Dhahiri shahiri leo ni leo maana kitendo cha mh.hadija kimewanyongonyeza sana watumishi wemzake pale kisutu, amewafanya wajione watoto wadogo ktk fani, siku alipomuachia liyumba aliwaacha pccb na wale jamaa toka kwa dpp wafanye watakavyo na pale watetezi wa liyumba walipo raise reasonable doubts alitulia kimya kama kibogoyo asiye na mamlaka, pccb siku ile hawakutegemea jamaa angetimiza masharti kwa 99% hivyo walipoona mseminari anatoka wakaona looh hapa ni kuchafua hali ya hewa kwa kupinga kila jambo lililoletwa mbele ya mh. Hadija, bado hata alipofanya maamuzi ya kumuachia liyumba mh.hadija hakujibu hoja zote za pande mbili na kuiacha hadhira ikiegemea kile walichosema dpp&pccb side kuwa ndio ukweli wenyewe.
Liyumba alitimiza mashariti yote isipokuwa mh. Hadija alikurupuka kutoa maamuzi yake na baadaye akaanza kufanya kazi kwa mujibu wa magazeti, mahakama kuu walipoliita faili waliona mapungufu machache sana ktk application ya dhamana ambayo kisheria hakimu anaweza kuruhusu dhamana huku marekebisho yakifanyika lakini hakukuwa na msimamo huo toka kwa hakimu, all in all pccb wanatakiwa kujibu tuhuma ya kutofuata procedure ya kumfungulia charge liyumba, na hapo ndipo mh.hadija alitakiwa kuanza napo.
Media ime exagarate the whole issue na sasa tusubiri leo maana liyumba akitia timu mh. Hadija atuonyeshe udhaifu wake na pia uwajibikaji.
Tusubiri mseminari kama atatia timu au la!!