Kesi ya Mbowe na wenzake inaanika hadi 'mambo ya siri za nchi'. DPP hujachelewa kuifuta

Sheria zipi ambazo wanazifuata ikiwa PGO ambayo ndio msaafu wao mkuu hawajui hata unafafananaje? Polisi wengi wanafanya kwa mazoea. Aghalabu kesi hii itawaamusha na kupitia walau hata page 3 za PGO, ili yasiwakute yaliyomkuta Boss wao!!
Hii ndio faida kwao nadhani

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe polisi kuzuia watu wasiingie CHADEMA MKaona ni haki kuingia.haya sasa hakimu azuie tu raia wasiingie
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu. Nafuatilia kwa kwenda mwenyewe Mahakamani. Hata sasa nipo Viunga vya Law School of Tanzania ilipo Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Sitaki kupitwa wala kusimuliwa. Najionea na kusikia mwenyewe moja kwa moja.

Yanayozungumzwa Mahakamani hapa yanashtua, yanaogofya na kuanika hata visivyofaa kuanikwa. Wengi wanaofuatilia wanajua kuwa kesi hiyo sasa imezaa kesi ndogo. Kesi ndogo ni imezaliwa baada ya Maelezo ya Mshtakiwa wa pili (Adamoo) kupingwa na upande wa Utetezi Mahakamani hapa. Ndipo Jaji Siyani anayeisikiliza kesi kuu alipotoa amri ya kuendeshwa kesi ndogo ndani ya kesi kuu kuhusu pingamizi hilo.

Mwisho wa kesi ndogo inayoendelea kutolewa ushahidi sasa ni kukubaliwa au kukataliwa kupokelewa kwa maelezo ya Adamoo yanayodaiwa aliyatoa huko Polisi alipokamatwa na kuhojiwa/kuchukuliwa maelezo. Yeye mwenyewe Adamoo kwenye ushahidi wake ameyakana Maelezo hayo akisema aliletewa yakiwa yameshaandikwa na kusainishwa chini ya vitisho vikubwa vya polisi (ACP Kingai). Jana shahidi wa pili (Bwana Ling'wenya) alianza kutoa ushahidi wake na anaendelea leo hii.

Kuna mambo yameshasemwa hapa Mahakamani na mashahidi wa Utetezi yanaogofya sana. Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?

Kuna jambo linaogofya zaidi. Ushahidi wa kwamba wanajeshi wanakamatwa na kuteswa na polisi waweza kupika chuki na hasira kwenye mioyo ya wawili hao na kuzua suitafahamu ambayo itashindikana hata kusemeka huko mbeleni. Yaani, kunaweza kukachemka 'bifu' kati ya wapambanaji hao. Ikifika hapo, hali itakuwa tete. DPP, hujachelewa kuzuia kuvuja zaidi mambo ya ndani kuliko maini ya nchi na kuzuia taharuki isiyo na hata mkuki.

Buriani Ole Nasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Pamoja na kwamba kesi inavyozidi kuendelea, ndivyo Mbowe anaendelea kuteseka, lakini kwaajili ya kuwafanya wananchi tujue uovu wa polisi, ni aheri DPP asiifute hiki kesi, iachwe ifike mwisho. Hukumu ya kesi ifanywe na mahakama ili maharamia wote ndani ya jeshi la polisi, na ukweli kuwa polisi inafanya kazi kama kikundi cha kigaidi, vifahamike wazi.

Na baadaye wananchi tuendelee kupiga kelele ili wale wauaji wa ndani ya jeshi la polisi wafikishwe mahakamani.
 
nimewahi kusema humu only in Tanzania unaona Komandoo anafukuzwa kazi tena mtu anauzoefu mkubwa wa vita ,then anajitafutia ajira binafsi anakamatwa na kuteswa na polisi.ukiangalia kilichomfukuzisha kazi ni mausuala ya kisaikolojia kutokana na kazi yake .
Unadhani Kuna mwanajeshi atafukuzwa akwambie tatizo???
Hata kusikia walifukuzwa tumesikia hapo mahakamani.

