Kesi ya Mbowe na wenzake inaanika hadi 'mambo ya siri za nchi'. DPP hujachelewa kuifuta

Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu. Nafuatilia kwa kwenda mwenyewe Mahakamani. Hata sasa nipo Viunga vya Law School of Tanzania ilipo Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Sitaki kupitwa wala kusimuliwa. Najionea na kusikia mwenyewe moja kwa moja.

Yanayozungumzwa Mahakamani hapa yanashtua, yanaogofya na kuanika hata visivyofaa kuanikwa. Wengi wanaofuatilia wanajua kuwa kesi hiyo sasa imezaa kesi ndogo. Kesi ndogo ni imezaliwa baada ya Maelezo ya Mshtakiwa wa pili (Adamoo) kupingwa na upande wa Utetezi Mahakamani hapa. Ndipo Jaji Siyani anayeisikiliza kesi kuu alipotoa amri ya kuendeshwa kesi ndogo ndani ya kesi kuu kuhusu pingamizi hilo.

Mwisho wa kesi ndogo inayoendelea kutolewa ushahidi sasa ni kukubaliwa au kukataliwa kupokelewa kwa maelezo ya Adamoo yanayodaiwa aliyatoa huko Polisi alipokamatwa na kuhojiwa/kuchukuliwa maelezo. Yeye mwenyewe Adamoo kwenye ushahidi wake ameyakana Maelezo hayo akisema aliletewa yakiwa yameshaandikwa na kusainishwa chini ya vitisho vikubwa vya polisi (ACP Kingai). Jana shahidi wa pili (Bwana Ling'wenya) alianza kutoa ushahidi wake na anaendelea leo hii.

Kuna mambo yameshasemwa hapa Mahakamani na mashahidi wa Utetezi yanaogofya sana. Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?

Kuna jambo linaogofya zaidi. Ushahidi wa kwamba wanajeshi wanakamatwa na kuteswa na polisi waweza kupika chuki na hasira kwenye mioyo ya wawili hao na kuzua suitafahamu ambayo itashindikana hata kusemeka huko mbeleni. Yaani, kunaweza kukachemka 'bifu' kati ya wapambanaji hao. Ikifika hapo, hali itakuwa tete. DPP, hujachelewa kuzuia kuvuja zaidi mambo ya ndani kuliko maini ya nchi na kuzuia taharuki isiyo na hata mkuki.

Buriani Ole Nasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mzee Tupa Tupa Acha inyeshe ili tujue panapovuja! all in all Kingai, Afande anayeitwa Goodluck na Mahita.. Hawa watu wanatakiwa wawekwe chini ya Ulinzi haraka!
 
Mfalme Nebukadineza wa Babel alipomkosea Mungu kama mtawala Mungu alimpeleka porini ambako aliishi Kwa Kula nyasi na kutembea kama ng`ombe. Hivyo Mungu huwaadhibu watawala wasiotenda haki kwa wakati wake.
Alimfanya akaishi Kondeni kama Hayawani.

Mungu ni mkali wa kuadhibu kama alivyofanya Tar 17 machi
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu. Nafuatilia kwa kwenda mwenyewe Mahakamani. Hata sasa nipo Viunga vya Law School of Tanzania ilipo Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Sitaki kupitwa wala kusimuliwa. Najionea na kusikia mwenyewe moja kwa moja.

Yanayozungumzwa Mahakamani hapa yanashtua, yanaogofya na kuanika hata visivyofaa kuanikwa. Wengi wanaofuatilia wanajua kuwa kesi hiyo sasa imezaa kesi ndogo. Kesi ndogo ni imezaliwa baada ya Maelezo ya Mshtakiwa wa pili (Adamoo) kupingwa na upande wa Utetezi Mahakamani hapa. Ndipo Jaji Siyani anayeisikiliza kesi kuu alipotoa amri ya kuendeshwa kesi ndogo ndani ya kesi kuu kuhusu pingamizi hilo.

