Shahidi #2 wa upande wa mashtaka Justine Kaaya katika ushahidi wake kaeleza ya kwake:
1. Alivyokutana na Mh. Mbowe
2. Alivyompa Mbowe taarifa za washirika wa Sabaya.
3. Alivyosafiri Longido, Arusha, Moshi.
4. Malipo aliyopata kutoka kwa Mh. Mbowe.
Shahidi anathibitisha kuwa, hakuwahi kusikia jinai yoyote ikijadiliwa kwenye mahusiano yake na Mh. Mbowe. Kwamba hakuwahi kuhusishwa katika mpango wala mkutano wowote wa kumdhuru mtu yeyote.
Shahidi anathibitisha kuwa hakuwahi kudhulumiwa au kujisikia kutokutendewa haki popote na Mheshimiwa Mbowe. Kwamba wala hakuwahi kusikia wala kuona Mh. Mbowe akipanga au kumtendea yeyote ndivyo sivyo.
Shahidi anathibitisha kuwa hakuwa na shaka yoyote na Mheshimiwa Mbowe au washirika aliokuwa nao. Ndiyo maana hakuwahi kutoa ripoti au taarifa popote ikiwamo polisi.
Hakuwahi kutoa onyo lolote la tahadhari au vyovyote kwa Sabaya, Jesca au washirika wa Sabaya kwa kuwa hakukuwa na sababu hiyo.
Zaidi sana kwa mukthadha wa kesi hii, Justin Kaaya hakuwahi hata kukutana na Adamoo, Ling'wenya, wala Lijenje kabla ya kukamatwa kwao.
Kwenye mazingira haya Justin Kaaya alikuwa na umuhimu gani kwenye kesi hii?
Au ni mwendelezo ule ule wa kustajaabu vigezo vya hukumu kama zile za mapingamizi?
Kesi ya Mbowe: Ushahidi upande wa Mashtaka unapochukuliwa kuwa ndiyo Dhahiri