Japo mpaka Sasa sijajua urio kaingiaje kwenye hii saga na kuwa mhalifu Tena,hii kesi inawezafunua mambo mazito,ambayo hakuna mtu alikuwa anayajua.

Acha tuongeze maji maharage.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu. Nafuatilia kwa kwenda mwenyewe Mahakamani. Hata sasa nipo Viunga vya Law School of Tanzania ilipo Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Sitaki kupitwa wala kusimuliwa. Najionea na kusikia mwenyewe moja kwa moja.

Yanayozungumzwa Mahakamani hapa yanashtua, yanaogofya na kuanika hata visivyofaa kuanikwa. Wengi wanaofuatilia wanajua kuwa kesi hiyo sasa imezaa kesi ndogo. Kesi ndogo ni imezaliwa baada ya Maelezo ya Mshtakiwa wa pili (Adamoo) kupingwa na upande wa Utetezi Mahakamani hapa. Ndipo Jaji Siyani anayeisikiliza kesi kuu alipotoa amri ya kuendeshwa kesi ndogo ndani ya kesi kuu kuhusu pingamizi hilo.

Mwisho wa kesi ndogo inayoendelea kutolewa ushahidi sasa ni kukubaliwa au kukataliwa kupokelewa kwa maelezo ya Adamoo yanayodaiwa aliyatoa huko Polisi alipokamatwa na kuhojiwa/kuchukuliwa maelezo. Yeye mwenyewe Adamoo kwenye ushahidi wake ameyakana Maelezo hayo akisema aliletewa yakiwa yameshaandikwa na kusainishwa chini ya vitisho vikubwa vya polisi (ACP Kingai). Jana shahidi wa pili (Bwana Ling'wenya) alianza kutoa ushahidi wake na anaendelea leo hii.

Kuna mambo yameshasemwa hapa Mahakamani na mashahidi wa Utetezi yanaogofya sana. Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?

Kuna jambo linaogofya zaidi. Ushahidi wa kwamba wanajeshi wanakamatwa na kuteswa na polisi waweza kupika chuki na hasira kwenye mioyo ya wawili hao na kuzua suitafahamu ambayo itashindikana hata kusemeka huko mbeleni. Yaani, kunaweza kukachemka 'bifu' kati ya wapambanaji hao. Ikifika hapo, hali itakuwa tete. DPP, hujachelewa kuzuia kuvuja zaidi mambo ya ndani kuliko maini ya nchi na kuzuia taharuki isiyo na hata mkuki.

Buriani Ole Nasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kama kuna jamba jema ambalo watanzania tunaomba litokee niJWTZ kuishughulikia polisi. Police have no manners at all. Limegeuka kuwa genge/idara ya chama tawala
 
Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?

Jana tarehe 27 September 2021
Inadhihirika kuna jambo zito lilipangwa, kesi hii ya kutunga ilipangwa kufunika jambo. Ndiyo maoni ya kijiwe chetu kuhusu yaliyojiri mahakamani tarehe 27 September 2021. 👇👇👇

NINI KILIKUWA KINAENDELEA JESHINI?
Je ndani ya jeshi kulikuwa na fukuto kuhusu mustakabali wa nchi kuendelea kutawaliwa na CCM?

Hii kesi inaibua mengi mtambuka kuhusu wanajeshi kuwekwa mahabusu na kuteswa
ndefu na Juu alikuwa amevaa Combat lakini siyo ya kitanzania

Nikamwambia Mimi nimekamatwa na tumeletwa hapa sijui ni Wapi

Akaniambia "Hapa ni Tazara Kituo cha Polisi"

Wakati naongea na Yule mrangi kuna mwingine akajitokeza kijana Mweusi, nikawambia nimeletwa hapa lakini Mimi nilikuwa ni Askari

Yule akijana Mweusi akasema Vipi MIC? MIC ni neno la Kijeshi

Nikamwambia Mbona wewe upo hapa.?

Akaniambia Mimi ni Askari nilikuwa naswali kwa Azizi Ally kambi yangu ni Twalipo

Alipokuwa amepaki Pikipiki nje akiwa anaswali ndani, wakamsubiri atoke wakampini wakamleta Tazara na akasema yupo Tazara kwa Miezi nane.

