GE2025 Kesi ya Uhaini ya Lissu yaahirishwa tena Mahakama ya Kisutu, hadi Julai 30, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wakuu!

Mwenyekiti CHADEMA Taifa Tundu Lissu kufikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu.

Kumbuka kwamba kwenye kesi hii Tundu Lissu anajitetea mwenyewe.

Je, leo mwamba anaachiwa au atarudishwa tena 'kukamilisha na kumalizia kabisa kabisa kabisaaaa upelelezi?'

Wacha tuone kitakachojiri!

Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu kutajwa tena leo Julai 15, uamuzi wa DPP kungojewa

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Antiphas Lissu inaendelea leo Julai 15, 2025 ikiwa ni siku 14 tokea iliposikilizwa mara ya mwisho, ambapo unangojewa uamuzi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na jalada ambalo ilielezwa kuwa lipo mezani kwake.

Ikumbukwe kuahirishwa kwa kesi hiyo inayotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi KIsutu, kulifikiwa baada ya Mahakama hiyo kukubali maombi ya upande wa Jamhuri ulioeleza kuwa mpaka tarehe hiyo Julai 1, 2025, bado DPP alikuwa ajafanya uamuzi wa jalada la kesi ambalo lipo mezani kwake.

Awali, kabla ya kutolewa uamuzi huo na mahakama, Tundu Lissu wakati akijitetea aliiomba Mahakama kuagiza upande wa Jamhuri kulipeleka shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania haraka kama wamekamilisha ushahidi au Mwendesha Mashtaka aonyeshe nia ya kutoendelea na shauri lake, hivyo amuachie huru (nolle prosequi). Ikumbukwe Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu inafungwa mikono kisheria kusikiliza kesi hiyo.

===

Ulinzi umeimarishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (SUGU),Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman tayari wamefika hapa Kisutu kufuatilia kesi ya uhaini inayomhusu Mwenyekiti wa chama chao Tundu Lissu.

Tayari Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche awasili katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.

Mabalozi na wawakilishi wa balozi mbalimbali nchini wakiwa katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama, Tundu Lissu.

Wakili wa Serikali Mkuu, wakati wa Usikilizaji wa kesi ya uhaini Na. 8607/2025 dhidi ya Tundu Lissu.

"Tarehe iliyopita tuliiambia Mahakama yako kwamba shauri hili lipo hatua ya kusomwa na kutolewa maamuzi. Upelelezi wake umekamilika kwa utimilifu wake na baada ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yaani Ofisi ya DPP kusoma jalada hili, umejiridhidha ushahidi uliopo unajitosheleza kwenda kupeleka kesi Mahakama Kuu".

Tundu Lissu apinga Kesi kuahirishwa tena

''Leo ni siku ya 97 niko Mahabusu na wafungwa waliohukumiwa Kifo nimechoka na hizi habari''

"Mkurugenzi wa Mashtaka tayari alishasoma jalada, kwa mujibu wa sheria lilipaswa kuwa mahakamani na ielezwe kuwa taarifa imeshapelekwa Mahakama Kuu – si vinginevyo,"

"Hii hali si ya kufurahisha. Nimekaa mahabusu kwa muda mrefu, niko karibu na wafungwa wa kunyongwa hadi kufa, halafu bado DPP hana uamuzi kama aendelee na kesi au la?"

"Mahakama zisiruhusu kufanya kazi zake kwa kuendeshwa na waendesha mashtaka, hatujatekeleza kukamilisha ushahidi ahirisha, unaahirisha! Eeeh! unaahirisha. Mheshimiwa unaahirisha tangu tarehe 10"

"Watu wa taifa hili wanajua, na ulimwengu unajua, hakuna kesi hapa bali ni Siasa. Ni mwaka wa uchaguzi, na mwaka wa uchaguzi kiongozi mkuu wa chama cha upinzani amekamatwa, amepewa kesi ya uhaini — si kwa sababu ni mhaini, bali kwa sababu ya Siasa, ili watu waende kwenye uchaguzi wasisumbuliwe na 'No Reforms, No Election'."

