Kesi ya Mbowe: Kibatala na Mallya wameiondolea Mahakama uwezo wa kumfunga Mbowe hata ikishinikizwa

wakati mwingine nikisikia watu wasio wanasheria wanavyojadili mambo ya kisheria huwa nawaonea huruma sana kwasababu it will take them 100 years to know the truth. hapo hakuna wanasheria, tafuteni wengine, fuateni ushauri huu mtakuja kunishukuru. hao sio criminal lawyers, kuna mawakili wa jinai wazuri na wanajua techniques kuliko hao, wao faida yao ni kwamba wanajipublicise na kupata wateja na kujulikana zaidi nchini ila sio kuwasaidia kwenye hiyo kesi.

Akili yako iko sawa na ya mleta mada 😁😁
 
amedanganywa nini mzee? kwamba wewe unajua mambo yote yanayotendeka hapa nchini? una tiss? una polisi? una vyombo vya uchunguzi?..utasemaje waongo wakati wewe mwenyewe hapo ulipo upo kiganjani mwa vyombo hivyo vinavyojua unaishije na unatakiwa kuishije kila siku? usilolijua ni kama usiku wa giza.
Kama hivyo vinakujua ni wewe... takataka 🚮🚮🚮 hamna kitu yoyote. Kama wewe unaabudu takataka ni wewe.
 
Kwa ushahidi huu waking’ang’ania kumfunga basi kunaweza kutokea fujo kubwa sehemu nyingi nchini siku ya hukumu na kuendelea mbele.

Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kinachoendelea Mahakamani.
 
hayo hapo juu yanaathiri nini ushahidi wa prosecution hasa ikizingatiwa shahidi hajui kiingereza, ameulizwa kwa kiswahili, maelezo yaliandikwa kwa kiswahili, na wapo mashahidi wengine wanatarajiwa kuitwa pengine kana kwamba ushahidi wa mtu mmoja tu huyo hata ukiwekwa pembeni utaangaliwa ushahidi wa wengine?....kujua kiswahili cha terrorist/terrorism au kutojua kunafifisha charge aliyosomewa? wakati pengine ameshaeleza maelezo ya nini maana ya ugaidi?.....je? wamejua nini lengo la prosecution kumwita shahidi huyo? kwamba walimwita kuja kuthibitisha nini among others kwasababu kuna wakati prosecution wanaweza kuita shahidi kuja kuthibitisha kitu kimoja tu miongoni mwa vingi na vingine vitathibitishwa na mashahidi wengine na akishathibitisha kile wanachokitaka tu wanakuacha tu wewe uulize maana za terrorism na matakataka yako yoote na kesi yao inabaki imesimama...ndio maigizo wanayoyafanya hao mawakili wenu. kwa bahati nzuri nilishawahi kuwa prosecutor na ninawaonea huruma chadema kwasababu kwa wanachokifanya mawakili wenu mtakuja kulia.
Hujui na hufuatilii kinachondelea mahakamani, je neno terrorist na terrorism yalianzia hapo mahakamani au kwenye ripoti ya polisi. Kama ni kwenye ripoti. Je yalitakiwa yawepo au, kumbuka umesema ripoti ilikuwa ya kiswahili, lengo la mawakili ni kulinganisha kama Shahidi ndiye aliandika ripoti hiyo kutokana na maelezo ya mdomo
 
Juzi nilikuwa kule Maria Space jamaa alikuwa anaongea toka kijiji kimoja kule mpanda alielezea jinsi watu kule wanavyofuatilia kwa kuu karibu mno kesi ya Mbowe na wenzie. Je ni vijiji vingapi kama hicho cha mpanda ambacho Watanzania wanafuatilia kesi hiyo kwa karibu kila siku? Na katika bandiko langu nilibold neno moja muhimu sana.
Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kinachoendelea Mahakamani.
 