Nikamuuliza shida nini.?

Akasema wanaoletwa hapa ni Kesi za Kigaidi.

Shahidi: Siku inayofuata nikiwa kwenye Cello siku inayofuata nikasikia Kilio, nikachungulia Kule Nyuma nikaona watu niliiokuwa nao Depo JKT , TPDF na 92KJ Komandoo (Wadepo wangu)

Nilishuhudia Chuma Chugulu na Alex akiwa na Kijitabu na wenzie wakiwa Wanadepo Wenzangu Kupitia Matundu ya Dirisha walikuwa wanamtesa Mtu. Ambapo baade nilimfahamu yule Mtu Kwa Majina anatolewa Kwenye Magari Mabovu alipokuwa anateswa kwa kushikwa na Mtu Mmoja na Mmoja yupo nyuma yake nilimfahamu aliyekuwa anateswa Kuwa ni Dennis Urio ambaye ni Luteni wa Jeshi ambaye alinitafutia hii Kazi ya VIP PROTECTION kwa Mwenyekiti wa Chadema

Mallya: Awali ulisikia Kilio baadae ukaona Mtu Mwenye kitabu na Rungu na baadae Urio anatolewa Kule kwenye Magari Mabovu, kwa aufahamu wako nani alikuwa anateswa Kule?

Shahidi: Kwa nilivyoona Mimi Leteni Dennis Urio ndiye alikuwa anateswa. Siwezi Kuwa na Ukahika nao ila Kama Dakika 15 Mpaka 20

Mallya: Kipi ulitangulia Kuona Kwanza Kati ya Wanadepo Wenzio na baade Askari Polisi na Urio?

Shahidi: Nilishuhudia Alex ndiye wa kwanza Kutoka baadae katoka Chuma Chungulu na Mapolisi wakiwa na Urio
 
Kama kuna jamba jema ambalo watanzania tunaomba litokee niJWTZ kuishughulikia polisi. Police have no manners at all. Limegeuka kuwa genge/idara ya chama tawala
Si rahisi kama unavyofikiri,haya mambo yataishia kufurahisha watu jf kama ndoto tu.
 
Jana tarehe 27 September 2021
Inadhihirika kuna jambo zito lilipangwa, kesi hii ya kutunga ilipangwa kufunika jambo. Ndiyo maoni ya kijiwe chetu kuhusu yaliyojiri mahakamani tarehe 27 September 2021. 👇👇👇

NINI KILIKUWA KINAENDELEA JESHINI?
Je ndani ya jeshi kulikuwa na fukuto kuhusu mustakabali wa nchi kuendelea kutawaliwa na CCM?

Hii kesi inaibua mengi mtambuka kuhusu wanajeshi kuwekwa mahabusu na kuteswa
Hii kesi ina mambo mengi. Afadhali tumepata kuyajua.
 
Unadhani Kuna mwanajeshi atafukuzwa akwambie tatizo???
Hata kusikia walifukuzwa tumesikia hapo mahakamani.

Japo mpaka Sasa sijajua urio kaingiaje kwenye hii saga na kuwa mhalifu Tena,hii kesi inawezafunua mambo mazito,ambayo hakuna mtu alikuwa anayajua.

Acha tuongeze maji maharage.
CCM mtaumbuka tu.
 
Pamoja na kwamba kesi inavyozidi kuendelea, ndivyo Mbowe anaendelea kuteseka, lakini kwaajili ya kuwafanya wananchi tujue uovu wa polisi, ni aheri DPP asiifute hiki kesi, iachwe ifike mwisho. Hukumu ya kesi ifanywe na mahakama ili maharamia wote ndani ya jeshi la polisi, na ukweli kuwa polisi inafanya kazi kama kikundi cha kigaidi, vifahamike wazi.

Na baadaye wananchi tuendelee kupiga kelele ili wale wauaji wa ndani ya jeshi la polisi wafikishwe mahakamani.
Mbowe hateseki. Yule ni Mwenye Haki anaishi kwa Matumaini kama Bwana Wa Majeshi Aishivyo.
 
Back
Top Bottom