waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 197
- 468
Kesi ya Mgogoro wa Ardhi baina ya Kanisa la Christ Synagogue Ministries lililopo Sakina jijini Arusha na wasimamizi wa mirathi Bernadette Changuru na Samweli Changuru imeahirishwa hadi Agosti 11 mwaka huu.
Shauri hilo namba 57/2021 linasikikizwa na Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Arusha,Mbele ya mwenyekiti wa Baraza hilo, Gladness Kagaluki ambapo jana lilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa .
Wakili wa upande wa mashtaka, Ismail Chaluo alieleza mahakama hiyo kwamba shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa ,hata hivyo upande wa wajibu maombi wakiwakilishwa na Wakili Ndibalema Johnson waliomba muda ili waweze kupitia madai ya walalamikaji na kujipanga kuyajibu mahakamani .
"Mheshimiwa mwenyekiti tunaomba muda wa siku 21 ili tukayapitie haya madai ya walalamikaji na tujipange kwa ajili ya kujibu hoja hizo za upande wa Pili"alisema Wakili Ndibalema.
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Kagaluki aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 11 mwaka huu litakapokuja kwa ajili ya kusikiliza.
Wakati huo huo shauri jingine mlalamikaji ambaye ni Kanisa la Christ Synagogue Ministries kupitia Wakili,Shaluo anaiomba mahakama hiyo kusikiliza shauri dogo namba 199/2021 ili kumpatia zuio la kuondolewa katika eneo lenye mgogoro alilojenga Kanisa hadi kesi ya Msingi itakaposikilizwa.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Baraza hilo la Ardhi na Nyumba, Hakimu, Kagaluki alitoa siku Saba kwa upande wa wajibu maombi kuweza kuwasilisha hoja za utetezi na kwamba shauri hilo limepangwa kusikilizwa Agosti 11 mwaka huu.
Akiongea nje ya mahakama wakili wa utetezi, Ndibalema Johnson alisema kuwa kesi ya Msingi inahusiana na mgogoro wa eneo baina ya Kanisa na wasimamizi wa mirathi Bernadette Changuru na Samweli Changuru ambapo Nabii wa Kanisa hilo Baraka Odillo anajaribu kujimilikisha eneo hilo alilokuwa amepanga.
Nje ya mahakama Msimamizi wa mirathi , Bernadette Changuru Mkazi wa Mbauda jijini Arusha,ambaye ni mke wa marehemu Silas Chunguru aliyefariki mwaka 2019 ,alisema kuwa mchungaji Odillo ni mpangaji wao Hadi Sasa na ameshitushwa na hatua ya kudai marehemu mumewe alimuuzia eneo hilo , kwani hadi Mei mwaka huu Nabii alikuwa aliendelea kulipa Kodi ya pango.
Ends....