Hawatakuewa hapa,wewe wape muda tu watarudi tena hapa kupiga mayowe mwisho wa kesi.Kwa sasa kila mtu hapa anajiona ni nguli wa kuchambua kinachoendelea Mahakamani,

kwamba ushindi kwao ni kutoa update hapa mitandaoni,umewashauri vizuri sana swala la kutafuta Wanasheria nguli wa kesi za jinai,lakini hawatakuelewa,wao kwao Kibatala ndiyo kila kitu,wanamuona mbobezi kwenye nyanja zote za kisheria.
Nitajie kesi gani ya jinai ambayo Kibatala amesimamia ameshindwa?
 
Jana tumesikia polisi akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya Mbowe. Tumesikia na siyo mara ya kwanza wakijitetea kwamba maelezo waliyoandika wamejisahau wakakosea yaani "typographical error".

Je, sheria na mahakama zinasema kuhusu hiki kinachoitwa "typographical error"?

Ukweli ni kwamba mtu unaweza kukosea kuandika kitu tofauti na ulivyotarajia. Ila wakati wa kusahihisha "typographical error"? jaji hajaanza kusikiliza kesi.

Bahati nzuri kesi hii imeenda hivyo upande wa akina Mbowe. Kama mnkumbuka wiki mbili zilizopita akina Kibatala, Mallya na wenzao waliomba kuwe na kesi ndogo yaani "trial within trial".

Msingi wa kesi ile ndogo ilikuwa maandihi au maelezo ya mtuhumiwa mmoja yasipokelewe kama ushahidi. Sasa hivi kidogokidogo tutaanza kuona akina Kibatala, Mallya walitumia akili ya ziada ambayo wote hatukuiona.

Pamoja na polisi kuendeshwa sana kwenye ile kesi ndogo hadi nchi nzima tukajua PGO polisi hawajui PGO bado ilikuwa ni vigumu kina Kibatala kushinda. Naamini hata akina Kibatala walijua wasingeshinda lakini kuna kitu walikuwa wanakiweka

Kwa nini hawakushinda na walijua hawatashinda? Hoja pale si polisi kuijua au kutoijuaPGO . Hoja kubwa pale ilikuwa kwamba kama mtuhumiwa aliandika maelezo kwa hiari yake au aliteswa ndipo akalazimishwa kuyaandika baada ya mateso.

Maadam mtuhumiwa alikiri kwamba ameandika lakini kwa mateso jaji hakuwa na namna ila kuitupilia mbali kesi ile. Ni vigumu kwa jaji au mtu yeyote kuthibitisha kwamba mtuhumiwa aliteswa ndipo akaandika maelezo.

Hapa msingi ni uleule kwamba huwezi kuandika maelezo halafu mbele ya jaji uyaruke kwa kisingizo cha "typographical error" au cha kuteswa kabla ya kuyaandika.

Hivyo, polisi, serikali na mahakama hawakujua wanachokitaka akina Kibatala na kimsingi walitaka ile hukumu ije vilevile kama ilivyokuja, yaani washindwe. Na akina Kibatalla walishindwa kama walivyotaka.

Sasa kushindwa kwa akina Kibatala kuna msaada gani kwako?

Ukiangalia kesi inavyokwenda sasa ndiyo utajua kwa nini walitaka washindwe kesi.

Hebu angalia wanachokifanya sasa hivi. Huwasikii tena wakiuliza maswali ya PGO. Wanajikita sana kushambulia ushahidi wa polisi unaoletwa mahakamani.

Wanasoma maelezo ya shahidi wa serikali aliyoyaandika kisha wanalinganisha na anachosema mahakamani. Kwa kufanya hivyo wamefaulu kukuta ujinga mwingi kwenye ushahidi wa polisi na mashahidi wote wanaoletwa na serikali

Mwisho wa siku ni kwamba kila polisi (shahidi) mmesikia akisema "hapo nilikosea kiandika" au wakisema hilo kosa ni "typographical error" kama alivyosema wa jana.

Hii maana yake akina Kibatala, Mallya na wenzao wameshafaulu kuiweka mahakamani katika kitanzi. Maana yake ushahidi wote wa maandishi jaji sasa hana mamalaka ya kuukataa. Hana mamlaka ya kuona kwamba hiyo ni "typographical error".

Mahakama hiyohiyo ilikataa mtuhumiwa kubadili ushahidi wake kwa kisingizo cha kuteswa hivyo ushahidi huo utaingia mahakamani.

Sasa polisi nao ushahidi wao hautaruhusiwa kubadilishwa. Alichoandika mtuhumiwa kitahesabika kama ushahidi na alichoandika polisi kitatumika kwenye hukumu. Hapa akina Kibatala wamecheza kama Pele na ilikuwa vigumu kugundua.

Kimsingi kama mahakama ilinuia kumfunga Mbowe kwa mbinu hii ya kina Kibatala imewashinda na inawezekana serikali inaweza isilete mshahidi wengi kama tulivyodhani

Vilevile mojawapo ya kesi muhimu kwa kesi hii ni ile ya Mahakama ya Rufani ya "Harish Ambaram Jina (By His Attorney Ajar Patel) v. Abdulrazak Jussa Suleiman".

Katika kesi hii mahakama iligundua tatizo kwenye malezo ya Patel yeye akajitetea kwamba alikosea kuandika yaani "typographical error".

Mahakama ya Rufani ikakataa utetezi huo ikamwambia "kama ulikosea kuandika "typographical error" basi ulitakiwa kurekebisha kabla ya siku ya kusikilizwa kesi". Kipindi cha jaji kusikiliza kesi siyo cha kurekebisha document.

Hivyo, akina KIbatala, Mallya naamini kesi hii wanaijua lakini kama hawaikumbuki basi iko kwenye ukurasa wa 134 wa ripoti za kesi Tanzania za mwaka 2004 yaani [2004] T.L.R. 134.

Wasalaam

Mkuu unasomeka vyema bila shaka sawia zaidi na Jaji Siami. Hata hivyo:

1. Tofautisha typographical errors na curable errors za IGP ajaye bwana Kingai.
2. Tofautisha shauri ndani ya shauri na shauri la msingi.
3. Tambua kuwa inawezekana zikawepo trials within trial zaidi kesi inapoendelea.
4. Kila utetezi watakapokataa maelezo ya mshitakiwa kuwa ushahidi, trial within trial itakuja na PGO zitasikika tena.
5. Kumbuka washtakiwa hawakuandika maelezo wenyewe bali walisaini maelezo yaliyoandikwa.
6. Tofautisha kuandika na kusaini yaliyoandikwa.
7. Kwamba utetezi walitaka kushindwa kesi? Si kuwa hukumu kwenye jamhuri ya wadanganyika ni maoni ya mtu mmoja bila ya kumsahau uelekeo wa ule mhimili mwingine?

Kesi ya Mbowe: Ushahidi upande wa Mashtaka unapochukuliwa kuwa ndiyo Dhahiri

8. Ndiyo maana huu:

IMG_20211021_190628_385.jpg

Ni msimamo murua kabisa.

9. Malya au Kibatala hawana hatima ya kesi kama ilivyo hapa chini:

IMG_20210823_165436_763.jpg
 
Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kinachoendelea Mahakamani.

Labda ungesema 80% wameminywa na serikali kwa nguvu zote wasijue kinachoendelea mahakamani?
 
Kwahiyo hilo tu ndiyo linakufanya uwe confortable na mwenendo wa kesi la watu kucheka Mahakamani? Ungejaribu kumwelewa hoja yake kwanza.

Nachokiona hapa ni siasa nyingi tu inaendelea kuliko uhalisia na ndiyo maana vitu vidogo kama hivyo ndiyo vinamake headlines hasa hapa JF maana kumejaa reporters ambao wana mlengo mmoja, lakini mwisho wa siku yale yale ya PGO yatakuja kujiriudia,na tutajazana hapa kutoa stress na makasiriko yetu mwisho wa kesi hii.

Watafutwe Wabobezi wa Sheria za makosa ya Jinai wadeal na hii kesi kumuokoa M/Kiti ambae naamini hana hatia,lakini kama mnataka tuendelee na kujaza thread za kuchekesha,mwisho wa siku hao kina terrosism ni Utalii wataibuka kidedea ndipo mtabaki midomo wazi.
Umeandika mengi ambayo hayana uhusiano na kinachoendelea mahakamani, Jf great thinkers wanafuatilia kesi kwa undani na kujibu hoja kutokana na jinsi mashahidi wanavyotoa ushahidi, yaani mwenendo wa kesi
 
Kesi kama hizi ambazo ni serious ,tulitegemea na jamhuri wangeandaa evidence za uhakika ,sasa kama evidence za kisayansi hamna tutaaminije kuwa hapa hakuna kubambikiana kesi .

Hamna Fingerprint, hamna DNA halafu useme hii silaha ilikuwa ya fulani na wanadai hii kesi ni Ugaidi

Kuna sehemu hii nchi inajikoroga ,kuna siku kitawaka
 
Unaandika maneno meeengi lakin utopolo mtupu!!!
Huyo Shahid wa 2 wa Jamhuri, inakuaje tarehe 20/8/2020 anayosema yupo na Mbowe Longido... lakin tarehe hiyohiyo alikuwa amekamatwa yupo gerezani ukonga. Yani unawezaje kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja, sehemu ambazo zinatofautiana kadri ya km 750? Alitoka gerezani saa 3 usiku akaenda na ndege Longido akaonana na Mbowe, halaf alipomaliza akapanda ndege tena ikamrudisha magereza?

Swali.... ushahidi wa shahid wa 3 uliandikwa kwa kiswahili? Una uhakika? Ripoti ya ushahidi wa silaha kutoka laboratory ya ballistic imeandikwa Kiingereza...umeiona!?? Je kuna ushahidi mkubwa zaidi ya hiyo ripoti? Kama ushahidi uliandikwa kwa kiswahili kichwa cha habari cha ripoti hiyo kuna maneno yalikosewa kama conspiracy yakaandikwa "consipirancy" hicho ni kiswahili?.... kwanza umeona hiyo ripoti ya huyo mtu wa ballistic imeandikwa kwa lugha gani?

Pili huyo Shahid wa 3 wa Jamhuri wa ballistic.. inakuaje unaleta maganda mawili ya risasi ya bunduki moja yanayotofautiana? Yaani yanayotumika kwenye bunduki tofauti? Halaf hapohapo anasema ni maganda ya risasi ya bastola moja, Kuna ushahidi hapo?
Moja wa Jf greater thinker ni wewe. Umeandika kutokana na jinsi unavyofuatlia mwenendo wa kesi kwa jinsi mashahidi wanavyotoa ushahidi, Great thinkers wote ahsanteni na tuendelee kufanya Jf iwe sehemu ya majadiliano ya kina na yenye kujenga
 
Hawatakuewa hapa,wewe wape muda tu watarudi tena hapa kupiga mayowe mwisho wa kesi.Kwa sasa kila mtu hapa anajiona ni nguli wa kuchambua kinachoendelea Mahakamani,

kwamba ushindi kwao ni kutoa update hapa mitandaoni,umewashauri vizuri sana swala la kutafuta Wanasheria nguli wa kesi za jinai,lakini hawatakuelewa,wao kwao Kibatala ndiyo kila kitu,wanamuona mbobezi kwenye nyanja zote za kisheria.
Sheria sio sehemu za siri ukitaka kuziona mpaka uvue nguo.
 
Kwahiyo hilo tu ndiyo linakufanya uwe confortable na mwenendo wa kesi la watu kucheka Mahakamani? Ungejaribu kumwelewa hoja yake kwanza.

Nachokiona hapa ni siasa nyingi tu inaendelea kuliko uhalisia na ndiyo maana vitu vidogo kama hivyo ndiyo vinamake headlines hasa hapa JF maana kumejaa reporters ambao wana mlengo mmoja, lakini mwisho wa siku yale yale ya PGO yatakuja kujiriudia,na tutajazana hapa kutoa stress na makasiriko yetu mwisho wa kesi hii.

Watafutwe Wabobezi wa Sheria za makosa ya Jinai wadeal na hii kesi kumuokoa M/Kiti ambae naamini hana hatia,lakini kama mnataka tuendelee na kujaza thread za kuchekesha,mwisho wa siku hao kina terrosism ni Utalii wataibuka kidedea ndipo mtabaki midomo wazi.
Kumbe unajua Mbowe hana hatia, ukimaanisha jamhuri wanamuweka gerezani Mbowe kwa mapenzi yao, sasa hao "wanasheria nguli" unaowataka watasaidia kitu gani?
 
