Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Dakika ndio zinakaribia, Nafikiri wananchi wanaosubiri kujua nini kitatokea mahakani leo na kama hii movie itafunika hata ile ya Balali wanaweza kuwa ni wengi na wenye shauku kuliko hata wakati wa kusubiri ile mechi ya juzi ya Stars.

Labda Liyumba ametumia kigezo cha "mpira dakika 90" ndo mana amekaa kimya kusubiri "official appointment" yake ya leo na hakimu Khadija.
 
Dhahiri shahiri leo ni leo maana kitendo cha mh.hadija kimewanyongonyeza sana watumishi wemzake pale kisutu, amewafanya wajione watoto wadogo ktk fani, siku alipomuachia liyumba aliwaacha pccb na wale jamaa toka kwa dpp wafanye watakavyo na pale watetezi wa liyumba walipo raise reasonable doubts alitulia kimya kama kibogoyo asiye na mamlaka, pccb siku ile hawakutegemea jamaa angetimiza masharti kwa 99% hivyo walipoona mseminari anatoka wakaona looh hapa ni kuchafua hali ya hewa kwa kupinga kila jambo lililoletwa mbele ya mh. Hadija, bado hata alipofanya maamuzi ya kumuachia liyumba mh.hadija hakujibu hoja zote za pande mbili na kuiacha hadhira ikiegemea kile walichosema dpp&pccb side kuwa ndio ukweli wenyewe.

Liyumba alitimiza mashariti yote isipokuwa mh. Hadija alikurupuka kutoa maamuzi yake na baadaye akaanza kufanya kazi kwa mujibu wa magazeti, mahakama kuu walipoliita faili waliona mapungufu machache sana ktk application ya dhamana ambayo kisheria hakimu anaweza kuruhusu dhamana huku marekebisho yakifanyika lakini hakukuwa na msimamo huo toka kwa hakimu, all in all pccb wanatakiwa kujibu tuhuma ya kutofuata procedure ya kumfungulia charge liyumba, na hapo ndipo mh.hadija alitakiwa kuanza napo.

Media ime exagarate the whole issue na sasa tusubiri leo maana liyumba akitia timu mh. Hadija atuonyeshe udhaifu wake na pia uwajibikaji.

Tusubiri mseminari kama atatia timu au la!!
 
PCCB wanatufanyia usanii mchana kweupe unawahurumia wa nini mkuu.

Mimi wameniudhi sana; hawa waliomba msaada wa wananchi kumtafuta. Sasa wamempata hawasemi kitu kwa Wananchi maana yake nini..!!??Grrrrrr...ningekuwa Dar es salaam kesho mapema asubihi ningefika Kisutu kusubiri; Liyumba akitoea hata kama akiletwa na hao hao PCCB mimi naenda kuwadai donge nono..!! Nasema nimemuona Liyumba Kisutu, nasikia mnamtafuta..!!

LOL LMAO!!! umenifurahisha sana. kwani watatoa shs ngapi nifunge kiduka changu hapa mbagala niende Kisutu?, umenipa wazo zuri sana! tena mie namsubiri kabla hajaingia kisutu tunazuia gari lake na kupiga picha kisha naanda kudai na wakikataa nafungua kesi!
 
Taarifa rasmi: Liyumba yuko mahakamani Kisutu tayari
 
amekuja mwenyewe pasi escort yao hao PCCB wala polisi, ni familia yake tu ndio amekuja nayo.
 
Hata mimi ningekuwa Liyumba nisingetoroka wala kujificha. Mtuhumiwa halisi wa ubadhirifu huu alishafariki na watu muhimu kama mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani na mkurugenzi fedha hawamo kwenye kesi hii.
La kuangalia kwenye kesi hii sasa ni hii sheria KANDAMIZI ya dhamana. Mtu anatuhumiwa tu kwamba kaiba au kasababisha hasara ya bilioni 221. Hili halijathibitishwa na mahakama anaambiwa atoe nusu ya kiasi hicho anachotuhumiwa kama dhamana! Hatuna akina NDYANABO wengine nchi hii?
 
Hata mimi ningekuwa Liyumba nisingetoroka wala kujificha. Mtuhumiwa halisi wa ubadhirifu huu alishafariki na watu muhimu kama mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani na mkurugenzi fedha hawamo kwenye kesi hii.
La kuangalia kwenye kesi hii sasa ni hii sheria KANDAMIZI ya dhamana. Mtu anatuhumiwa tu kwamba kaiba au kasababisha hasara ya bilioni 221. Hili halijathibitishwa na mahakama anaambiwa atoe nusu ya kiasi hicho anachotuhumiwa kama dhamana! Hatuna akina NDYANABO wengine nchi hii?


Nimekupata Mkuu Wildcard,
Ni lazima wawajibishwe wengi hapa. Si kuonea tu wachache ili kufaidisha umma. Naona hapa kuna kisasi kinalipizwa!!!!!!! Mnayakumbuka ya Babu Seya!!!! Watu walikutana katika anga zao kama vile vyombo ya angani vilivyogongana vile!!!! Tehe!! Tehe!!!
 
