Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

Suala la msingi hapa ni kwamba
1. Waliopo mahakamani hapo ndio walioonekana sehemu ya ukamataji? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
2. Tarehe na muda unaodaiwa ukamataji kufanyika hao watu wanaoshitakiwa walikuwepo eneo hilo? Kama jibu ni ndio kusudi limetimia
3. Ni kweli kwamba waliokamatwa na kushitakiwa mahakamani walikuwa wakinywa pombe, kusajili simu na kuwasiliana kwa njia ya simu katika tarehe na muda tajwa? Kama jibu ni ndio, kusudi limetima
4. Ni kweli kwamba baada ya kukamatwa washitakiwa na kupekuliwa katika eneo walilokutwa walikutwa wakiwa na silaha na kete za dawa za kulevya? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
5. Ni kweli kwamba baada ya kukamatwa washitakiwa na kupekuliwa kuna nyaraka ziliandikishwa kisha mashihidi kadhaa wakashuhudia kilichofanyika kisha wakasaini kuthibitisho kilichoandikwa ni sahihi? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
Ameshindwa watambua watuhumiwa mahakamani

Maelezo yake sehem kubwa amepingana nayo/kuyakataa

Vitu walivyokamatwa navyo anapingana idadi na Kingai lkn pia anapingana na maelezo yake yeye mwenyewe kwa kutoa figure mbili tofaut

Kimsingi ushahidi wake n ushahidi ambao hauna mashiko

Sain alizo sain sehem nne tofaut hakuna inayofanana na nyenzie

Kwenye maelezo yake anaonyesha alisain sehem Moja tu ila leo anaiambia mahakama n sehem 4.. anaulizwa anasema imetokea tu

Mashahidi wote watatu so far ni matatizo tupu
 
Hapo wana ccm ndiyo wanaamini kuwa mh Mbowe akifungwa ndiyo cdm imekufa.
CDM haiwezi kufa kwa kukosekana kiongozi mwandamizi fulani kwa sababu roho ya uasi imeenea kwa watu mbalimbali na inaambukizana kwa kiwango kilekile kadri siku zinavyosonga mbele
 
Ndio maana kitabibu ni kweli baadhi ya watu wana uwezo wa kuona mbali au karibu kwa hiyo hakuna tatizo katika maelezo yake ya ushahidi.

Wakili ameshindwa kuhoji kama ana matatizo ya kuona na kwamba alishathibishwa hospitalini ili adai cheti cha kupimwa kwake. Mawakili wanaojifunza wanafikiri kila kinachofundishwa darasani ndicho kilichoko kwenye uhalisia ndio maana pakawepo na shule ya sheria (Law School) kumwandaa na uwanja wa hoja tunduizi
Wakili ahoji kwanini wakati shahidi ameshajitega mwenyewe, kasema kuna wakati macho yake yanaona wakati mwingine hayaoni vizuri.

Sasa wakili akiamua kusema wakati shahidi anatazama watuhumiwa wakipekuliwa macho yake yalikuwa hayaoni vizuri atakuwa amekosea wapi?

Na kwa mtindo huo kuna haja gani ya kuagiza vyeti vyake? ili wakili wa utetezi ajitege mwenyewe? hebu fungua akili hiyo, zaidi, shahidi amekiri wakati watuhumiwa wanapekuliwa hakuwa amevaa miwani, mpaka hapo case closed.

Kama ana miwani maana yake ana matatizo ya macho, na ili aone vizuri lazima avae miwani ndio maana akapewa hospitalini baada ya kupimwa, kutokuivaa kwake eneo la tukio kumemaliza mjadala.
 
Huo ukweli utajulikana vipi bila ushahidi usiotia shaka au kujichanganya?
Ishu ni kwamba.
Ni kwamba ni kweli watuhumiwa walikamatwa na hyo bastola na hizo kete katika eneo hilo.
hayo mengine yanaweza yakawa makosa ya upelelezi na mashahidi.
Ila lengo hapo NI hyo bastola na hizo kete.na hao watuhumiwa Kama ni wenyewe
 
Ndio maana kitabibu ni kweli baadhi ya watu wana uwezo wa kuona mbali au karibu kwa hiyo hakuna tatizo katika maelezo yake ya ushahidi.