Jana tumesikia polisi akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya Mbowe. Tumesikia na siyo mara ya kwanza wakijitetea kwamba maelezo waliyoandika wamejisahau wakakosea yaani "typographical error".

Je, sheria na mahakama zinasema kuhusu hiki kinachoitwa "typographical error"?

Ukweli ni kwamba mtu unaweza kukosea kuandika kitu tofauti na ulivyotarajia. Ila wakati wa kusahihisha "typographical error"? jaji hajaanza kusikiliza kesi.

Bahati nzuri kesi hii imeenda hivyo upande wa akina Mbowe. Kama mnkumbuka wiki mbili zilizopita akina Kibatala, Mallya na wenzao waliomba kuwe na kesi ndogo yaani "trial within trial".

Msingi wa kesi ile ndogo ilikuwa maandihi au maelezo ya mtuhumiwa mmoja yasipokelewe kama ushahidi. Sasa hivi kidogokidogo tutaanza kuona akina Kibatala, Mallya walitumia akili ya ziada ambayo wote hatukuiona.

Pamoja na polisi kuendeshwa sana kwenye ile kesi ndogo hadi nchi nzima tukajua PGO polisi hawajui PGO bado ilikuwa ni vigumu kina Kibatala kushinda. Naamini hata akina Kibatala walijua wasingeshinda lakini kuna kitu walikuwa wanakiweka

Kwa nini hawakushinda na walijua hawatashinda? Hoja pale si polisi kuijua au kutoijuaPGO . Hoja kubwa pale ilikuwa kwamba kama mtuhumiwa aliandika maelezo kwa hiari yake au aliteswa ndipo akalazimishwa kuyaandika baada ya mateso.

Maadam mtuhumiwa alikiri kwamba ameandika lakini kwa mateso jaji hakuwa na namna ila kuitupilia mbali kesi ile. Ni vigumu kwa jaji au mtu yeyote kuthibitisha kwamba mtuhumiwa aliteswa ndipo akaandika maelezo.

Hapa msingi ni uleule kwamba huwezi kuandika maelezo halafu mbele ya jaji uyaruke kwa kisingizo cha "typographical error" au cha kuteswa kabla ya kuyaandika.

Hivyo, polisi, serikali na mahakama hawakujua wanachokitaka akina Kibatala na kimsingi walitaka ile hukumu ije vilevile kama ilivyokuja, yaani washindwe. Na akina Kibatalla walishindwa kama walivyotaka.

Sasa kushindwa kwa akina Kibatala kuna msaada gani kwako?

Ukiangalia kesi inavyokwenda sasa ndiyo utajua kwa nini walitaka washindwe kesi.

Hebu angalia wanachokifanya sasa hivi. Huwasikii tena wakiuliza maswali ya PGO. Wanajikita sana kushambulia ushahidi wa polisi unaoletwa mahakamani.

Wanasoma maelezo ya shahidi wa serikali aliyoyaandika kisha wanalinganisha na anachosema mahakamani. Kwa kufanya hivyo wamefaulu kukuta ujinga mwingi kwenye ushahidi wa polisi na mashahidi wote wanaoletwa na serikali

Mwisho wa siku ni kwamba kila polisi (shahidi) mmesikia akisema "hapo nilikosea kiandika" au wakisema hilo kosa ni "typographical error" kama alivyosema wa jana.

Hii maana yake akina Kibatala, Mallya na wenzao wameshafaulu kuiweka mahakamani katika kitanzi. Maana yake ushahidi wote wa maandishi jaji sasa hana mamalaka ya kuukataa. Hana mamlaka ya kuona kwamba hiyo ni "typographical error".

Mahakama hiyohiyo ilikataa mtuhumiwa kubadili ushahidi wake kwa kisingizo cha kuteswa hivyo ushahidi huo utaingia mahakamani.

Sasa polisi nao ushahidi wao hautaruhusiwa kubadilishwa. Alichoandika mtuhumiwa kitahesabika kama ushahidi na alichoandika polisi kitatumika kwenye hukumu. Hapa akina Kibatala wamecheza kama Pele na ilikuwa vigumu kugundua.