Hatimaye kile kitendawili cha ni wapi alipo mshitakiwa Liyumba kimeteguliwa.Hivi ninavyo post thread hii mshitakiwa amefikishwa mahakamani kisutu na maafisa wa TAKUKURU.

Atapandishwa kizimbani muda si mrefu na ndipi itajulikana kama anafutiwa dhamana au la.Stay tuned!
 
hata mimi ningekuwa liyumba nisingetoroka wala kujificha. Mtuhumiwa halisi wa ubadhirifu huu alishafariki na watu muhimu kama mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani na mkurugenzi fedha hawamo kwenye kesi hii.
La kuangalia kwenye kesi hii sasa ni hii sheria kandamizi ya dhamana. Mtu anatuhumiwa tu kwamba kaiba au kasababisha hasara ya bilioni 221. Hili halijathibitishwa na mahakama anaambiwa atoe nusu ya kiasi hicho anachotuhumiwa kama dhamana! Hatuna akina ndyanabo wengine nchi hii?

rip ndyanabo
 
oooooooooops sasa tunapumua kumbe kweli alikuwa kwa mganga wa kienyeji.
Ngoja tusubili kinacho jili....
 
Liyumba bwana si mchezo ni moto wa kuotea mbali ila mradi tu una mapesa kibao ebu soma habari kamili
kutokana na habari za kuaminika kutoka vyanzo vya habari kutoka makachero wapenda nchi yao Tanzania stori ya liyumba ni kama hivi:-
mawakili wake walisuka mpango kabambe na hakimu aliyemuachia kwa kumpa kitu kidogo ili amuachie kwa dhamana ya siku tatu akisingizia kuwa atakuwa nje huku wakikagua na kuhakiki nyaraka alizowakilisha ili apate mdhamana, hii ya kutoonekana kwa liyumba hakimu anajuwa kwa vile mwanzo hakimu aliwakalia, lakini mawakili wakamwambia wataongeza dau kubwa mara mbili, baada ya hapa hakimu alikubuli kiasi hicho kwa maana kwamba hata akiachishwa kazi na kikwete kwa manufaa ya umma atazitumia pesa hizo ambazo yeye hakimu anasema hata kama angefanye kazi kwa miaka 65 asingeweza kuzipata.makachero wanasema kuwa usafiri wa kutumia ulikuwa tayari upo siku hiyo na kama asingetolewa siku hiyo angekaa kwa wiki mbili tena na huku akiwa amepoteza nauli!inaeleza kuwa ndiyo maana liyumba hakutaka kubadilisha kitabu chake cha kusafiria kwa vile anakitabu kingine ambacho muda wake unaisha 2018.Inaelezwa kuwa liyumba alielewa wazi juu ya kukamatwa kwake na kufunguliwa mashitaka,liyumba alipanga kujificha katika nchi 4 au kujimaliza, lakini rafiki yake wa karibu alimushauri hakuna haja ya kufanya hivyo kwa vile serikali ya sasa hivi inaendesha mambo yake kienyeji hivyo si rahisi kama akitorokea nchi za nje itakuwa si kazi rahisi kumfuatilia,akimtolea mfano wa mzee balali!na kwamba anapesa ya kuisha popote pale duniani hivyo swala la kujimaliza alilitoa.makachero wapenda nchi yao wanaripoti kuwa baada ya liyumba kupewa dhamana ile alikaa nyumbani kwake kwa saa 4 na robo hivi ndiyo akasindikizwa na gari moja nyeusi SUV kukiwa na watu wanne kwenye gari hilo mbele wawili na nyuma mmoja na liyumba alikaa kiti cha nyuma kabisa ili asionekana na watu.Inaelezwa pia kuwa mtu aliyekaa mbele na dereva alikuwa na pesa cash ya kutosha mshahara ya walimu wa shule za msingi katika wilaya Dadoma vijijini! ili kama ikitokezea bahati mbaya kugungulika watoe chochote ili waendelee na safari,hata hivyo bahati nzuri hakuna aliyewauliza katika safari hiyo, Inaelezwa kwamba kabla ya kuanza safari aliongea na mkapa,mramba,yona, mama anna mkapa,na maafisa wa benki waliomdhamini(hawa wanajuwa kila kitu hasa OTTO)hata hivyi inaelezwa kuwa alijaribu bila mafanikio kuwapigia simu bwana lowasa,chenge,na mbunge wa igunga bwana rostom lakini simu zao zilikuwa zikiita bila kupokelewa!makachero hao wanazidi kubainisha kuwa gari ile ilikuwa na pesa aina tatu,Tsh,Ksh na US $.nchi ambazo alifikiria kukimbilia ni sweden,denmark,marekani na Pakistani hata hivyo makachero wanasema denmark na sweden alikuwa anaogopa sana kwa vile nchi hizo ni maswahiba wakubwa wa Tanzania hasa kwa ajili ya heshima ya Baba wa Taifa na pakistani makachero wanadai alikuwa anaogopa hali ya usalama wa nchi ile kwa vile kuna watu wa kujilipua mabomu hivyo alisema asingeweza kuishi maisha ya kuogopa mara mbili, kushikwa na wachungu wa pesa za walalahoi wa tanzania na kufa kwa mabomu!kwa asilimia kubwa alipenda kwenda marekani alikofia bosi wake! Makachero wanazidi kueleza kuwa tayari ameshanunua nyumba huko marekani eti kwa vile nyumba huko ni bei poa muda huu kwa ajili ya kuporomoka kwa uchumi wa nchi hiyo.makachero hao wanasema amenunua nyumba inaitwa single house kwenye kitongoji cha clinton maryland zip code 20735 katika barabara ya Piscataway kwa dhamani ya US $ 320,000. Habari inaeleza kuwa aliyemtafutia nyumba hiyo ni mtanzania mmoja anayejishughulisha na uuzaji wa nyumba huko amerika, habari zinadizi kueleza kuwa mtanzania huyo inawekana hajui huyu liyumba nani kwani huyu jamaa muuza nyumba ni muumini sahihi na mfuasi wa Baba wa Taifa ambaye amekuwa hakubaliani na hali ya mwelekeo wa serikali na jinsi ufisadi unavyoua nchi.Bila shaka jamaa huyu anaweza kumlipoti kwa polisi iwapo tu akijuwa liyumba ni FISADI wa kutupwa.
Pia makachero hawa wanasema wananchi wamechukia sana wanasema kuwa iwapo watamtia machoni hakimu aliyemuachia eti watajichukulia hatua mkononi!!!ingawa hawakueleza ni hatua gani watamchukulia,habari hizo zinaeleza kuwa hata wanajeshi wamechukizwa na mwenondo wa ufisadi wa wazi wazi na serikali kutochuwa hatua zifuaazo.
Hata hivyo makachero hao wanasema jaji mkuu hajala chakula tangu iliporipotiwa kuwa liyumba ametoweka,ingawa mwanasheria wa serikali na waziri masha hawajalala tangu siku iliporipotiwa liyumba haonekani.


