Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: John Heche ameanza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shahidi wa nne ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, Septemba 9, 2026 amekamilisha sehemu zote za utetezi wake.

1788957352500.png

​
Mapema leo baada kesi kuanza mawakili wa Serikali waliendelea na maswali ya dodoso ambapo baada ya mawakili hao kutamatisha, mshtakiwa alipewa ruhusa na majaji kuanza kuuliza maswali ya ufafanuzi ambayo hayakuchukua muda mrefu.

Fuatilia mwenendo wa Kesi >>>Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda kundelea kutoa ushahidi Mahakamani

Baada ya hatua hiyo, majaji wameahirisha shauri hilo kwa muda wa saa moja na nusu hadi saa nane na nusu mchana huu, ambapo shahidi wa tano upande wa utetezi John Heche, atapandishwa kizimbani kwaajili ya kuanza kumtetea Lissu.

Katika video hii yupo Wakili Peter Madereka ndani ya ukumbi wa Mahakama naye akifuatilia mwenendo wa Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Mahakama imerejea muda huu, saa nane na dakika arobaini na tano, na John Heche amepanda Kizimbani kwa ajili ya kutoa ushahidi wake dhidi ya Kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu.

1788956071162.png

Updates kutoka Mahakamani kuhusu mwenendo wa Kesi ya Uhaini

Sehemu ya 382

Shahidi wa 5 wa Lissu katika kesi ya Uhaini kwa Upande wa Utetezi ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA upande wa Bara anaitwa John Wegesa Heche.

Ajuaye, Wakili wa Serikali amesimama na kusema jopo letu liko vilevile na tuko tayari kuendelea

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa unasemaje?
Lissu na yeye anasema yupo tayari.

Jaji Ndunguru anasema sasa kulikuwa na uamuzi mdogo pending kuhusu mashahidi wengine wa kwako mshtakiwa, ruling iko tayari unasemaje?

Lissu anasema Waheshimiwa Majaji kama nakumbuka mlisema nianze na hawa Mashahidi kwanza then nikimaliza ndio mtatoa ruling hivyo tumalizane na shahidi huyu then mtatoa ruling.

Jaji Ndunguru ameanza kufanya consultations na majaji wenzake kama dakika 3 then anauliza Upande wa Mashtaka mnasemaje

Ajuaye: Tupo tayari kama alivyosema Lissu tuendelee na ushahidi kisha Mahakama itatoa uamuzi.

Jaji Ndunguru anasema tunakubaliana tutaendelea na huyu shahidi na jioni mwishoni tutasoma huo uamuzi kwa kifupi ili kila upande ujue status ya hao mashahidi.

Haya sasa tuendelee.

Lissu: Waheshimiwa Majaji Shahidi wangu wa tano ni John Wegesa Heche
Jaji Ndunguru: Shahidi tuambie majina yako
Heche: John Wegesa Heche
Jaji Ndunguru: Unaishi wapi?
Heche: Tarime na Mwanza
Jaji Ndunguru: Umri?
Heche: Miaka 45
Jaji Ndunguru: Dini
Heche: Mkristo, Msabato
Jaji Ndunguru: Kazi
Heche: Makamu Mwenyekiti Chadema Bara

Jaji Ndunguru tuendelee,

Lissu: Shahidi umekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMATangu lini?
Heche: Nimekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara tangu Tarehe 22 Januari 2025
Lissu: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anapatikanaje?
Heche: Waheshimiwa majaji, Makamu Mwenyekiti anapatikana kwa kuchaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa chama wa Taifa
Lissu: Makamu Mwenyekiti anatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha muda gani?
Heche: Waheshimiwa majaji Makamu Mwenyekiti anatumikia nafasi hiyo kwa miaka 5
Lissu: Waeleze Majaji nani alikiwa mtangulizi wako?
Heche: Waheshimiwa majaji kabla ya mimi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti ni Tundu Lissu ambaye sasa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
Lissu: Kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama ulikuwa na nafasi gani ya chama?
Heche: Kabla ua kuwa Makamu Mwenyekiti nilikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama
Lissu: Kamati Kuu ni chombo cha aina gani katika muundo wa Chama?
Heche: Kamati Kuu ni chombo cha Utendaji cha Baraza Kuu
Lissu: Wajumbe wa Kamati Kuu wanapatikanaje kwa ufahamu wako.

