Kesi ya Mdee na wenzake 18 yaitia aibu CHADEMA

Kesi ya Mdee na wenzake 18 yaitia aibu CHADEMA

Sisi wanachama wa CHADEMA tunataka kuona, kusikia na kufanya mambo yanayosaidia kujenga, kukuza na hatimaye CHADEMA kuingia ikulu.

Kwa mara nyingine CHADEMA imenasa kwenye mtego wa ulimbo wa CCM. CHADEMA Inahangaika na kuwaondoa wanawake wao bungeni kwenye uchaguzi ambao cHADEMA walikataa kuutambua matokeo yake mpaka Leo.

Kesi hii ya kutaka akina Mdee watoke bungeni ilipaswa kutanguliwa na CHADEMA kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020 kwanza. CHADEMA walipaswa kuishia kwenye kuwafukuza uanachama akina Mdee TU basi na sio kukaza shingo lazima watoke kwenye bunge ambalo wao hawalikubali.

Kesi Yao ingekuwa na mashiko kama chadema wangepinga wabunge wote wa bunge kuweko bungeni maana hawakuchaguliwa kihalali kwa kutumia tume wasioikubali kuwa sio huru.

Maadam hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi basi bunge pia sio halali kwao. Kumlazimisha Mdee TU kuwa ndiye wakutoka bungeni badala ya bunge zima ni kukosa dira na mwelekeo. Kwangu Mimi akina Mdee hawapaswi kuwa bungeni sawa na wabunge wengine wote kutokana na namna uchaguzi mzima ulivyoendeshwa. Njaa Kali, undugu na ukabila ndiyo sababu ya kuwashupalia akina Mdee.
Taifa lina vijana wenye fikra finyu sana, ulipo huelewi hata kwamba wao kuwepo bungeni ni kuikanyaga katiba. Hata madhara ya tendo hilo hujui, kwako cha muhimu ni chama tu
 
Ni ubinafsi tu.mambo mengi yapo hovyo.wangewaacha akina mdee waendelee na hilo Bunge,na chama kama chama waendelee kujipanga kwa yajayo wapambanie katiba mpya na zaidi tume huru ya uchaguzi
 
Wale kina mama wasimbe wengine wanawaonea wivu hawa wasimbe wengine!
 
Nchi hii ina watu wa ovyo sana .kwa perception aliyo nayo mtoa post kweli nimeamini kuna haja ya kureview mitaala yetu kuanzia awali mpaka elimu ya juu
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
CHADEMA wakubali tu walishindwa uchaguzi 2020 wala wasione aibu CCM wenzao walijipanga na sera nzuri kwa wananchi lakini Tundu alishindwa kushawishi watu matokeo yake akaponza chama chake chote sasa waache usanii wa maridhiano ili wapewe nafasi za kuteuliwa(njaa inawatafuna huku mtaani) kisa walishindwa kuwashawisha wapiga kura saizi wanawasumbua walioshinda uchaguzi huo sio ustaarabu kwa kweli mbona 2025 sio mbali wavumilie tu tushinde nao vijiweni[emoji23][emoji23].Siasa sio ajira ya kudumu watu wakikuchoka kama yule ya Mbeya na Arusha unakaa benchi kwani wewe ni nani bwana.
 
Jambo ambalo viongozi wa chadema hawapendi kuliweka wazi kujibu maswali yafuatayo:

1. Je, mwafaka (kama upo) umesabababisha chadema kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020?

2. Chadema inanufaikaje na akina Mdee kutoka bungeni Sasa?

3. Je, wabunge wa CCM ni halali?

4. Je, akina Mdee wakitoka bungeni watapeleka watu wengine kuchukua nafasi zao?

5. Chadema inapata hasara gani kwa akina Mdee kuwepo bungeni?

6. Je, ni lini chadema watatangaza kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa 2020?
Ungeongeza na swali hili kuwaachia akina mdee ubunge wa mchongo ni sehemu ya muafaka ?ingekuwa poa sana
 
Chadema wanapaswa kujua kuwa kipindi Cha awamu ya Tano kulikuwa na mambo mengi sana. Ni kipindi Cha kusameheana kwa watanzania wote kwakweli, maana hakukuwa na formula ya aina yoyote iliyokuwa ikifanya kazi. Inasikitisha kuona wanachadema wenyewe hawataki reconsolidation ndani ya Chama ila wanataka reconsolidation kwenye taifa. Ujinga mtupu
Reconciliation not as stated.
 
