Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Habari,
Elizabeth Michael akiwa na Marehemu Steven Kanumba
Kesi ya mauaji bila kukusudia inaendelea sasa hivi Mahakama Kuu, Kanda ya Dar. Upande wa utetezi unaendelea kutoa ushahidi ambapo leo ni Mke wa Dr. Slaa mama Mushumbusi ambaye alikuwa ni daktari wa Marehemu anatoa ushahidi ambao utasomwa na Askari Polisi aliyemsimamia wakati anaandika maelezo.
.....................Updates.......................
Mmoja ya wateja wangu, marehemu Steven Kanumba kwa mara ya kwanza alikuja kwangu mwaka 2011 kwa ajili ya kutoa sumu mwilini.
Kanumba alikuwa akisumbuliwa na matatizo mbalimbali na wakati akimhudumia alibaini alikuwa akifanya mazoezi ya kutanua misuli na alimshauri kuyaacha.
Mushumbusi katika maelezo hayo anasema Kanumba alimweleza alihisi kuwa na maumivu ya moyo na alimuomba ampe ushauri.
Marehemu alikuwa na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo, alikuwa anasikia maumivu ktk ubongo na akili kuchoka.
Katika maelezo hayo, amesema siku Kanumba alipokwenda kwake alikuwa na watu wengi, hivyo alimuomba apange siku nyingine na kabla ya kuonana alisikia kuwa amefariki dunia.
Baada ya Detective Sergeant Nengea kumaliza kusoma ushahidi, Jaji amesema kuwa Detective Sergeant Nengea hawezi kuulizwa swali lolote kwa kuwa yeye alikuwa anasoma ushahidi wa mtu ambaye uliandikwa na sio yeye ndio alikuwa shahidi.
Baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao, Mahakama Kuu kesho itasikiliza maoni ya Baraza la wazee kuamua kama Lulu ana hatia au lah.
Elizabeth Michael akiwa na Marehemu Steven Kanumba
.....................Updates.......................
Ushahidi wa Josephine Mushumbusi unasomwa na Detective Sergeant Nengea