Heche: Kuna wanaoingia kwa nafasi zao ndani ya chama kwa vyeo vyao kwa mfano Makamu Mwenyekiti wa chama kwa maana ya Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu ambao mmoja anatoka Bara na mwingine Zanzibar , Wenyeviti wa Mabaraza ya chama, (Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee), Wenyeviti wa kanda za chama, kuna kanda 10 ambazo 8 ni kutoka bara na 2 kutoka Zanzibar, Wajumbe wanaochaguliwa na Baraza Kuu la Chama na Kuna Wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Lissu: Kwa ufahamu wako jumla ya wajumbe wa kamati kuu ni wangapi?
Heche: Wajumbe wa kamati kuu wako 29
Lissu: Waeleze majaji majukumu ya kamati kuu ni nini

Heche: Kusimamia secretariat ya chama Taifa ambacho ndio chombo cha utendaji wa shughuli za chama za kila siku, kufanya maamuzi ya vikao ya mambo yanayojitokeza au shughuli za utendaji mara kwa mara, kufuatilia shughuli za utendaji wa chama, kupitia mihutasari ya nyuma na kuidhinisha, kupanga vikao vya Baraza Kuu la chama, Kupitisha agenda zinazokwenda kwenye Baraza Kuu la Chama

Lissu: Waeleze Majaji umekuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama kwa muda gani?
Heche: Nimekuwa mjumbe wa Kamati Kuu tangu mwaka 2011 hadi sasa ni miaka 15.

Sehemu ya 383

Lissu: K
abla ya kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu uliwahi kushikilia nafasi gani?
Heche: Nimekuwa Katibu wa Tawi la CHADEMA Students Organisation, Tawi la St. Augustine University of Tanzania (SAUT) Mwanza kuanzia mwaka 2006 hadi 2009.

Nimekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa mwaka 2011-2014, Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti (2016-2019) ambayo ilinifanya kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu pamoja na Mwenyekiti wa BAVICHA ilinifanya kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu pia.

Kanda ya Serengeti ni Kanda yenye mikoa mitatu: Mara, Shinyanga na Simiyu

Lissu: Nje ya uongozi wa kichama waeleze majaji uzoefu wako wa uongozi nje ya uongozi wa chama

Heche: Nimekuwa Diwani wa kuchaguliwa mwaka 2008 baada ya diwani aliyekuwepo kufariki wa kata ya Tarime mjini. Nilichaguliwa nikiwa bado mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mt. Augustino Mwanza, nimekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini 2015-2020.

Lissu: Kuna nafasi zingine ndani na nje ya nchi nje ya hizo ulizozisema

Heche: Nikiwa Mwenyeki wa BAVICHA nilikuwa mjumbe wa Bodi ya International Young Democratic Union 2011-2014

Lissu: Naomba uwaeleze waheshimiwa majaji unavyonifahamu mimi , umenifahamu kwa muda gani na mimi ni mtu wa aina gani kwa unavyonifahamu mimi

Heche: Namfahamu Mwenyekiti wangu kama mtu mwadilifu, Mkweli, mzalendo anayeipenda nchi hii, msomi mzuri wa sheria, Mwanademokrasia wa kweli, mtu anayependa maendeleo ya nchi hii, mtu anayependa kushindanisha mawazo kwa hoja, mtu ambaye amekuwa mbunge na miongoni mwa wabunge bora kabisa tangu mimi sijawa mbunge na ni kiongozi jasiri ambaye haogopi kusema ukweli, kwa lugha yetu ni mpiganaji wa kweli.

Kwasisi watu tunaotokea Tarime hasa mimi nilimfahamu Mwenyekiti alipokuja Tarime kuja kumtetea aliyekuwa diwani wa kata ya Tarime mjijni kwasasa ni Marehemu Chacha Wangwe, aliyekuwa anawatetea wamiliki wa maeneo yalikuwa yanachimbwa madini baadhi yao ni Augustino Sasi.

Lissu: Kwanini Mzee Sasi, what is so special about him?