"Nchi yetu imechafuka kwasbababu ya Kesi hii"

"Mheshimiwa umeambiwa kwamba naomba huruma ya Mahakama. Mimi siombi huruma ya Mahakama. Siombi, sijaomba na sitaomba. Ninachotaka, utaratibu wa Mahakama usichezewe. Mawakili wa Serikali na DPP wanachezea utaratibu wa Mahakama. Mimi siyo aina ya watu ambao wataomba huruma ya Mahakama, kwa sababu nasimamia ninachoamini kuwa ni kweli. Wanaomba huruma ya Mahakama ni wenye hatia."

Kesi ya Uhaini ya Lissu yaahirishwa tena Mahakama ya Kisutu, hadi Julai 30, 2025

eti amechoka kukaa mahabusu,

mbona hachoki kuropoka?🐒
 
Ulishtakiwa kwa kosa la uhaini au uchochezi dhidi ya kijiji gani hicho ndugu yangu, pole sana.
Tarafa nzima... sasa nawashangaa mnaosema kua Lissu ni mtu wa kwanza kujitetea mwenyewe.
 
Unajua Sheria gani wewe kumzidi Lisu?. Anaongea Siasa?. mbona mpaka Leo mnajambiana tu kuleta ushahidi?. Nyinyi ndiyo mnaleta siasa. Hiyo kesi kashawapiga kitambo tu kwa wanaojua sheria.hata kufungua msingefungua
Hizi ni hisia na mihemko.. Lissu kujua sheria anajua kwakua ndiyo kazi yake ila uwezi kusema anajua sheria kuliko watu wote.. umesikia Mzee wa MIGA..Hivi bado mnalishitaki Taifa huko MIGA.
 
Mkuu Yule MTU Sheria anaijua vema sana na kama kweli ingeenda kisheria inavyotakiwa basi ingekuwa imeisha siku nyingi tu.
Anajua sheria alafu leo yupo behind bars? Ebu kuweni serious bhana..Lissu anaongea harakati za kisiasa mahakamani nasio sheria mkuu. Nyie mnamvimbisha tu kichwa mwenzenu huku akiendelea kukaa mahabusu.
 
Hizi ni hisia na mihemko.. Lissu kujua sheria anajua kwakua ndiyo kazi yake ila uwezi kusema anajua sheria kuliko watu wote.. umesikia Mzee wa MIGA..Hivi bado mnalishitaki Taifa huko MIGA.
Mihemko unayo wewe uliyesema anaongea Siasa. Ndiyo maana nikakuuliza unajua Sheria kumzidi Lisu?. Kuhusi miga mngefanikiwa msingempiga risasi dodoma. Madini bado anachimba yule yule barrick. Asilimia ni Ile Ile tu alichookoa magu ni Ile pesa ya mtu Kati. Asilimia 16 ambapo serikali ilikua inapata asilimia 3 na 13 wajanja walikua wanaila ndani ya ccm hiyo hiyo.
Mngemnyang'anya barrick ndiyo angeenda miga. Au ujui Kama barrick anaendelea kuchimba north Mara bulyihuru na anamazinzia masanzo bugwagi?.
 
Mkuu, mbona anataja hadi vifungu vya sheria?
Unamsikiliza kwa umakini lakini.. Maelezo yake mengi niya kisiasa.Itoshe Lissu kwa yaliyomkuta miaka michache iliyopita kuna mambo ambayo yameathiri sana. Lissu kwasasa anaona he has nothing to loose. Anaweza ata kuropoka jambo lolote because anajua yeye alishajaribu kuonja umauti. TAIFA NA SERIKALI INABIDI KUA MAKINI NAE SANA
 