bullet7.gif
na Masalu Rufirija, Majengo Tabora-Tanzania, - 24.02.09 @ 05:38 | #12384
 
........ Duh movie imeishia bapaya yaani ingekuwa bomba kweli kama asingefika maana tungeunganisha dots mpaka basi.........
 
Basi tena haka ka movie kalikuwa katamu lakini kamekuwa kafupi mno. Uzuri wa ka game ka 'hide and seek' ni kuendelea kutafuta.

Nilitamani apotee jumla ili waliofanya yale madudu waanze kutafutana uchawi.

All and all kwa vile sterling hauwawi, lets watch the true non fiction movie ya court battle of which the PCCB are going to loose anyway.
 
Hatimaye kile kitendawili cha ni wapi alipo mshitakiwa Liyumba kimeteguliwa.Hivi ninavyo post thread hii mshitakiwa amefikishwa mahakamani kisutu na maafisa wa TAKUKURU.

Atapandishwa kizimbani muda si mrefu na ndipi itajulikana kama anafutiwa dhamana au la.Stay tuned!
Asante kwa taarifa, tunasubiri updates
 
Hatimaye kile kitendawili cha ni wapi alipo mshitakiwa Liyumba kimeteguliwa.Hivi ninavyo post thread hii mshitakiwa amefikishwa mahakamani kisutu na maafisa wa TAKUKURU.
Atapandishwa kizimbani muda si mrefu na ndipi itajulikana kama anafutiwa dhamana au la.Stay tuned!
Mkuu,amefikishwa Kisutu na maafisa wa TAKUKURU!?Kuna post nimeziona kule kwenye thread mama zikisema kuwa kafika bila escort yeyote...
Sasa kama TAKUKURU walishakuwanae mbona waliendelea na tangazo lao la donge nono??
 
Akiitwa Stephen Spielberg hapa lazima itoke movie itakayoshinda OSCAR!
 
Du ngomanzito mbona hii ni kubwa sana?? imekuwaje sasa hata akaahirisha safari muheshimiwa huyu?
 
Lazima mfahamu kuna tofauti ya sheria na haki (vitu viwili tofuti), Liyumba alipewa dhamana na mahakama, TAKUKURU wakakata rufaa. Faili likarudishwa Kisutu ili rufani ya dhamani isikilizwe. Kesi ilipangwa tarehe 24 Feb. Sasa wao TAKUKURU walikuwa wanamtafutia nini? Maana kisheria Liyumba yupo mahakamani akiwa upande wa pili wa TAKUKURU . Sasa wewe utamtafutaje mshitakiwa wewe mwenyewe? Polisi wapo, mahakama ipo. Nadhani hawa TAKUKURU wana matatizo yao, walipaswa wamhoji Liyumba kabla ya kumpeleka Kisutu. TAKUKURU wana haki ya kuhoji dhamana lakini wafuate sheria.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom