Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake Watatu kuendelea tena tarehe 26/10/2021

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio Taarifa mpya niliyoipata kutoka kwenye ofisi moja ya Ubalozi Jijini Dar es Salaam, nilipoenda kwa masuala ya kibiashara , Kwamba Yule Mwamba wa siasa za Tanzania , Mtemi Isike , Laingwanan au Ustaadh Aboubakar Mbowe kama anavyojulikana huko Zanzibar , kesho atafikishwa kwenye Mahakama ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi katika Muendelezo wa Kesi inayomkabili .

Hata hivyo Taarifa hii imethibitishwa na Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika .

%23MboweSioGaidi.jpg

Bali kisichofahamika ni jina la Jaji mpya aliyeangushiwa Jumba bovu la kuendesha Kesi hiyo ya moto unaobabua mwili na akili.

Mungu Ibariki Chadema
 
Hakuna marefu yasiyo na mwisho!

Hili nalo litapita!!

Mungu ndiye hakimu wa kweli , kwa wenye Nia njema, kesi hii ni ya kumkabidhi Mungu, maana Mungu anasema "Vita yako ni Vita yangu"

Anayeweza kuwashughulikia CCM na mahakama zao ni Mungu pekee.
 
Majaji Tanzania wanajivika ukatuni kwenye taaluma ya heshima tangu enzi ya torati...yule aliyepewa cheo ....na kuhadaa taaluma na weledi.....Ila hata akiwa anaoga au kabla hajalala au akiwa anasali Jambo hili dhambi hii inamrudia Sana....mwili wake utapungukiwa na Kinga kwa kasi na hata umauti .....hicho cheo atakuwa nacho kwa mda si mrefu
 
Hii ndio Taarifa mpya niliyoipata kutoka kwenye ofisi moja ya Ubalozi Jijini Dar es Salaam, nilipoenda kwa masuala ya kibiashara , Kwamba Yule Mwamba wa siasa za Tanzania , Mtemi Isike , Laingwanan au Ustaadh Aboubakar Mbowe kama anavyojulikana huko Zanzibar , kesho atafikishwa kwenye Mahakama ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi katika Muendelezo wa Kesi inayomkabili .

Hata hivyo Taarifa hii imethibitishwa na Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika .

View attachment 1986530

Bali kisichofahamika ni jina la Jaji mpya aliyeangushiwa Jumba bovu la kuendesha Kesi hiyo ya moto unaobabua mwili na akili.

Mungu Ibariki Chadema

Asante kwa taarifa mkuu japo:

IMG_20211021_190628_385.jpg
 
Huyo mama asijifanye suala la kuonea watu magerezani halioni. Tunamshitakia Mungu wa mbingu na Dunia. Haiwezekani utese watu kiasi hicho
Huyo uliyemtaja yaani simwelewi kabisa, Rais unashabikia mtu kupigwa kesi ya ugaidi kwa msaada wa vyombo vya habari na kudanganya umma eti wengine wamehukumiwa tayar!

Sijui nitatokaje kwenye dhambi hii ya chuki!!?
 
Ninachelea kuijadili hii kesi nje ya mahakama.

Je, itakuwa dhambi nikisema mwelekeo wa kesi hii kwa mujibu wa hukumu ya kesi ndogo inaonesha kabisa misingi ya HAKI kusiginwa?

Sitaki kabisa kuijadili lakini nafsi inaniambia kuna jambo halipo sawa kwenye hii kesi.

Mahakama itende haki na ioneshe haki inatendeka
 
Majaji Tanzania wanajivika ukatuni kwenye taaluma ya heshima tangu enzi ya torati...yule aliyepewa cheo ....na kuhadaa taaluma na weledi.....Ila hata akiwa anaoga au kabla hajalala au akiwa anasali Jambo hili dhambi hii inamrudia Sana....mwili wake utapungukiwa na Kinga kwa kasi na hata umauti .....hicho cheo atakuwa nacho kwa mda si mrefu
Huyo mtu alipewa fursa ya kujijengea heshima, kaikataa. Kuna watu kweli kichwani haziwatoshi!

Hii kesi inaelekea ukingoni. Haiendi popote hii.
 
Nchi nyingine, Jaji ni nafasi ya heshima, lakini kwetu hapa, kuwa jaji ni sawa sawa na Polisi, msajili wa vyama vya siasa, mwenyekiti/mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi, wakurugenzi wa Wilaya. Wote, hakuna mwenye weledi, wanafanya kazi kama tarishi, wanasubiria amri ya mwenyekiti wa CCM.

Kwa sasa hizo ni nafasi, kwa kiasi kikubwa ni alama ya ibilisi. Mpaka sasa, hakuna hata mmoja aliyeonesha kwa vitendo kuwa hataki ushirika na ibilisi. Hakuna aliyeonesha kuwa anataka kuwa mtumwa wa weledi wake, kama ambavyo watu wenye akili na weledi hupenda kuwa. Hawa wa kwetu wameamua kuwa watumwa wa CCM, na CCM ina ushirika wa kudumu na inilisi. By implication, nao wameamua kuishi kwenye ndoa na ibilisi. Siku zote ibilisi, lazima mwishowe akupeleke kwenye majuto.
 
Huyo mama asijifanye suala la kuonea watu magerezani halioni. Tunamshitakia kwa Mungu wa mbingu na Dunia. Haiwezekani utese watu kiasi hicho
Huyu mama kila akizungumzia HAKI, anadhihirisha unafiki wa hali ya juu. Na kila anapolitamka hilo neno, ajue anachota laana mbele za Mungu. Mungu hana ushirika na mtu mnafiki.
 
Nchi nyingine, Jaji ni nafasi ya heshima, lakini kwetu hapa, kuwa jaji ni sawa sawa na Polisi, msajili wa vyama vya siasa, mwenyekiti/mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi, wakurugenzi wa Wilaya. Wote, hakuna mwenye weledi, wanafanya kazi kama tarishi, wanasubiria amri ya mwenyekiti wa CCM.

Kwa sasa hizo ni nafasi, kwa kiasi kikubwa ni alama ya ibilisi. Mpaka sasa, hakuna hata mmoja aliyeonesha kwa vitendo kuwa hataki ushirika na ibilisi. Hakuna aliyeonesha kuwa anataka kuwa mtumwa wa weledi wake, kama ambavyo watu wenye akili na weledi hupenda kuwa. Hawa wa kwetu wameamua kuwa watumwa wa CCM, na CCM ina ushirika wa kudumu na inilisi. By implication, nao wameamua kuishi kwenye ndoa na ibilisi. Siku zote ibilisi, lazima mwishowe akupeleke kwenye majuto.
Tatizo lilianza hasa awamu ya 5 walipoanza kuteuliwa watu kutoka nje ya mapendekezo ya tume ya utumishi wa mahakama. Ndio sababu uliona hata yule hakimu aliyewahukumu Sugu na Masonga alipendekezwa kwa mdomo kuwa jaji.
 
Back
Top Bottom