Wakili ameshindwa kuhoji kama ana matatizo ya kuona na kwamba alishathibishwa hospitalini ili adai cheti cha kupimwa kwake. Mawakili wanaojifunza wanafikiri kila kinachofundishwa darasani ndicho kilichoko kwenye uhalisia ndio maana pakawepo na shule ya sheria (Law School) kumwandaa na uwanja wa hoja tunduizi
Ameulizwa maswali ya kufunika hili jambo

Hakuwai iambia mahakama au judge kama ana tatizo la kuona au ili aone vizuri anahitaj miwani , na ameitikia hajafanya hivyo

Malya kasogea hatua 7 kamuuliza vitu kajibu , kibatala kamwambia aangalie nje atajae anavyoona kataja pia kiufasaha, point yako inafia humo manake kafanyia majaribio hapo hapo mahakamani na watu wawili tofaut na kajibu vizuri
 
Wakili ahoji kwanini wakati shahidi ameshajitega mwenyewe, kasema kuna wakati macho yake yanaona wakati mwingine hayaoni vizuri.

Sasa wakili akiamua kusema wakati shahidi anatazama watuhumiwa wakipekuliwa macho yake yalikuwa hayaoni vizuri atakuwa amekosea wapi?

Na kwa mtindo huo kuna haja ya kuagiza vyeti vyake? ili wakili wa utetezi ajitege mwenyewe? hebu fungua akili hiyo, zaidi, shahidi amekiri wakati watuhumiwa wanapekuliwa hakuwa amevaa miwani, mpaka hapo case closed.

Kama ana miwani maana yake ana matatizo ya macho, na ili aone vizuri lazima avae miwani ndio maana akawa nayo, kutokuivaa kwake eneo la tukio kumemaliza mjadala.
Wakili sio jaji, mwenye maamuzi ya mwisho ni jaji na hahitaji kuomba ushauri wa wakili kutoka upande wowote wenye maslahi na kesi elewa hilo mbona kichwa ngumu?
 
Suala la msingi hapa ni kwamba
1. Waliopo mahakamani hapo ndio walioonekana sehemu ya ukamataji? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
2. Tarehe na muda unaodaiwa ukamataji kufanyika hao watu wanaoshitakiwa walikuwepo eneo hilo? Kama jibu ni ndio kusudi limetimia
3. Ni kweli kwamba waliokamatwa na kushitakiwa mahakamani walikuwa wakinywa pombe, kusajili simu na kuwasiliana kwa njia ya simu katika tarehe na muda tajwa? Kama jibu ni ndio, kusudi limetima
4. Ni kweli kwamba baada ya kukamatwa washitakiwa na kupekuliwa katika eneo walilokutwa walikutwa wakiwa na silaha na kete za dawa za kulevya? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
5. Ni kweli kwamba baada ya kukamatwa washitakiwa na kupekuliwa kuna nyaraka ziliandikishwa kisha mashihidi kadhaa wakashuhudia kilichofanyika kisha wakasaini kuthibitisho kilichoandikwa ni sahihi? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
Sasa mbona hawajafunguliwa na kesi ya madawa ya kulevya!?
 
Wakili sio jaji, mwenye maamuzi ya mwisho ni jaji na hahitaji kuomba ushauri wa wakili kutoka upande wowote wenye maslahi na kesi elewa hilo mbona kichwa ngumu?
Nilichokuonesha hapo wakili lazima avutie upande wake na ndicho kilichofanyika, habari ya wakili sio jaji sijui umeitoa wapi, siku zote kazi ya wakili ni kumshawishi jaji.
 
Anita Valerian Mtaro shahidi #4 mkristo mwuuza pombe za kienyeji, alitimba mahakamani incognito ndani ya vazi la kiislam akiwa pia katupia barakoa lenye kumwachia macho ya kuweza kuona peke yake.

Shahidi huyu wa upande wa mashtaka amesikika akisema alishuhudia zoezi zima la kukamatwa kwa washitakiwa #2 na #3.

Kwamba alishuhudia yote yaliyojiri hadi kujitolea kutoa maelezo yake kwa niaba ya upande wa mashtaka central polisi Moshi.

Hata hivyo shahidi haelezi kwanini polisi walimpenda zaidi yeye, ikizingatiwa washtakiwa hawakukamatiwa kwake na wala yeye hakuwa karibu zaidi na eneo la tukio kuliko wengine wote waliokuwapo.

