Kesi ya Mbowe: Kibatala na Mallya wameiondolea Mahakama uwezo wa kumfunga Mbowe hata ikishinikizwa

Kesi ya Mbowe: Kibatala na Mallya wameiondolea Mahakama uwezo wa kumfunga Mbowe hata ikishinikizwa

Amedanganywa nini mzee? kwamba wewe unajua mambo yote yanayotendeka hapa nchini? una tiss? una polisi? una vyombo vya uchunguzi?

Utasemaje waongo wakati wewe mwenyewe hapo ulipo upo kiganjani mwa vyombo hivyo vinavyojua unaishije na unatakiwa kuishije kila siku? usilolijua ni kama usiku wa giza.
KWA mbowe ni gaidi alikimbia nchi na wenzake walisha hukumiwa
 
Umechambua na kueleza vizuri kabisa lakini je ndio mlengo wao hao wanasheria
Wewe unafikiri nini maana ya maswali yao. Unaonekana hupendi uwe ndiyo mlengo wao. Vumilia tu mkuu, hii kesi imewakalia vibaya waandaaji (Jamhuri).
 
Uelewa kisoda
Sawa bora mi hata kwenye mchezo wa draft kitatumika, ila wewe mwenye uelewa tusaidie tuelewe sasa je ni sahihi hayo makosa yakiuandishi yalikua yanatokea kwny document za polisi tuu ila kwenye document za washtakiwa ni sahihi japo mwandishi ni mmoja.?
 
Hujui na hufuatilii kinachondelea mahakamani, je neno terrorist na terrorism yalianzia hapo mahakamani au kwenye ripoti ya polisi. Kama ni kwenye ripoti. Je yalitakiwa yawepo au, kumbuka umesema ripoti ilikuwa ya kiswahili, lengo la mawakili ni kulinganisha kama Shahidi ndiye aliandika ripoti hiyo kutokana na maelezo ya mdomo
Note:Report ya hafidhi imeandika " TERROLISM"
 
Wakati mwingine nikisikia watu wasio wanasheria wanavyojadili mambo ya kisheria huwa nawaonea huruma sana kwasababu it will take them 100 years to know the truth. hapo hakuna wanasheria, tafuteni wengine, fuateni ushauri huu mtakuja kunishukuru.

Hao sio criminal lawyers, kuna mawakili wa jinai wazuri na wanajua techniques kuliko hao, wao faida yao ni kwamba wanajipublicise na kupata wateja na kujulikana zaidi nchini ila sio kuwasaidia kwenye hiyo kesi.
Nani kakuchapa?! Unechapwa wewe.
 
Kwa hyo wew ndio mwanasheria mzuri?Upuuzi mtupu
Mkuu huyu jamaa anateseka sana kwa nini asiende mahakamani akaungana na wale mawakili wa serikali au basi awaite hao wanasheria nguli??
 
Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kinachoendelea Mahakam

Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kuishi ktk imani hiyo ni kujidanganya sana
Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kinachoendelea Mahakamani.

Nakubaliana na wewe kuwa watakuwa wamemuonea wakimfunga Mh.Mbowe,lakini swala la kutokea fujo sehemu nyingi hapa Nchini hilo sahau na wala haliwezi tokea kamwe.Wabongo wanahangaika na ugumu wa maisha na pengine 80% wala hawajui hata kinachoendelea Mahakamani.
Kuishi ktk imani hiyo ni kujidanganya sana. Kama huamini endelea kukandamiza watu na kuwanyima uhuru wao historia itakufunza kwani historia haikuwahi kudanganya. Chukulia mfano wa Swaziland yanayotokea hivi sasa utajifunza kitu
 
Jana tumesikia polisi akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya Mbowe. Tumesikia na siyo mara ya kwanza wakijitetea kwamba maelezo waliyoandika wamejisahau wakakosea yaani "typographical error".

Je, sheria na mahakama zinasema kuhusu hiki kinachoitwa "typographical error"?

