Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Prof Mahalu ni fisadi kama walivyo wengine aliyebobea katika fraud na kisheria huyo ndo mwenyewe wanayo law firm yao kama sikosei maeneo ya O'Bay na ni mmoja wa washirika wakubwa wa ndg Joseph Sinde Warioba ambaye naye ni mwanahisa katika hiyo law firm.

Uadui labda alikuwa anambypass na kumdharau kwa sababu yeye ni prof na jamaa ni graduate wa kawaida. Naweza kusema hivyo kwa sababu watu pia walidai kuwa Muungwana alikuwa na bifu na Mwandosya wakati wakiwa pale madini.

Ila all in all hawa majamaa kutokana na huo uprofesa wao huwa wanajifanya wajuaji katika kila kitu so may be jamaa kwa vigezo akamchukulia hatua.
 
tUSUBIRIE MATOKEO YA KESI........NDIO HAPO TUNAWEZA KUONGEA LOLOTE KWA SASA NGOJA MAHAKAMA ITUMIE BUSARA /UHURU WAKE KUAMUA........
 
Takukuru: Mahalu alifanya udanganyifu

Mariam Mogella
Daily News;
Friday,October 24, 2008

Ofisa wa Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) tawi la Sumbawanga, Isidoni Kyando (36) ambaye ni shahidi wa sita katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, jana alidai mahakamani kuwa ni kweli washitakiwa walitumia mkataba wa pili kufanya udanganyifu na wizi huo.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam mbele ya Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa, Sivangilwa Mwangesi, Kyando alidai alishiriki kuchunguza ubadhirifu katika ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, lililonunuliwa kwa Euro milioni tatu.

Alidai washitakiwa wote wawili, Profesa Mahalu na Ofisa Utawala, Grace Martin walidai lilinunuliwa kwa bei hiyo, wakati kwa mujibu wa uchunguzi, ilibainika kuwa Euro milioni moja tu ndizo fedha mshitakiwa wa kwanza, Profesa Mahalu aliziomba kutoka Serikali ya Tanzania.

Shahidi huyo alidai wakati wa uchunguzi wake nchini Italia, alishirikiana na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Takukuru, Alex Mfungo na bosi wao, Edward Hoseah; na baada ya kupata taarifa, walikusanya baadhi ya vielelezo na kufuatilia nyaraka kwa siri kujua kama ni sahihi au la na pia walipofika Italia, walichukua baadhi ya vielelezo walivyopewa na washitakiwa na waliwahoji.

Kyando alidai washitakiwa walimpa mkataba ulioonyesha jengo limenunuliwa kwa Euro milioni tatu, kwa mujibu wa Mwanasheria wa Italia, Marco Papi alishuhudia na kusajili mkataba mmoja wa Euro milioni moja na kwa utaratibu wa Italia, lazima mkataba upitie kwa mwanasheria.

Alidai washitakiwa walidai walipata ridhaa kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marten Lumbanga, lakini baada ya kuhojiwa, alikanusha kuhusika na uuzaji huo. Pia alidai hata taarifa za uuzaji huo kuwasilishwa bungeni, zilikuwa za uongo na Rais anaweza kudanganywa kupewa taarifa za uongo.

Shahidi huyo alidai kuwa uchunguzi alioufanya, uligundua fedha hizo zilikuwa zimeingia katika akaunti mbili tofauti na moja ilionyesha jina la kampuni na risiti iliyotolewa hakuitambua kama ni ya muuzaji au la, kwa sababu hakuhoji na risiti hiyo ilitolewa mahakamani kama kielelezo.

Kyando alidai "Mimi kama mchunguzi, mkataba wa pili uliandaliwa na mshitakiwa wa kwanza kwa ajili ya ubadhirifu aliokusudia kuufanya na ulikuwa na lengo la kuidanganya Serikali ya Tanzania."

Baada ya kumaliza ushahidi huo, Wakili wa Serikali Posia Lukosi alisema walikuwa na shahidi mmoja jana na wanategemea kuita wengine, hivyo waliomba kesi hiyo iahirishwe. Hakimu Mwangesi aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Katika kesi hiyo, Profesa Mahalu anashitakiwa pamoja na aliyekuwa Ofisa Utawala Grace Martin; ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kula njama na kuibia Serikali ya Tanzania kiasi cha Euro 2,065,827.60 (Sh bilioni tatu), mjini Rome, Italia wakati wakiwa watumishi kwenye ubalozi huo mwaka 2002.
 