Shahidi huyu muuza mbege, alianza kwa kueleza aliona watu watatu wakinywa bia, wakiongea na simu, na kusajili line za simu. Shahidi huyo akadai tena kuona watu 2 waliokuwa wakipita pita kwenda na kurudi, huku wakiongea na simu.

Vipi haya yote kutokea muda huo huo?

Shahidi anadai zoezi zima la ukamataji lilianza saa 7 mchana likachukua takribani dakika 45 kisha safari ya kwenda central ikaanza. Akaandikisha maelezo kisha akaya saini saa 7 kamili mchana.

Zaidi sana shahidi anadai washitakiwa kwenye kukaguliwa walikuwa na bastola (A5340), kete za madawa ya kulevya na Simu zao tu.

Hawakuwa na pesa, hata 1/-.

Maajabu zaidi ya Mussa ya shahidi huyu ni kuwa ana sahihi tofauti tofauti akiwa kasimama na akiwa amekaa. Pia baina ya za kukaa nazo ni tofauti kama ambavyo za baina ya kusimama zilivyo tofauti.

Bila shaka ndiyo sababu upande wa mashtaka hawakutaka kabisa shahidi aanguke pale kizimbani 😁😁.

Shahidi ni mpangaji RAU madukani. Kumbe:

View attachment 1994875

Chama cha Mapinduzi - CCM.

CCM hoyeee!
Huyu shahidi hajisomi kabisa, naona ni chakuula ya jumanne au malewo, ukisikiliza kwa makini huyu hakuwepo eneo la tukio
 
Wewe kwa akili zako hayo maelezo ya polisi yana ukweli gani kama waliwakamata watuhumiwa saa saba wakamfanyia mahojiano kwa 45mins it means walimaliza naye saa 13:45 kisha maelezo hayo hayo akayasaini saa saba kamili.....inakuingia akilini?

Hapo hizo hesabu zao waligawanya walizidisha au walitoa?may be walijumlisha who knows!
Maelezo yake yaliandikwa kabla ya ukamataji.
 
Wakili sio jaji, mwenye maamuzi ya mwisho ni jaji na hahitaji kuomba ushauri wa wakili kutoka upande wowote wenye maslahi na kesi elewa hilo mbona kichwa ngumu?
Unaweza kuwa una hoja. Lakini pia hufichi mahaba yako na chuki yako kwa Mbowe..Waambieni hao Askari wenu heshima ya kazi yao ni pamoja na kutenda haki...
 
Shahidi anatakiwa kuwa 'willing to volunteer' kuwa shahidi kwa upande wa ulalamikaji au mlalamikiwa

Huwezi kuchukua shahidi yeyote ambaye huna uhakika anaweza kubadilika katikati ya kesi na kutoa maelezo yanayousaidia upande mwingine (hostile witness) ndio maana polisi walitathimini kwanza ni yupi afaaye kutoa ushahidi bila kuyumbishwa kwa hongo au vitisho.
Utajuaje kuwa huyu hawezi kuchukua hongo na mmeenda kuvamia nae mmekutana nae hapo hapo...
 
Wewe kwa akili zako hayo maelezo ya polisi yana ukweli gani kama waliwakamata watuhumiwa saa saba wakamfanyia mahojiano kwa 45mins it means walimaliza naye saa 13:45 kisha maelezo hayo hayo akayasaini saa saba kamili.....inakuingia akilini?

Hapo hizo hesabu zao waligawanya walizidisha au walitoa?may be walijumlisha who knows!

Mkuu dakika 45 si za mahojiano. Hizo ni muda wa sekeseke la kuwakamata kuwakagua, kuorodhesha walivyokuwa navyo na kusainisha makaratasi ya awali ya mali.

Dakika hizi 45 ni za sehemu ya tukio hazijumuishi muda wa kuandikisha maelezo Central Moshi wala wa safari RAU - Central.

Hiiiiii bagosha.
 
Ishu ni kwamba.
Ni kwamba ni kweli watuhumiwa walikamatwa na hyo bastola na hizo kete katika eneo hilo.
hayo mengine yanaweza yakawa makosa ya upelelezi na mashahidi.
Ila lengo hapo NI hyo bastola na hizo kete.na hao watuhumiwa Kama ni wenyewe
Hilo ndilo linaloendelea kwenye dodoso za huyu shahidi #4. Tusubiri hitimisho la dodoso kwa huyu shahidi.
 
Back
Top Bottom