Ni vizuri kama Samia alidanganywa kwa kuwa hali ya utulivu kitaifa iko vizuri sana, Mbowe akiwa Ukonga maximum prison and remand. Serikali inapanga mipango ya kiuchumi, watalii wanakuja nchini, wawekezaji wanaleta mtaji na shughuli za uchumi zinaamka taratibu baada ya kulala kwa miaka 5.
Maandamano na mikutano ambayo Mbowe alikuwa anaianzisha Rais SSH akiwa mpya kwenye uRais inge vuruga Nchi sana.
Binafsi napongeza kazi ya vyombo vya Dola yaani TISS, POLICE nk kwa kuwa wangelegea kidogo ingekula kwa Mama yetu Samia. Na kama hamujui ndiyo kazi ya vyombo vya dola, siyo kuiibia kura CCM.
Ila nawalaani washauri wa Mbowe na hao wafadhili wao wa ulaya kwa kushindwa kumuambia Mbowe kuwa ile ilikuwa BAD TIMING. Mbowe angesubiri mpaka March 2022 Mama akiwa na mwaka ndipo amuambie kuwa "baada ya kupanga uchumi, tunataka Katiba sasa"
Mimi nami ni muumini wa Katiba Mpya, msije mkaniita MATAGA. Nenda kasome post zangu za miaka 5 iliyopita ndiyo utanijuwa.