How come mawakili wa utetezi hawakuomba huyo lijenje na meja urio waletwe mbele ya mahakama?
Mwambie kaselabantu au james mapalala tuone kama atakubaluana nàwe
Niliambatanisha hiyo hukumu nikiamini utaipitia kuona mapungufu yake, kisheria, na hatimaye uipinge ipasavyo. Badala yake ulioyaandika ni hisia zaidi za kuthibitisha lawama dhidi yake Jaji
Jibu hoja, panya buku!Kwa Sabaya mnakenua meno haki imetendeka ,kwa Mbowe haki haikutendeka.
Acheni kuingilia Uhuru wa Mahakama kenge nyinyi.
Hoja zako zina mashiko kasoro hitimisho lako lina walakini (harufu ya chuki). Ushauri wangu, mapungufu yaliyomo kwenye Hukumu hiyo, naamini Wakili Kibatala na Wenzake watayatumia kwenye kesi ya msingiSasa nakurejea nakurejea:
Kama ilivyo katika kesi zote, ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi hukinzana. Ndipo inapokuja kazi ya mahakama ambapo ni kutumia yote yanayowezekana kupata ukweli ili kuhukumu kwa haki na kwa mujibu wa sheria.
Ushahidi wa upande wa mashtaka na wa utetezi kama ulivyo kwa Jaji uko hapa:
Hoja za Mawakili wa Serikali dhidi ya Adamoo
Kwa ajili ya hukumu, Jaji katumia ushahidi wa mashtaka (Kingai, Mahita na Msemwa) pekee kwamba huo ndiyo ulio kweli na kweli tupu.
Jaji kautupilia mbali ushahidi wote wa utetezi (Adamoo, Ling'wenya, na mke wa Adamoo). Bila shaka kwamba wote huo hauaminiki.
Vigezo alivyovitumia kukubali yote ya Kingai, Mahita na Msemwa havina uhalali wowote.
Vigezo alivyovitumia kuutupilia mbali ushahidi wote wa utetezi havina uhalali wowote.
"Detention register ya Moshi haikuwapo kuonyesha mizunguko ya Adamoo Moshi, japo kujiridhisha. Adamoo ana makovu mwilini ambayo yangeweza kukaguliwa hospitali, kujiridhisha"
Moses Lijenje alitumika kuwatishia beyond imagination kuwa alikuwa kesha tupwa kama shinikizo juu ya yaliyotokea Moshi.
Jaji hakuona umuhimu wa Moses Lijenje kuwapo mahakamani ili kujiridhisha na ukweli wa madai ya upande wa utetezi?!
Kazi yake Jaji ilikuwa nini basi pale mahakamani akiwa amekabiliwa na majumuisho ya ushahidi wa pande mbili zenye kukinzana 100%?
Ikumbukwe si jambo geni katika hukumu Jaji kuwa biased kwa sababu mbalimbali.
Ni sahihi basi kuona kuwa Jaji Siyani amekuwa biased kuelekea upande wa mashtaka kwa kuamua kutumia ushahidi wao pekee kwa ajili ya hukumu kwa sababu zake binafsi.
Kwani Jaji Siyani yeye ni malaika kuweza kujua ushahidi wa haki na wa uongo kuwa ni upi kwa kusikiliza tu bila kuchukua hatua zozote zaidi za kujiridhisha pasipo kuwa na shaka, kwa minajili ya kutenda haki?
Maswaliyataendelea kumfuata Jaji Siyani hadi kaburini:
Kwanini ushahidi pekee aliotumia kuamulia kesi ni ule tu wa Kingai, Mahita na Msemwa kuwa ndiyo wa kweli pekee?
Kwanini si ule wa Adamoo, Ling'wenya au mkewe Adamoo?
Kwanini si ushahidi wote?
Kwa hakika Jaji Siyani ameidogosha hadhi ya mahakama mbele za mamilioni waliomshuhudia akifanya hivyo.