Kimsingi kama mahakama ilinuia kumfunga Mbowe kwa mbinu hii ya kina Kibatala imewashinda na inawezekana serikali inaweza isilete mshahidi wengi kama tulivyodhani

Vilevile mojawapo ya kesi muhimu kwa kesi hii ni ile ya Mahakama ya Rufani ya "Harish Ambaram Jina (By His Attorney Ajar Patel) v. Abdulrazak Jussa Suleiman".

Katika kesi hii mahakama iligundua tatizo kwenye malezo ya Patel yeye akajitetea kwamba alikosea kuandika yaani "typographical error".

Mahakama ya Rufani ikakataa utetezi huo ikamwambia "kama ulikosea kuandika "typographical error" basi ulitakiwa kurekebisha kabla ya siku ya kusikilizwa kesi". Kipindi cha jaji kusikiliza kesi siyo cha kurekebisha document.

Hivyo, akina KIbatala, Mallya naamini kesi hii wanaijua lakini kama hawaikumbuki basi iko kwenye ukurasa wa 134 wa ripoti za kesi Tanzania za mwaka 2004 yaani [2004] T.L.R. 134.

Wasalaam
Sisi Wahaya tuna msemo usemao, "Ekyawe kijunda n 'okara"!
 
Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kinachoendelea Mahakamani.
Wewe siyo JF greater thinker, unawezaje kusema wabongo hawafuatlii kinachoendelea mahakamani bila hoja wala utafiti ila kwa mawazo yako, je kufuatilia mahakamani ni mpaka ufike mahakamani, je Habari na mwenendo wa kesi unatangazwa au umesusiwa,
 
wakati mwingine nikisikia watu wasio wanasheria wanavyojadili mambo ya kisheria huwa nawaonea huruma sana kwasababu it will take them 100 years to know the truth. hapo hakuna wanasheria, tafuteni wengine, fuateni ushauri huu mtakuja kunishukuru. hao sio criminal lawyers, kuna mawakili wa jinai wazuri na wanajua techniques kuliko hao, wao faida yao ni kwamba wanajipublicise na kupata wateja na kujulikana zaidi nchini ila sio kuwasaidia kwenye hiyo kesi.
Wewe unaejua sheria funguka[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
hayo hapo juu yanaathiri nini ushahidi wa prosecution hasa ikizingatiwa shahidi hajui kiingereza, ameulizwa kwa kiswahili, maelezo yaliandikwa kwa kiswahili, na wapo mashahidi wengine wanatarajiwa kuitwa pengine kana kwamba ushahidi wa mtu mmoja tu huyo hata ukiwekwa pembeni utaangaliwa ushahidi wa wengine?....kujua kiswahili cha terrorist/terrorism au kutojua kunafifisha charge aliyosomewa? wakati pengine ameshaeleza maelezo ya nini maana ya ugaidi?.....je? wamejua nini lengo la prosecution kumwita shahidi huyo? kwamba walimwita kuja kuthibitisha nini among others kwasababu kuna wakati prosecution wanaweza kuita shahidi kuja kuthibitisha kitu kimoja tu miongoni mwa vingi na vingine vitathibitishwa na mashahidi wengine na akishathibitisha kile wanachokitaka tu wanakuacha tu wewe uulize maana za terrorism na matakataka yako yoote na kesi yao inabaki imesimama...ndio maigizo wanayoyafanya hao mawakili wenu. kwa bahati nzuri nilishawahi kuwa prosecutor na ninawaonea huruma chadema kwasababu kwa wanachokifanya mawakili wenu mtakuja kulia.
Kama uliwahi kuwa prosecutor basi ulikuwa wa Mahakama ya kangaroo. Ukisoma maelezo ya mleta mada Hakuna popote anapoongelea terrorism kuwa utalii kama alivyojinasibu Shahidi wenu. Anachoongea mleta mada ni MAKOSA yaliyopo katika Documents wanazoleta mahakamani ambazo Kila wakiulizwa Kwa nini je umekosea, wanakiri zina MAKOSA, wakiulizwa Kwa nini wanasema hiyo ni "CURABLE".

Hapa ndipo anaposimamia mleta mada na siyo vichekesho unavyodhani Mwanasheria Makini anavijali. Hayo ya UTALII Yana faida kuionesha Mahakama jinsi Shahidi asivyopswa kuaminika. Kwenye kesi yoyote kama kweli wewe ulikuwa Prosecutor kesi inajengwa kama nyumba ukiamzia na msingi. Na siku hizi MPELELEZI (R) MPELELEZI ndiye picha ya kesi. Kingai ndiye picha ya kesi hii huku amejaa "Curable mistakes".

Polisi walipokuwa waendesha mashtaka walikuwa wakiforce vitu kwenda na ndicho unavhojaribu kufanya hapa, wao walikamata, wakapeleleza, wakashitaki na Kwa baadhi ya matukio wakalazikisha hukumu. Hii si kesi ya kitoto, ni kesi kubwa ambayo Kwa ujinga wa Polisi Kingai na Cpl Hafidh eti wanasema ni kesi ya kawaida. Kwa ukubwa wake haikutakiwa kuandaliwa kizembe hivyo labda kama dhumuni ni kuleta utani mahakamani Hata kama wakishindwa waseme "We were not serious to that extent".
 
Kama uliwahi kuwa prosecutor basi ulikuwa wa Mahakama ya kangaroo. Ukisoma maelezo ya mleta mada Hakuna popote anapoongelea terrorism kuwa utalii kama alivyojinasibu Shahidi wenu. Anachoongea mleta mada ni MAKOSA yaliyopo katika Documents wanazoleta mahakamani ambazo Kila wakiulizwa Kwa nini je umekosea, wanakiri zina MAKOSA, wakiulizwa Kwa nini wanasema hiyo ni "CURABLE". Hapa ndipo anaposimamia mleta mada na siyo vichekesho unavyodhani Mwanasheria Makini anavijali. Hayo ya UTALII Yana faida kuionesha Mahakama jinsi Shahidi asivyopswa kuaminika. Kwenye kesi yoyote kama kweli wewe ulikuwa Prosecutor kesi inajengwa kama nyumba ukiamzia na msingi. Na siku hizi MPELELEZI (R) MPELELEZI ndiye picha ya kesi. Kingai ndiye picha ya kesi hii huku amejaa "Curable mistakes".
Polisi walipokuwa waendesha mashtaka walikuwa wakiforce vitu kwenda na ndicho unavhojaribu kufanya hapa, wao walikamata, wakapeleleza, wakashitaki na Kwa baadhi ya matukio wakalazikisha hukumu. Hii si kesi ya kitoto, ni kesi kubwa ambayo Kwa ujinga wa Polisi Kingai na Cpl Hafidh eti wanasema ni kesi ya kawaida. Kwa ukubwa wake haikutakiwa kuandaliwa kizembe hivyo labda kama dhumuni ni kuleta utani mahakamani Hata kama wakishindwa waseme "We were not serious to that extent".
Nazani atakuelewa!!!!
 
Hawatakuewa hapa,wewe wape muda tu watarudi tena hapa kupiga mayowe mwisho wa kesi.Kwa sasa kila mtu hapa anajiona ni nguli wa kuchambua kinachoendelea Mahakamani,

kwamba ushindi kwao ni kutoa update hapa mitandaoni,umewashauri vizuri sana swala la kutafuta Wanasheria nguli wa kesi za jinai,lakini hawatakuelewa,wao kwao Kibatala ndiyo kila kitu,wanamuona mbobezi kwenye nyanja zote za kisheria.
Unateseka ukiwa wapi?

Taja hao wanasheria ghuli tuwajue

Shaidi: Nilipanda basi la kimanjaro linatoka singida nikashukia Arusha

Baada ya mwana ccm kaaya kutoa ushahidi kuhusisha basi la Kilimanjaro

Mmiliki wa base la Kilimanjaro nae kaanza kugombana na dereva wake ni kwanin walibalidilisha rout ya Dar to Arusha na kuipeleka Singida to Arusha bila ruhusa yake
 
Back
Top Bottom