Kesi ya Yanga vs Morisson kusikilizwa

Kesi waliyopeleka yanga ni dhidi ya morrison.
Hivyo wakishinda hiyo kuwa ni mchezaji wao itawabidi kurudi TFF kuishtaki simba kuwa imechezesha mchezaji wao.
Sidhani kama kesi iliyopo kule ni simba kuchezesha mchezaji wa yanga.
Mbona unarudi nyuma mkuu? Yanga wameenda cas kwasababu wameona TFF wameshinda kutatua mgogoro wao na Morrison. Ndio maana nimeuliza je hao cas kazi yao ni kusikiliza tu hawapo kwaajili ya kutoa hukumu? Kama wanatoa hukumu kwanini Yanga warudi tena kwa TFF ambao walishindwana mwanzoni?
 
Na mapungufu ya mkataba sio jambo linaloweza kufanya mkataba usiwe halali, kwa mapungufu yaliyo kuwepo mkataba ulikuwa halali kabisa, na TFF wakasahau kwamba Yanga wanaweza kwenda kwenye mamlaka ya juu zaidi
Hapo ndipo mtego ulipo. Tff walifikiri Yanga watakubali yaishe.
 
Yanga akishinda jamaa zetu itabidi hata ubingwa wauteme,hapo ndio tutaona vita hapatakalika msimbazi zitapigwa ngumi hadharani wenyewe kwa wenyewe bonge la mtifuanona sijui manara wakati huo atakua wapi
 
Hapo ndipo mtego ulipo. Tff walifikiri Yanga watakubali yaishe.
Na ndio maana Tp mazembe baada ya kuona As vita wamechezesha mchezaji ambaye bado alikuwa na mkataba timu aliyotoka, moja moja walipeleka kesi yao kule CAS, na mwisho wa siku As vita kupokwa point za mechi alizocheza yule mchezaji na kuchukuliwa Ubingwa wao kabisa
 
Naombea yasitokee haya ukitoa mechi zote alizo cheza Morrison Simba inashuka daraja
 
Naombea yasitokee haya ukitoa mechi zote alizo cheza Morrison Simba inashuka daraja
Labda kama ikionekana Morrison ndo alifanya udanganyifu huo wa kutokuwa na mkataba maana yake aliwahadaa simba ili aende bure kwa mapenzi yake, hivyo adhabu atapewa yeye ya faini na Kutojihusisha na soka kwa miaka kadhaa au Simba kulipa faini pamoja na signing fee ya Morrison kwa pamoja na hii ndo naiona inaenda kutokea
 
Hata sio kishabiki hapa.....
Mkataba wenye mapungufu means haupo valid, na kama haupo valid means mchezaji yupo huru.

Uko sahihi, mkataba wenye mapungufu unakua voidable na utakua valid endapo upande mwingine utaridhia kuendelea nao pamoja na hayo mapungufu lakini akigoma tu huo ni void tayari so huwezi ku-enforce huo mkataba.
 
AS Vita walikuwa ni sehemu ya washtakiwa, lakini kesi ya morrison si Simba wala TFF walioshtakiwa, ni kesi ya mkataba kati ya Yanga na Morrison, atakayeshindwa atalipa fidia na wala sio kufungiwa.
 
AS Vita imenyanywa ubingwa wa Congo kwa kosa gani kama una fatilia mpira, kipindi kile Mazembe aliondolewa akapewa ushindi Simba haikua champions league? Ujinga ni mzigo
Kesi ya Simba na Mazembe, Simba waliishtaki Mazembe na sio mchezaji Bukungu, na waliopewa adhabu ni Mazembe na sio Bukungu.
 
Atapokonywa na nani?
Shirikisho linalosimamia mpira lilimtangaza kuwa mchezaji huru.
Je ni kosa kumsajili mchezaji aliye huru kama ilivyothibitishwa na TFF?
Mmh unasemea hawa tff thimba
 
Unapotosha mkuu

Mchezaji anapokuwa na mgogoro haruhusiwi kuchezeshwa hadi mgogoro uamuliwe kisheria

Tulia utaona mwenyewe hukumu itakavokuwa
 
Yanga hawakubaliani na hio kauli ya TFF ndo maana wakaenda kushtaki FIFA na CAS.... Yanga wanasema bado walikuwa na mkataba na Morisson....
Yanga akishinda, Simba watakuwa na kosa la kumchezesha mchezaji ambaye alikuwa na mkataba na timu nyingine
Yes, umeliweka vema
 
Yaani hapa nimechanganyikiwa! kwamba yanga akitufunga kesho anayo nafasi ya kubeba makombe mawili?
 
Kama yanga atashinda ipo wazi Simba atakuwa amemsajir mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine n kosa kisheria hivyo atanyang'anywa point kwa mechi alizocheza mchezaji
Na timu iliyochin yake kama point zake zitaizid Simba itakuwa bingwa

Juzi hapa as Vita imeporwa point tisa kwa kumchezesha mchezaj aliyekuwa na mkataba na tp mazembe na hvyo mazembe kuwa bingwa japo kesi iliamuliwa na federation ya huko Congo lakn mazembe alifungua shitaka katika shirikisho Hilo dhid ya mchezaj huyo na s as Vita

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Uko sahihi, mkataba wenye mapungufu unakua voidable na utakua valid endapo upande mwingine utaridhia kuendelea nao pamoja na hayo mapungufu lakini akigoma tu huo ni void tayari so huwezi ku-enforce huo mkataba.
Kwenye mikataba ya wachezaji kuna mapungufu yakitokea kwenye mkataba huo na huwa hayana madhara kwenye mkataba, ila kuna makosa kama kutokuwepo kwa saini mojawapo kati ya pande mbili za mkataba ndo pungufu pekee kwenye mkataba huwa linafanya mkataba usiwe halali, Je, kwenye mkataba wa morrison na Yanga kulikuwa na mapungufu gani?
 
Yanga akishinda jamaa zetu itabidi hata ubingwa wauteme,hapo ndio tutaona vita hapatakalika msimbazi zitapigwa ngumi hadharani wenyewe kwa wenyewe bonge la mtifuanona sijui manara wakati huo atakua wapi
Hakuna sheria hiyo ndugu siku hizi,FIFA ilishasema atakapokabidhiwa kombe team bali kila kitu kimeishia hapo,kama mtakuwa na mengine yataendelea lakini suala la kombe halitopatikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…