Kesi ya Mauaji ya George Sanga na wenzake yafutwa, waachiwa huru na kukamatwa tena

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Leo tarehe 12 Februari 2024 Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewasilisha Mahakamani nia ya kutoendelea na kesi ya mauaji inayowakabili George Sanga, Optatus Nkwera na Goodlucky Mfuse.

Baada ya kufutwa kwa kesi hiyo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewakamata tena na kuwafungulia mashtaka yale yale katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe.

Hivyo kesi imeanza upya, kwa kuanza mchakato katika Mahakama za chini. Itakumbukwa George Sanga na wenzake wamekamatwa tarehe 26 Septemba 2020, ambapo mpaka leo wametimiza siku 1,234 gerezani.

Kuhusu tuhuma za mauaji, zaidi soma Njombe: Viongozi wa CHADEMA wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa




Tumesema Mara nyingi humu na kwingineko kwamba HAKUNA MAHALI POPOTE KWENYE DUNIA HII AMBAPO SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU , Hatimaye Kijana George Sanga na Wenzake wameachiwa huru baada ya Mahakama kujiridhisha kwamba WALIBAMBIKWA KESI YA UONGO KWA SABABU YA SIASA ZA KISHAMBA ZA AWAMU YA TANO
 
Magufuli alikuwa kweli na dhamira ya dhati kuo zana nchi inasonga mbele. Ila aliwafanyia ukatili mkubwa sana wapinzani wake wa kisiasa, naamini hatatokea Tena kiongozi dhalimu Kwa upinzani kama yeye. Mwendo Ameumaliza Mungu wake amlipe inavyomstahili. Pole sana Bwana George Sanga, Haki siku zote huishinda dhuluma mwishoni.
 
CCM ni Chama Cha Mashetani. Yaani walitaka George na wenzake wahukumiwe kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kutungwa.
 
X wameandika eti wamekamatwa tena? Ni kweli
 
Hakika
 
Viongozi makatili wapo lumumba. Fikiria mtu kama makonda ameua na kuteka wangapi? Leo yupo wapi? Sabaya kafanywa nn?
 
Huyu mtu wamemtesa bila hatia yoyote, amekaa gerezani miaka mingi kama mfungwa aliyehukumiwa, bahati nzuri kwake amejaliwa sura angavu yenye huruma isiyo na dalili ya kulipa kisasi, huyu anastahili kufidiwa kwa namna yoyote, sio tu na wale dhalimu waliompa kesi ya uongo, hata na wapigania haki wa nchi hii

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Naomba CDM wakae na kutafakari jinsi kuwasaidia hata mitaji kurudisha maisja yao mstari wamepigania chama sana kukaa gerezani muda wote huu maisha yao vurugwa Sanaa wanaanza zero kabisa kwa sasa.....naomba sana hiloo
 
Wekeni namba tuwachangie makamanda.
 
Mkiambiwa muende shule mnaishia kwenda kupiga makelele darasani. Ona sasa hujui hata TAFSIRI YA NENO GAIDI . Unapuyanga tu kama zuzu
Kuna mtu nimemtaja? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯🌟🌟🌟πŸ”₯πŸ”₯

Nimesema Gaidi anadunda mitaani sijataja mtaa kama ni nchini Somalia au Lebanon πŸ˜‚πŸ˜‚

Umeshtuka Sana🐼

Mlozi wahed πŸ˜‚πŸ”₯
 
Tatizo siyo ugaidi wala gaidi lahasha. Tatizo lako hujui tafsiri ya neno gaidi na ugaodi. Siyo kosa lako ni matokeo ya kiwa mpiga kelele maarufu darasani
 
Tatizo siyo ugaidi wala gaidi lahasha. Tatizo lako hujui tafsiri ya neno gaidi na ugaodi. Siyo kosa lako ni matokeo ya kiwa mpiga kelele maarufu darasani
Hiyo tafsiri ya Gaidi utaikuta ofisini kwa Kibatala πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯
 
Magaidi hao waliokuleta duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…