Kesi ya Mbowe; Umejifunza nini kipya?

Kesi ya Mbowe; Umejifunza nini kipya?

Nimejifunza kuwa kesi ya ugaidi inaendeshwa na ushahidi wa makaratasi.

Makaratasi yameandikwa ukataji miti kama mojawapo ya ugaidi. Lakini haujaletwa hata wembe ambao ungetumika kukatia hiyo miti.

Magaidi walipanga kulipua ila sijaona vilipuzi vilivyokamatwa. Walikua wanaenda kulipua na fegi au.

Nimeona pia magaidi wa aina yake, wasiomiliki silaha ya kueleweka zaidi ya bastola ya mchongo.

Nimejifunza pia kwamba kuna muda shahidi anakua competent mpaka jaji anahisi anaoneshwa majibu. Jaji anashindwa kuficha ukweli kwamba katumwa kuonea anaamua kuropoka.

Pia makampuni ya mawasiliano yakiongozwa na tigo, si ya kuamini hata kidogo. Wanaweza toa taarifa za mteja bila mteja kuarifiwa.
 
Nimegundua yafuatayo.

Kwamba Police wanaweza kukubambikia kesi wakati wowote.

Kwamba wana uwezo wa kutafuta mashaidi wa uongo bila aibu.

Kwamba wana uwezo wa kutengeneza kidhibiti/vidhibiti vya uongo eg nyaraka za Serekali bila uoga.

Kwamba Police wengi uwezo wao wa kufikiri na kutenda ni wa kiwango cha chini sana ukilinganisha na cheo au vyeo walivyonavyo.

Kwamba Police hawafuati miongozo yao wenyewe PGO watafanyakazi kwa namna ya kihuni na unabaishaji na hata udhalilisha na kibaya zaidi wanatumika kisiasa.

Kwamba Mahakama zetu zipo kwaajili ya kuwatumikia wanasiasa wenye madaraka.

Kwamba Mahakama haitoi haki

Kwamba Majaji wengi ni wababaishaji wa kiwango cha kutisha.

Kwamba Mahakama na DPP ni kitu kimoja zinafanyakazi pamoja hasa kesi inapokuwa ya kisiasa.Mshitaki na mtoa haki wanashirikiana na wanatafuta namna bora ya kukunyima haki.

Kwamba mawakili wa Serekali si watetezi wa haki !.

Kwamba nchi hii hatuko salama linapokuja swala la haki,ikiwa wanajeshi Makomandoo wanaweza kuteswa,kusingiziwa kesi mbaya tena pasipo hofu ni nani yuko salama.

Kwamba Matatizo mengi niliyotuma orozesha hapo juu yataweza kutatuliwa na KATIBA MPYA.
 
Naanza uzi huu kufuatia maelezo ya wale waliofuatia kesi hii kwa karibu kwamba wamejifunza/gundua mengi ambayo hawakuwa hapo mwanzo wanayajua. Sasa ili kuwadirikisha wale wasioifuatia, au waliokuwa na gap ya kufuatia, tupe uliloligundua kwa sharti ueleze shahidi nani alilisema, hoji hilo. Hii ni ili kusiwe na fake news!

1- Nimegundua kuwa baadhi ya askari wanawabambikia kesi raia wema- ushahidi wa xxx
2-
3- n.k.
1. Nimejifunza umuhimu wa kusoma na kuzielewa sheria za nchi na hata za nchi zingine (ambazo zinaendana na sheria zetu au ambazo ni 'persuasive authorities' katika mahakama zetu).
2. Nimejifunza kwamba usikubali kuchukuliwa na kukochiwa kutoa ushahidi mahakamani maana utaondolewa kwenye reli wakati wa cross-examination na utaaibika mwenyewe - wanasheria wetu wako vizuri.
3. Nimejifunza pia sheria ni dhana pana na hivyo hata kwa wanasheria wetu wa pande zote - upande wa mashtaka na wa utetezi - wanahitaji kujiendeleza zaidi katika uwasilishaji na utumiaji wa kesi za rejea. Kwenye pande zote wakati wa 'cross-examination' wako vizuri: hivyo nawapongeza.
 
