Kesi ya Uhaini: Brenda Rupia ndani ya Mahakamani kutoa ushahidi kesi ya Lissu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776

Muktasari:​

  • Shahidi wa tatu wa utetezi, Amani Golugwa, amemaliza kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu. Baada ya maswali ya dodoso kutoka upande wa mashtaka na maswali ya ufafanuzi kutoka upande wa utetezi kukamilika, kesi imeahirishwa kwa saa moja na nusu. Inatarajiwa kuendelea saa 9:30 Alasiri, ambapo shahidi wa nne wa utetezi, John Heche atapanda kizimbani.
Soma mwenendo wa Kesi >> Kesi ya Uhaini: Amani Golugwa, amemaliza kutoa ushahidi kesi ya Lissu

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia Jonas, tayari yupo ukumbi wa Mahakama ambapo atasimama Kizimbani kama Shahidi wa 4.

Mahakama imerejea muda huu Saa 9:45 Alasiri.

Sehemu ya 362

Majaji wameingia na Waandishi wa Habari walikuwa wamejaa pale mahali alipokaa shahidi Na. 4 wa Utetezi ambae ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Brenda Rupia.

Tundu Lissu ameshaingia Mahakamani.

Anasimama Ajuaye anasema wako tayari kuendelea lakini kwenye jopo lao anapungua Nasoro Katuga.

Lissu anasema yuko tayari kuendelea na Shahidi wake anaitwa Brenda Jonas Rupia.

Jaji: Unaitwa nani?
Brenda: Naitwa Brenda Jonas Rupia
Jaji: Hilo jina la mwisho ni R Sio L
Brenda: Ni R sio L
Jaji: Miaka yako ni mingapi?
Brenda: Nina Miaka 34 Tarehe 10 nitakuwa na 35.
Jaji Ndunguru: Unaishi wapi?
Brenda: Basihaya Kata ya Bunju.
Jaji Ndunguru: Kazi yako?
Brenda: Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi Chadema.
Jaji Ndunguru: Dini yako je?
Brenda: Mkristu.
Jaji Ndunguru: Utaapishwa hapo.

Mimi Brenda Rupi naapa kwamba ushahidi nitakaoutoa utakuwa wa kweli tupu. Mungu nisaidie.

Jaji Ndunguru: Utamuongoza au atajiongoza mwenyewe?
Lissu: Nitamuongoza asije akaogelea hapa. Sasa shahidi nitakuongoza na uzungumze taratibu na ujibu maswali yangu.

Swali la kwanza umesema unaishi Basihaya Kata ya Bunju iko wapi?

Brenda: Iko ndani ya jimbo la Kawe, Mkoa wa Dar es salaam.
Lissu: Hii kazi ya ukurugenzi umeianza kuanzia lini?
Brenda: 12/03/2025 nilipoteuliwa na Kamati Kuu ya Chama.
Lissu: Kabla ya hiyo Tar. 12/03 ulikuwa nani?
Brenda: Katibu wa BAWACHA Mkoa wa Kichama Kinondoni.
Lissu: Unafikiri Majaji wanajua BAWACHA ni nini?
Brenda: BAWACHA ni kifupi cha Baraza la wanawake CHADEMA.
Lissu: Hiyo nafasi ya Katibu BAWACHA kinondoni uliishikilia kwa muda gani?
Brenda: Tangu mwaka 2024.
Lissu: Kabla ya Katibu Kinondoni ulikuwa nani?
Brenda: Mwenyekiti wa Chama kata ya Mwananyamala, Jimbo la Kinondoni. Mwenyekiti BAWACHA jimbo la Kinondoni. Na Katibu wa BAWACHA Mkoa wa Kinondoni.
Lissu: Miaka ikoje?
Brenda: Kuanzia 2015 lakini exactly dates sikumbuki.
Lissu: Nje ya Chama yani achana na hizo nafasi za ndani. Wewe ni nani?
Brenda: Kitaaluma mimi nimesomea Bachelor of science in accounting katika University of Gloucestershir
Jaji Ndunguru: Hebu taja spelling tafadhali.
Lissu: Mwaka gani?
Brenda: 2009 hadi 2013
Lissu: Ulipata tuzo gani au award uliyopata baada ya kusomea
Brenda: Nilipata certificate ya Bachelor degree of science in accounting.
Lissu: Kisomo kingine chochote kama unacho kama unacho?
Brenda: Ni hiyo tu.
Lissu: Uzoefu wako wa kazi za kitaaluma nje ya kazi za kisiasa ulizofanya?
Brenda: Baada ya kuhitimu chuo nilifanya kazi ya accounting kwa mwaka mmoja na baada ya hapo nilianza kufanya biashara.
Lissu: Hiyo kazi gani na wapi na mwaka gani?
Brenda: Niliajiriwa Tazi Cars inajishughulisha na kuuza magari kama Accountant na baada ya hapo nikaacha kufanya kazi kariakoo za biashara binafsi.
Lissu: Toka lini mpaka lini? Ulifanya kazi
Brenda: Nilianza kufanya kazi mwaka 2013 hadi 2014 kuelekea 2015 ambapo niliacha baada ya mwaka mmoja na baada ya hapo nikaanza kuuza Human hair kama mjasiliamali wa kuuza urembo na baadae electronics.
Lissu: Ukisema urembo una maana gani?
Brenda: Vifaa vya urembo
Lissu: Tuzungumzie kesi ambayo unaitolea ushahidi. Waeleze Majaji kuhusu ufahamu wako kuhusu Mkutano wa Tar. 03/04
Brenda: Chama kilialika watia nia makao makuu ya Chama Mikocheni kuja kuzungumzia kuhusiana na msimamo wa No Reforms: No Election.
Lissu: Hao watia nia ni watu gani?
Brenda: Ni wale wanachama waliokuwa na nia ya kugombea uchaguzi wa mwaka 2025.
Lissu: Mlizungumzia mambo gani?
Brenda: No Reforms No Election ni msimamo wa Chama ulioelezea kuwa yanahitajika mabadiliko ya Sheria za Kiuchaguzi
Lissu: Huo mkutano aliuandaa nani?
Brenda: Sekretarieti ya Chama chini ya Katibu Mkuu John Mnyika.

