Jana tumesikia polisi akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya Mbowe. Tumesikia na siyo mara ya kwanza wakijitetea kwamba maelezo waliyoandika wamejisahau wakakosea yaani "typographical error".
Je, sheria na mahakama zinasema kuhusu hiki kinachoitwa "typographical error"?
Ukweli ni kwamba mtu unaweza kukosea kuandika kitu tofauti na ulivyotarajia. Ila wakati wa kusahihisha "typographical error"? jaji hajaanza kusikiliza kesi.
Bahati nzuri kesi hii imeenda hivyo upande wa akina Mbowe. Kama mnakumbuka wiki mbili zilizopita akina Kibatala, Mallya na wenzao waliomba kuwe na kesi ndogo yaani "trial within trial".
Msingi wa kesi ile ndogo ilikuwa maandishi au maelezo ya mtuhumiwa mmoja yasipokelewe kama ushahidi. Sasa hivi kidogokidogo tutaanza kuona akina Kibatala, Mallya walitumia akili ya ziada ambayo wote hatukuiona.
Pamoja na polisi kuendeshwa sana kwenye ile kesi ndogo hadi nchi nzima tukajua PGO polisi hawajui PGO bado ilikuwa ni vigumu kina Kibatala kushinda. Naamini hata akina Kibatala walijua wasingeshinda lakini kuna kitu walikuwa wanakiweka
Kwa nini hawakushinda na walijua hawatashinda? Hoja pale si polisi kuijua au kutoijuaPGO . Hoja kubwa pale ilikuwa kwamba kama mtuhumiwa aliandika maelezo kwa hiari yake au aliteswa ndipo akalazimishwa kuyaandika baada ya mateso.
Maadam mtuhumiwa alikiri kwamba ameandika lakini kwa mateso jaji hakuwa na namna ila kuitupilia mbali kesi ile. Ni vigumu kwa jaji au mtu yeyote kuthibitisha kwamba mtuhumiwa aliteswa ndipo akaandika maelezo.
Hapa msingi ni uleule kwamba huwezi kuandika maelezo halafu mbele ya jaji uyaruke kwa kisingizo cha "typographical error" au cha kuteswa kabla ya kuyaandika.
Hivyo, polisi, serikali na mahakama hawakujua wanachokitaka akina Kibatala na kimsingi walitaka ile hukumu ije vilevile kama ilivyokuja, yaani washindwe. Na akina Kibatalla walishindwa kama walivyotaka.
Sasa kushindwa kwa akina Kibatala kuna msaada gani kwako?
Ukiangalia kesi inavyokwenda sasa ndiyo utajua kwa nini walitaka washindwe kesi.
Hebu angalia wanachokifanya sasa hivi. Huwasikii tena wakiuliza maswali ya PGO. Wanajikita sana kushambulia ushahidi wa polisi unaoletwa mahakamani.
Wanasoma maelezo ya shahidi wa serikali aliyoyaandika kisha wanalinganisha na anachosema mahakamani. Kwa kufanya hivyo wamefaulu kukuta ujinga mwingi kwenye ushahidi wa polisi na mashahidi wote wanaoletwa na serikali
Mwisho wa siku ni kwamba kila polisi (shahidi) mmesikia akisema "hapo nilikosea kiandika" au wakisema hilo kosa ni "typographical error" kama alivyosema wa jana.
Hii maana yake akina Kibatala, Mallya na wenzao wameshafaulu kuiweka mahakamani katika kitanzi. Maana yake ushahidi wote wa maandishi jaji sasa hana mamalaka ya kuukataa. Hana mamlaka ya kuona kwamba hiyo ni "typographical error".
Mahakama hiyohiyo ilikataa mtuhumiwa kubadili ushahidi wake kwa kisingizo cha kuteswa hivyo ushahidi huo utaingia mahakamani.
Sasa polisi nao ushahidi wao hautaruhusiwa kubadilishwa. Alichoandika mtuhumiwa kitahesabika kama ushahidi na alichoandika polisi kitatumika kwenye hukumu. Hapa akina Kibatala wamecheza kama Pele na ilikuwa vigumu kugundua.
Kimsingi kama mahakama ilinuia kumfunga Mbowe kwa mbinu hii ya kina Kibatala imewashinda na inawezekana serikali inaweza isilete mshahidi wengi kama tulivyodhani
Vilevile mojawapo ya kesi muhimu kwa kesi hii ni ile ya Mahakama ya Rufani ya "Harish Ambaram Jina (By His Attorney Ajar Patel) v. Abdulrazak Jussa Suleiman".
Katika kesi hii mahakama iligundua tatizo kwenye malezo ya Patel yeye akajitetea kwamba alikosea kuandika yaani "typographical error".
Mahakama ya Rufani ikakataa utetezi huo ikamwambia "kama ulikosea kuandika "typographical error" basi ulitakiwa kurekebisha kabla ya siku ya kusikilizwa kesi". Kipindi cha jaji kusikiliza kesi siyo cha kurekebisha document.
Hivyo, akina KIbatala, Mallya naamini kesi hii wanaijua lakini kama hawaikumbuki basi iko kwenye ukurasa wa 134 wa ripoti za kesi Tanzania za mwaka 2004 yaani [2004] T.L.R. 134.
Wasalaam