View attachment 2860213
NI MTIKISIKO!
Kiungo punda, kisiki wa Klabu ya Yanga Khalid Aucho ‘Daktari’ na Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ kwa pamoja wako mapenzini na mwanadada mrembo wa kuitwa Caren Simba.
Kiungo huyo Mganda anayetajwa kama sehemu ya mafanikio ya Yanga kwa msimu wa tatu mfululizo, na msanii asiyekaukiwa matukio, Harmonize haifahamiki kwa uhakika ni nani aliyeanza kuwa na mrembo huyo, na kama kila mmoja anafahamu uwepo wa mwenzake!
Kwa kiasi kikubwa, kuna uwezekano Harmonize anafahamu uwepo wa ‘Daktari’ Aucho kama bwana mwenza kutokana na mienendo yake ya ‘kumega kisela’ ambayo huiweka wazi hadi kutungia wimbo ‘Side Niggah’
NI WAFUASI WA SHEIKH KIPOOZEO…
Kutokana na historia ya wanawake waliowahi kujihusisha nao kimapenzi, wote wawili Aucho na Harmonize ni wazi ni wapenzi wa neema za Allah a.k.a mizigo kama asemavyo kipoozeo.
Khalid aliyekuwa kwenye mahusiano pekee yaliyofahamika na mwanadada kutokea kituo cha habari cha Uganda BBS Sumi, huku Harmonize akiwa na Kajala… wote wakiwa ni wanadada ‘waliojaaliwa’ neema hizo za Allah!
Ex wa Aucho, Sumi
View attachment 2860225
Mwanadada huyo Caren ambaye ni mzazi mwenza wa Baraka Prince, shughuli zake zinazofahamika ni uigizaji na kwa kiasi kidogo ameonekana katika video za muziki wa Bongo Fleva huku wimbo maarufu ukiwa ni Single Again kutoka kwa Harmonize.
AJISOGEZA KWA PACOME ZOUZOUA!
View attachment 2860223
Kwa habari za chinichini ni kwamba mwanadada huyo yuko mbioni kulisaka penzi la Mchezaji ‘Profesa’ Pacome pia kutokea Yanga.
Wakati jitihada hizo za Caren juu ya Pacome zingali zikiendelea, Khalid Aucho bado anamshikilia mrembo huyo.
Itakuwaje kama Pacome akinasa Ulimbo? Yatakuwa kama ya Kevin De Bruyne na Thibaut Courtois kwenye bifu lisiloisha juu ya mwanamke?
Mungu apishilie mbali!
Heri ya Mwaka Mpya wadau wangu katika ubuyu…
Chanzo chetu ni kilekile nyeti,
Nifah.