Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

Shahidi ana ugonjwa wa macho pia hakumbuki vizuri lakini ameweza kukumbuka namba ya bunduki haleluya
Naomba Wandishi wa habari waende Rau kutembelea hiyo bar ya mbege waone kama huyo mama watakayemkuta hapo anafanana na ushahidi alioutoa. Mama muuza mbege hawezi kuongea hivyo. Nina wasiwasi wametumia jina lake tu. Ndiyo maana alifunga ushungi na barakoa....!!
 
Ishu ni kwamba.
Ni kwamba ni kweli watuhumiwa walikamatwa na hyo bastola na hizo kete katika eneo hilo.
hayo mengine yanaweza yakawa makosa ya upelelezi na mashahidi.
Ila lengo hapo NI hyo bastola na hizo kete.na hao watuhumiwa Kama ni wenyewe
Kama lengo ni kuonesha kukamatwa na kete hiyo haisaidii chochote kwa sababu hakuna kesi ya dawa za kulevya iliyoko mahakamani
 
Naomba Wandishi wa habari waende Rau kutembelea hiyo bar ya mbege waone kama huyo mama watakayemkuta hapo anafanana na ushahidi alioutoa. Mama muuza mbege hawezi kuongea hivyo. Nina wasiwasi wametumia jina lake tu. Ndiyo maana alifunga ushungi na barakoa....!!
Watakuwa wamemlipa ujira wa kutosha kumleta hapo na maushungi zake! Tangu lini muuza mbege akawa na hali hiyo??
 
Naomba Wandishi wa habari waende Rau kutembelea hiyo bar ya mbege waone kama huyo mama watakayemkuta hapo anafanana na ushahidi alioutoa. Mama muuza mbege hawezi kuongea hivyo. Nina wasiwasi wametumia jina lake tu. Ndiyo maana alifunga ushungi na barakoa....!!

Uwezekano ni kuwa Anita Valerian wa RAU na Anita Valerian (Ninja) wa mahakamani jana ni watu wawili tofauti.

Bahati mbaya ni kuwa Mh. Jaji hafanyi jitihada yoyote kujiridhisha bali kutafuta visingizio.

Hata waandishi wakienda huko haitasaidia kitu kwa sababu yaonyesha (tusipokomaa) wanayo hukumu mkononi.

Huyu Jaji kulikuwa na haja ya kumtaka ajitoe.

Hilo nalo reverberation yake itakuwa inatosha kuwafahamisha kuwa haturidhiki.
 
Anita Valerian Mtaro shahidi #4 mkristo mwuuza pombe za kienyeji, alitimba mahakamani incognito ndani ya vazi la kiislam akiwa pia katupia barakoa lenye kumwachia macho ya kuweza kuona peke yake.

Shahidi huyu wa upande wa mashtaka amesikika akisema alishuhudia zoezi zima la kukamatwa kwa washitakiwa #2 na #3.

Kwamba alishuhudia yote yaliyojiri hadi kujitolea kutoa maelezo yake kwa niaba ya upande wa mashtaka central polisi Moshi.

Hata hivyo shahidi haelezi kwanini polisi walimpenda zaidi yeye, ikizingatiwa washtakiwa hawakukamatiwa kwake na wala yeye hakuwa karibu zaidi na eneo la tukio kuliko wengine wote waliokuwapo.

Shahidi huyu muuza mbege, alianza kwa kueleza aliona watu watatu wakinywa bia, wakiongea na simu, na kusajili line za simu. Shahidi huyo akadai tena kuona watu 2 waliokuwa wakipita pita kwenda na kurudi, huku wakiongea na simu.

Vipi haya yote kutokea muda huo huo?

Shahidi anadai zoezi zima la ukamataji lilianza saa 7 mchana likachukua takribani dakika 45 kisha safari ya kwenda central ikaanza. Akaandikisha maelezo kisha akaya saini saa 7 kamili mchana.

Zaidi sana shahidi anadai washitakiwa kwenye kukaguliwa walikuwa na bastola (A5340), kete za madawa ya kulevya na Simu zao tu.

Hawakuwa na pesa, hata 1/-.

Maajabu zaidi ya Mussa ya shahidi huyu ni kuwa ana sahihi tofauti tofauti akiwa kasimama na akiwa amekaa. Pia baina ya za kukaa nazo ni tofauti kama ambavyo za baina ya kusimama zilivyo tofauti.

Bila shaka ndiyo sababu upande wa mashtaka hawakutaka kabisa shahidi aanguke pale kizimbani 😁😁.

Shahidi ni mpangaji RAU madukani. Kumbe:

View attachment 1994875

Chama cha Mapinduzi - CCM.

CCM hoyeee!
Oyeeeee. Chama cha mazuzu hiki
Hawawezi hata kujibu hoja wanakimbilia mahakamani
 
Hivyo si anaweza sema yeyote tu mkuu?

Thamani ya ushahidi si inakuja kwenye kuaminika mjomba?

Anaaminika kiasi gani shahidi huyu kwenye shitaka nyeti hili?
Exactly, witness credibility is in question
 
Uwezekano ni kuwa Anita Valerian wa RAU na Anita Valerian (Ninja) wa mahakamani jana ni watu wawili tofauti.

Bahati mbaya ni kuwa Mh. Jaji hafanyi jitihada yoyote kujiridhisha bali kutafuta visingizio.

Hata waandishi wakienda huko haitasaidia kitu kwa sababu yaonyesha (tusipokomaa) wanayo hukumu mkononi.

Huyu Jaji kulikuwa na haja ya kumtaka ajitoe.

Hilo nalo reverberation yake itakuwa inatosha kuwafahamisha kuwa haturidhiki.
Mkuu, Nakubaliana na wewe. Ila kama investigating journalist akiingia hapo, ni rahisi sana kupata ukweli.

Naamini Anita wa jana ni Police au UWT, siyo yule mama muuza mbege.
 
Mkuu, Nakubaliana na wewe. Ila kama investigating journalist akiingia hapo, ni rahisi sana kupata ukweli.

Naamini Anita wa jana ni Police au UWT, siyo yule mama muuza mbege.

Nakubaliana na wewe 100% taabu yetu ineptness.

Kwanini hata Chadema Hai wasifanye hiyo ground work wakatuhabarisha?
 
Back
Top Bottom