Heche: Mzee Sasi alikuwa mwenyekiti wa kijiji cha Kewanja kupitia Chama Cha Mapinduzi na alifungwa miaka 30 kwa hizi kesi za uonevu na Kunyang’anywa mali ikiwemo ardhi yake.

Baada ya kutoka gerezani Mzee Sasi alijiunga na chama chetu na akachaguliwa kuwa diwani na nimekuwa nae kwenye Baraza la Madiwani mwaka 2008 nikamkuta yeye kwenye kipindi cha pili.

Lissu: Waeleze majaji watu wengine ambao niliwatetea kwa kumbukumbu zako
Heche: Idadi kamili sikumbuki ila lilikuwa kundi kubwa sana zaidi ya 20 wakiwemo wakina Chacha Wangwe, Mzee Augustino Sasi na wengine wengi.
Lissu: Waeleze Majaji kulikuwa na kitu gani 3/4/2025
Heche: Waheshimiwa majaji kulikuwa na kikao cha watia nia, watu ambao wanataka kugombea kupitia chama chetu, tulikuwa nao makao makuu ya chama
Lissu: Lengo la huo mkutano na watia nia lilikuwa nini

Heche: Lengo la mkutano huo na watia nia lilikuwa ni kuwaeleza msimamo wa chama wa No Reforms No Election, kwahiyo lengo lilikuwa ni kuwaelimisha kwanini chama kimechukua msimamo huo kutokana na uamuzi wa chama wa tangu Desemba 2024 ambavyo vilikuwa vimetangulia.

Lissu: Waeleze Majaji hivyo ni vikao gani vilivyotangulia

Heche: Nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu hivyo nimeshairiki hivyo vikao na baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 kuvurugwa nchi nzima na wagombea wetu kuenguliwa kwa zaidi ya 80% na Wagombea wetu wengine kuenguliwa, wengine kuuwawa kama vile Manyoni na Dar es Salaam

Lissu: Nini kilitokea baada ya yote haya?

Heche: Kamati Kuu ya Chama chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe ilikaa 3/12/2024 na kujadili na kuazimia kwamba ule haukuwa uchaguzi bali ni uchafuzi na mauaji hivyo chama kiliazimia kupitia kamati kuu msimamo wa No Reforms No Election, Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi.

Sehemu ya 384 itaendelea hapa hivi punde.....
Part 384

Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza John Heche.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ni mabadiliko gani yasipofanyika hakuna uchaguzi.

Heche: Kamati Kuu iliazimia mabadiliko makubwa ya kikatiba na ya kisheria, kuondoa mamlaka makubwa ya Rais kuunda Tume ya Uchaguzi ambayo yeye anateua wajumbe, Wakurugenzi ambapo yeye ni mgombea au chama chake. Yaani kama Simba na Yanga wanacheza halafu Yanga watoe refa.

Watu wamecheka 😂😂😂😂 Makamu anaongea kwa ufasaha na utulivu wa hali ya juu.

Mhe. Lissu: Tume gani unamaanisha?

Heche: Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa huru na bila upendeleo.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uzoefu wako wewe na matatizo ya chaguzi za nchi hii.

Heche: Waheshimiwa Majaji, mimi nimegombea mara kadhaa, nimekuwa diwani na nimekuwa mbunge. Katika chaguzi za nchi hii na nimeshiriki kampeni za chama, nimeshiriki uchaguzi mdogo wa Arumeru, Busanda Geita, Igunga, Kinondoni 2018 na nimeshiriki chaguzi nikiwa mgombea wa Ubunge 2015 na 2020.

Chaguzi zote hizi ziliambatana na maumivu makubwa, mauaji ya wanachama, kuenguliwa wagombea wa CHADEMA, kunyimwa fomu za viapo vya mawakala wetu, mawakala wetu kuondolewa kwenye vituo wakati zoezi linaendelea, ratiba zetu kuingiliwa na Polisi na kuvurugwa kwa Mikutano ya kampeni, wagombea wetu kunyimwa fomu za matokeo zile zinazoonyesha umepata kura ngapi, kura za uongo kuingizwa na Polisi kubeba vibegi vya kura feki na migambo pia wanaosimamia, na wagombea wetu kuenguliwa kwa sababu za hovyo kama vile eti hawajui kusoma na kuandika.

