Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

Hivyo si anaweza sema yeyote tu mkuu?

Thamani ya ushahidi si inakuja kwenye kumsimika mjomba?

Anaaminika kiasi gani shahidi huyu kwenye shitaka nyeti hili?
Swali NI kuwa walikamatwa na hivyo vitu katika eneo hilo?
 
Nilichoelewa Mimi watuhumiwa hao walikamatwa hapo wakiwa na bastola na hizo kete.
huyo ndo aliona.
Muuza mbege wakati wote yupo mafuta aliwezaje kuwa na kumbukumbu ya matukio yote wakati yupo mafuta?
 
Kuona sio tatizo ila mazingira Mpaka anaona yanatia shaka sana, pamoja mlolongo wa tukio zima,hamna kitu pale
Ishu ni kwamba.
Ni kwamba ni kweli watuhumiwa walikamatwa na hyo bastola na hizo kete katika eneo hilo.
hayo mengine yanaweza yakawa makosa ya upelelezi na mashahidi.
Ila lengo hapo NI hyo bastola na hizo kete.na hao watuhumiwa Kama ni wenyewe
 
Shahidi wa leo anaishi hatua kumi kutoka eneo la tukio, lakini wapo wanaouza duka la vipodozi waliokuwa karibu zaidi na eneo la tukio walipokamatwa watuhumiwa lakini polisi hawakuhangaika nao, walienda kumchukua huyu wa mbali ambaye ni mpangaji na kada mwenzao ili wamlishe upupu bila shida.
Kesho wakati wa kuhojiwa na upande wa utetezi ndiyo atatapishwa ndoano .

Kama alipangwa kuja kuhujumu mh Mbowe basi kesho ndiyo siku yake ya kuaibishwa.

Inaonekana hajiamini na ndiyo akawa amejifunika hadi usoni na hata iq yake naona ipo low.
 
Hapa hakuna kesi naona CCM na tawi lao wanajisahau sana kuedit baadhi ya "scenes" kabla hazijaenda hewani..

Ushauri wangu wajaribu hata kuona filamu za Jackie Chan alivyokua akifanya miaka ya 1980
Hawawezi kuona mapungufu yao maana Mungu kapanga kuwaumbua mbele ya jamii
 
Muuza mbege wakati wote yupo mafuta aliwezaje kuwa na kumbukumbu ya matukio yote wakati yupo mafuta?
Watuhumiwa kwani wamemkana kuwa hakuwepo?
hii kesi inafundisha Sanaa.
Ila nikiri akina kibatala wanajitahidi Sanaa kupangua hoja.
Mwanzo nilikuwa naona mawakili wanakula hela bure.ila kwa Sasa nawaheshimu.
Kuugeuza ukweli kuwa UONGO,na UONGO kuwa ukweli sio kazi ndogo
 
Ccm wanajisumbua kwa mambo ya kubumba tu kisa kumdhoofisha mpigania haki na kudai katiba.
 
Shahidi anatakiwa kuwa 'willing to volunteer' kuwa shahidi kwa upande wa ulalamikaji au mlalamikiwa

Huwezi kuchukua shahidi yeyote ambaye huna uhakika anaweza kubadilika katikati ya kesi na kutoa maelezo yanayousaidia upande mwingine (hostile witness) ndio maana polisi walitathimini kwanza ni yupi afaaye kutoa ushahidi bila kuyumbishwa kwa hongo au vitisho.
Kwa hiyo wakaona mlevi wa mbege ndiye hawezi kubadilika?
 