I worked with this guy at UDSM when he was Dean of the Faculty of Law. I never knew that he can be so corrupt. It is very hard to tell who are the corrupt elements in the society just by their faces, that is why it is necessary to overhaul our constitution and introduce strong mechanisms of check and balance, which currently are non-existent.

Corrupt hata kwa wake za watu. Grace martin ni mke wa mtu na alimchukua. Aliyemwoa na kumpeleka Italy hayuko naye tena kisa Mahalu. Let us see
 
Je Kikwete na Prof. Mahalu kuna nini?? Mwenye fununu tunaomba utufunuliye hili fumbo.

Mtu akimzalilisha shemeji yako wewe utamfanyaje,,, Kule kibosho mkuu wa kaya alikuwa na kademu kule ambako ni dada yake na mume wa zamani wa Grace.
 
Mtu akimzalilisha shemeji yako wewe utamfanyaje,,, Kule kibosho mkuu wa kaya alikuwa na kademu kule ambako ni dada yake na mume wa zamani wa Grace.

So this is payback time? A la Babu Seya?
 
Prof. Mahalu ni fisadi ambaye amekuwa akiandikwa kwenye vijiwe miaka na miaka. Bahati nzuri za arobaini zake zimefika.

Mkapa wa kumkingia kifua yuko hoi kwa ufisadi.

Dean mzima wa facult of law UDSM, leo anakuja ku forge receipt? Aibu kweli kweli.
 
Mtu akimzalilisha shemeji yako wewe utamfanyaje,,, Kule kibosho mkuu wa kaya alikuwa na kademu kule ambako ni dada yake na mume wa zamani wa Grace.

Huyo Grace Martin kama ni mkibosho basi kule kwao siku hizi watakuwa wanamsifia kuwa ni "shujaa aliyeumia vitani", maana hela aliyojaribu kukwiba si haba, bilioni tatu ni hela bwana! Tamaduni nyingine kaaaaz kwel kwel !
 
Prof. Mahalu ni fisadi ambaye amekuwa akiandikwa kwenye vijiwe miaka na miaka. Bahati nzuri za arobaini zake zimefika.

Mkapa wa kumkingia kifua yuko hoi kwa ufisadi.

Dean mzima wa facult of law UDSM, leo anakuja ku forge receipt? Aibu kweli kweli.

Unajua hii serikali yetu imezubaa sana, huyu angetakiwa ahekiwe kila mahali alipowahi kupita utakuwa tu haya madudu yake ya wizi, najua toka alipokuwa elimu ya Juu alikuwa akifanya uhuni, aibuu sana rafiki wa karibu wa nunda lenyewe Mkapa!
 
Corrupt hata kwa wake za watu. Grace martin ni mke wa mtu na alimchukua. Aliyemwoa na kumpeleka Italy hayuko naye tena kisa Mahalu. Let us see

Its the other way round! Grace ndiye "aliyempeleka" mumewe Italy by virtue of her position kama Foreign Service Officer!
 
Sasa ikawaje, nani "aliyemtema" mwenzie?

Kutemana sielewi maana hadi sasa Grace bado anatumia jina la mumewe "Martin" na siyo maiden -"Olotu".
Kuna speculations za kila aina na sipendi kuendeleza umbeya.Mwenye ushahidi aweke hapa.
 
Its the other way round! Grace ndiye "aliyempeleka" mumewe Italy by virtue of her position kama Foreign Service Officer!

To the best of my knowledge, Christopher Martin ndiye aliyempeleka Grace Italy. Before Martin alikuwa Italy na kwa sababu mume alikuwa huko ikabidi Grace amfuate. That was during birthday ya Baba wa Mama Mkapa mwaka 1999 kama sijakosea huko Moshi.
 
To the best of my knowledge, Christopher Martin ndiye aliyempeleka Grace Italy. Before Martin alikuwa Italy na kwa sababu mume alikuwa huko ikabidi Grace amfuate. That was during birthday ya Baba wa Mama Mkapa mwaka 1999 kama sijakosea huko Moshi.

interesting!
 