Ungeongeza na swali hili kuwaachia akina mdee ubunge wa mchongo ni sehemu ya muafaka ?ingekuwa poa sana
Eti muafaka afanye Samia TU Ila wao waendelee kuparurana ndani ya chama, ujinga gani huu. Mwafaka lazima uanzie ndani ya vyama vyao kwanza
 
Umeandika maelezo mengi alafu mashudu tupu.
Pinga kwa hoja. Tuambie faida mtakayoipata chadema kama wabunge wenu 19 watafurushwa bungeni. Hamna haya kabisa. Bawacha Kuna vijimama vinaota kwenda bungeni vikagange njaa zao. Halima ni chadema na chadema ni Halima. Tunafahamu kuwa kila mtu chadema anakwenda bungeni kwa maslahi yake binafsi, ndiyo maana wabunge wetu kila mmoja anamiliki Mali nyingi, na wengine wanakula Bata ughaibuni kwa ksngizio Cha usalama wa maisha yao
 
Jambo ambalo viongozi wa chadema hawapendi kuliweka wazi kujibu maswali yafuatayo:

1. Je, mwafaka (kama upo) umesabababisha chadema kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020?

2. Chadema inanufaikaje na akina Mdee kutoka bungeni Sasa?

3. Je, wabunge wa CCM ni halali?

4. Je, akina Mdee wakitoka bungeni watapeleka watu wengine kuchukua nafasi zao?

5. Chadema inapata hasara gani kwa akina Mdee kuwepo bungeni?

6. Je, ni lini chadema watatangaza kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa 2020?
Halima kiboko !! Katengeneza chawa inaitwa kavulata!!
 
Wanaume wa chadema wanapelekewa moto na wanawake waliowatengeneza wenyewe
Baada ya kusoma comment hii, ikabidi niende kwenye ID yako.
Nilichogundua ni kuwa kama huna sononi, afya ya akili ni mgogoro,basi malezi yako ya utotoni yalikuwa ya kimasikini kulikopelekea upate udumavu wa akili.
Pole sana kijana.
Mungu atakusaidia upate nafuu na upone.
 
Jambo ambalo viongozi wa chadema hawapendi kuliweka wazi kujibu maswali yafuatayo:

1. Je, mwafaka (kama upo) umesabababisha chadema kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020?

2. Chadema inanufaikaje na akina Mdee kutoka bungeni Sasa?

3. Je, wabunge wa CCM ni halali?

4. Je, akina Mdee wakitoka bungeni watapeleka watu wengine kuchukua nafasi zao?

5. Chadema inapata hasara gani kwa akina Mdee kuwepo bungeni?

6. Je, ni lini chadema watatangaza kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa 2020?
Hawana majibu zaidi ya matusi na kejeli.
 
Pinga kwa hoja. Tuambie faida mtakayoipata chadema kama wabunge wenu 19 watafurushwa bungeni. Hamna haya kabisa. Bawacha Kuna vijimama vinaota kwenda bungeni vikagange njaa zao. Halima ni chadema na chadema ni Halima. Tunafahamu kuwa kila mtu chadema anakwenda bungeni kwa maslahi yake binafsi, ndiyo maana wabunge wetu kila mmoja anamiliki Mali nyingi, na wengine wanakula Bata ughaibuni kwa ksngizio Cha usalama wa maisha yao
Halima Simjui Wala hanijui, tunachakata ukweli TU. Hakuna ubishi kuwa vyama vya upinzani ni kama saccos TU, vinaenda bungeni kutibu njaa zao binafsi. Mwaka 1995 Lyatonga alishindwa uchaguzi na kulalamika kuwa kaibiwa kura, tena kwenye uchaguzi ule hata masanduku ya kura da es salaam yalifika kesho yake kwenye vituo vya kupigia kura, lakini watu hawakugomea ubunge, chaguzi zilizofuata Lipumba, Mbowe, Silaa, Lowasa retrospectively waliibiwa kura sana Lakini wabunge wakiwemo Lissu, Mbowe, Sugu, Mnyika, Msigwa, hawakugomea bunge kabisa pamoja na kulalama kuwa uchaguzi sio fair and free. Kioja ni mwaka 2020 ambao mgombea Lissu nae kaibiwa kura vilevile kama wengine, lakini mwaka huu ndio tunaambiwa hakuna kukanyaga bungeni milele. Hapa ndipo ulipo upuuzi wenyewe. Mara hii kwakuwa Lissu kaibiwa kura na wagombea wanaume wote hawakutangazwa kushinda ndio basi hata dada zetu wasiende kwenye saccos ili nao kujenga hoteli kubwa kama sugu? Huu ni udikteta na ubinafsi uliokithiri.
 
