omujubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 4,326
- 2,506
Mwalimu Nyerere alitupatia 'mateso' kama vile kocha anavyowafanyisha wachezaji mazoezi magumu. Hakuwa na nia ya kukomoa mtu bali alikuwa na visions zake za miaka 100 mbele wakati waliomzunguka walikuwa na vision za mwezi mmoja mbele. Sio ajabu yeye aliliangalia taifa kwa ukubwa wake lakini huwezi amini waliomfuatia (wengi walimzunguka) mtu mwenye hadhi ya uwaziri unakuta upeo wake si kuangalia hata watu wa mkoa wake bali familia yake na mkewe tu.
Katika maadui alopambana nao mmoja alikuwa ni UJINGA, waliomfuatila walidharau na matokeo yake wajinga wamekuwa wengi na kwa vile mfumo ni wa 'wengi wape' sasa wamejipenyeza hadi kwenye nafasi za maamuzi na kuzaa haya, Dunia inatuangalia na kutucheka