Kesi ya Mbowe: Ushauri wa Bure kwa Mawakili Wasomi - Utetezi

Kesi ya Mbowe: Ushauri wa Bure kwa Mawakili Wasomi - Utetezi

Awali ya yote pokeeni pongezi za dhati kwa kazi takatifu mnayoifanya ya kuisaka haki katika mazingira magumu.

Kazi yenu ni ngumu zaidi hasa ikizingatiwa kuwa mafanikio yoyote yanayopatikana yanahatarisha matumbo ya watu yenye uchu uliopitiliza.

Jambo moja la hakika lenye kutia moyo ni kuwa tupo watanzania mamilioni nyuma yenu. Hawa wako katika kada zote, weledi mbalimbali na karama za aina zote. Tafsiri halisi ya maneno haya:

View attachment 2006502

Ni dhahiri kuwa ipo nia na mikakati ya dhati ya kuipora haki mchana kweupe. Mifano iko mingi na iko wazi.

Albert Einstein anasema:

“Insanity is doing the same thing over and over and expecting different results.”

Tunayo sababu ipi ya kutegemea majibu tofauti sasa?

Muhimu kujipanga kivingine. Muhimu kuendelea kukusanya ushahidi ukiwamo bora zaidi kila inapowezekana dhidi yao.

Wajumbe wa kujitolea kwenye haya tupo wengi. Tusipuuzie wala kudharau jambo. Twende kwenye uhalisia zaidi yakiwamo matumizi ya sayansi, kuwaumbua majambazi hawa wa haki:

View attachment 2006651

Tulete mashahidi zikiwemo video kutokea RAU madukani. Kama vipi mahakama iombwe kwenda sehemu zinazotajwa ikiwamo RAU madukani.

Mahita na kundi lake walipita kushoto na wenzao kulia. Eneo kulikuwa wazi na walipaki nyuma ya hilo banda. Waonyeshe Lijenje angeweza kutoweka vipi bila kuonekana.

Mahakama iombwe kutumia mamlaka yake kuwalazimisha kumleta Lijenje, wako naye.

Mahakama iombwe kushurutisha taarifa zozote kupatikana popote kwa mustakabala wa haki.

Mizunguko ya Kingai na kundi lake Moshi - Arusha - Moshi - Dar - Mbweni ithibitishwe siyo kwa maneno matupu.

Maneno matupu hayavunji mfupa na mkono mtupu haulambwi

Aluta Continua!

---------

Detention Register: Jaji Tiganga yuko Majaribuni - Kiza Kinene

(S.M.P2503 - credit kwako mkuu)
HUWEZI KUMFUNDISHA JAJI KUFANYA KAZI YAKE WEWE NI NANI?
 
Leo yasikie - Luvanda, Siyani, Tingatinga ni ukakasi mtupu.
Jamaa anasemaga anaenda Kuzipiti hoja na kutazama Sheria zinavyosema ili aje atoe maamuzi. Kumbe anatuingiza chaka, anachokwenda kuangalia ni jinsi gani ayatupilie mbali mapingamizi ya washitakiwa kwa kupewa tuition ya nguvu
 
Jamaa anasemaga anaenda Kuzipiti hoja na kutazama Sheria zinavyosema ili aje atoe maamuzi. Kumbe anatuingiza chaka, anachokwenda kuangalia ni jinsi gani ayatupilie mbali mapingamizi ya washitakiwa kwa kupewa tuition ya nguvu

Huwa anakwenda kutafuta visingizio 😁😁.
 
Back
Top Bottom