Ishu ni kwamba.
Ni kwamba ni kweli watuhumiwa walikamatwa na hyo bastola na hizo kete katika eneo hilo.
hayo mengine yanaweza yakawa makosa ya upelelezi na mashahidi.
Ila lengo hapo NI hyo bastola na hizo kete.na hao watuhumiwa Kama ni wenyewe
Dawa ya shahidi muongo ni kina Kibatala na kesho huyo mama ataitapika ndoano
 
Swali NI kuwa walikamatwa na hivyo vitu katika eneo hilo?
Suala la msingi hapa ni kwamba
1. Waliopo mahakamani hapo ndio walioonekana sehemu ya ukamataji? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
2. Tarehe na muda unaodaiwa ukamataji kufanyika hao watu wanaoshitakiwa walikuwepo eneo hilo? Kama jibu ni ndio kusudi limetimia
3. Ni kweli kwamba waliokamatwa na kushitakiwa mahakamani walikuwa wakinywa pombe, kusajili simu na kuwasiliana kwa njia ya simu katika tarehe na muda tajwa? Kama jibu ni ndio, kusudi limetima
4. Ni kweli kwamba baada ya kukamatwa washitakiwa na kupekuliwa katika eneo walilokutwa walikutwa wakiwa na silaha na kete za dawa za kulevya? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
5. Ni kweli kwamba baada ya kukamatwa washitakiwa na kupekuliwa kuna nyaraka ziliandikishwa kisha mashihidi kadhaa wakashuhudia kilichofanyika kisha wakasaini kuthibitisho kilichoandikwa ni sahihi? Kama jibu ni ndio basi kusudi limetimia
 
Swali NI kuwa walikamatwa na hivyo vitu katika eneo hilo?

Mashtaka wanasema walikamatwa navyo wenyewe na upande wa utetezi wanakanusha.

Polisi wanajulikana kwa kubambika kesi. Hamza anaweza kuwa alikuwa ni shahidi mwaminifu kwenye hilo.

Watakuja mashahidi waliokuwa pia eneo la tukio watakaosema hawakukutwa na vitu hivyo.

Si ndipo umuhimu wa Ushahidi wa kuaminika unapokuja?

Au wewe huoni hivyo ndugu yangu?
 
Nilichoelewa Mimi watuhumiwa hao walikamatwa hapo wakiwa na bastola na hizo kete.
huyo ndo aliona.
Kashindwa tambua watuhumiwa mahakamani.

Pia yeye anatoa idadi ya kete 83 wakati kingai anasema 58 tu

Na maelezo yake kaandika kete 21 huku kaiambia mahakama kete 25 tena

Kwenye maelezo anasema amesain sehem moja maelezo ya leo anasema alisain 4.. mbaya zaid hakuna inayofanana na nyenzie

Maelezo yake mengi yanapishana kama mtu alie hadhithiwa
 
Ndio maana kitabibu ni kweli baadhi ya watu wana uwezo wa kuona mbali au karibu kwa hiyo hakuna tatizo katika maelezo yake ya ushahidi.

Wakili ameshindwa kuhoji kama ana matatizo ya kuona na kwamba alishathibishwa hospitalini ili adai cheti cha kupimwa kwake. Mawakili wanaojifunza wanafikiri kila kinachofundishwa darasani ndicho kilichoko kwenye uhalisia ndio maana pakawepo na shule ya sheria (Law School) kumwandaa na uwanja wa hoja tunduizi
Kitabibu, wanaposema mtu ana uwezo wa kuona karibu, mita 10 siyo umbali unaosema ni karibu. Umbali wa karibu hauzidi mita 1. Ndiyo maana anayeshindwa kuona karibu, akitaka kusoma, hupeleka kitu anachotaka kukisoma, umbali wa 50 - 100cm, na siyo mita 5 au 10.
 
Hayo ni mawazo yako binafsi hayana uthibitisho wa kidaktari kwahiyo ni mfilisi
 
Lengo la ushahidi wake ni kuonesha kwamba ukamataji wa watuhumiwa ulifuata taratibu, na pia maelezo ya polisi ni ya kweli.

Hakuna anayepinga kuhusu lengo la ushahidi.

Hata hivyo thamani ya ushahidi si inatokana na ambavyo unaweza kuaminika kuwa ni wa kweli?
 
Back
Top Bottom