Baada ya kusoma comment hii, ikabidi niende kwenye ID yako.
Nilichogundua ni kuwa kama huna sononi, afya ya akili ni mgogoro,basi malezi yako ya utotoni yalikuwa ya kimasikini kulikopelekea upate udumavu wa akili.
Pole sana kijana.
Mungu atakusaidia upate nafuu na upone.
Wanawake bhana, sasa kuwashwa gani huko hadi kufuatilia I'D yangu.? Njoo nikukune bc mlango uko wazi wewe suKUMA.
 
Unanchanganya mambo,tuanze hivi,kwa mujibu wa katiba,huwezi kuwa Mbunge bila udhamini wa chama,hiyo ni fact ya kwanza,
Kina mdee wapo bungeni kwa udhamini wa chama gani?wakati Chadema iliisha wafukuza chamani kwa utovu wa nidhamu!?
Kazi yako muhimu ni kuwafukuza uanachama, Wacha hao waliowapeleka bungeni wamalizane nao wao wenyewe. Kiherere Cha nn?
 
Ungeongeza na swali hili kuwaachia akina mdee ubunge wa mchongo ni sehemu ya muafaka ?ingekuwa poa sana
Kaka hata mamlaka za maamuzi zimefungwa mikono Yao nyuma. Awamu ya Tano kila mtu aliyekuwepo anafahamu ilikuwa ni awamu ya aina gani. Hivi unadhani Rais JPM alikuwa hajui kama akina Halima wako bungeni? Ndio maana nasema awamu ya Tano isifukue makaburi tugange yajayo kuanzia ndani vya vyama vyenyewe. Huenda akina Halima hawakwenda bungeni kwa hiari yao. Kama akina Halima wangekataa kwenda bungeni huwenda wangepatwa na jambo.
 
Sisi wanachama wa CHADEMA tunataka kuona, kusikia na kufanya mambo yanayosaidia kujenga, kukuza na hatimaye CHADEMA kuingia ikulu.

Kwa mara nyingine CHADEMA imenasa kwenye mtego wa ulimbo wa CCM. CHADEMA Inahangaika na kuwaondoa wanawake wao bungeni kwenye uchaguzi ambao cHADEMA walikataa kuutambua matokeo yake mpaka Leo.

Kesi hii ya kutaka akina Mdee watoke bungeni ilipaswa kutanguliwa na CHADEMA kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020 kwanza. CHADEMA walipaswa kuishia kwenye kuwafukuza uanachama akina Mdee TU basi na sio kukaza shingo lazima watoke kwenye bunge ambalo wao hawalikubali.

Kesi Yao ingekuwa na mashiko kama chadema wangepinga wabunge wote wa bunge kuweko bungeni maana hawakuchaguliwa kihalali kwa kutumia tume wasioikubali kuwa sio huru.

Maadam hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi basi bunge pia sio halali kwao. Kumlazimisha Mdee TU kuwa ndiye wakutoka bungeni badala ya bunge zima ni kukosa dira na mwelekeo.

Kwangu Mimi akina Mdee hawapaswi kuwa bungeni sawa na wabunge wengine wote kutokana na namna uchaguzi mzima ulivyoendeshwa. Njaa Kali, undugu na ukabila ndiyo sababu ya kuwashupalia akina Mdee.
Sawa Mdee ,Chadema wamekusikia nadhani
 
Mfano unaotoa hauna mashiko, ukiachana na uchama tambua kwanza kuwa chadema pia Ni wananchi, na Wana haki ya kuhoji kitu chenye hakiendi sawa, na pia usisahau hao wabunge waliovikwa/ jivika kivuli Cha chadema wanakula jasho la watanzania
Binafsi naona chadema wako sawa ktk hili
Jasho la wananchi kuliwa kuko palepale Hata kama akina Halima wasingekwenda bungeni bungeni wangekwenda CCM kuzijaza nafasi
 
Back
Top Bottom