Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
- ..... mnaojua sheria zaidi hebu tuambieni sheria inasema nini maana hapo juu ninachokiona ni sheria at work na sio majungu?........
Uongo mwiko vinginevyo utashikiwa mwiko
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
MBONA hivyo mpenzi wangu? Nakaa hapa, nikiwa mbali na wewe, nakuwazia weeee, na kutamani kuwa na wewe, kumbe wewe umejimwaga kwenye ziwa la uchafu. Ndiyo mpenzi, lazima niseme.
Si tulikaa tukakubaliana kwamba mimi nije huko nitafute kazi ili tuweze kujipanga vizuri katika maisha yetu ya baadaye? Siyo? Na tulipoagana, si tulisema kwamba imani ni msingi wa mapenzi. Sasa wakati nakumic kupita kiasi iweje unikasirikie eti kwa nini nakaa mbali na wewe. Sasa wataka nifanyeje?
Huoni kwamba mfuko wetu wa pamoja unaanza kutuna kidogokidogo kutokana na juhudi zangu? Huoni mpenzi? Na biashara yako si imeongezeka kwa sababu ya kakijimshahara kangu. Kwa kweli mpenzi sikulala kabisa baada ya kusikia hasira zako jana kwenye simu eti mimi nakula raha nikiwa mbali na wewe. Si haki kunishambulia namna hiyo hata kidogo. Watia doa kubwa sana katika moyo wangu mweupeeeeeeeeeeeeeeeee juu yako.
Au umenichoka mpenzi? Kama umenichoka si useme tu, si kunishambulia kwa mambo ambayo sijayafanya, au ambayo nimeyafanya kwa makubaliano yetu sisi wawili. Wawezaje kufikiri kwamba naanza kukusahau wakati nakuwazia kila siku kila saa na kufanya jitihada zote kuweza kudunduliza kabla hujaniliza. Na umeniliza kweli safari hii. Nimeumia sana. Nakupenda sana. Jitihada zangu zote ni kwa ajili yetu tu. Najua jana uliomba radhi kabla ya kukata simu lakini sitaki kabisa uingiwe na madudu kichwani tena.
Haya, tuache hayo maana na mimi sitaki kukushambulia pia maana hata ninapoumia moyo bado unadunda kwa mapenzi kwako. Nakupenda, mpenzi usiniponde.
Juzi niliangalia fainali bongo star search ya Uingereza nikashangaa sana. Ulimwona yule mama mzeemzee mnenemnene hana shepu kabisa? Hajui kuvaa, hajui kupanga nguo zake vizuri, mdomo umeenda upande lakini licha ya yote hayo, akawa wa pili katika mashindano. Hebu fikiria angekashifiwa namna gani angekuwa hapa.
‘Hebu liangalie, linene, utamvutia nani ukiwa jukwaani.'
‘Huna staa kwalitii wewe. Hebu tupishe'
Oh nilisahau, kwanza watamcheka wakati anajaribu kuimba na kunong'onezana kama wanafunzi wa darasa la tatu.
Labda pawe na Bongo Jaji Search kuchagua majaji wa vipaji, si majaji wa kujiona bora wao tu. Kisha tuwe na Star Search yenyewe.
Na tukibaki kwa majaji, kuna jambo moja linasumbua kichwa changu mpenzi. Tukiwa shuleni, au tuseme hata tukiwa nyumbani, si tunafundishwa kusema ukweli! Mama yangu kwa kweli hakuwa mshika fimbo hata kidogo lakini alipogundua nimesema uongo .... weeeee!!! Mpaka makalio yalikuwa hayakaliki tena. Uongo mwiko vinginevyo utashikiwa mwiko. Hivyo nilichukia uongo moja kwa moja.
Haya na shuleni pia, ukikamatwa na kosa, utaanza wapi kumwambia mwalimu eti huna hatia, lazima athibitishe kwamba ulikula shea ya mwenzio. Walimu watakucharaza hadi ujute kuzaliwa. Sipendi kabisa tulivyocharazwa lakini nikiangalia hali ya nyumbani na shuleni nashukuru kwamba nilifundwa kuwa mkweli. Hata kama nimefanya kosa, bora kukiri kuliko kujifanya mwamba na kukana.