Hoja zako zina mashiko kasoro hitimisho lako lina walakini (harufu ya chuki). Ushauri wangu, mapungufu yaliyomo kwenye Hukumu hiyo, naamini Wakili Kibatala na Wenzake watayatumia kwenye kesi ya msingi
Chuki? Chuki ya Nini na itoke wapi? Nini sikukijua kabla, wakati au baada ya hukumu hii?
...
View attachment 1983458
Wenye fikira/mtazamo/mategemeo kuwa Katiba (au inavyodaiwa Katiba mpya) ni mwarobaini ya kila tatizo/kero nchini, ni wafinyu au wavivu wa fikra.
Katiba yoyote ile inaweka misingi ya mahusiano, lakini, kamwe haibadili tabia ya mtu. Ni kwa sababu hiyo ndio maana kuna Katiba ikitafsiriwa kwa vitendo (utekelezaji wake) kwa Sheria., Kanuni na Taratibu.
Kilichotokea ni kwamba mmoja ya watu watatu waliotuhumiwa na Mbowe alikiri kosa. Upande wa utetezi wanadai kwamba alikiri baada ya kuteswa na kutishwa. Nafikiri walikosa ushahidi wa kutosha na hiyo inaweza kuwa sababu kwa mahakama kutupilia mbali madai yaoMi sielewi, ina maana huyo shaidi alitoa statement ya kuwatia hatiani, ndo maana upande wa utetezi wanahaha kuweka pingamizi ili hiyo statement isitumike kwenye case,, kwani hawezi kuikana statement wakati case ikiendelea?, Kesi inadai mbowe gaidi,, swali alifanya ugaidi gani na wapi?,
Kama statement inadai alipanga kufanya,, endapo mshitakiwa atakana statement, mahakama itamla imisha? [emoji848][emoji848]
Si umfuate kisogo wewe dada??Kwa Sabaya mnakenua meno haki imetendeka ,kwa Mbowe haki haikutendeka.
Acheni kuingilia Uhuru wa Mahakama kenge nyinyi.
Uchambuzi wako wa hukumu ulikuwa na hoja nzito, lakini sioni uhusiano wa kesi dhidi ya Mbowe na Katiba ya JMT.Hayo ni mawazo yako mkuu kama ambavyo yeyote anaweza kuwa na yake.
Si sahihi ku "assert" mawazo yako juu ya wengine kana kwamba wewe ni malaika.
Ustaarabu huwa kila mtu aheshimu mawazo ya wengine, tusemezane, tushawishiane kwa hoja na mwisho wengi wape.
Au nasema uongo ndugu yangu?
Hii kanuni 'Judges like Caesar's wife must be beyond suspicion' naona inakuwa kama inasahaulika na kwa sababu hiyo kunakuwa na mashaka kuhusu independence na impartiality ya mahakama.Rufaa itakatwa lakini hiyo hakuondoi ukweli kuwa Jaji yuko upande wa prosecution. Jaji hatuko neutral.
Jaji kachukua ushabiki wa Kingai, Mahita na Msekwa at face value kuwa ni sahihi kama ulivyo.
Hakuzingatia lolote kutoka upande wa utetezi.
Uchambuzi wako wa hukumu ulikuwa na hoja nzito, lakini sioni uhusiano wa kesi dhidi ya Mbowe na Katiba ya JMT.
Hivyo basi, najiuliza kama kungekuwa na Katiba Mpya ingezuia Mbowe kutuhumiwa au yeye kutenda makosa anayotuhumiwa.
Je, wewe Mkuu brazaj, Katiba iliyopo inakuathiri kwa vipi?
Hii kanuni 'Judges like Caesar's wife must be beyond suspicion' naona inakuwa kama inasahaulika na kwa sababu hiyo kunakuwa na mashaka kuhusu independence na impartiality ya mahakama.
Yaani uchomwe na bisibisi, uning'inizwe miguu juu, halafu maelezo yawe ya hiari, mateso yalikuwa ya nini? Hata mie si mwana sheria ila nauwezo wa kutafakari na kupima maelezo na hali na mazingira yaliyokuwepo, nahisi hukumu imeadhiriwa na majukumu mapya!