Mihemko unayo wewe uliyesema anaongea Siasa. Ndiyo maana nikakuuliza unajua Sheria kumzidi Lisu?. Kuhusi miga mngefanikiwa msingempiga risasi dodoma. Madini bado anachimba yule yule barrick. Asilimia ni Ile Ile tu alichookoa magu ni Ile pesa ya mtu Kati. Asilimia 16 ambapo serikali ilikua inapata asilimia 3 na 13 wajanja walikua wanaila ndani ya ccm hiyo hiyo.
Mngemnyang'anya barrick ndiyo angeenda miga. Au ujui Kama barrick anaendelea kuchimba north Mara bulyihuru na anamazinzia masanzo bugwagi?.
Ndiyo najua sheria za biashara na uwekezaji wa kimataifa kuliko Lissu. Hivi wakati kamanda anasema atawashauri wawekezaji watushitaki alikua na malengo yapi? Mwisho hakuna mtu ambae anapenda Lissu akae gerezani ila LISSU INABIDI AJUE KUA ILI TAIFA NI KUBWA KULIKO YEYE.
 
Kama wanamnyonga si wamnyonge tu ieleweke. Wanambana halafu karibia na uchaguzi huko DPP anaibuka eti hataki kuendelea na kesi. Wana bahati maana angewapelekea moto mpaka mama mwenye macho ya kungu angeomba poo.
 
Wakuu!

Mwenyekiti CHADEMA Taifa Tundu Lissu kufikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu.

Kumbuka kwamba kwenye kesi hii Tundu Lissu anajitetea mwenyewe.

Je, leo mwamba anaachiwa au atarudishwa tena 'kukamilisha na kumalizia kabisa kabisa kabisaaaa upelelezi?'

Wacha tuone kitakachojiri!

Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu kutajwa tena leo Julai 15, uamuzi wa DPP kungojewa

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Antiphas Lissu inaendelea leo Julai 15, 2025 ikiwa ni siku 14 tokea iliposikilizwa mara ya mwisho, ambapo unangojewa uamuzi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na jalada ambalo ilielezwa kuwa lipo mezani kwake.

Ikumbukwe kuahirishwa kwa kesi hiyo inayotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi KIsutu, kulifikiwa baada ya Mahakama hiyo kukubali maombi ya upande wa Jamhuri ulioeleza kuwa mpaka tarehe hiyo Julai 1, 2025, bado DPP alikuwa ajafanya uamuzi wa jalada la kesi ambalo lipo mezani kwake.

Awali, kabla ya kutolewa uamuzi huo na mahakama, Tundu Lissu wakati akijitetea aliiomba Mahakama kuagiza upande wa Jamhuri kulipeleka shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania haraka kama wamekamilisha ushahidi au Mwendesha Mashtaka aonyeshe nia ya kutoendelea na shauri lake, hivyo amuachie huru (nolle prosequi). Ikumbukwe Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu inafungwa mikono kisheria kusikiliza kesi hiyo.

===

Ulinzi umeimarishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (SUGU),Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman tayari wamefika hapa Kisutu kufuatilia kesi ya uhaini inayomhusu Mwenyekiti wa chama chao Tundu Lissu.

Tayari Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche awasili katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.

Mabalozi na wawakilishi wa balozi mbalimbali nchini wakiwa katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama, Tundu Lissu.

Wakili wa Serikali Mkuu, wakati wa Usikilizaji wa kesi ya uhaini Na. 8607/2025 dhidi ya Tundu Lissu.

"Tarehe iliyopita tuliiambia Mahakama yako kwamba shauri hili lipo hatua ya kusomwa na kutolewa maamuzi. Upelelezi wake umekamilika kwa utimilifu wake na baada ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yaani Ofisi ya DPP kusoma jalada hili, umejiridhidha ushahidi uliopo unajitosheleza kwenda kupeleka kesi Mahakama Kuu".

Tundu Lissu apinga Kesi kuahirishwa tena

''Leo ni siku ya 97 niko Mahabusu na wafungwa waliohukumiwa Kifo nimechoka na hizi habari''

"Mkurugenzi wa Mashtaka tayari alishasoma jalada, kwa mujibu wa sheria lilipaswa kuwa mahakamani na ielezwe kuwa taarifa imeshapelekwa Mahakama Kuu – si vinginevyo,"

"Hii hali si ya kufurahisha. Nimekaa mahabusu kwa muda mrefu, niko karibu na wafungwa wa kunyongwa hadi kufa, halafu bado DPP hana uamuzi kama aendelee na kesi au la?"

