Khadija Kopa atoa ya moyoni kuhusu fununu za mahusiano ya mwanaye Zuchu na Diamond Platnumz

Khadija Kopa atoa ya moyoni kuhusu fununu za mahusiano ya mwanaye Zuchu na Diamond Platnumz

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Mtunzi na mwimbaji mashuhur wa nyimbo za taarabu kutoka Zanzibar Khadija Omar Kopa amepasua mbarika kuhusu uhusiano wa bintiye Zuhura Othman Soud almaarufu kama Zuchu na bosi wa WCB Diamond Platnumz.

Hii ni kufuatia uvumi unaoenezwa kuwa nyota hao wawili wa Bongo wanachumbiana baada yao kuonekana hotelini pamoja siku ya Krismasi.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Mbengo TV, Bi Kopa alipuuzilia mbali madai hayo huku akisema alishtuka sana uvumi kuhusu mahusiano ya bintiye na Diamond ulipovumishwa mitandaoni.

Kopa alisema bintiye aliwasiliana na bintiye na akamueleza hali halisi kuwa huo ni uvumi tu usio na msingi. Zuchu alimhakikishia mamake kuwa Diamond amekuwa akionyesha heshima kubwa kwake na hakuna chochote kinachoendelea kati yao.

"Wakati ule Zuhura aliniambia Diamond anamheshimu sana na hajawahi hata siku moja kuniambia vitu vya kipuzi. Nilishtuka maanake watu walikuwa wanavumisha kupita kiasi. Nilishangaa mbona walivumisha kupita kiasi. Mimi mwenyewe sikushughulika sana. Nilimuuliza Zuhura mbona watu walivumisha sana ama kuna kitu chochote. Aliniambia hamna wala hajawahi kuvunjiwa heshima hata siku moja. Mimi nilichukulia kama kitu cha kawaida" Alisema Khadija Kopa.

Bi Kopa aliweka wazi kuwa kwa miaka mingi Diamond anamchukulia kama mamake na amekuwa akimheshimu sana.

Alisema kwamba yeye ndiye aliyempeleka Zuchu Wasafi na wakati ule Diamond alimchukulia binti yake kama mdogo wake.

"Diamond mimi ananiona kama mamake kusema ukweli. Tangu zamani, kabla ata huyo Zuchu hajaenda Wasafi, amenichukulia kama mamake. Siku niliyomwelekeza mwanangu ata kabla aende WCB nilimwambia wewe ndio meneja wangu. Alimchukulia kama mdogo wake, hamtanii" Alisema Kopa.

Gwiji huyo wa Taarab alisema Diamond alishangaa wakati alipokabidhiwa Zuchu WCB kwani alimuona kama mwanadada mpole sana.

Alisema kwamba binti yake aliwahi kumtambulisha mwanamume mmoja tu kama mpenzi wake ila mahusiano yao hayakudumu

unnamed (1).jpg
 
Diamond naye sijui anakwama wapi KUOA kazi yake kuvicharaza vibinti 😂 na anawatafuna sana haloo
lisemwalo lipo, kama halipo laja

Vigezo vyote vya kuoa Mondi anavyo sasa sijajua nini tatizo, au anaogopa akioa atashuka kimuziki (sidani), au majukumu(sio wa kushindwa yule) au ndio masharti ya upande ule....

NB: Chawa wa WCB msinitukane ni mtazamo tu msijenge chuki🤣
 
Huyo msanii, maisha yake ni sanaaa.. Na ndoa sio sanaaa wala usaniii..
 
Diamond naye sijui anakwama wapi KUOA kazi yake kuvicharaza vibinti [emoji23] na anawatafuna sana haloo
lisemwalo lipo, kama halipo laja

Vigezo vyote vya kuoa Mondi anavyo sasa sijajua nini tatizo, au anaogopa akioa atashuka kimuziki (sidani), au majukumu(sio wa kushindwa yule) au ndio masharti ya upande ule....

NB: Chawa wa WCB msinitukane ni mtazamo tu msijenge chuki[emoji1787]
Unaambiwa Dimond ni mfuatiliaji mzuri sana wa thread na comment za Liverpool VPN humu jukwaani.
 
Back
Top Bottom