Kesi ya Mbowe: Hadi sasa sijaona ushahidi wowote unaoonesha kulikuwa na ugaidi

Kesi ya Mbowe: Hadi sasa sijaona ushahidi wowote unaoonesha kulikuwa na ugaidi

Hivi hawa mashahidi si wanalipwa na Jamhuri?

Mwenye koneksheni basi na mimi nikale hela hizo kwa kusema uongo
Hahahaha huogopi maswali ya wakili msomi kibatala na jopo lake?
 
Ujue haifurahishi hata kidogo yaani mashahidi wote hakuna hata mmoja aliyeleta ushahidi wenye mashiko badala yake wamegeuka kuwa komedian...
Mashahidi wanaanzaga kwa kujiamini sana hasa wanapoongelea ujuzi wao, kama yule askari mtaalamu wa ballistic, alisema amesoma ndani na nje nchi nyingi sana lkn alipobanwa maswali na kina kibatala akasahau utaalam wake akasema terrorism ni mambo ya utalii.
 
Shahidi anasema saini zinatofautiana kwasababu zingine alisaini akiwa amesimama zingine akiwa amekaa.

Mwingine anasema hakumbuki rangi ya shati maana hakuvaa miwani lkn aliweza kuona rangi ya bastola na kusoma namba zake.[emoji23]

Ngoja tuendelee kuweka kambi huku tukisubiria vituko vya mashahidi wengine. Maana kila anayekuja, anakuja na vituko vyake!
 
Neno ugaidi na matukio ya kigaidi hayajaeleweka vizuri nchini! Ndo maana wengine wanashindwa kutofautisha tourism, terrorist na terrorism!

Ni dhahiri kuwa ile kauli ya SSH inaitesa mahakama, mashahidi na watuhumiwa!
Vyeti vya kudesa. Polisi wana tatizo la vyeti wanavyo tumia sio vyao. Yaani form four leaver hajui maan aya terrorism na tourism?? Bado anaitwa ofisa wa serikali...
 
Takribani mashahidi wanne hadi sasa wameshatoa ushahidi wao lakini kati ya hao wote sijaona ushahidi wenye nguvu ya kuwatia hatiani watuhumiwa wa ugaidi...

Ongezeni mbinu za utetezi mahakamani badala ya kujaribu kupata huruma mitandaoni
 
Ongezeni mbinu za utetezi mahakamani badala ya kujaribu kupata huruma mitandaoni
Kwani kina Kibatala na Mtobesya wanatetea mitandaoni.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Shahidi hana Maelezo katika Kifurushi cha Comito

Kwa hiyo Ushahidi wake Hauwezi Kuingia Kwa Mujibu wa Kifungu cha 246 cha CPA

Hakuna Maelezo yake, na Nimeulizana na Wenzangu Kama Upande wa Mashtaka Uliomba Mwanzoni Ombi lolote nimeambiwa Hapana
 
Kwani kina Kibatala na Mtobesya wanatetea mitandaoni.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Shahidi hana Maelezo katika Kifurushi cha Comito...
Yes namna hii ni sawa... Vita halisi iko court room lakini twita na jf ni changamsha kijiwe tu
 
Mpaka leo bado sijaelewa lengo mahsusi la yale mahojiano kati Salim Kikeke na huyu Mama! Na wakati huo huo mchakato wa kesi ukiwa unaendelea mahakamani.

The way alivyokuwa anajieleza mbele ya camera siku ile! Namna alivyo elezea kwa kujiamini!, na ukija kwenye uhalisia! unaona kabisa aina ya Mtawala tuliye naye.
Alishasema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja.
 
Takribani mashahidi wanne hadi sasa wameshatoa ushahidi wao lakini kati ya hao wote sijaona ushahidi wenye nguvu ya kuwatia hatiani watuhumiwa wa ugaidi...
La muhimu kwenye kesi feki si mashahidi bali jaji. Laiti Jamhuri wangekuwa na nia ya kuachana na kesi hii ingeshafutwa kitambo. Plan is kumfunga Mbowe kisha Samia atoe msamaha kama ule wa kwa UAMSHO ikidhaniwa atapata political mileage.
 
Mallya: Sasa ulisema Hapa Mahakamani Leo kuwa Results ni No Records?

Shahidi anatoa Macho tu hajibu swali, anashangaa

Mallya: Mheshimiwa Jaji nasubiri Jibu

Shahidi: nilicho present Leo ndiyo kilichokuwepo

Mallya: Kwa hiyo umeleta au hujakileta

Shahidi: Hakipo
 
Back
Top Bottom