Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Diplomatic immunity ingeapply kama angekuwa anashitakiwa na Italy, hapa naona tunapigwa changa la macho!
 
LOL! what a joke. Now they are just throwing out any garbage hoping something will stick.
 
nahisi jamaa yupo mbioni kukimbia nje ya nchi ili akapate hiyo Diplomatic immunity, mambo ya Tanzania ni ya ajabu kwelikweli, hiyo kesi ya jamaa hipo wazi kabisa na ushahidi wote upo sasa kwa nini sijuhi hukumu haitolewi?
 
- Haya ni masuala ya sheria sio siasa za ufisadi, mnaojua sheria zaidi hebu tuambieni sheria inasema nini maana hapo juu ninachokiona ni sheria at work na sio majungu? Hii kesi itaishia kuwa yale yale ya kukurupuka na siasa kumbe ni cheap popularity sheria wala haiko karibu!

Respect.

FMEs!
 
Kuhusu technicalities ni kweli wanasheria wetu wanatumia kama kichaka cha kujificha ili issue ya msingi isiongelewe. Kuhusu kesi ya Dito sio tu kwamba Mungu alimchukua ila aliichukua na kesi yenyewe ambayo hukumu yake ilikuwa ni kifo baada ya kuona wanadamu wanapindisha ukweli.

Mahakama ndio ilitakiwa iseme kama ni murder case au manslaughter na sio polisi!
 
Hata tukatae au tukubali, lakini vyombo vya habari vya ThisDay na Kulikoni vimesaidia sana kuibua ufisadi ndani na nje ya nchi.

Tatizo ni namna ambavyo serikali inavyoshughulikia hizi kesi. Hawa Advocates (private) wana ujanja sana, kama kesi has a lucrative pay, hawalali!!!! ni kupekua vitabu kutafuta technical failures tu. Sasa je hawa wetu wa serikali wana muda wa kukaa na kupitia vifungu vyote muhimu ili wawe competent kubishana kisheria??

Kuna kesi moja nilihudhuria for interest tu, yaani wanasheria wa serikali waligaragazwa kama kibaka, hadi unaona kabisa anataka kutamka tu nimeshindwa mzee. Nilishangaa sana , their competence!!!. Kesi nyingi za msingi hawataziweza, zitawashinda.

Wajiandae tu kuja kujibu za fidia.
 
Mkimsoma "Hidaya" katika Raia Mwema mutaelewa maana yake nini. Kwa faida ya JF na kwa hisani ya Raia Mwema, nawawekea Hidaya hapa chini baada ya maelezo yangu.

Ila kuhusu kibali cha DPP kilitolewa na ndiye aliyeandaa mashitaka yaliyowasilishwa Kisutu. LAkini jambo la msingi ni kwamba, hivi kwanini kama anajiamini hajatenda kosa akimbie usikilizwaji wa kesi na sasa atake kuzuia isisikilizwe? Siku zote alikuwa wapi?