Ukweli ni kwamba mtu unaweza kukosea kuandika kitu tofauti na ulivyotarajia. Ila wakati wa kusahihisha "typographical error"? jaji hajaanza kusikiliza kesi.

Bahati nzuri kesi hii imeenda hivyo upande wa akina Mbowe. Kama mnakumbuka wiki mbili zilizopita akina Kibatala, Mallya na wenzao waliomba kuwe na kesi ndogo yaani "trial within trial".

Msingi wa kesi ile ndogo ilikuwa maandishi au maelezo ya mtuhumiwa mmoja yasipokelewe kama ushahidi. Sasa hivi kidogokidogo tutaanza kuona akina Kibatala, Mallya walitumia akili ya ziada ambayo wote hatukuiona.

Pamoja na polisi kuendeshwa sana kwenye ile kesi ndogo hadi nchi nzima tukajua PGO polisi hawajui PGO bado ilikuwa ni vigumu kina Kibatala kushinda. Naamini hata akina Kibatala walijua wasingeshinda lakini kuna kitu walikuwa wanakiweka

Kwa nini hawakushinda na walijua hawatashinda? Hoja pale si polisi kuijua au kutoijuaPGO . Hoja kubwa pale ilikuwa kwamba kama mtuhumiwa aliandika maelezo kwa hiari yake au aliteswa ndipo akalazimishwa kuyaandika baada ya mateso.

Maadam mtuhumiwa alikiri kwamba ameandika lakini kwa mateso jaji hakuwa na namna ila kuitupilia mbali kesi ile. Ni vigumu kwa jaji au mtu yeyote kuthibitisha kwamba mtuhumiwa aliteswa ndipo akaandika maelezo.

Hapa msingi ni uleule kwamba huwezi kuandika maelezo halafu mbele ya jaji uyaruke kwa kisingizo cha "typographical error" au cha kuteswa kabla ya kuyaandika.

Hivyo, polisi, serikali na mahakama hawakujua wanachokitaka akina Kibatala na kimsingi walitaka ile hukumu ije vilevile kama ilivyokuja, yaani washindwe. Na akina Kibatalla walishindwa kama walivyotaka.

Sasa kushindwa kwa akina Kibatala kuna msaada gani kwako?

Ukiangalia kesi inavyokwenda sasa ndiyo utajua kwa nini walitaka washindwe kesi.

Hebu angalia wanachokifanya sasa hivi. Huwasikii tena wakiuliza maswali ya PGO. Wanajikita sana kushambulia ushahidi wa polisi unaoletwa mahakamani.

Wanasoma maelezo ya shahidi wa serikali aliyoyaandika kisha wanalinganisha na anachosema mahakamani. Kwa kufanya hivyo wamefaulu kukuta ujinga mwingi kwenye ushahidi wa polisi na mashahidi wote wanaoletwa na serikali

Mwisho wa siku ni kwamba kila polisi (shahidi) mmesikia akisema "hapo nilikosea kiandika" au wakisema hilo kosa ni "typographical error" kama alivyosema wa jana.

Hii maana yake akina Kibatala, Mallya na wenzao wameshafaulu kuiweka mahakamani katika kitanzi. Maana yake ushahidi wote wa maandishi jaji sasa hana mamalaka ya kuukataa. Hana mamlaka ya kuona kwamba hiyo ni "typographical error".

Mahakama hiyohiyo ilikataa mtuhumiwa kubadili ushahidi wake kwa kisingizo cha kuteswa hivyo ushahidi huo utaingia mahakamani.

Sasa polisi nao ushahidi wao hautaruhusiwa kubadilishwa. Alichoandika mtuhumiwa kitahesabika kama ushahidi na alichoandika polisi kitatumika kwenye hukumu. Hapa akina Kibatala wamecheza kama Pele na ilikuwa vigumu kugundua.

Kimsingi kama mahakama ilinuia kumfunga Mbowe kwa mbinu hii ya kina Kibatala imewashinda na inawezekana serikali inaweza isilete mshahidi wengi kama tulivyodhani

Vilevile mojawapo ya kesi muhimu kwa kesi hii ni ile ya Mahakama ya Rufani ya "Harish Ambaram Jina (By His Attorney Ajar Patel) v. Abdulrazak Jussa Suleiman".

Katika kesi hii mahakama iligundua tatizo kwenye malezo ya Patel yeye akajitetea kwamba alikosea kuandika yaani "typographical error".

Mahakama ya Rufani ikakataa utetezi huo ikamwambia "kama ulikosea kuandika "typographical error" basi ulitakiwa kurekebisha kabla ya siku ya kusikilizwa kesi". Kipindi cha jaji kusikiliza kesi siyo cha kurekebisha document.

Hivyo, akina KIbatala, Mallya naamini kesi hii wanaijua lakini kama hawaikumbuki basi iko kwenye ukurasa wa 134 wa ripoti za kesi Tanzania za mwaka 2004 yaani [2004] T.L.R. 134.

Wasalaam
Let's wait for day-break.
 
Kwa ushahidi huu waking’ang’ania kumfunga basi kunaweza kutokea fujo kubwa sehemu nyingi nchini siku ya hukumu na kuendelea mbele.
Hakutakuwa na fujo zozote hata nzi wenyewe hawataruka...tuipe Mahakama imani Mungu yupo atatenda.
 
Hayo hapo juu yanaathiri nini ushahidi wa prosecution hasa ikizingatiwa shahidi hajui kiingereza, ameulizwa kwa kiswahili, maelezo yaliandikwa kwa kiswahili, na wapo mashahidi wengine wanatarajiwa kuitwa pengine kana kwamba ushahidi wa mtu mmoja tu huyo hata ukiwekwa pembeni utaangaliwa ushahidi wa wengine?

Kujua kiswahili cha terrorist/terrorism au kutojua kunafifisha charge aliyosomewa? wakati pengine ameshaeleza maelezo ya nini maana ya ugaidi?.....je? wamejua nini lengo la prosecution kumwita shahidi huyo?

Kwamba walimwita kuja kuthibitisha nini among others kwasababu kuna wakati prosecution wanaweza kuita shahidi kuja kuthibitisha kitu kimoja tu miongoni mwa vingi na vingine vitathibitishwa na mashahidi wengine na akishathibitisha kile wanachokitaka tu wanakuacha tu wewe uulize maana za terrorism na matakataka yako yoote na kesi yao inabaki imesimama.

Ndio maigizo wanayoyafanya hao mawakili wenu. kwa bahati nzuri nilishawahi kuwa prosecutor na ninawaonea huruma chadema kwasababu kwa wanachokifanya mawakili wenu mtakuja kulia.
Acha pombe zitakuua.
 
Ndugu unazunguka zunguka kote huko kwanini? HAPO HAKUNA KESI, kilichopo mahakamani ni mgogoro wa kisiasa kati ya Freeman Mbowe/CHADEMA na serikali/CCM.

Ni CCM wamegaragazwa kwa hoja ktk uwanja wa siasa, na kwa kuwa wana dola, basi wameamua kuitumia kunyanyasa na kuonea wapinzani wao. Lakini kumbuka hili, kwamba, the LINE HAS BEEN DRAWN because THAT CAN'T WORK ANYMORE.

KUMBUKA HILI; Hakuna shahidi mwingine yeyote wa JAMHURI anayeweza kuja ku - repair uharibifu wa ushahidi wao wa uongo uliokwisha kufanywa na mashahidi wao hususani Kingai na wale wajinga na waongo wengine wawili...
Yaani yule wa Longido, Kaaya a.k.a Power Tiller na Koplo Hafidhi wa Forensic Police Investigation Department aliyetoa tafsiri ya "terrorism" kuwa hayo ni "mambo ya utalii."

Kama mpaka hapo hujatambua tu kuwa hawa watu waleta mashitaka haya ni waongo na ni wanabambikia kesi watu, basi wewe utakuwa mjinga wa mwisho katika dunia hii.
Wanajiona wababe wa kupanga lakini kupangua ni zerooo.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Hayo hapo juu yanaathiri nini ushahidi wa prosecution hasa ikizingatiwa shahidi hajui kiingereza, ameulizwa kwa kiswahili, maelezo yaliandikwa kwa kiswahili, na wapo mashahidi wengine wanatarajiwa kuitwa pengine kana kwamba ushahidi wa mtu mmoja tu huyo hata ukiwekwa pembeni utaangaliwa ushahidi wa wengine?

Kujua kiswahili cha terrorist/terrorism au kutojua kunafifisha charge aliyosomewa? wakati pengine ameshaeleza maelezo ya nini maana ya ugaidi?.....je? wamejua nini lengo la prosecution kumwita shahidi huyo?

Kwamba walimwita kuja kuthibitisha nini among others kwasababu kuna wakati prosecution wanaweza kuita shahidi kuja kuthibitisha kitu kimoja tu miongoni mwa vingi na vingine vitathibitishwa na mashahidi wengine na akishathibitisha kile wanachokitaka tu wanakuacha tu wewe uulize maana za terrorism na matakataka yako yoote na kesi yao inabaki imesimama.

Ndio maigizo wanayoyafanya hao mawakili wenu. kwa bahati nzuri nilishawahi kuwa prosecutor na ninawaonea huruma chadema kwasababu kwa wanachokifanya mawakili wenu mtakuja kulia.
Wewe ni cynical tu. Credibility ya ushahidi huendana pia na reliability ya kilichosemwa na Shahid, sound-mindedness ya shahidi, uelewa WA shahidi katika jambo analolitolea ushahidi (collectively, credibility of witness). Sasa unaweza kusema kuwa Kingai amerhibitisha ushahidi gani pasipo chembe ya shaka? Na huyo Power Kaaya ushahidi wake ni credible kiasi gani? Na huyo koplo wa polisi anayeandika nyaraka muhimu ya ushahidi kwa makosa obvious ushahidi wake utaaminiwaje na Mahakama?
Pengine wewe ni prosecutor kwa kuwa ulikuwa ukilipwa mishahara si kwa utaalam!
 
Wewe ni cynical tu. Credibility ya ushahidi huendana pia na reliability ya kilichosemwa na Shahid, sound-mindedness ya shahidi, uelewa WA shahidi katika jambo analolitolea ushahidi (collectively, credibility of witness). Sasa unaweza kusema kuwa Kingai amerhibitisha ushahidi gani pasipo chembe ya shaka? Na huyo Power Kaaya ushahidi wake ni credible kiasi gani? Na huyo koplo wa polisi anayeandika nyaraka muhimu ya ushahidi kwa makosa obvious ushahidi wake utaaminiwaje na Mahakama?
Pengine wewe ni prosecutor kwa kuwa ulikuwa ukilipwa mishahara si kwa utaalam!
huna akili au huna experience mahakamani. nilichokuambia ni kwamba, what if you expunge ushahidi wa huyo shahidi mmoja ambaye kwa demeanour au coherence ya ushahidi wake ataonekana hayupo credible, kesi ya prosecution imefia hapo au imeathirika vipi kwa ushahidi wa huyo mmoja?so the whole evidence is centred on that only single witness? subirini mwisho utakuja kuniambi.
 
Hii kesi ya kubumba haiihtaji expert wa criminal case, shahidi wa tatu bado hakuna ushahidi hauwezi kumui implicate mtuhumiwa.
ajabu yake wote wanaosema ni ya kubumba hawajui chochote kilichopo kwenye jalada. wazungu wamekuja wameona ushahidi wakanyamaza kimya wasubiri huruma ya mahakama, lakini kajambanani wa mbagala huko asiyejua chochote ila ameaminishwa na cdm kuwa ni ya kubumba ndio anasema hivyo. foolish, badala ya kupambana mahakamani vizuri mnaleta siala.
 
Kwenda huko wewe bushlayer.....kwenye sheria hakuna kitu kinachoitwa truth bali kuna facts.
we mburura kabisa, shahidi anapoapa pale mahakamani huwa anaapa kusema nini kama sio ukweli mtupu?
 
