hati ya nyumba yake iliyoko Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam yenye thamani ya Sh800 milioni, ambayo hata hivyo ililalamikiwa na upande wa mashitaka kwamba imetolewa katika mazingira tata kwa kuwa haijafikisha kiwango cha Sh50 bilioni walizotakiwa kutoa

Juzi Wakili wa serikali, Prosper Mwangumila aliileza mahakama kwamba, Liyumba bado hajapatikana.

Hakimu alisema amri ya kumkamata Liyumba bado inaendelea na ya kuwakamata wadhamini imesitishwa hadi kesi itakapotajwa Februari 24, mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mawakili wanaomtetea mtuhumiwa huyo waliulalamikia upande wa mashitaka kwa kitendo chake cha kuwanyanyasa ndugu wa mtuhumiwa huyo ambapo walidai kuwa uliwanyang’anya baadhi ya mali zao.

Mmoja wa mawakili hao wa utetezi, Majura Magafu aliiomba mahakama kutoa amri ya kuutaka upande wa mashitaka kuacha kuinyanyasa familia ya Liyumba na kwamba warudishe gari ya mmoja wa wadhamini ambayo waliikamata.

Akijibu hoja hiyo, Hakimu Msongo aliutaka upande wa utetezi kama una maombi yoyote kuyapeleka kwa utaratibu wa mahakama kwa kuwa juzi haikuwa tarehe ya kesi.

Wakati akitoa dhamana hiyo Februari 17, mwaka huu, Hakimu Msongo alisema mshitakiwa huyo, atakuwa nje kwa dhamana ya Sh882 milioni wakati mahakama inajiridhisha na hati nyingine zilizopingwa na upande wa mashitaka.

Alisema mshitakiwa atatakiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kiasi kilichobaki cha Sh54,417,344,800.23 endapo mahakama itabaini kuwa hati hizo zina kasoro.

Hata hivyo baada ya kutolewa maamuzi hayo Wakili wa serikali Justus Mulokozi alisema hawajaridhika na maamuzi yaliyotolewa na kwamba watakaa kuyajadili na kuyatolea maamuzi.

Upande wa mashitaka ulipinga kupokelewa kwa hati 10 kati ya 11 zilizowasilishwa mahakamani hapo na upande wa utetezi kwa madai kuwa zina kasoro, zikiwemo za kuwa na mali zisizokuwa za kudumu kama mbuzi, ng’ombe na kuku.

Siku mbili baada ya mtuhumiwa huyo kuachiwa huru na mahakama kutokana na kutimiza masharti, mahakama ilitoa amri ya kukamatwa tena jambo lilosababisha wadhamani wake kushikiliwa kwa muda na kisha kuachiwa.

Liyumba na Kweka walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza , Januari 27, mwaka huu kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia hasara serikali kiasi cha Sh 221 bilioni. Kweka bado hajapata dhamana
Source: Gazeti la Mwananchi
 
Hivi ni yule yule Masha aliyekuwa anasemea kuhusu maslahi ya Taifa mbele.....duuhh
 
TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini(Takukuru) imetangaza kutoa donge nono kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye hadi hivi sasa hajulikani halipo.

Donge nono limefanya hata wazazi wa albino kuwasaliti watoto wao kwa vipande vya fedha. Kama ni donge zito basi hata mkulu A Liyumba anaweza kuuzika.
 
Hivi ni yule yule Masha aliyekuwa anasemea kuhusu maslahi ya Taifa mbele.....duuhh

Ni huyo huyo Masha aliyekuwa na jeuri ya kuingilia mchakato wa vitambulisho eti kwa maslahi ya taifa. Kaaaazi kweli kweli.
 
tukisema Masha hastahili kuongoza Wizara hiyo wengine wanaweza kusema tuna chuki naye "binafsi"..
 
Kuna kitu unakitafuta na utakipata.....what? Mwanasheria mahiri kijana na degree za marikani hawezi ongoza wizara?....hell no...nahisi umekosea...
 
Yo Yo

Michango yako haina maslahi kwa taifa na huna credibility!!! Nimeisha kuambia ninakufahamu shauri yako hahahahahah mzee week end vipi!! I am just chilling hapa!
 
Nina wasiwasi Masha ameshajua kuwa jamaa ameshakimbia nje ya Nchi na nina uhakika anajua ni wapi au nchi gani aliyokimbilia ndio anatafuta kupewa taarifa ili aonyeshe kuwa kazi anaimudu , vipi utakurupuka tu useme wao ni serikali na sisi ni serikali ,hivi kuna serikali ngapi hapa Tanzania ? Kama yeye ni sehemu ya kuwajibika kumtafuta si kungojea kupewa habari nchi zingine vyombo vyenye mamlaka vinagombea mambo kama haya hata havingoji kupelekewa habari vinaingia kazini na kumtafuta muhusika na pindi atakae wahi kumkama anajitangazia ushindi kuwa ni bora kuliko wengine ,na zaidi huwa mambo haya yanatokea Uingereza na Marekani vyombo vya ulinzi kila mmoja kivyakevyake na hakuna anaengoja kuambiwa na kila mmoja analifuatilia jambo kwa ukaribu kabisa hakuna kulala lakini hapa jamaa anasema anangoja apelekewe Taarifa ,watu si walimpelekea taarifa ajiuzulu mbona hakujiuzulu ? Eti jamani kama anachongojea ni taarifa si alishapelekewa aondoke madarakani ,sasa anangojea taarifa ipi wakati ya kuwajibika hakuifanyia kazi >wizi mtupu/.
 
