Sasa nakurejea nakurejea:
Kama ilivyo katika kesi zote, ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi hukinzana. Ndipo inapokuja kazi ya mahakama ambapo ni kutumia yote yanayowezekana kupata ukweli ili kuhukumu kwa haki na kwa mujibu wa sheria.
Ushahidi wa upande wa mashtaka na wa utetezi kama ulivyo kwa Jaji uko hapa:
Hoja za Mawakili wa Serikali dhidi ya Adamoo
Kwa ajili ya hukumu, Jaji katumia ushahidi wa mashtaka (Kingai, Mahita na Msemwa) pekee kwamba huo ndiyo ulio kweli na kweli tupu.
Jaji kautupilia mbali ushahidi wote wa utetezi (Adamoo, Ling'wenya, na mke wa Adamoo). Bila shaka kwamba wote huo hauaminiki.
Vigezo alivyovitumia kukubali yote ya Kingai, Mahita na Msemwa havina uhalali wowote.
Vigezo alivyovitumia kuutupilia mbali ushahidi wote wa utetezi havina uhalali wowote.
"Detention register ya Moshi haikuwapo kuonyesha mizunguko ya Adamoo Moshi, japo kujiridhisha. Adamoo ana makovu mwilini ambayo yangeweza kukaguliwa hospitali, kujiridhisha"
Moses Lijenje alitumika kuwatishia beyond imagination kuwa alikuwa kesha tupwa kama shinikizo juu ya yaliyotokea Moshi.
Jaji hakuona umuhimu wa Moses Lijenje kuwapo mahakamani ili kujiridhisha na ukweli wa madai ya upande wa utetezi?!
Kazi yake Jaji ilikuwa nini basi pale mahakamani akiwa amekabiliwa na majumuisho ya ushahidi wa pande mbili zenye kukinzana 100%?
Ikumbukwe si jambo geni katika hukumu Jaji kuwa biased kwa sababu mbalimbali.
Ni sahihi basi kuona kuwa Jaji Siyani amekuwa biased kuelekea upande wa mashtaka kwa kuamua kutumia ushahidi wao pekee kwa ajili ya hukumu kwa sababu zake binafsi.
Kwani Jaji Siyani yeye ni malaika kuweza kujua ushahidi wa haki na wa uongo kuwa ni upi kwa kusikiliza tu bila kuchukua hatua zozote zaidi za kujiridhisha pasipo kuwa na shaka, kwa minajili ya kutenda haki?
Maswaliyataendelea kumfuata Jaji Siyani hadi kaburini:
Kwanini ushahidi pekee aliotumia kuamulia kesi ni ule tu wa Kingai, Mahita na Msemwa kuwa ndiyo wa kweli pekee?
Kwanini si ule wa Adamoo, Ling'wenya au mkewe Adamoo?
Kwanini si ushahidi wote?
Kwa hakika Jaji Siyani ameidogosha hadhi ya mahakama mbele za mamilioni waliomshuhudia akifanya hivyo.