Case hii ilikwisha kwenye ile hukumu ndogo ambayo mahakama ili kubali kuchukua ule ushahidi ambao yasemakana hao makomando wali sign kukiri kutumiwa kutenda ugaidi....

hiki kinacho endelea mahakamani ni kupoteza muda tuuu... lakini hukumu ilishatolewa...
Mimi toka ile hukumu ndogo niliacha kufatilia hii case kwasababu hukumu ile ndogo itakuwa na mchango mkubwa sana kwenye hukumu kubwa....
 
Kwahiyo hilo tu ndiyo linakufanya uwe confortable na mwenendo wa kesi la watu kucheka Mahakamani? Ungejaribu kumwelewa hoja yake kwanza.

Nachokiona hapa ni siasa nyingi tu inaendelea kuliko uhalisia na ndiyo maana vitu vidogo kama hivyo ndiyo vinamake headlines hasa hapa JF maana kumejaa reporters ambao wana mlengo mmoja, lakini mwisho wa siku yale yale ya PGO yatakuja kujiriudia,na tutajazana hapa kutoa stress na makasiriko yetu mwisho wa kesi hii.

Watafutwe Wabobezi wa Sheria za makosa ya Jinai wadeal na hii kesi kumuokoa M/Kiti ambae naamini hana hatia, lakini kama mnataka tuendelee na kujaza thread za kuchekesha, mwisho wa siku hao kina terrosism ni Utalii wataibuka kidedea ndipo mtabaki midomo wazi.
Hata mumeo aliibuka kidedea na chama chake, 2020, lakini March 2021 chalii!
 
Kama uliwahi kuwa prosecutor basi ulikuwa wa Mahakama ya kangaroo. Ukisoma maelezo ya mleta mada Hakuna popote anapoongelea terrorism kuwa utalii kama alivyojinasibu Shahidi wenu. Anachoongea mleta mada ni MAKOSA yaliyopo katika Documents wanazoleta mahakamani ambazo Kila wakiulizwa Kwa nini je umekosea, wanakiri zina MAKOSA, wakiulizwa Kwa nini wanasema hiyo ni "CURABLE".

Hapa ndipo anaposimamia mleta mada na siyo vichekesho unavyodhani Mwanasheria Makini anavijali. Hayo ya UTALII Yana faida kuionesha Mahakama jinsi Shahidi asivyopswa kuaminika. Kwenye kesi yoyote kama kweli wewe ulikuwa Prosecutor kesi inajengwa kama nyumba ukiamzia na msingi. Na siku hizi MPELELEZI (R) MPELELEZI ndiye picha ya kesi. Kingai ndiye picha ya kesi hii huku amejaa "Curable mistakes".

Polisi walipokuwa waendesha mashtaka walikuwa wakiforce vitu kwenda na ndicho unavhojaribu kufanya hapa, wao walikamata, wakapeleleza, wakashitaki na Kwa baadhi ya matukio wakalazikisha hukumu. Hii si kesi ya kitoto, ni kesi kubwa ambayo Kwa ujinga wa Polisi Kingai na Cpl Hafidh eti wanasema ni kesi ya kawaida. Kwa ukubwa wake haikutakiwa kuandaliwa kizembe hivyo labda kama dhumuni ni kuleta utani mahakamani Hata kama wakishindwa waseme "We were not serious to that extent".
tatizo lako huna akili, mallya alikuwa anatest uelewa wa shahidi kuhusu ugaidi na akamuuliza ugaidi kwa kiingereza jambo ambalo shahidi asiye convesant na kiingereza hakulijua vizuri, kutojua tofauti kati ya terrorism na terrorist kunaathiri vipi ushahidi katika nchi ya waongea kiswahili, hiyo imeathiri ushahidi wake wote? credibility yake imepungua (kwa maana ya kusema ukweli ataonekana amesema uongo kwa ushahidi alioutoa kwasababu ameshindwa kuelewa maana ya terrorism/tourism)...ndio maana kila siku mnafungwa.
 
Back
Top Bottom