To the best of my knowledge, Christopher Martin ndiye aliyempeleka Grace Italy. Before Martin alikuwa Italy na kwa sababu mume alikuwa huko ikabidi Grace amfuate. That was during birthday ya Baba wa Mama Mkapa mwaka 1999 kama sijakosea huko Moshi.

hapana,baada ya kufunga ndoa,grace alipata post ya kwenda sweden.au uswiss(hapa sina huhakika ni nchi ipi kati ya hizi,)ndipo baadaye akahamishiwa italy.ningekuwa bongo nilikuwa na nafasi nzuri ya kujua kwani ni mtu ambaye tulikuwa tunafahamiana sana bila matatizo.
 
hapana,baada ya kufunga ndoa,grace alipata post ya kwenda sweden.au uswiss(hapa sina huhakika ni nchi ipi kati ya hizi,)ndipo baadaye akahamishiwa italy.ningekuwa bongo nilikuwa na nafasi nzuri ya kujua kwani ni mtu ambaye tulikuwa tunafahamiana sana bila matatizo.

She then went to Italy as her man were in Italy! So all in all she is not the one made Martin go to Italy!
 
Naibu Katibu Mkuu amkandamiza Mahalu.

Na Pauline Richard.

NAIBU Katibu Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Edwin Mikongoti (56), ameieleza mahakama kuwa haufahamu mkataba uliotumika kununua jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Mikongoti alisema hayo mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Sivangilwa Mwangesi wakati akitoa ushahidi dhidi ya kesi inayemkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Iltalia, Profesa Costalic Mahalu na mwenzake.

Shahidi huyo ambaye kabla ya wadhifa huo aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Mambo ya Ndani, alidai kuwa katika nafasi hiyo, kazi yake kubwa ilikuwa kuhifadhi mikataba mbalimbali ya ununuzi wa majengo hapa nchini.

Alisema akiwa katika wizara hiyo alihusishwa katika ununuzi wa ofisi na nyumba ya balozi wa Kampala na nyumba ya watumishi wa serikali Lilongwe Zambia na hakuwahi kuona mkataba wa Italy.

"Ni kweli mimi natunza mikataba mbalimbali ya ununuzi, lakini mkataba uliotumika katika ununuzi wa jengo la Rome mimi siufahamu" alisema shahidi huyo ambaye ametoka nchini Uswis kwa ajili ya kutoa ushahidi dhidi kesi hiyo.

Hata hivyo shahidi huyo aliyekuwa akiongozwa na Wakili wa Serikali, Ponsiano Lukosi alidai kuwa, katika utendaji wake wa kazi hajawahi kununua jengo kwa mkataba zaidi ya mmoja kama inavyodaiwa katika kesi hiyo.

Alifafanua zaidi kwamba, kwa kawaida ununuzi ukishafanyika katika nchi fulani ofisi yake inatuma taarifa katika wizara husika na wizara hiyo ndio inakuwa na jukumu la kutuma tume kwenda kukagua majengo hayo.

Aliongeza kuwa mikataba hiyo husainiwa na mbele ya shahidi wa serikali ambaye huchaguliwa na ubalozi wa nchi ambayo majengo hayo yamenunuliwa.

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Novemba 7, mwaka huu upande wa Mashitaka utakapoita mashahidi wengine kwa ajili ya kuendelea kutoa ushahidi.

Kabla ya kuahirisha kesi hiyo upande wa mashitaka uliokuwa unaongozwa na Wakili Lukosi uliiomba mahakama iwapatie muda mrefu wa kuita mashahidi kwa madai kwamba asilimia kubwa ya mashshidi wa kesi hiyo wanatoka nje ya nchi.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababishia hasara serikali ya Euro 2,065,827.60 wakati wakiwa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia
 
If I may be allowed to play the devil's advocate,naomba niulize:
1.Kwani wana JF, tukiachilia mbali mambo ya kisheria na technicalities nyingine, hii kesi ya Mahalu inatofautiana vipi na suala la EPA ?- wahusika katika masuala haya mawili japo ni tofauti, kimsingi wote wameiibia serikali kwa njia ya udanganyifu. Kiasi cha fedha iliyoibiwa ni kikubwa - tunaongelea mabilioni.Kwanini basi Prof. Mahalu asingepewa nafasi naye arudishe fedha "aliyoiba" ili iwasaidie watanzania?