Hapa kwa Masha sio kweli tumepatikana. Kumbe kazi ya kumtafuta Liyumba ni ya PCCB peke yao? Nadhani kuna something fishy hapa, haiwezekani mshtakiwa muhimu namna hiyo apotee na waziri aseme anahitaji kuandikiwa barua ya kuombwa msaada wa kumtafuta, hiki kama si kichekesho sijui ni nini? Masha kwa kulinda heshima yake (ambayo hata hivyo hana) bora wakati fulani akae kimya, kwani watu huenda wakadhani ana busara, kuliko akifungua mdomo kutoa upumbavu.
 
And the episode continues!!!!!!!

Na Boniface Meena

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini(Takukuru) imetangaza kutoa donge nono kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye hadi hivi sasa hajulikani halipo.

Wakati Takukuru ikifikia hatua hiyo, tayari kuna wananchi ambao wametoa taarifa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa wanaweza kutoa taarifa za alipo Liyumba.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani alisema wameamua kutangaza doge nono ambalo hakulitaja ni kiasi gani cha fedha ili wananchi wasaidie kupatikana kwa Liyumba.

Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Dk Edward Hoseah ,anakaribisha watu ambao wanaweza kutoa taarifa au kusaidia alipo Liyumba ili aweze kukamatwa.

"Kuna wananchi tumesikia wako tayari kuisaidia Takukuru, tunawakaribisha na Dk Hoseah anawakaribisha ili waweze kutusaidia na donge nono litatolewa kwa atakayesaidia kukamatwa kwa Liyumba," alisema Kapwani.

Wakati Takukuru ikifikia maamuzi hayo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kama Takukuru itahitaji msaada wa Wizara hiyo kumtafuta Liyumba iko tayari kutoa msaada huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili Waziri wa Wizara hiyo, Lawrance Masha alisema wakipewa maombi ya kumtafuta Liyumba, watasaidia kumtafuta kwa kuwa wote ni Serikali.

"Juzi nilitoa tamko kuwa hatujaletewa maombi ya kumtafuta, lakini Takukuru wakituletea tutafanya hivyo, kwa kuwa sisi ni Serikali," alisema Masha.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifuta dhamana ya Liyumba Februari 19 na kutoa amri ya kuwakamata wadhamini wake ambao walikamatwa siku hiyohiyo na baadaye kuachiwa.

Wadhamini hao ni wafanyakazi wa BoT Benjamin Nduguru (mhasibu wa benki hiyo) na Agaterus Oto (Afisa Usalama wa ndani wa benki hiyo).

Hata hivyo, licha ya mahakama kufuta dhamana kuwakamata wadhamini hao, ilitoa amri ya kumtafuta na kumkamatwa Liyumba,

Liyumba pamoja na aliyekuwa Meneja Miradi wa BoT, Deogratius Kweka wameshitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo na kuisababishia hasara serikali jumla ya Sh221 bilioni.

Liyumba alipewa dhamana na Makimu Mkaazi wa Kisutu, Hadija Msongo kwa kutumia hati ya nyumba yake iliyoko Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam yenye thamani ya Sh800 milioni, ambayo hata hivyo ililalamikiwa na upande wa mashitaka kwamba imetolewa katika mazingira tata kwa kuwa haijafikisha kiwango cha Sh50 bilioni walizotakiwa kutoa

Juzi Wakili wa serikali, Prosper Mwangumila aliileza mahakama kwamba, Liyumba bado hajapatikana.

Hakimu alisema amri ya kumkamata Liyumba bado inaendelea na ya kuwakamata wadhamini imesitishwa hadi kesi itakapotajwa Februari 24, mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mawakili wanaomtetea mtuhumiwa huyo waliulalamikia upande wa mashitaka kwa kitendo chake cha kuwanyanyasa ndugu wa mtuhumiwa huyo ambapo walidai kuwa uliwanyang’anya baadhi ya mali zao.

Mmoja wa mawakili hao wa utetezi, Majura Magafu aliiomba mahakama kutoa amri ya kuutaka upande wa mashitaka kuacha kuinyanyasa familia ya Liyumba na kwamba warudishe gari ya mmoja wa wadhamini ambayo waliikamata.

Akijibu hoja hiyo, Hakimu Msongo aliutaka upande wa utetezi kama una maombi yoyote kuyapeleka kwa utaratibu wa mahakama kwa kuwa juzi haikuwa tarehe ya kesi.

Wakati akitoa dhamana hiyo Februari 17, mwaka huu, Hakimu Msongo alisema mshitakiwa huyo, atakuwa nje kwa dhamana ya Sh882 milioni wakati mahakama inajiridhisha na hati nyingine zilizopingwa na upande wa mashitaka.