"Mahakama zisiruhusu kufanya kazi zake kwa kuendeshwa na waendesha mashtaka, hatujatekeleza kukamilisha ushahidi ahirisha, unaahirisha! Eeeh! unaahirisha. Mheshimiwa unaahirisha tangu tarehe 10"

"Watu wa taifa hili wanajua, na ulimwengu unajua, hakuna kesi hapa bali ni Siasa. Ni mwaka wa uchaguzi, na mwaka wa uchaguzi kiongozi mkuu wa chama cha upinzani amekamatwa, amepewa kesi ya uhaini — si kwa sababu ni mhaini, bali kwa sababu ya Siasa, ili watu waende kwenye uchaguzi wasisumbuliwe na 'No Reforms, No Election'."

"Nchi yetu imechafuka kwasbababu ya Kesi hii"

"Mheshimiwa umeambiwa kwamba naomba huruma ya Mahakama. Mimi siombi huruma ya Mahakama. Siombi, sijaomba na sitaomba. Ninachotaka, utaratibu wa Mahakama usichezewe. Mawakili wa Serikali na DPP wanachezea utaratibu wa Mahakama. Mimi siyo aina ya watu ambao wataomba huruma ya Mahakama, kwa sababu nasimamia ninachoamini kuwa ni kweli. Wanaomba huruma ya Mahakama ni wenye hatia."

Kesi ya Uhaini ya Lissu yaahirishwa tena Mahakama ya Kisutu, hadi Julai 30, 2025

Inajulikana wazi, watamchelewesha mpaka wakishateuana (October) sio uchaguzi. Watamuachia.
 
Ndiyo najua sheria za biashara na uwekezaji wa kimataifa kuliko Lissu. Hivi wakati kamanda anasema atawashauri wawekezaji watushitaki alikua na malengo yapi? Mwisho hakuna mtu ambae anapenda Lissu akae gerezani ila LISSU INABIDI AJUE KUA ILI TAIFA NI KUBWA KULIKO YEYE.
Akusema atawashauri acha kuwa muongo kila mtu amemsikiliza Lisu akiwa bungeni kuhusu miga. Kwanini unakuwa muongo ili iweje?. Alisema Kama tunataka kuwatoa kwanza tujitoe miga tusiwe mwanachama wa miga ili wasitushitaki miga. Ila tusipokitia miga watatushitaki. Sasa unasema uongo ili iweje?.
Hata Kama umpendi Lisu acha kumnenea uongo.
Wewe ndiyo tunatakiwa kujua kuwa HAKI NI KUWA KULIKO TAIFA. Sababu hata MUNGU ANASEMA kwa HAKI ATAYAHUKUMU MATAIFA
 
In fact,
kwasabb ya uropokaji, ubishi na maneno mengi yasioyohusiana na kesi mahususi,

muungwana ataeleza madai mengine kabisa na kupoteza muda wa mahakama na kisha atarudishwa korokoroni kama kawaida hadi wakati mwingine 🐒
Wewe na waliokutuma wote ni wapumbavu.
 
Akusema atawashauri acha kuwa muongo kila mtu amemsikiliza Lisu akiwa bungeni kuhusu miga. Kwanini unakuwa muongo ili iweje?. Alisema Kama tunataka kuwatoa kwanza tujitoe miga tusiwe mwanachama wa miga ili wasitushitaki miga. Ila tusipokitia miga watatushitaki. Sasa unasema uongo ili iweje?.
Hata Kama umpendi Lisu acha kumnenea uongo.
Wewe ndiyo tunatakiwa kujua kuwa HAKI NI KUWA KULIKO TAIFA. Sababu hata MUNGU ANASEMA kwa HAKI ATAYAHUKUMU MATAIFA
Haki bila wajibu ni utumwa
 
Alaaniwe laana zote bi Mashavu na yale yule wa zamani kwake yawe madogo.
Ameen
 
Back
Top Bottom