Lakini sasa nimeanza kuhoji mawazo yangu. Labda ni ya zamani. Maana naona huko mahakamani ni kinyume kabisa. Hata kama umekamatwa unabugia vyakula vya mwenzio, unatakiwa kukana kwamba hujawahi kula hata siku moja katika maisha yako. Kisha unatafuta mtu mwingine aape kwamba usingeweza kula vyakula vile maana wakati ule ulikuwa umelazwa mahututi hospitalini. Eti huu ndio mchezo wa mahakama. Na unaweza kufanikiwa kushinda ‘mchezo huu' na kutoka huku wote wanajua fika ni wewewewe tu uliyebugia pale.
Nadhani hii ndiyo maana mafisadi hawaogopi hata siku moja. Hata wakikamatwa wanafisadi sehemu nyingine wanajua wanao uwezo wa kuwa fisadihaki pia. Ufisadihaki si kuhonga tu ingawa hii ni njia moja. Iweje wote waliotuhumiwa kutula laivu wanaweza kupata wanasheria wenye uwezo wa kupindua vitabu chinijuu ili watoke kwa visingizio vya kipumbavu kabisa. Eti neno moja halikukaa sawasawa katika mashtaka hivyo lazima mtu aachiwe ili aweze kuendelea kutula tena.
Inakera sana mpenzi. Sanasana jamaa wanajua watakula rumande siku chache tu lakini mwisho watatoka na kuendelea kula raha mstarehe. Watatumia wataalamu wale kupinda sheria hadi sheria ikanyage haki. Nakumbuka kusoma mahali fulani kwamba Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Kwingine wana Wizara ya Haki, lakini kwetu ni Wizara ya Sheria. Labda ndiyo maana. Waweza kupinda sheria lakini huwezi kupinda haki.
Nilijaribu mawazo hayo kwa Binti Bosi juzi. Lo, kosa mpenzi. BB anajifanya mpinzani anapotaka kumchokoza baba yake lakini bado anasoma na watoto wa haohao, anakula maisha na haohao, lazima awatetee.
‘We Hidaya unajua nini wewe? Yaani unajiunga na wenzio wenye wivu na inda?'
‘Hapana dada. Nasema tu kwamba naona wengine wanaachiwa huru kwa kupinda sheria tu, si kwa haki.'
‘Na kama wameshtakiwa kwa inda tu? Mbele ya sheria huna hatia hadi ithibitishwe kwamba unayo?'
‘Ni sawa dada. Na wala sitaki mtu ahukumiwe kwa makosa. Lakini inakuwaje wenye uwezo ndio watoke, sisi hohehahe hatuwezi kwa sababu hatuwezi kumwajiri profesa wa kupinda sheria.'
‘Nani kasema wanapinda sheria. Wewe Hidaya ukoje leo. Ili haki itendeke lazima sheria ifuatwe. Na kama kuna dosari katika mashtaka lazima ifichuliwe.'
Hapo mpenzi ilibidi ‘nikubali kosa' kabla sijahukumiwa vingine maana BB alionekana kuwaka moto kwelikweli.
‘Sawa dada. Nimekosea. Asante kwa kunielewesha.'
‘Vizuri sana. Daima usisahau kwamba shida ya hapa Tanzania ni kwamba imejengeka wazo kwamba mtu akiwa tajiri lazima ni fisadi'
‘Ndiyo dada.'
‘Ndiyo. Hatutaki kutambua kwamba mtu anatajirika kutokana na juhudi na akili yake.'
‘Ndiyo dada.'
‘Hata kama kuna mazingira ya kosa, si kosa hadi yathibitishwe. Hapa tunalinda haki ya watu!'
‘Ndiyo dada'
‘Na kama wengine wanazubaa shauri yao.'
‘Ndiyo dada.'
‘Na acha kunindiyo dada, ndiyo dada kama ule wimbo wa kihuni wa ‘Ndiyo mzee'. Nasema ukweli mimi.'
‘Ndiyo dada.'
‘Nimesema ...'
‘Ndi ... samahani, ni kweli dada nakubali.'
Basi BB akaondoka. Lakini mimi bado naona kwamba katika baadhi ya kesi hizo, kama haki haiingiliwi, basi inanunuliwa. Huu anayeitwa wakili ni kwa sababu ni wenye akili ya kufanya nyekundu ionekane buluu. Kwa nini wenye kesi kubwakubwa daima hawapatikani?