Hakuna jipya lolote la kujifunza.
Ule upuuzi watu wengi tumekuwa tukifanyiwa.
Tunaishi kwenye jamii iliyojaa dhulma na uovu. Kuna baadhi yetu ni mashetani.
 
Nimejifunza ya kuwa Saameer alishamaliza hii kesi na majaji wanaijua hukumu, kinachoendelea mahakamani ni vunga tu na matumizi mabaya ya pesa za kodi.
 
Nimeelewa case ya Trial with trial inamaana kubwa sana

Nimeelewa kumbe DR inawezwa kuchanwa na kugundishwa na gundi ya minyaa

Nimeelewa kumbe unaweza ukawa upo chini ya polisi then ukala nao chakula na mo energy ya kushushia

Nimealewa kumbe rau madukani unaweza kusimama, kunywa mbege na kutengeneza lain kwa wakati mmoja

Nimeelewa kumbe basi la Kilimanjaro linatoka singida na kuishia Arusha kwa rout za kuiba ili shahidi afike mahakamani

Hii case Ina maajabu pale jaji anampa pole police officer kwa kuulizwa maswali mazito

Nimeelewa inawekana marafiki zangu baadhi watakuwa magereza ila wanebadilishiwa majina

Nimeelewa general mahita alikuwa na roho mbaya tena akamzaa mtoto wake anaroho mbaya

Note: Nimetoa angalizo kwa watoto wangu wakiume na wajukuu zangu wasije kuoa wanawake wanaotoka kwenye ukoo wenye vinasaba kama nilivyooredhesha

1.Jaji sayani
2. Jaji Tiganga
3. Chavula
4.kidando
5.Kingai
6.Goodluck
7.Jumanne
8.Siro
 
Nimejifunza:
1. Katika jeshi la polisi kuna vikundi vya wahuni wanaofanya kazi nje ya utaratibu(PGO) na IGP hana sauti katika ilo
2. Jaji mkuu na IGP ni kivuli tu
3. Majaji sio waheshimiwa pia hawapo huru (wanapokea maelekezo toka juu) katika kuendesha kesi
 
Mkali niwezeshe nisome yalio jiri jana na leo Mahakamani kuhusu Mbow 0625780268 kwa wasap asante.
 
Hakuna jipya lolote la kujifunza.
Ule upuuzi watu wengi tumekuwa tukifanyiwa.
Tunaishi kwenye jamii iliyojaa dhulma na uovu. Kuna baadhi yetu ni mashetani.
Ni kweli na ndiyo mafunzo niliyopata na namna mojawapo ya kusaidia kuondoa 'huo upuuzi' ni kujifunza na kuzielewa sheria zinasema nini na zinataka nini au hazitaki nini.
 
Kwenye kesi hii nimejifunza kwamba
HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO ANAUWEZO MKUBWA KUAMUA KESI KULIKO JAJI
 
Funzo tulo sawa na wapemba anaweza kuwa tajiri mkubwa lakini choo hajengi cha maana. Mfumo wetu wa haki jinai na mahakama kwa ujumla ni mbovu wote na sijui malaika gani ataweza ku overhaul.

Huko kwa Dpp ndio usiseme, haki za watuhumiwa hakuna, police hawana proffessional conduct ni ile gonga nyundo tuu msumari uzame hakuna logic kabisa. Hata Kenya kuna unafuu. Sababu kibwa ni hata watendaji kuheshimu sheria za utendaji wao wa kazi. Kuwa na Regulatory police oversight body na mchawi mkubwa ni hizi kazi za kuteuana zinaua sana uadilifu na ethical workplace practice. Watu waombe kazi na interview ioneshwe TBC hata IGP, majaji, mahakimu watu wenye udahifu wanakuwamo na kuleta udhaifu zaidi .
 
Nimejifunza jambo moja la muhimu sana.Kuwa kuna watu wako pembeni wanapalilia ugali wao.Wao kila siku nikusema Mh wetu ni gaidi wakati kihalisia,kila aliyeifuatilia hii kesi,,haina mashiko kabisa. Hata Mwenda zake angekuwepo leo,,angewaponda watengeneza kesi.
 
Back
Top Bottom