Alisema mshitakiwa atatakiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kiasi kilichobaki cha Sh54,417,344,800.23 endapo mahakama itabaini kuwa hati hizo zina kasoro.

Hata hivyo baada ya kutolewa maamuzi hayo Wakili wa serikali Justus Mulokozi alisema hawajaridhika na maamuzi yaliyotolewa na kwamba watakaa kuyajadili na kuyatolea maamuzi.

Upande wa mashitaka ulipinga kupokelewa kwa hati 10 kati ya 11 zilizowasilishwa mahakamani hapo na upande wa utetezi kwa madai kuwa zina kasoro, zikiwemo za kuwa na mali zisizokuwa za kudumu kama mbuzi, ng’ombe na kuku.

Siku mbili baada ya mtuhumiwa huyo kuachiwa huru na mahakama kutokana na kutimiza masharti, mahakama ilitoa amri ya kukamatwa tena jambo lilosababisha wadhamani wake kushikiliwa kwa muda na kisha kuachiwa.

Liyumba na Kweka walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza , Januari 27, mwaka huu kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia hasara serikali kiasi cha Sh 221 bilioni. Kweka bado hajapata dhamana.

Source Mwananchi
 
"Wakati Takukuru ikifikia maamuzi hayo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kama Takukuru itahitaji msaada wa Wizara hiyo kumtafuta Liyumba iko tayari kutoa msaada huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili Waziri wa Wizara hiyo, Lawrance Masha alisema wakipewa maombi ya kumtafuta Liyumba, watasaidia kumtafuta kwa kuwa wote ni Serikali."

"Juzi nilitoa tamko kuwa hatujaletewa maombi ya kumtafuta, lakini Takukuru wakituletea tutafanya hivyo, kwa kuwa sisi ni Serikali," alisema Masha.

Source: Mwananchi

Wakuu hii mi naona kali. Hivi fugitive anapokata kamba kwenye mkono wa sheria polisi inabidi waandikiwe barua kuombwa wamkamate? i thought ilikua ni automatic duty yao kumkamata.... Nilikua sijui!

Sina hakika Bwana MAsha alimmanisha nini... Kama ningekua mimi ningesema "serikali inalifanyia kazi suala la Liyumba na Kazi iko motomoto"

Sijui Masha Karogwa? Au ni zezeta? au ni mtu asiyejua kazi yake? Waziri mwenye dhamana kama yeye hawezi kusubiri barua ya PCCB (inayohusika na rushwa) kumtafuta fugitive!!!!!!!!!!!!... sasa rushwa na utoro vyote vishughulikiwe na PCCB? MAsha angechukua cha utoro amuachie PCCB kuhangaka na rushwa !

Zile salamu za Mjomba [Mrisho Mpoto] nadhani mjomba hajazikamata sawasawa...

Siku si nyingi, tutaishi kama wanyama

Mshahara wa dhambi ni mauti; na gharama ya dhambi ni kupoteza utu...
 
Bila shaka viungo vya Albino vimeanza kumwishia huyo mwanasheria makini na msomi waziri wa mambo ya ndani!! Kuna shida sana na viongozi wetu jamani anyway viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe!
 
tukisema Masha hastahili kuongoza Wizara hiyo wengine wanaweza kusema tuna chuki naye "binafsi"..

Nadhani kijichuki hicho binafsi kipo...

Jamani inabidi nirudi tena kuweka wazi kuhusu Masha. Inaonekana huyu waziri haeleweki na watu japo anafanya kazi zake kwa mipangilio maalum. Katika hili, Takukuru iko chini ya Ikulu, Police iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kesi imepelekwa mahakamani na Takukuru. Baada ya jamaa Liyumba kukitoa, waliopeleka kesi mahakamani ndio waliopewa jukumu la kumsaka. Sasa hii ni operation. Lazima Takukuru iwe na stratergy zake za kumnasa, zikiwemo kama ilivyoelezwa katika taarifa zao, matumizi ya resources zote zilizo chini yao, i.e. fedha, watu na vifaa.

Sasa niniyi mnataka wakati huo huo, Polisi nao waweke stratergy na kutumia resources zake kwa kazi ambayo tayari inafnywa na chombo kingine cha serikali. Hii italeta confusion ya hali ya juu.

Kitu kinachotakiwa hapa na alicho dai Masha ni kuwa, iwapo Takukuru inaona uwezo wake ni mdogo na inataka msaaada wa Polisi basi waseme hivyo na baadaye wakae na kuweka stratergy ya pamoja. Kwa mtindo huo wa kuunganisha nguvu, wanaweza kumnasa.

Hivyo ndio utaratibu wa kazi. Sio kuvamia tu kazi za watu wengine. Endapo itatokea katika utekelezaji wa kazi zake za kawaida, Polisi ikamuona mtuhumiwa Liyumba, hapo inaweza kumkamata kama mtuhumiwa mwingine yeyote.

Kama Masha angekurupuka tu na kwaambia Mapolisi wake wamtafute Liyumba, ninyi ndio mngekuwa wa kwanza kulalamika kuwa anaingilia kazi za Takukuru. Ama sivyo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom