MastaKiraka
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 5,736
- 18,648
Kaligraph Jones ni Rapper mkali na amefanikiwa kufika mainstream kwa Africa mashariki, ila uwezo wake ukilinganisha na Rappers kama Nikki mbishi, One the incredible na Mex cortez bado ni mdogo, nimechagua hao rappers watatu kutoka TZ kwa sababu ya uwezo wao mkubwa kwenye ku flow vitu vyenye tija ama kushambulia mpinzani kwa ufanisi kupitia lugha ya kiswahili na Kiingereza (Bi Lingual) kitu ambacho kaligraph anajivunia nacho, tofauti ni kwamba hao watatu hawajafanikiwa kwenda mainstream, ila kama anataka battle atagaragazwa vibaya sana na hao ndugu watatu na ndio inawezekana ikawa nafasi ya kuwapeleka mainstream east Africa. BTW Nyashinski akiamua kurudi zama zake za ku Rap anaweza kumkalisha Kaligraph Round ya kwanza na kuiteketeza kabisa career ya Kaligraph.