Kesi ya Mirathi ya Dkt. Likwelile: Vicky Kamata ashindwa, mahakama yasema ndoa yao haikuwa halali

Kesi ya Mirathi ya Dkt. Likwelile: Vicky Kamata ashindwa, mahakama yasema ndoa yao haikuwa halali

Ndugu ukifuatilia hiyo nakala ya kesi kuna ukakasi. Cheti cha ndoa kilicholetwa mahakamani ni cheti cha ndoa ya kiserikali. Imefungwa 1986. Je ndoa ya kiserikali imefungwa kuwa ya mke mmoja tu kama ya Kikristo? Halafu hapo kati mzee alioa mke mwingine. Na je kama alichana na mke wa kwanza miaka tuseme zaidi ya kumi japo ndoa haijavunjwa bado itahesabika kama ndoa? Ngoja nirudi nyuma kwenye sheria ya ndoa niangalie hizo dynamics
Hata wangetengana miaka 20 kama haikuvunjwa mahakamani
Bado ni ndoa Hallali
Mahakama inpokea vithibitisho sio maneno
 
Hapo hata mimi nimeishiwa na maneno. Sema nafarijika kuwa hilo bandiko ni la kutengeneza tu, siyo hukumu ya Judge, hawezi kufanya makosa ya kjinga namna hiyo.

Barua haina muhuri wala tarehe.

Hapo anarushwa roho Vicky Kamata, kimtandao.

Tusiamini kila linaloletwa kwenye hii mitandao.
Ni kweli hukumu imetoka Vicky mwenyewe aliandika Instagram kulalamika pia
 
Nina swali moja, kwenye mwenendo wa kesi inasemekana Dr alioa 1986. Ndoa ya kiserikali. Mwaka 94 akasheherekea ndoa ya kikristo. Je unapewa vyeti viwili? Kama cheti cha kwanza ndicho halali je ndoa ya kiserikali ni ya mke mmoja au wake wengi?
Ndio alipewa vyeti viwili
Katika cheti Cha ndoa Kuna sehemu ya mke mmoja na wake wengi unachagua
Lakini cheti hicho hicho kinatymika kanisani mchungaji au padri anajaza sehemu ya mke mmoja anaweka tick
Kwa sababu kanisani huwezi kuchagua ndoa ya wake wengi
 
Tuliobahati kufika mahakamani kwa siku chache wakati wa kesi hii tulicheka sana na kujifunza. Picha linaanza anaombwa cheti cha ndoa katoa kumbe ni batili baada ya mahakama kujiridhisha. Ilikua hivi, jina la kanisa feki, pastor feki basi mahakamani ikaomba mshenga, msimamizi wa harusi jibu la Vick eti wooote kwa sasa ni marehemu.

Kwa jitihada za watoto halali wa Mzee wakafanya safari mpaka Sengerema kufika kwenye kanisa husika, kanisa lilkakata kutambua cheti hicho. Pia akafikiwa anaesemekana ndio kafungisha ndoa alirubuniwa majina yake kutumika kama pastor lakini yeye hana taaluma hiyo kabisa.

Ila anamtambua Vick kama jirani na class mate wake tu. Basi mahakama pia ikaomba picha ya harusi yao Vicky anasema zimepotea. Sema wazee marafiku wa Dkt. Likwelile wanasema tangu enzi za uhai wa marehemu alikua anasema Vick kwangu kafata mali na si vinginevyo.

Hivyo aliwachia OG mirathi ambayo imekuja kuwasaidia watoto leo. Dkt. aligawa fei too much sema mdangaji hakuridhika kabisa. Kila MTU alipata chake kabisa. Napenda kuwapongeza wazee wamjini kusaidia watoto wa marehemu hata pale mlipohitajika mliacha safari zenu na kuja mahakamani. Mungu awasimamie na awape maisha marefu mnoo.

Naomba nikutambue Mzee wa msafara, mkuu wa ruti, Mzee wa mjini na marafiki wooote wa marehemu na familia kwa ujumla. Sema Vick anapenda ulozi jamani mpaka nikimuangaliaga nabakia kusema hii ni Hatare na nusu. Full waganga kutoka kwao kanda ya ziwa ogopa mganga hajui kiswahili ni kilugha tu. Lakini leo mahakama imewashinda. Sema watoto wa marehemu acheni uzungu sana.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]mganga hajui kiswahili
Kuna Mungu wa Kweli halafu Kuna shetani kwenye Mungu shetani hakai na Haki ya Mtu haipotei
 
Wakati anaona na Vicky mlijuaje kama alikua hajaivunja mahakamani? Kwa hiyo mnataka kusema katibu mkuu wa wizara ya fedha alikua na upungufu wa akili? Maana wameona bado yupo kwenye utumishi serikalini.

Ndio haina wake wawili ila inavunjwa mahakamani. Je huyo mzee watu wana uhakika haikuvunjwa mahakamani?
Kama ilivunjaa mahakamani si alitajiwa apeleke uthibitisho wa talaka
Kama hakupeleka inaa maana hakuna talaka
Mahakama inahitaji vithibitisho sio maelezo ya mdomo
 
Hawa wanawake Kaz ipo mshua.... Yaaan leo anasema baba yenu hanizid assets, hajui ata cash in hand au bank ni assets au kakariri mpk nyumba tuu.... Na kuita nyumba ety vijumba.... Anywe Savannah alale
Ana dharau demu balaa...means alikua na assets sanaa[emoji38][emoji38][emoji38]ndo akome Sasa kuuvagaa mtumbwi wa vibwengo
Sasa yeye Si angemuacha tu na vijumba vyake hvyo yeye angefanga yake kimya kimya
 
Wanawake wengi wa sasa ni waporaji majambazi tu.. eti mtu anamkuta jamaa ametafuta Mali miaka 30 nyuma, amezaa watoto, anaibuka mwanamke mtoto wa mtu mwingine huko kwa kigezo Cha mapenzi anaitaka hiyo Mali Kwa muda wa miaka hata mitatu tu, huo ni uporaji ambao wanawake wanao fanikiwaga ktk hilo sijui kama wanabakigi salama na kuishi kwa amani , sidhani

Majizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, hawezi kudai. Labda kama umeendeleza kutokana na mali za ndoa. Kwa sababu kwenye mgwanyo wa mali. Lazima Kwanza mali ziwe za ndoa na kuwe na uthibitisho kuwa mhusika amechangia kwenye upatikanaji wake. Na anachopata ni kulingana na mchango wake katika kuipata mali hiyo!
Asante kwa kunielewesha mkuu
 
Back
Top Bottom