GE2025 Kesi ya uhaini ya Lissu kusikilizwa Mahakama Kuu, Septemba 8, 2025

GE2025 Kesi ya uhaini ya Lissu kusikilizwa Mahakama Kuu, Septemba 8, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chma cha Demorasia na Maendeleo (CHADEMA)Taifa, Tundu Lissu, imepangwa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Septemba 8, 2025 katika hatua ya kusoma hoja za awali.

IMG_6063.jpeg

Taarifa hiyo, iliyotolewa na Wakili Gaston Shundo Garubindi, Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, na kuwekwa pia kwenye ukurasa wa X na Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, imeeleza kuwa maandalizi ya awali ya shauri hilo yamekamilika.

Ikumbukwe Agosti 18, 2025, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilibainisha kuwa kesi hiyo inakwenda Mahakama Kuu baada ya hatua za kisheria kukamilika.
1756882004995.jpeg
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa kwa wanachama, wafuasi wake na kwa wananchi wote kuwa Septemba 08, 2025 Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam itaanza kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu.

Awali kupitia mfumo wa mashauri ya Mahakama, kesi hii ilionesha kupangiwa Septemba 12, 2025 lakini kwa mujibu wa Mahakama (summons) alioupokea Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, usikilizwaji wa kesi sasa rasmi utaanza Septemba 08, 2025.

"CHADEMA tunaona wazi kuwa kesi hii haina sura ya kawaida ya jinai bali ni mwendelezo w mipango ya kisiasa ya Serikali ya Rais Samia Suluhu dhidi ya Mwenyekiti Lissu na chama chetu kwa lengo la kukandamiza haki za msingi za wananchi" - Taarifa ya CHADEMA

CHADEMA kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Brenda Rupia ametoa wito kwa wananchi wote, wananchama, wanaharakati, vijana, wanawake, wazee, pamoja na jamii ya kimataifa kufuatilia kwa karibu na kufika Mahakamani kwa wingi siku hiyo.


CHADEMA.jpg
 
Samia hawezi siasa za ushindani . Hana lolote alijualo kuhusu TANZANIA
 
Back
Top Bottom