Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Ukiangalia ukubwa wa uchaguzi wa Kenya na hoja zilizowasilishwa kwenye Mahakama ya Kenya. Bila ya shaka utagundua kwamba mahakama ya Kenya ina utendaji kazi uliotukuka kuliko mahakama yetu Tanzania.
Kwenye mahakama ya Tanzania kuna kesi ya kina Halima Mdee na wenzake, ambayo kwa zaidi ya mwaka sasa iko mahakamani inazururishwa wala hatima yake haijulikani. Nilichojifunza inawezekana majaji wetu Tanzania hawajali weledi wa kazi yao na wala huwa hawaoni aibu kwa kuendesha kesi kwa muda mrefu bila ya sababu za msingi.
Kesi nyingi kwenye mahakama ya Tanzania huchukua muda mrefu bila ya sababu za kisheria au kufuata mfumo wa uendeshaji kesi mahakamani. Matokeo yake hata hukumu ikitolewa haina maana yoyote ile kutokana na mazingira yatakayokuwepo.