Uongo mwiko vinginevyo utashikiwa mwiko
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
MBONA hivyo mpenzi wangu? Nakaa hapa, nikiwa mbali na wewe, nakuwazia weeee, na kutamani kuwa na wewe, kumbe wewe umejimwaga kwenye ziwa la uchafu. Ndiyo mpenzi, lazima niseme.
Si tulikaa tukakubaliana kwamba mimi nije huko nitafute kazi ili tuweze kujipanga vizuri katika maisha yetu ya baadaye? Siyo? Na tulipoagana, si tulisema kwamba imani ni msingi wa mapenzi. Sasa wakati nakumic kupita kiasi iweje unikasirikie eti kwa nini nakaa mbali na wewe. Sasa wataka nifanyeje?
Huoni kwamba mfuko wetu wa pamoja unaanza kutuna kidogokidogo kutokana na juhudi zangu? Huoni mpenzi? Na biashara yako si imeongezeka kwa sababu ya kakijimshahara kangu. Kwa kweli mpenzi sikulala kabisa baada ya kusikia hasira zako jana kwenye simu eti mimi nakula raha nikiwa mbali na wewe. Si haki kunishambulia namna hiyo hata kidogo. Watia doa kubwa sana katika moyo wangu mweupeeeeeeeeeeeeeeeee juu yako.
Au umenichoka mpenzi? Kama umenichoka si useme tu, si kunishambulia kwa mambo ambayo sijayafanya, au ambayo nimeyafanya kwa makubaliano yetu sisi wawili. Wawezaje kufikiri kwamba naanza kukusahau wakati nakuwazia kila siku kila saa na kufanya jitihada zote kuweza kudunduliza kabla hujaniliza. Na umeniliza kweli safari hii. Nimeumia sana. Nakupenda sana. Jitihada zangu zote ni kwa ajili yetu tu. Najua jana uliomba radhi kabla ya kukata simu lakini sitaki kabisa uingiwe na madudu kichwani tena.
Haya, tuache hayo maana na mimi sitaki kukushambulia pia maana hata ninapoumia moyo bado unadunda kwa mapenzi kwako. Nakupenda, mpenzi usiniponde.
Juzi niliangalia fainali bongo star search ya Uingereza nikashangaa sana. Ulimwona yule mama mzeemzee mnenemnene hana shepu kabisa? Hajui kuvaa, hajui kupanga nguo zake vizuri, mdomo umeenda upande lakini licha ya yote hayo, akawa wa pili katika mashindano. Hebu fikiria angekashifiwa namna gani angekuwa hapa.
‘Hebu liangalie, linene, utamvutia nani ukiwa jukwaani.'
‘Huna staa kwalitii wewe. Hebu tupishe'
Oh nilisahau, kwanza watamcheka wakati anajaribu kuimba na kunong'onezana kama wanafunzi wa darasa la tatu.
Labda pawe na Bongo Jaji Search kuchagua majaji wa vipaji, si majaji wa kujiona bora wao tu. Kisha tuwe na Star Search yenyewe.
Na tukibaki kwa majaji, kuna jambo moja linasumbua kichwa changu mpenzi. Tukiwa shuleni, au tuseme hata tukiwa nyumbani, si tunafundishwa kusema ukweli! Mama yangu kwa kweli hakuwa mshika fimbo hata kidogo lakini alipogundua nimesema uongo .... weeeee!!! Mpaka makalio yalikuwa hayakaliki tena. Uongo mwiko vinginevyo utashikiwa mwiko. Hivyo nilichukia uongo moja kwa moja.