Mwisho wa kesi ndogo inayoendelea kutolewa ushahidi sasa ni kukubaliwa au kukataliwa kupokelewa kwa maelezo ya Adamoo yanayodaiwa aliyatoa huko Polisi alipokamatwa na kuhojiwa/kuchukuliwa maelezo. Yeye mwenyewe Adamoo kwenye ushahidi wake ameyakana Maelezo hayo akisema aliletewa yakiwa yameshaandikwa na kusainishwa chini ya vitisho vikubwa vya polisi (ACP Kingai). Jana shahidi wa pili (Bwana Ling'wenya) alianza kutoa ushahidi wake na anaendelea leo hii.

Kuna mambo yameshasemwa hapa Mahakamani na mashahidi wa Utetezi yanaogofya sana. Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?

Kuna jambo linaogofya zaidi. Ushahidi wa kwamba wanajeshi wanakamatwa na kuteswa na polisi waweza kupika chuki na hasira kwenye mioyo ya wawili hao na kuzua suitafahamu ambayo itashindikana hata kusemeka huko mbeleni. Yaani, kunaweza kukachemka 'bifu' kati ya wapambanaji hao. Ikifika hapo, hali itakuwa tete. DPP, hujachelewa kuzuia kuvuja zaidi mambo ya ndani kuliko maini ya nchi na kuzuia taharuki isiyo na hata mkuki.

Buriani Ole Nasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hiyo kesi iendelee kwa sababu imegeuka kuwa darasa kubwa la Elimu ya Uraia na haki za Binadamu; imeweka bayana maovu ya jeshi la polisi! Kesi iendelee ili watawala wajue kwamba hawajui! Walichodhamiria kummaliza Mbowe na CDM sasa kimezua aibu kubwa kwa serikali ya JMT, kesi iendelee, kama wanajeshi wataamua kuweka mambo sawa, basi naiwe hivyo tu! Hali hii haiwezi kuruhusiwa kuendelea bila kikomo! Kesi iendelee! Pumzika kwa Amani William Ole Nasha. #MboweSioGaidi #FreeChrisCyrilo
 
Kuna wakili yule wa serikali anaonekana ni jeuri na mtu wa majungu sana, kuna maswali alikuwa akimuuliza Adamo akitaka kujua yale ambayo yanafanyika kule DRC, kuna wakati anachonokoa kutaka kufahamu ni kwa jinsi gani Makomando wanavyofanya kazi.

DPP aingilie kati kuepuka haya kutokea maana tunapoelekea huko siri nyingi zitawekwa wazi, pia itatengeneza uhasama kati ya majeshi haya wawili jeshi la polisi na jeshi la wanannchi.

Swali langu? Hadi huyo luteni Urio kuteswa huko ni kwamba Jenerali Mabeyo hana taarifa na kinachoendelea kwa vijana wake, inasikitisha sana.
Acha kesi isikilizwe kumbe nchi hii yetu ina mambo yakikatili sana kiasi hicho nimesikitika sana
 
nimewahi kusema humu only in Tanzania unaona Komandoo anafukuzwa kazi tena mtu anauzoefu mkubwa wa vita ,then anajitafutia ajira binafsi anakamatwa na kuteswa na polisi.ukiangalia kilichomfukuzisha kazi ni mausuala ya kisaikolojia kutokana na kazi yake .
 
Polisi ni mtu anae aminiwa kuleta amani katika jamii. Mtaani mkiishi na polisi hawezi kwenda dukani, watoto wote wana fahari ya kutumwa dukani na polisi.

Sasa unapoona au kusikia baba/kaka yako anarudi nyumbani anachechemea baada ya kuchukuliwa na polisi. Vijana watapoteza mapenzi na jeshi la polisi.
 
Siro an aushaushshidi. Mbowe sio malaika. As per Siro
 
Huyo gaidi anatupotezea muda afungwe haraka miaka 50
 
Back
Top Bottom