Kesi ya Mbowe na wenzake inaanika hadi 'mambo ya siri za nchi'. DPP hujachelewa kuifuta

Kesi ya Mbowe na wenzake inaanika hadi 'mambo ya siri za nchi'. DPP hujachelewa kuifuta

nimewahi kusema humu only in Tanzania unaona Komandoo anafukuzwa kazi tena mtu anauzoefu mkubwa wa vita ,then anajitafutia ajira binafsi anakamatwa na kuteswa na polisi.ukiangalia kilichomfukuzisha kazi ni mausuala ya kisaikolojia kutokana na kazi yake .
aliye - engineer haya yote ni Mzee wa kutoboa watu misumari chini na ulinzi wa mwendazake. hii nchi kuna watu wameumizwa saaaana.
 
Yaani vijana wa Sirro wanawashughulikia vijana wa Mabeyo?

Maisha yanaenda kwa kasi sana..

Enzi zetu tulishuhudia Polisi wakijishusha mbele ya JWTZ.

Kama haya yametokea kweli, sasa naamini kinachosemwa kwenye kuchelewesha taarifa za msiba wa Meko.... lazima kuna jambo lilikuwa linapangwa
 
Polisi wanaposhughulika na muhalifu hawaangalii wewe ni nani bali wanafuata sheria inavyoelekeza.

RIP Ole Nasha
You are very right...

Lakini, katika scenario hii, polisi wala hawashughulikii uhalifu bali wanawatengenezea watu makosa ili wawapake "mavi" ya uhalifu ili waonekane ni wahalifu na kisha wapewe hukumu isiyo haki...

Hiki ndicho kinachotokea sasa...
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu. Nafuatilia kwa kwenda mwenyewe Mahakamani. Hata sasa nipo Viunga vya Law School of Tanzania ilipo Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Sitaki kupitwa wala kusimuliwa. Najionea na kusikia mwenyewe moja kwa moja.

Yanayozungumzwa Mahakamani hapa yanashtua, yanaogofya na kuanika hata visivyofaa kuanikwa. Wengi wanaofuatilia wanajua kuwa kesi hiyo sasa imezaa kesi ndogo. Kesi ndogo ni imezaliwa baada ya Maelezo ya Mshtakiwa wa pili (Adamoo) kupingwa na upande wa Utetezi Mahakamani hapa. Ndipo Jaji Siyani anayeisikiliza kesi kuu alipotoa amri ya kuendeshwa kesi ndogo ndani ya kesi kuu kuhusu pingamizi hilo.

Mwisho wa kesi ndogo inayoendelea kutolewa ushahidi sasa ni kukubaliwa au kukataliwa kupokelewa kwa maelezo ya Adamoo yanayodaiwa aliyatoa huko Polisi alipokamatwa na kuhojiwa/kuchukuliwa maelezo. Yeye mwenyewe Adamoo kwenye ushahidi wake ameyakana Maelezo hayo akisema aliletewa yakiwa yameshaandikwa na kusainishwa chini ya vitisho vikubwa vya polisi (ACP Kingai). Jana shahidi wa pili (Bwana Ling'wenya) alianza kutoa ushahidi wake na anaendelea leo hii.

Kuna mambo yameshasemwa hapa Mahakamani na mashahidi wa Utetezi yanaogofya sana. Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?

Kuna jambo linaogofya zaidi. Ushahidi wa kwamba wanajeshi wanakamatwa na kuteswa na polisi waweza kupika chuki na hasira kwenye mioyo ya wawili hao na kuzua suitafahamu ambayo itashindikana hata kusemeka huko mbeleni. Yaani, kunaweza kukachemka 'bifu' kati ya wapambanaji hao. Ikifika hapo, hali itakuwa tete. DPP, hujachelewa kuzuia kuvuja zaidi mambo ya ndani kuliko maini ya nchi na kuzuia taharuki isiyo na hata mkuki.

Buriani Ole Nasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kama ndipo ilipofikia na hatujui yajayo, itoshe kusema umetoa ushauri/maoni mazuri yanayohitaji kufanyiwa kazi na wahusika iwapo kama ni kesi isiyokuwa na mashiko na labda haikustahili kuwepo.
 
Tatizo polisi hawana accountability kwa mabaya wanayotenda,mpaka sasa ilitakiwa walalamikiwa wa utesaji huo wawe wamesimamishwa kazi pending uchunguzi wa tuhuma dhidi yao . Toka Magufuli alipochukua uongozi kumekua na malalamiko mengi ya raia dhidi ya polisi lakini hakuna hatua stahiki zimechukuliwa kurekebisha hili tatizo.
 
Kama ndipo ilipofikia na hatujui yajayo, itoshe kusema umetoa ushauri/maoni mazuri yanayohitaji kufanyiwa kazi na wahusika iwapo kama ni kesi isiyokuwa na mashiko na labda haikustahili kuwepo.
Wandaaji wote wa mpango huu wawajibishwe haraka iwezekanavyo. Tukianza na Kingai pamoja na Mahita. Vinginevyo kesi iendelee wazidi kuanikwa.
 
Yaani vijana wa Sirro wanawashughulikia vijana wa Mabeyo?

Maisha yanaenda kwa kasi sana..

Enzi zetu tulishuhudia Polisi wakijishusha mbele ya JWTZ.

Kama haya yametokea kweli, sasa naamini kinachosemwa kwenye kuchelewesha taarifa za msiba wa Meko.... lazima kuna jambo lilikuwa linapangwa
Jwtz imekuwa ya wachumba?
 
Acheni uoga mmezidi kutishia uhai viongozi wa nchi. Huyu au yule akifanya hivi mnamtishia kifo. Saiv mmetulizwa kimyaaaaa sijaona tena vitisho kwa ndungai wala mama Samia. MLIZIDI MKOME
 
Back
Top Bottom