Wametangaza hadharani kuwa wamewafukuza, kwao wanapaswa kuishia hapo.
Kumbe wameishia hadi wapi? Hapo ndipo walipoishia...!
CHADEMA haijaenda mahakamani. Waliofukuzwa uanachama ndo wameshitaki. Na mshitakiwa mmojawapo ni CHADEMA. Labda ungesema, wasiitikie wito wa mahakama. Je, wakifanya vile hiyo ndo itakuwa akili siyo?
Maana bunge hili la Sasa liketokana na uchaguzi ambao chadema hawautambui na matokeo yake.
Ndivyo ilivyo, hakijabadilika kitu. Wewe shida yako nini kwani?
Sasa shida Yao nini kutaka lazima akina Mdee watoke kwenye bunge wasilolitambua?
Usichoelewa ni nini kwani? Unajua ili mtu awe mbunge kikatiba anatakiwa awe na sifa gani? In case kama hujui, ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa!
Kwa hiyo si CHADEMA wanaowatoa Bungeni hao kinamama. Ni sheria na katiba zinawatoa...!
Na unajua ni kwanini hawa kina mama wameenda mahakamani?
In case kama hujui, wameenda kuutetea uanachama wao ili wasikose sifa ya kuwa wabunge...!!!
Kama chadema wangeyakubali matokeo tangu mwanzo shauri kama hili lisingekuwepo kama lilivyo Sasa. Wake kimya TU kwakweli.
Unajua uandikacho kweli wewe? Kwani mambo ya ndani ya chama cha CHADEMA na bunge yanahusianaje kwa mfano? CHADEMA wamefanya yawahusuyo, that's all. Hayo mengine hayawahusu. Hawana shida na Bunge. Unaelekeza lawama hizi kwa watu wasiohusika. Think twice and carefully, mwisho wa siku utaelewa tu...
Mimi nilidhani wanakwenda mahakamani kusimamisha bunge Zima kuwa halikupatikana kihalali, kumbe ni akina Mdee TU.
Ndio maana nakuambia hujui usemalo kwa sbb ya kukosa uelewa na ufahamu wa kisheria na kikatiba!!
Kwa sheria na katiba yetu ya 1977 utatumia sheria gani kwenda kusimamisha bunge zima lisifanye kazi?
Narudia tena. CHADEMA wanashughulika na mambo ya ndani ya chama na wanachama wao. Na kwa kwa kweli wako sahihi na ndiyo maana maamuzi yao yamei - shock system nzima...
Haya uyaonayo ndugu
kavulata ni matokeo ya aftershock. Yaani ni matokeo ya maamuzi smart kabisa ya CHADEMA. Hakuna kingine..
Wewe unasema usichokijua. Pole sana..!!