Kesi ya Sabaya: Ushahidi wa Video za CCTV waonesha shahidi akitoa fedha benki alizomkabidhi Ole Sabaya

Majani nyie mnaliwa na hao mbuzi!
Hiyo ndio hulka yenu hapo lumumba bado laana tu kuwatafuna.
JamiiForums1999776609_240x320.jpg

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa lazima atundikwe mingine 30, atakuta mkewe ana mtoto wa miaka 20 by the time anatokamo...kijana ni JAMBAZI tena sugu...too sad Million 90 uzipate bure bure tu bila kufanya kazi, tena unachukua kwa mwenzio as simple as that.
halafu ile rufaa atashindwa. Jamaa alijidanganya sana aisee, alijitoa fahamu kabisa.

Pale Hai jamaa alikuwa anatisha kila mtu, mbabe, mshenzi, fedhuli, jambazi, kuliko uingie kwenye 18 nafuu ukajifia mwenyewe.

Maskini aliamiñu Magufuli ataishi milele.

Sipati picha Jiwe angekuwepo mpk Leo hawa jamaa na genge lao la WASIOJULIKANA kina Makonda, Musiba, Sabaya, Kheri James nk wangekuwa washapoteza wangapi.

Kifo Cha Jiwe Ni mpango wa Mungu kuinusuru nchi hii.
 
Pale Hai jamaa alikuwa anatisha kila mtu, mbabe, mshenzi, fedhuli, jambazi, kuliko uingie kwenye 18 nafuu ukajifia mwenyewe.
Pale hai kuna bibi alitaka kuvua nguo ampe laana kwa mateso aliyowapa wajukuu zake, watu wakamzuia ila aliongea maneno kwa uchungu mkubwa mno.

Kuna nyumba aliita golgota (Nyumba ya mateso) ukiingia humo ukitoka mzima piga magoti kwa muumba wako.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imelazimika kuahirisha kuendelea kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya shahidi wa 10, Francis Mrosso kudai kuwa anajisikia vibaya.

Shahidi huyo wa Jamhuri, jana alipomaliza kuongozwa kutoa ushahidi wake na Mawakili Waandamizi wa Serikali, Tarsila Gervas na Felix Kwetukia aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi leo.

Shahidi huyo alidai kuwa hali yake siyo nzuri na hajisikii vizuri baada ya kuona video clips sita zikionyesha matukio mbalimbali ya Januari 22, 2021 akiwa Benki ya CRDB tawi la KwaMromboo, Arusha alipoenda kutoa Sh90 milioni.

Ikiwa leo ni siku ya tatu tangu aanze kutoa ushahidi wake kuanzia Novemba 22, 2021 shahidi huyo jana alimalizia ushahidi wake ambapo mahakamani hapo iliwekwa flash yenye clip sita kutoka Benki hiyo, zikimwonyesha namna alivyokwenda kutoa fedha hizo akiwa na baadhi ya watuhumiwa wenzake Sabaya.

Mrosso, ambaye ni mmiliki wa gereji ya Mrosso Injector Pump Service jana alionekana kuwa kimya wakati video hizo zikionyeshwa kwa vipande mahakamani hapo.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo, shahidi huyo alipomaliza kuongozwa kutoa ushahidi wake aliiomba mahakama impe muda atoke nje kwa dakika chache kabla ya kurejea kuanza kuhojiwa na mawakili wa utetezi, ombi ambalo mahakama iliridhia.

Baada ya kurejea ndani ya chumba cha mahakama hiyo, Mrosso alimuomba Hakimu aahirishe kesi hiyo hadi leo kwa kuwa hajisikii vizuri baada ya kuona matukio hayo kutoka kwenye CCTV Camera yaliyoonyeshwa mahakamani hapo.

Mara baada ya ombi hilo, wakili wa utetezi, Mosses Mahuna alidai haoni sababu ya msingi ya shahidi kutaka apumzike.

Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofmed Mtenga aliomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kuwa shahidi hayuko sawa baada ya kuona video hizo za Januari 22, 2021.

Hakimu Kisinda aliridhia ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29, mwaka huu ambapo shahidi huyo ataanza kuhojiwa na mawakili wa utetezi.

Awali akiongozwa na mawakili hao, shahidi huyo kupitia video hizo aliwatambua washtakiwa Enock Mnkeni, John Aweyo na Jackson Macha walioonekana katika matukio tofauti ya video hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa alilazimika kutoa kiasi hicho cha fedha kwa Sabaya na vijana wake kwani walimtishia kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi ama kumpoteza.

“Hizo fedha nilizotoa kwa kulazimishwa ili nisifunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na walisema kwa midomo yao akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Hai kuwa nisipotoa feha hizo watanipoteza,”alidai Mrosso.

Mwananchi

Maoni yangu:
Serikali ya Awamu ya 6 ikianza kuchunguza kesi za watu waliopotea/potezwa katika Awamu ya 5 kwenye mazingira ya kutatanisha basi wasiende mbali sana, Waanze kumuhoji Sabaya, inaonesha either yeye alikuwa kwenye kundi la wapotezaji au alikuwa anajua nini kinafanyika.
 
Ofcoz, akikumbuka namna milioni 90 yake ilivyoporwa na kuachwa masikini, lazima ajisikie vibaya aisee...

Sijui huyu Sabaya pesa zote hizi za dhuluma alizipeleka wapi huku akiacha machozi ya familia za watu yakidondoka...

Ama kweli dhambi ni mbaya sana aisee. Ona ivyomtesa yeye na familia yake yote...

Machozi ya aliodhulumu mali na uhai wao hayataenda bure hakika...!!
 
Rest in hell mwendazake a.k.a Chatoman
 
Kaona alivyotoa 90mil kirahis rahis had kaugua
 
Ofcoz, akikumbuka namna milioni 90 yake ilivyoporwa na kuachwa masikini, lazima ajisikie vibaya aisee...

Sijui huyu Sabaya pesa zote hizi za dhuluma alizipeleka wapi huku akiacha machozi ya familia za watu yakidondoka...

Ama kweli dhambi ni mbaya sana aisee. Ona ivyomtesa yeye na familia yake yote...

Machozi ya aliodhulumu mali na uhai wao hayataenda bure hakika...!!
Sabaya ni Mzalendo wa awamu ya 5
 
Maoni yangu:
Serikali ya Awamu ya 6 ikianza kuchunguza kesi za watu waliopotea/potezwa katika Awamu ya 5 kwenye mazingira ya kutatanisha basi wasiende mbali sana, Waanze kumuhoji Sabaya, inaonesha either yeye alikuwa kwenye kundi la wapotezaji au alikuwa anajua nini kinafanyika.
Pia bila kuwasahau Kingai, Mahita, Goodluck, Jumanne na wezao
 
Je ni wangapi walipewa kesi za uhujumu uchumi (wengine ugaidi) katika awamu ya 5 kwa style hii ya Mrosso? Tukaaminishwa majukwaani kwamba ni Mafisadi, wahujumu uchumi, wakwepa kodi, makuwadi wa mabeberu n.k., kumbe hawakutimiza matakwa binafsi ya hawa majambazi na Baba yao! Ni wakati sasa serikali awamu ya 6 kuangalia kwa jicho la 3 kesi zote zilizofunguliwa awamu ya 5.
 
Well said MAN OF GOD
 
Back
Top Bottom