2.Kwa upande wa Mahalu na mwenzake, kwa vile ameshafikishwa mahakamani, ni vigumu kwao kama watuhumiwa kupewa "ofa" ya kurudisha fedha ili wasamehewe. Lakini kwa hawa jamaa wa EPA ni rahisi baada ya kurudisha fedha kushtakiwa maana this is like an admission to guilt na haihitaji uchunguzi wa ziada.Kigugumizi kinakujaje ilihali suala liko wazi kabisa?.. na hata mtu ambaye hajasoma sheria anaona wazi kuwa waliorudisha fedha ni kama wamekubali kuwa waliiba.Waliorudisha fedha ndio haswaa walipaswa kushtakiwa.Ambao hawajarudisha fedha ni kama vile wana dispute kuwa hawajachukua/hawajaiba fedha na hivyo basi wako radhi suala likaamuliwe mahakamani.

3.DPP na wahusika wengine, its high time waache kucheza na technicalities za kisheria na kuhakikisha haki inatendeka.Tanzania tutaendelea kuwa kichekesho kwa wenye kujali utawala wa sheria hadi lini?..
DPP PLEASE SHOW THAT U R A REAL LAWYER - PROSECUTE THE EPA GLUTTONS TO THE FULLEST EXTENT OF THE LAW!
 
Case hii itaisha lini?
Mahakama yaamuru Prof Mahalu na mwenzake wana kesi ya kujibu

Na Tausi Ally

ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Afisa utawala wa ubalozi huo, Grace Martin, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wamepatikana na kesi ya kujibu.

Balozi huyo na afisa wake pia wanatuhumiwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni.

Uamuzi huo ulitangazwa jana asubuhi na Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, Sivangilwa Mwangesi, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani ili itolewe uamuazi.

Akitoa uamuzi huo, hakimu Mwangesi alisema amepitia maelezo ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na vielelezo tisa vilivyotolewa ili kuthibitisha makosa dhidi ya watuhumiwa hao na kushawishika kuwa washtakiwa wana kesi ya kujibu.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, watuhumiwa wanatakiwa kuanza kujitetea Mei 4, mwaka huu na kuwataka washtakiwa hao kupitia mawakili wao kueleza njia watakayotumia katika kujitetea.

Hali kadhalika, wataje idadi ya mashahidi wao katika kesi hiyo.

Akijibu hoja hiyo, wakili Bob Makani anayemtetea Balozi Mahalu alidai kuwa mteja wake atajitetea yeye mwenyewe kwa njia ya kiapo na kwamba mashahidi wataitwa katika utetezi utakavyokuwa unaendelea.

Kwa upande wake, wakili Malima anayemtetea Martin, alidai mteja wake ataanza kujitetea yeye mwenyewe kwa njia ya kiapo na kwamba wataita mashahidi watatu.

Mara ya mwisho, ushahidi kuhusu kesi hiyo, ulichukuliwa katika ukumbi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam ambako mahakama ilikuwa inamsikiliza shahidi mmoja akiwa Roma Italia.

Hatua hiyo ilikuja baada ya shahidi huyo Marko Papi ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Italia kushindwa kuja Dar es Salaam, kutoa ushahidi wake.

Hatua hiyo iliulazimisha upande wa mashtaka, kuchukua ushahidi wake kwa njia ya video.

Hata hivyo kabla ya kuanza kuchukuliwa kwa ushahidi huo, kulitokea malumbano kati ya upande wa utetezi na ule wa mashitaka, malumbano yaliyodumu kwa dakika 45.

Mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi Mabere Marando, alipinga kupokelewa kwa ushahidi huo kutoka Italia kwa madai kuwa ni kinyume na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Shahidi huyo aliyewahi kutoa ushahidi wake Machi 14, mwaka jana alidai kuwa yeye alipokea mkataba wa mauzo wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia wa Euro 1, 032, 913.80 ambao unatambulika kisheria nchini humo.

Alidai sheria ya Italia inaruhusu mkataba mmoja wa wazi kama ule mauzo aliosaini yeye.

Baada ya kusikiliza hoja zote, hakimu Mwangesi aliutaka upande wa utetezi kufunga ushahidi kwa kuwa kesi hiyo ni ya muda mrefu na imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuleta mashahidi.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Septembe 23 mwaka 2002 huko Roma Italia, Mahalu na Grace Martin wakiwa waajiriwa wa Serikali ya ya Tanzania, walisaini hati ya malipo yenye namba D2/9/23/9/02 ikionyesha kuwa bei ya ununuzi wa jengo la ubalozi ni Euro 3,098,741.58.

Inadaiwa kuwa maelezo hayo yalikuwa ni ya uongo na yenye nia ya kumdanganya mwajiri wao.
 
Back
Top Bottom