Haya na shuleni pia, ukikamatwa na kosa, utaanza wapi kumwambia mwalimu eti huna hatia, lazima athibitishe kwamba ulikula shea ya mwenzio. Walimu watakucharaza hadi ujute kuzaliwa. Sipendi kabisa tulivyocharazwa lakini nikiangalia hali ya nyumbani na shuleni nashukuru kwamba nilifundwa kuwa mkweli. Hata kama nimefanya kosa, bora kukiri kuliko kujifanya mwamba na kukana.
Lakini sasa nimeanza kuhoji mawazo yangu. Labda ni ya zamani. Maana naona huko mahakamani ni kinyume kabisa. Hata kama umekamatwa unabugia vyakula vya mwenzio, unatakiwa kukana kwamba hujawahi kula hata siku moja katika maisha yako. Kisha unatafuta mtu mwingine aape kwamba usingeweza kula vyakula vile maana wakati ule ulikuwa umelazwa mahututi hospitalini. Eti huu ndio mchezo wa mahakama. Na unaweza kufanikiwa kushinda ‘mchezo huu' na kutoka huku wote wanajua fika ni wewewewe tu uliyebugia pale.
Nadhani hii ndiyo maana mafisadi hawaogopi hata siku moja. Hata wakikamatwa wanafisadi sehemu nyingine wanajua wanao uwezo wa kuwa fisadihaki pia. Ufisadihaki si kuhonga tu ingawa hii ni njia moja. Iweje wote waliotuhumiwa kutula laivu wanaweza kupata wanasheria wenye uwezo wa kupindua vitabu chinijuu ili watoke kwa visingizio vya kipumbavu kabisa. Eti neno moja halikukaa sawasawa katika mashtaka hivyo lazima mtu aachiwe ili aweze kuendelea kutula tena.
Inakera sana mpenzi. Sanasana jamaa wanajua watakula rumande siku chache tu lakini mwisho watatoka na kuendelea kula raha mstarehe. Watatumia wataalamu wale kupinda sheria hadi sheria ikanyage haki. Nakumbuka kusoma mahali fulani kwamba Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Kwingine wana Wizara ya Haki, lakini kwetu ni Wizara ya Sheria. Labda ndiyo maana. Waweza kupinda sheria lakini huwezi kupinda haki.
Nilijaribu mawazo hayo kwa Binti Bosi juzi. Lo, kosa mpenzi. BB anajifanya mpinzani anapotaka kumchokoza baba yake lakini bado anasoma na watoto wa haohao, anakula maisha na haohao, lazima awatetee.
‘We Hidaya unajua nini wewe? Yaani unajiunga na wenzio wenye wivu na inda?'
‘Hapana dada. Nasema tu kwamba naona wengine wanaachiwa huru kwa kupinda sheria tu, si kwa haki.'
‘Na kama wameshtakiwa kwa inda tu? Mbele ya sheria huna hatia hadi ithibitishwe kwamba unayo?'
‘Ni sawa dada. Na wala sitaki mtu ahukumiwe kwa makosa. Lakini inakuwaje wenye uwezo ndio watoke, sisi hohehahe hatuwezi kwa sababu hatuwezi kumwajiri profesa wa kupinda sheria.'
‘Nani kasema wanapinda sheria. Wewe Hidaya ukoje leo. Ili haki itendeke lazima sheria ifuatwe. Na kama kuna dosari katika mashtaka lazima ifichuliwe.'
Hapo mpenzi ilibidi ‘nikubali kosa' kabla sijahukumiwa vingine maana BB alionekana kuwaka moto kwelikweli.
‘Sawa dada. Nimekosea. Asante kwa kunielewesha.'
‘Vizuri sana. Daima usisahau kwamba shida ya hapa Tanzania ni kwamba imejengeka wazo kwamba mtu akiwa tajiri lazima ni fisadi'
‘Ndiyo dada.'
‘Ndiyo. Hatutaki kutambua kwamba mtu anatajirika kutokana na juhudi na akili yake.'
‘Ndiyo dada.'
‘Hata kama kuna mazingira ya kosa, si kosa hadi yathibitishwe. Hapa tunalinda haki ya watu!'
‘Ndiyo dada'
‘Na kama wengine wanazubaa shauri yao.'
‘Ndiyo dada.'
‘Na acha kunindiyo dada, ndiyo dada kama ule wimbo wa kihuni wa ‘Ndiyo mzee'. Nasema ukweli mimi.'
‘Ndiyo dada.'
‘Nimesema ...'
‘Ndi ... samahani, ni kweli dada nakubali.'
Basi BB akaondoka. Lakini mimi bado naona kwamba katika baadhi ya kesi hizo, kama haki haiingiliwi, basi inanunuliwa. Huu anayeitwa wakili ni kwa sababu ni wenye akili ya kufanya nyekundu ionekane buluu. Kwa nini wenye kesi kubwakubwa daima hawapatikani?
Ni kama vile tunadanganyana. Weka ndani kwa siku mbili tatu ili sisi tusio na kitu tufurahi kwamba hatimaye mafisi wamepatikana kisha afutiwe mashtaka eti yalikuwa na makosa, wakati tunaona kosa bado liko palepale. Na kubwa zaidi, kwa nini msingi wa mahakama uwe ni kusema uongo, ukane na kukana huku ukijua fika umetenda. Tunafundisha nini hapa? Mama yangu alikosea kunifundisha niseme ukweli? Eti uongo haulipi wakati tunaona unalipa kila siku.
Akupendaye kwa dhati mpenzi wangu, kwa dhati ya nyati,
Na hapo nimesema kweli, kweli tupu, Mungu anisaidie,
Hidaya,
 
Diplomatic immunity ingeapply kama angekuwa anashitakiwa na Italy, hapa naona tunapigwa changa la macho!


Kuna Barozi wa Poland Nchini Marekani aligonga mtu na kuua akiwa amelewa, Marekani ilichofanya ni kuondoa hiyo immunity mara moja na kusweka Lupango, bado yuko jela toka 1999.
 
Hawa wanataka kuendelea kuivuta hii case sijui mpaka lini?

Mahakama: Balozi Prof Mahalu hana kinga ya kushitakiwa
Na Nora Damian (Mwananchi)

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na mwenzake kutaka kupitiwa upya kwa mwenendo wa kesi yao ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni.

Jaji Juxon Mlay alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ina mamlaka zote kisheria kuendesha kesi hivyo akaamuru kesi hiyo iendelee kusikilizwa katika mahakama hiyo.

Awali katika maombo ya upande wa utetezi ulidai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ua kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa washtakiwa wanakinga ya kibalozi na kwamba makosa hayo yalifanyika nje ya Tanzania.

Alisema hoja kuhusu ushahidi wa mwisho uliochukuliwa kwa njia ya video hawezi kuizungumzia kwa sabababu suala hilo tayari lilishatolewa uamuzi na Mahakama ya Kisutu.