Sasa nitaanza na sababu moja moja.

Shahidi yuko nondo sana, anajua vitu mpaka anakera.

Uchaguzi kwa mfano wa Arumeru Mashariki, aliuwawa alikuwa ni Katibu wa CHADEMA wa Kata ya Usa River, ilikuwa kati ya 2012/2013. Aliuwawa Msafiri Mbwambo kwa kuchinjwa na Chainsaw. Aliuwawa na watu wanaosadikika kuwa ni wanachama wa CCM na mpaka leo hakuna aliyekamatwa wala kufungwa kwa sababu ya mauaji hayo.

Hapa Dar es Salaam, Kinondoni mwaka 2018, aliuwawa Mwenyekiti wa Kata ya Hananasif wa CHADEMA anaitwa Daniel Yona. Vilevile hakuna uchunguzi wala mtu aliyewahi kukamatwa.

Waheshimiwa Majaji, tulipokuwa tunaenda kuchukua viapo vya mawakala Februari mwaka 2018, uchaguzi huo wa Kinondoni, tulinyimwa fomu na Mkurugenzi alikuwa anaitwa Kagurumjuli.

Tulipokuwa tunafuatilia, tulishambuliwa kwa risasi na Polisi, baadhi ya wanachama wetu kuumizwa na binti anayeitwa Akwilina Akwilini aliuwawa kwa kupigwa risasi. Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam alikuwa anaitwa Mambosasa alithibitisha kuwa aliuwawa kwa risasi.

Mhe. Lissu: Kitu gani kiliendelea?

Heche: Hakuna askari aliyekamatwa isipokuwa sisi tulishtakiwa, mimi, Freeman Mbowe, John Mnyika kipindi hicho akiwa Naibu Katibu Mkuu, Vincent Mashinji ambaye alikuwa Katibu Mkuu, Peter Msigwa alikuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Ester Bulaya alikuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Halima Mdee alikuwa Mbunge wa Kawe, Ester Matiko alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini na Salum Mwalimu alikuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji mlishtakiwa kwa kosa gani na kesi iliishia wapi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, kwenye hiyo kesi hao wote walikuwa wajumbe wa Kamati Kuu. Walishtakiwa na kufungwa na makosa yalikuwa tofauti tofauti, mwingine count 4, wengine uchochezi, mkusanyiko usiokuwa na kibali.

Mhe. Lissu: Kabla sijasahau, hiyo kadhia ilinikosakosaje mimi?

Heche: Wakati huo Tundu Lissu alikuwa ameshambuliwa sana kwa risasi, kwahiyo alikuwa anapata matibabu nje ya nchi kutokana na kushambuliwa mwaka 2017. Ila angekuwepo lazima angekuwa na sisi.

Mhe. Lissu: Uamuzi wa hiyo kesi ulikuwaje?

Heche: Uamuzi wa hiyo kesi tulifungwa kwa miezi sita au faini. Mimi nililipishwa milioni 40, wengine milioni 30, ila kwa ujumla zilikuwa zaidi ya milioni 310.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ilikuwa kwenye Mahakama gani.

Heche: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi hii ilisikilizwa na Hakimu Mashauri na baadaye alipanda cheo na kuwa Jaji.

Part 385 itaendelea kwenye post inayofuata.
Part 385

Mhe. Lissu: Baada ya kuhukumiwa, kitu gani kilifuata?

Heche: Tulikata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania na hukumu ilitupiliwa mbali na iliamuliwa turudishiwe fedha zetu, lakini mpaka sasa hatujarudishiwa. Mimi sijarudishiwa milioni 40 zangu. Naona kabisa nimedhulumika licha ya kwamba Mahakama ilisema turudishiwe pesa zetu.

Watu wamecheka sana 😂😂😂😂😂😂😂

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nani aliamua hiyo kesi Mahakama Kuu.

Heche: Jaji Mugeta.

Mhe. Lissu: Ulisema kulikuwa na mauaji ya Akwilina Akwilin, hiyo habari ya mauaji iliishia wapi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, hiyo habari iliishia hapo na hakuna askari aliyekamatwa wala kufungwa kwa hayo mauaji licha ya kwamba Mambosasa kusema kuwa ni Polisi ndio waliua.

Mhe. Lissu: Matukio mengine yapo ya mauaji wakati wa uchaguzi? Yaelezee.

Heche: Mwaka 2015 wakati nimeenda kufanya kampeni Kata ya Nyanungu, Tarime Vijijini, tulishambuliwa na akauwawa Bhoke Mwita Waitei. Alishambuliwa na wafuasi wa CCM akauwawa. Walikamatwa watu na ilikuwa mchana, baadaye wakaachiwa na baadae kesi haikuendelea.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwenye uchaguzi huohuo wa 2015 kilitokea kitu gani Jimbo la Busanda?

Heche: Kwenye uchaguzi huohuo aliuwawa mgombea wetu Alphonce Chem Mawazo, alikuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Busanda. Hata kumzika kwake ilibidi tu-contest mahakamani, maana tuliambiwa tusimuage eneo la wazi mpaka Mahakama ilipoamua kuwa tukamzike.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji Alphonce Mawazo alikuwa na cheo gani kabla ya kuwa mgombea?

Heche: Alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya wauaji wa Mawazo.

Heche: Sikumbuki vizuri mwisho wake.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nini kilitokea kwenye uchaguzi wa Tarime jimboni kwako mwaka 2020?

Heche: Wakati nafunga kampeni kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020, Nyamongo Kata ya Matongo, tulivamiwa na kushambuliwa kwa risasi, wakauwawa watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa. Aliuwawa Chacha Isangora na Chacha Ngabya.

Wote waliowashambulia hawa mabwana ni watu wanaofahamika. Walikamatwa na maganda ya risasi yalikutwa pale. Ni viongozi wa CCM, mwingine alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji. Maganda ya risasi yalichukuliwa na Polisi, walikamatwa na baadaye wakaachiwa. Familia zimebaki na wajane kwa sababu ya mauaji yanayotokana na uchaguzi.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji iwapo kuna tukio jingine la mauaji kwenye Jimbo la Tarime.

Heche: Waheshimiwa Majaji, Polisi walimuua mdogo wangu, Suguta Heche.

Alikamatwa na Polisi eneo la Sirari, Wilaya ya Tarime mwaka 2018, akafungwa pingu mikono kwa nyuma, akachomwa singe na walifanya attempt ya kwenda kumtupa. Walinzi wa eneo hilo, ambapo walitaka kumtupa, waliwaona, hivyo walirudi naye kituo cha Polisi.

RPC wa wakati huo alitoa taarifa kwa umma kuwa ameuwawa na Polisi na akaahidi kuwa huyo aliyeua, ambaye ni askari Polisi, kuwa atashughulikiwa. Lakini baadaye askari huyo aliachiwa na kuhamishwa kituo cha kazi.

Mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.

Mimi naamini mauaji yale yalifanywa kwa sababu ya kunikomoa, kukomoa familia yangu, msimamo wangu wa kuwa CHADEMA, na hata kesi hiyo ilishughulikiwa kama njia ya kunikomoa kwamba tuna uwezo wa kukufanyia chochote na hatua zozote zisichukuliwe.

Hapa Heche ameongea kwa uchungu sana.

Part 386​

Mhe. Lissu:
Waeleze Majaji, kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 nilipokuja kwenye kampeni za Urais, kwenye mkutano wa Nyamongo, Tarime, kitu gani kilitokea?

Heche: Tundu Lissu alikuwa Mgombea Urais mwaka 2020. Mkutano wa kwanza ulikuwa Kata ya Sirari na Tarime Mjini. Kesho yake tulipanga kufanya mkutano Kata ya Nyamongo, eneo linaitwa Matongo.

Tulipofika kwenye junction ya kwenda Matongo, eneo linaitwa Kiwanja cha Polisi, walituzuia kuingia Matongo kwa mabomu ya machozi. Ikasababisha fujo kubwa sana za raia, watu walijeruhiwa, vyombo vya usafiri viliharibiwa kwa risasi na mabomu ya machozi, watu waliumizwa. Lengo lilikuwa kutawanya watu wasije kutusikiliza.

Baada ya hapo wakaacha, mkutano uliendelea, ila waliamini kuwa watu wametishika na hawatatusikiliza. Bahati nzuri ilikuwa Tarime, sio rahisi watu kutawanyika kwa vitisho vya mabomu na maji ya kuwasha.

Wakati Mgombea wetu wa Urais anafanyiwa hivi, mgombea wa CCM, si Magufuli au Samia wa sasa, amewahi kufanyiwa hivi kwenye mikutano ya kampeni?

Mhe. Lissu:
Waeleze Majaji, siku ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Jimbo la Rorya kilitokea kitu gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, siku ya Uchaguzi Mkuu 2020, Jimbo la Rorya, ambapo Ezekia Dibogo Wenje alikuwa anagombea Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, walivamiwa na Polisi nyumbani kwao Shirati.

Polisi walishambulia ndugu yake Wenje, anaitwa Nyatega Wenje, aliuwawa kwa mashambulio hayo.

Huyu Nyatega Wenje alikuwa ni ndugu yake na Ezekia Wenje.

Mhe. Lissu: Ezekia Wenje, mgombea, yeye kitu gani kilimtokea?

Heche: Waheshimiwa Majaji, katika hilo tukio Ezekia Wenje alinusurika kuuawa, akakimbilia Kenya na baadaye uhamishoni Canada.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji juu ya hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya Nyatega Wenje.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu juu ya hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya wauaji wa Nyatega Wenje.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji, nimemaliza ya leo. Naomba tuahirishe hadi kesho.

Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka mnasemaje?

Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, hatuna pingamizi.

Jaji Ndunguru: Kwa kuwa muda umeenda, shauri linaahirishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi.

Inapigwa: “High Cooouuuurrrrt!”

Majaji wanatoka.

Tuonane kesho, muwe na jioni njema.

Via:
Hilda Newton
 
Huyu ataharibu. Naona ana hasira sana. Atapanik afu atakosa point.
 
  • Kicheko
Reactions: ---
Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Shahidi ambae anafuata ni John Heche
msaga sumu mkuu right?

Je, atamkaanga chairman wake kama walivyofanya viongozi wengine wa chadema taifa kizimbani?🐒
 
Uache kuwa unaanzisha mada wakati hauna updates na kama wewe ni Mfanyakazi wa JF basi lete updates sio kuamzisha tu mada alafu hauna content
 
msaga sumu mkuu right?

Je, atamkaanga chairman wake kama walivyofanya viongozi wengine wa chadema taifa kizimbani?🐒

Mashahidi aiseeee wamempa shida sana kabuga. Serikali inabidi tujipange na tutafute maswali ya maana. Sababu haya ya kwetu yanawapa uhuru wanaelezea mambo ambayo hatukutaka kabisa yawe wazi. Ni kama walitaka ifikie hatua waongee haya. Mpaka najiuliza Serikali kweli haikuwa na watu wenye akili na uelewa mzuri
 
heche ndio funika bovu,
atahakikisha chairman wake hachomoki alikojichomeka ili apige ufisadi kwa uhuru zaidi pale chadema.

we utaona 🐒
 
Shahidi wa nne ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, Septemba 9, 2026 amekamilisha sehemu zote za utetezi wake.

Mapema leo baada kesi kuanza mawakili wa Serikali waliendelea na maswali ya dodoso ambapo baada ya mawakili hao kutamatisha, mshtakiwa alipewa ruhusa na majaji kuanza kuuliza maswali ya ufafanuzi ambayo hayakuchukua muda mrefu.

Fuatilia mwenendo wa Kesi >>>Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda kundelea kutoa ushahidi Mahakamani

Baada ya hatua hiyo, majaji wameahirisha shauri hilo kwa muda wa saa moja na nusu hadi saa nane na nusu mchana huu, ambapo shahidi wa tano upande wa utetezi John Heche, atapandishwa kizimbani kwaajili ya kuanza kumtetea Lissu.
Asante sana mkuu kwa kutuletea habari motomoto. Naomba uendelee kutuletea updates kadri unavyozipata. Ubarikiwe sana mkuu.
 
MiCCM ni mijitu ya kichoko na kiquma sana.
 
Back
Top Bottom