Ni kama vile tunadanganyana. Weka ndani kwa siku mbili tatu ili sisi tusio na kitu tufurahi kwamba hatimaye mafisi wamepatikana kisha afutiwe mashtaka eti yalikuwa na makosa, wakati tunaona kosa bado liko palepale. Na kubwa zaidi, kwa nini msingi wa mahakama uwe ni kusema uongo, ukane na kukana huku ukijua fika umetenda. Tunafundisha nini hapa? Mama yangu alikosea kunifundisha niseme ukweli? Eti uongo haulipi wakati tunaona unalipa kila siku.
Akupendaye kwa dhati mpenzi wangu, kwa dhati ya nyati,
Na hapo nimesema kweli, kweli tupu, Mungu anisaidie,
Hidaya,
Diplomatic immunity ingeapply kama angekuwa anashitakiwa na Italy, hapa naona tunapigwa changa la macho!
Mahakama: Balozi Prof Mahalu hana kinga ya kushitakiwa
Na Nora Damian (Mwananchi)
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na mwenzake kutaka kupitiwa upya kwa mwenendo wa kesi yao ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni.
Jaji Juxon Mlay alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ina mamlaka zote kisheria kuendesha kesi hivyo akaamuru kesi hiyo iendelee kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Awali katika maombo ya upande wa utetezi ulidai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ua kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa washtakiwa wanakinga ya kibalozi na kwamba makosa hayo yalifanyika nje ya Tanzania.
Alisema hoja kuhusu ushahidi wa mwisho uliochukuliwa kwa njia ya video hawezi kuizungumzia kwa sabababu suala hilo tayari lilishatolewa uamuzi na Mahakama ya Kisutu.
Pia alisema sheria za Tanzania zinaweza kuingilia nchi yeyote na kwa mtu yeyote mwenye kinga ambaye atakuwa ametenda makosa nje ya nchi isipokuwa rais.
Mwenye kinga ya moja kwa moja ni rais tu na suala hilo liko kwenye katiba kwa washitakiwa hawa kinga ingeweza kuwasaidia wakiwa kule Italia, lakini si hapa kwetu,?alisema Jaji Mlay.
Hata hivyo akizungumza nje ya mahakama mara baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi, Bobu Makani alisema watakata rufaa kwasababu hawajaridhika na uamuzi huo.
Mahalu na aliyekuwa ofisa Utawala wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Grace Martin wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh2 bilioni.
Mei 4, mwaka huu washitakiwa hao walitakiwa waanze kujitetea, lakini mawakili wao waliwasilisha Mahakama Kuu maombi ya kupitiwa upya kwa mwenendo wa kesi yao.
Katika maombi yao, upande wa utetezi unadai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo vinginevyo kiwepo kibali cha Jaji Mkuu.
Pia wanadai kuwa ushahidi wa mwisho uliochukuliwa kwa njia ya video haukuchukuliwa kihalali kwasababu hakuna sheria inayoruhusu kufanya hivyo.
Upande wa utetezi pia unadai kuwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka kuruhusu kesi hiyo isikilizwe kilichelewa kutolewa, kwani wakati washitakiwa wanafikishwa mahakamani hakikuambatanishwa na hati ya mashitaka.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika ubalozi wa Tanzania nchini Italia waliisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 2 bilioni wakati wa ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo.
Juni 2 mwaka huu, kesi hiyo ilipotajwa kwa mara nyingine, upande wa utetezi ulidai kuwa washitakiwa hao hawakupaswa kushitakiwa kwasababu walikuwa na kinga maalumu kwa vile walikuwa maafisa wa ubalozi.
Mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi Mabere Marando alieleza hayombele ya Jaji Juxon Mlay wa Mahakama Kuu wakati wa kusikilizwa maombi ya washitakiwa hao ya kutaka kupitiwa upya mwenendo wa kesi yao iliyoko katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Marando alidai kuwa washitakiwa ni wanadiplomasia na wana kinga maalumu hivyo mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao vinginevyo kinga yao iwe imeondolewa.
Makosa yametendeka Italia lakini yamesikilizwa Kisutu ambayo haina mamlaka kisheria, vinginevyo wangepata kibali cha Jaji Mkuu lakini hawakufanya hivyo,alidai Marando.