Pia alisema sheria za Tanzania zinaweza kuingilia nchi yeyote na kwa mtu yeyote mwenye kinga ambaye atakuwa ametenda makosa nje ya nchi isipokuwa rais.

Mwenye kinga ya moja kwa moja ni rais tu na suala hilo liko kwenye katiba kwa washitakiwa hawa kinga ingeweza kuwasaidia wakiwa kule Italia, lakini si hapa kwetu,?alisema Jaji Mlay.

Hata hivyo akizungumza nje ya mahakama mara baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi, Bobu Makani alisema watakata rufaa kwasababu hawajaridhika na uamuzi huo.

Mahalu na aliyekuwa ofisa Utawala wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Grace Martin wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh2 bilioni.

Mei 4, mwaka huu washitakiwa hao walitakiwa waanze kujitetea, lakini mawakili wao waliwasilisha Mahakama Kuu maombi ya kupitiwa upya kwa mwenendo wa kesi yao.

Katika maombi yao, upande wa utetezi unadai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo vinginevyo kiwepo kibali cha Jaji Mkuu.

Pia wanadai kuwa ushahidi wa mwisho uliochukuliwa kwa njia ya video haukuchukuliwa kihalali kwasababu hakuna sheria inayoruhusu kufanya hivyo.

Upande wa utetezi pia unadai kuwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka kuruhusu kesi hiyo isikilizwe kilichelewa kutolewa, kwani wakati washitakiwa wanafikishwa mahakamani hakikuambatanishwa na hati ya mashitaka.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika ubalozi wa Tanzania nchini Italia waliisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 2 bilioni wakati wa ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo.

Juni 2 mwaka huu, kesi hiyo ilipotajwa kwa mara nyingine, upande wa utetezi ulidai kuwa washitakiwa hao hawakupaswa kushitakiwa kwasababu walikuwa na kinga maalumu kwa vile walikuwa maafisa wa ubalozi.

Mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi Mabere Marando alieleza hayombele ya Jaji Juxon Mlay wa Mahakama Kuu wakati wa kusikilizwa maombi ya washitakiwa hao ya kutaka kupitiwa upya mwenendo wa kesi yao iliyoko katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Marando alidai kuwa washitakiwa ni wanadiplomasia na wana kinga maalumu hivyo mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao vinginevyo kinga yao iwe imeondolewa.

Makosa yametendeka Italia lakini yamesikilizwa Kisutu ambayo haina mamlaka kisheria, vinginevyo wangepata kibali cha Jaji Mkuu lakini hawakufanya hivyo,alidai Marando.

Wakili huyo alidai kuwa hata upokeaji wa ushahidi wa mwisho kwa njia ya video kutoka nchini Italia ulifanywa kinyume kwani hakuna sheria yoyote inayoruhusu kufanya hivyo.

Alidai kuwa kuna upungufu mwingi waliyouona katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo waliyawasilisha lakini walipuuzwa.

Hata kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kinachoruhusu kesi hiyo isikilizwe Kisutu kimetengenezwa baada ya sisi kulalamika, kwasababu katika hati ya mashitaka hakikuwepo,alidai Marando.

Marando alidai kuwa hati ya mashitaka ilipelekwa mahakamani Januari 11, 2007 na washitakiwa wakafikishwa mahakamani Januari 22, 2007 lakini kibali cha DPP kilitolewa Aprili 25, 2007.

Akijibu hoza hizo Wakili wa Serikali, Boniface Stanslaus alidai kuwa sio mapungufu yote ambayo mahakama ya juu inaweza ikayatolea maamuzi na kwamba Mahakama ya Kisutu ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kuhusu makosa kufanyika nchini Italia, alidai kuwa katika hati ya mashitaka hakuna sehemu inayosema yamefanyika jijini Roma ila inaonyesha yamefanyika ubalozi wa Tanzania ambao uko Roma ambao kisheria ni sawa na Tanzania.

Hata hivyo wakili huyo alipotakiwa na Jaji Mlay kutaja sheria hiyo alishindwa.

Alidai kuwa ushahidi wa njia ya video ulishatolewa uamuzi mahakamani na kwamba, washitakiwa walipaswa kusubiri kesi hiyo iishe ili wasubiri kukata rufaa kama hawakuridhika.

Pia wakili huyo wa serikali alikiri kuwa washitakiwa wana hadhi, lakini akasema si kila wanachokifanya kinakuwa na kinga na kwamba tuhuma walizonazo zilikuwa na uhusiano na shughuli za kibalozi.

