Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
KESI YA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE No. 2207/58, KESI YA FIDEL CASTRO 1953 NA KESI YA TUNDU LISSU
Nimeamka na Maktaba.
Kwa haraka haraka nimepitia kijuujuu vitabu hivi viwili vya watu maarufu duniani - Mwalimu Julius Nyerere na Fidel Castro wa Cuba wakishtakiwa na serikali zao zilizokuwa madarakani kipindi wao wanadai uhuru wa nchi zao.
Ukimsoma Mwalimu na yale aliyosema mwaka wa 1958 utatingisha kichwa.
Hakika dunia inazunguka.
Ukimaliza kumsoma Mwalimu msome Fidel Castro, ''History Will Absolve Me,'' wala usimalize kitabu kizima.
Maneno yake ya mwanzo yanatosha.
Yaweke maneno haya ya Fidel Castro mkono wa kulia na ya Mwalimu mkono wa kushoto unasoma huku kisha unerejea ulikotoka.
Ukimaliza msikilize Tundu Lissu.
Nina hakika utapigwa na bumbuazi.
Nasita kuyaweka maneno ya Mwalimu yaliyochapwa katika Sauti ya TANU mwaka wa 1958 yaliyomsababishia kushtakiwa.
Tuna mengi ya kujifunza katika historia kwani historia ni mwalimu mzuri.
Sifa kubwa ya msomi wa sayansi ya siasa ni kuwa na uwezo wa kutabiri.
Kesi ya Tundu Lissu itakuwa ya aina yake.