Nimeipangilia vizuri bila kubadilisha maneno au maudhui ya ushahidi, na nimeacha maoni yako kama yalivyo:

Part 363​

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake No. 4, Brenda Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA HQ.

Mhe. Lissu: Sekretarieti ni nini?

Brenda: Chombo cha utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Chama.

Mhe. Lissu: Hiki chombo cha Sekretarieti kinajumuisha wajumbe gani?

Brenda: Katibu Mkuu wa Chama, Manaibu wawili, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Brenda Rupia, Mambo ya Nje, John Kitoka, Mkurugenzi wa Fedha, Titho Kitalika, Mkurugenzi wa Organizesheni na Uchaguzi, John Pambalu, Mtaalamu wa Rasilimali, Lenard Magere, Makatibu wa Mabaraza ambayo kwa Wazee ni Hellen Kayanza, Kwa Wanawake Pamela Massey na BAVICHA ni Dua Lyamzito.

Mhe. Lissu: Mwingine hayupo?

Brenda: Mkurugenzi wa Sheria, Gaston Garubindi.

Mhe. Lissu: Tarehe ya kikao kinaamua ilikuwa lini?

Brenda: Vikao huwa vinafanyika kila siku yani.

Mhe. Lissu: Vikao viliamua nini?

Brenda: Tualike watia nia na pia umma ufahamu kuwa tutakuwa na kikao na watia nia.

Mhe. Lissu: Nini kiliendelea baada ya hapo?

Brenda: Mkurugenzi aliandika taarifa kwa umma na watia nia tar. 27/03 kwamba tutakuwa na mkutano na wanahabari. Niliandika mwenyewe na kuweka kwenye ukurasa wa Chama wa mitandao ya kijamii na kuwapatia pia waandishi wa habari.

Mhe. Lissu: Naomba urudie hicho ulichokisema?

Brenda: Niliandika Barua na kuiweka kwenye kurasa za mitandao na baada ya hapo nilialika vyombo vya habari kuhusu mkutano huo.

Mhe. Lissu: Unasemaje kuhusu mimi ndio niliyealika vyombo vya habari?

Brenda: Sio kweli Mh. Tundu sio aliyealika vyombo vya habari na sio yeye aliyeandaa Mkutano.

Mhe. Lissu: Mnapowaalika waandishi wa habari kuna maelekezo yoyote ya ziada?

Brenda: Tumewaalika waje wafanye coverage ya mkutano kati ya watia nia na Chama?

Mhe. Lissu: Au niulize kwa Kiingereza, were there any instructions to journalist on how to perfom their duties before the meeting?

Brenda: Honourable Judges there were no any instructions to journalist whatsoever from any one of us on how they should perfom their duties in that particular meeting or any other meeting conducted by Chadema.

Mhe. Lissu: Watu gani walihudhuria mkutano huo?