Wakili huyo alidai kuwa hata upokeaji wa ushahidi wa mwisho kwa njia ya video kutoka nchini Italia ulifanywa kinyume kwani hakuna sheria yoyote inayoruhusu kufanya hivyo.
Alidai kuwa kuna upungufu mwingi waliyouona katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo waliyawasilisha lakini walipuuzwa.
Hata kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kinachoruhusu kesi hiyo isikilizwe Kisutu kimetengenezwa baada ya sisi kulalamika, kwasababu katika hati ya mashitaka hakikuwepo,alidai Marando.
Marando alidai kuwa hati ya mashitaka ilipelekwa mahakamani Januari 11, 2007 na washitakiwa wakafikishwa mahakamani Januari 22, 2007 lakini kibali cha DPP kilitolewa Aprili 25, 2007.
Akijibu hoza hizo Wakili wa Serikali, Boniface Stanslaus alidai kuwa sio mapungufu yote ambayo mahakama ya juu inaweza ikayatolea maamuzi na kwamba Mahakama ya Kisutu ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Kuhusu makosa kufanyika nchini Italia, alidai kuwa katika hati ya mashitaka hakuna sehemu inayosema yamefanyika jijini Roma ila inaonyesha yamefanyika ubalozi wa Tanzania ambao uko Roma ambao kisheria ni sawa na Tanzania.
Hata hivyo wakili huyo alipotakiwa na Jaji Mlay kutaja sheria hiyo alishindwa.
Alidai kuwa ushahidi wa njia ya video ulishatolewa uamuzi mahakamani na kwamba, washitakiwa walipaswa kusubiri kesi hiyo iishe ili wasubiri kukata rufaa kama hawakuridhika.
Pia wakili huyo wa serikali alikiri kuwa washitakiwa wana hadhi, lakini akasema si kila wanachokifanya kinakuwa na kinga na kwamba tuhuma walizonazo zilikuwa na uhusiano na shughuli za kibalozi.
Baada ya kusikiliza hoja zote, Jaji Mlay aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 8 mwaka huu atakapotoa uamuzi. Mahalu na Grace Martin walitakiwa waanze kujitetea Mei 4 mwaka huu baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaona wana kesi ya kujibu lakini mawakili wao waliwasilisha maombi Mahakama Kuu wakiomba kupitiwa upya kwa mwenendo wa kesi hiyo.
suala ni kwamba kama mahakama itamtia hatiani hizo kelele zitabakia za chura tuuu..Tatizo la uamuzi wa Mahalu ni kifo cha mwenye nyumba kwa kugongwa na nyoka:Kitakachofuata hapo ni msiba na matokeo kuku atachinjwa, siku ya mazishi mbuzi atachinjwa, kumaliza tatu na kuondoa matanga ndama atakwenda na maji na arobaini ikifika basi ng'ombe atakiona cha moto kisa nini eti nyoka alimgonga baba mwenye nyumba; wengi tu wataunga huo msafara, wenye masikio na wasikie.
Tatizo la kesi hii ni.....................selective justice.........................wako wapi katibu mkuu Bw. Philemon Luhanjo na Waziri wa Mambao ya nje JK kuwepo kwenye hii kesi.....................kwa sababu ulaji huu ulipojitokeza wakati wao ndiyo viongozi pale........................sasa iwaje wao wakae kando huku ndiyo walikuwa wahimili wa mwisho katika wizara tajwa?
Check ur facts..huyo wala hakuwepoTatizo la kesi hii ni.....................selective justice.........................wako wapi katibu mkuu Bw. Philemon Luhanjo na Waziri wa Mambao ya nje JK kuwepo kwenye hii kesi.....................kwa sababu ulaji huu ulipojitokeza wakati wao ndiyo viongozi pale........................sasa iwaje wao wakae kando huku ndiyo walikuwa wahimili wa mwisho katika wizara tajwa?
Tatizo la kesi hii ni.....................selective justice.........................wako wapi katibu mkuu Bw. Philemon Luhanjo na Waziri wa Mambao ya nje JK kuwepo kwenye hii kesi.....................kwa sababu ulaji huu ulipojitokeza wakati wao ndiyo viongozi pale........................sasa iwaje wao wakae kando huku ndiyo walikuwa wahimili wa mwisho katika wizara tajwa?
Check ur facts..huyo wala hakuwepo