Baada ya kusikiliza hoja zote, Jaji Mlay aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 8 mwaka huu atakapotoa uamuzi. Mahalu na Grace Martin walitakiwa waanze kujitetea Mei 4 mwaka huu baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaona wana kesi ya kujibu lakini mawakili wao waliwasilisha maombi Mahakama Kuu wakiomba kupitiwa upya kwa mwenendo wa kesi hiyo.
 
Hakika mimi mpaka sasa najiuliza kwanini kesi hii isimamiwe na PCCB? kwani kesi hii ni ya rushwa?

Nikisoma vizuri naona kesi hii inaangukia kwenye KUGHUSHI.

Sasa iweje ichukuliwe kama ya rushwa.

Labda wanasharia mnifafanulie hapo.

Dr Hamza (Barubaru)
 
Tatizo la uamuzi wa Mahalu ni kifo cha mwenye nyumba kwa kugongwa na nyoka:Kitakachofuata hapo ni msiba na matokeo kuku atachinjwa, siku ya mazishi mbuzi atachinjwa, kumaliza tatu na kuondoa matanga ndama atakwenda na maji na arobaini ikifika basi ng'ombe atakiona cha moto kisa nini eti nyoka alimgonga baba mwenye nyumba; wengi tu wataunga huo msafara, wenye masikio na wasikie.
suala ni kwamba kama mahakama itamtia hatiani hizo kelele zitabakia za chura tuuu..

ni kweli viongozi wengi serikalini wamechafuka na rushwaa ila bado kutiwa hatiani na huwezi kulazimisha nao wakamatwe kisa wewe umefunguliwa kesiii!!!! tehe tehe tehe..

na kwa sasa wajijue hawako pamoja kiasi hicho kwani wanaviziana tuu ni masuala ya muda.

naingojea kesi ya RICHMOND 2016....new people in power looking for their enemies in attaining power and creating popularity for next election...
 
Akina Balozi Mahalu kuanza kutoa utetezi Februari 24

Saturday, 29 January 2011
Tausi Ally

BALOZI wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na aliyekuwa Ofisa utawala wa ubalozi huo, Grace Martin, Februari 24, mwaka huu wataanza kutoa utetezi wao dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi na kusababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh2 bilioni inayowakabili.

Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Ilvin Mgeta, wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Kabla ya hakimu Mgeta kusema hayo, Wakili wa Serikali, Zuber Mkakatu, alidai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kuomba mahakama kupanga tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi.

Hakimu Mgeta alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea dhidi ya mashtaka yanayowakabili.

Katika kesi hiyo, tayari upande wa mashtaka umefunga ushahidi baada ya mashahidi wao saba kumaliza kutoa ushahidi.

Mahalu na Martin wanadaiwa kuwa, Septemba 23, 2002 katika ubalozi wa Tanzania jijini Roma, wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walisababishia hasara serikali ya Euro 2,065,827.60.

Washtakiwa hao wanadaiwa kusaini vocha yenye namba D2/9/23/9/02 ikionyesha kuwa, bei ya ununuzi wa jengo la ubalozi ni Euro 3,098,741.58 maelezo ambayo yalikuwa ni ya uongo na yenye nia ya kumdanganya mwajiri wao.

Pia, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa, Oktoba Mosi, 2002 walitumia hati ya malipo ya Euro 3,098,741.58 wakionyesha kuwa, muuzaji wa jengo hilo alipokea fedha hizo huku wakijua ni uongo.
 
Tatizo la kesi hii ni.....................selective justice.........................wako wapi katibu mkuu Bw. Philemon Luhanjo na Waziri wa Mambao ya nje JK kuwepo kwenye hii kesi.....................kwa sababu ulaji huu ulipojitokeza wakati wao ndiyo viongozi pale........................sasa iwaje wao wakae kando huku ndiyo walikuwa wahimili wa mwisho katika wizara tajwa?
 