Brenda: Watia nia wote, wajumbe wa sekretarieti, pamoja na viongozi wakuu wa Chama.

Mhe. Lissu: Una assume majaji wanawafahamu hao viongozi wakuu?

Brenda: Manaibu Katibu wakuu wawili Amani Golugwa, Ally Ibrahim, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Mzee, Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche, Mwenyekiti Tundu Lissu na waandishi wa Habari.

Mhe. Lissu: Kwa unavyokumbuka roughly ulikuwa na watu wangapi?

Brenda: Roughly watu 250.

Mhe. Lissu: Waandishi gani walikuja?

Brenda: Chanzo TV, Mwanzo TV, Jambo TV, ITV, na vingine vya online. Mwananchi pia walikuwepo.

Mhe. Lissu: Walikujaje hawa waandishi?

Brenda: Walikuja na camera na wengine ni pen and paper.

Maoni: Huyu Brenda ana kauzungu fulani. Anakichezea sana Kingereza wakati watu wanakitumia kukifanyia mambo ya msingi. 😂😂 Yeye Kiswahili ndio kinamsumbua sana.

Mhe. Lissu: Upo ushahidi wanasema kuna matangazo yalirushwa live?

Brenda: Ni ngumu kusema moja kwa moja kuna ambao wanarekodi na kurusha matangazo.

Mhe. Lissu: Utaratibu wa kufanya kazi yao ni upi?

Brenda: Walikuwepo pale na camera zao na wanachukua matangazo hayo siwezi kusema walikuwa live.

Mhe. Lissu: Mimi nilifanya nini haswa siku hiyo?

Brenda: Mwenyekiti alikuwa mzungumzaji mwalikwa kwenye mkutano huo ambaye ulitoa hotuba kama Mwenyekiti kuhusiana na No Reforms No Election.

Mhe. Lissu: Nani alikuwa mzungumzaji mkuu?

Brenda: Mwenyekiti alikuwa Mzungumzaji Mkuu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kitu kingine chochote ulichokiona Mwenyekiti alikifanya?

Brenda: Sikuona jukumu lingine lolote ambalo Mwenyekiti amelifanya.

Part 364​

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake, Brenda Rupia.

Mhe. Lissu: Shitaka linasema mimi ndiye niliyerusha hayo mashitaka specifically kule Jambo TV?

Brenda: Hayo sio mashitaka ya kweli, ni uongo. Sio aliyerusha matangazo na sio mfanyakazi wa Jambo TV na sio majukumu yake. Kwanza alikuwa hafahamu kama Jambo TV watakuja.

Anasimama Ajuaye Zengeli anasema, naona muda kama umeisha. Naomba tuahirishe, sasa hivi ni saa 11 na dakika kadhaa. Ilivyofika saa 11 na dakika 2 ndio ameanza.

Jaji Ndunguru: Nafikiri shahidi anaweza kumalizia leo tuendelee, si ndio Mshitakiwa?

Mhe. Lissu: Nitadanganya kama nitatumia nusu saa. Ila hautakuwa mrefu.

Mhe. Lissu: Sasa sema nani mmiliki wa hizo content zinazochukuliwa?

Brenda: Ni mmiliki wa chombo husika ndiye anakuwa mmiliki wa content zinazokuwa generated.

Mhe. Lissu: Specifically kuhusiana na content iliyokuwa generated na Jambo TV, ni nani aliyekuwa mmiliki wa hayo matangazo ya Jambo TV?

Brenda: Jambo TV wenyewe ndio walikuwa wamiliki wa content husika, kwahiyo Mkurugenzi wa Jambo TV ndiye mmiliki wa yote waliyoyachukua siku hiyo.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji, kwa vile nimeambiwa time imeshapita saa 11, naomba basi tuahirishe ili tuweze kuendelea.

Jaji: Au na wewe umechoka?

Mhe. Lissu: Sehemu nyingine tutaendelea kesho. Anatabasamu.

Majaji wanateta pale juu.

Jaji Ndunguru: Sasa mtakumbuka leo ilikuwa ni mwisho wa hii kesi. Zimeongezwa siku 14 kuanzia leo ili tuweze kukamilisha hii kesi. Mambo mengine yasiyohusu kesi hii naomba mjitahidi mtafute pa kwenda kuyazungumzia.

Mhe. Lissu: Mimi sina shida, labda wenzetu hawa.

Jaji Ndunguru: Kesi imeahirishwa hadi saa tatu kamili. Tuwahi kesho mapema.
 
Majitu ya ovyo yanayobambikiza watu kesi za mchongo utayajua tu.
 
Back
Top Bottom