Tatizo la kesi hii ni.....................selective justice.........................wako wapi katibu mkuu Bw. Philemon Luhanjo na Waziri wa Mambao ya nje JK kuwepo kwenye hii kesi.....................kwa sababu ulaji huu ulipojitokeza wakati wao ndiyo viongozi pale........................sasa iwaje wao wakae kando huku ndiyo walikuwa wahimili wa mwisho katika wizara tajwa?

kesi hii ni magumashi tupu hakuna la maana pale
 
Tatizo la kesi hii ni.....................selective justice.........................wako wapi katibu mkuu Bw. Philemon Luhanjo na Waziri wa Mambao ya nje JK kuwepo kwenye hii kesi.....................kwa sababu ulaji huu ulipojitokeza wakati wao ndiyo viongozi pale........................sasa iwaje wao wakae kando huku ndiyo walikuwa wahimili wa mwisho katika wizara tajwa?
Check ur facts..huyo wala hakuwepo
 
Tatizo la kesi hii ni.....................selective justice.........................wako wapi katibu mkuu Bw. Philemon Luhanjo na Waziri wa Mambao ya nje JK kuwepo kwenye hii kesi.....................kwa sababu ulaji huu ulipojitokeza wakati wao ndiyo viongozi pale........................sasa iwaje wao wakae kando huku ndiyo walikuwa wahimili wa mwisho katika wizara tajwa?

You are thinking like a layman! Umeambiwa akina Mahalu walisaini Vocha na kuisababishia hasara serikali, sasa hapa Luhanjo na JK wanaingiaje hapa? Kama wanawajibika ni kisiasa (which is discretionary) na kamwe si kisheria!
 
This is just one of those very embarassing aspects about Tanzania's legal system. It is a shame. Theft occured in 2002 and nine years later the case is still in our courts. There might be some reasons, but the most important ones might include corruption (most likely), negligence of all those involved in the case-prosecutors and magistrates, intefrence from higher authorities.

Mind you, this is not the only case which is going at a snail's pace. The Mramba and co., the Patels of EPA, other EPA cases, etc. If I compare what is happening in Tanznaia's legal system with what is happening elsewhere in the world, I tend to believe that maybe there is no need for a legal system in our country as it serves to punish the down-trodden.
 
By JULIUS BWAHAMA,
5th May 2011

THE defence in a corruption case against former Tanzanian ambassador to Italy Prof Costa Ricky Mahalu and counsellor Grace Martin has sent a letter to President Jakaya Kikwete requesting him to appear before the Kisutu Resident Magistrate's court as a witness.

The accused are charged with causing the government of Tanzania a loss of 2m Euros during the purchase of an embassy building in Italy.

Defence lawyer Mr Mabere Marando told the 'Daily News' that he had sent a letter on May 2 this year to ask the President to appear as a witness.

He said according to the Presidential Affairs Act, if one wishes to have the president appear in court as a witness he or she does so through the Chief Secretary to the cabinet and if the president finds it impossible to appear he can submit an affidavit.

Mr Marando said after submitting in court the affidavit, the advocate can ask the magistrate to use it as evidence and in case the prosecution objects then the advocate can ask the witness to appear physically.

"In case the prosecution objects the use of the affidavit as evidence then I will have to ask the witness to appear physically," Marando told the 'Daily News' on Thursday.

The advocate added that there would be a total of ten witnesses in Mahalu's defence among them former president Mr Benjamin Mkapa, the current President, Mr Jakaya Kikwete, former Finance Minister Mr Basil Mramba and Mahalu himself.

Meanwhile, Mr Marando on Tuesday submitted an affidavit of former president Benjamin Mkapa at the court.

The affidavit was submitted in reply to a letter which was requesting Mr Mkapa to appear as a witness for the defence.

In the affidavit Mr Mkapa made an oath and stated among other things that the embassy building in Rome was purchased during his term as executive president of the United Republic of Tanzania.

He states that through the process of government machinery, he was made aware of the fact that the government's valuation reports for the building identified for purchase by government was established by the Ministry of Works at USD 3.0m and Ministry for Lands and Urban Development at Euro 5.5m.

Mr Mkapa states that through the process of government machinery, he was made aware of the fact that the embassy building was purchased at USD 3m then equivalent to Euros 3,098,741.40.

He also states that through the process of government machinery, he was made aware of the fact that the Ambassador of Tanzania in Rome was given full authority to oversee and execute the process which led to the purchase of the embassy building through a government's power of attorney and that he inaugurated the building in Rome on February 23, 2003.

Lastly he states that for the entire period he has worked with the ambassador in his various capacities in government service, Mahalu depicted a strong character of sincerity, honesty, obedience and worked hard, qualities which led to his being awarded with one of the Highest National Honours by the President of the Republic of Italy on an Italian National Commemoration Day, long after he had left the country.

The case will resume on May 31 this year when the defence witnesses will begin to testify.
 
Back
Top Bottom